Mama ni dhahabu yenye thamani kubwa duniani

The Lastdream

JF-Expert Member
Jan 23, 2024
1,596
3,500
Salaama?

Leo nilkuwa napitia picha za zamani, nikakutana na picha ambayo ilinifanya nilie kwa furaha, mwanamke shupavu, aliyejaa tabasamu usoni akiwa na beseni lake nyuma akiwa amebeba mtoto aliyefungwa na kanga. Hakika nimekumbuka mbali sana.

Mimi kipindi nakua mzee wangu alikuwa mlevi sana, stori moja ambayo naikumbuka yenye historia kubwa ni siku moja nilipotaka kwenda chooni.

sasa pale tulipokuwa tukiishi pembeni kulikuwa na nyumba ya jiran ilikuwa na mbwa lakini mbwa wale walikuwa hawana matunzo wanarandaranda tu, usiku huo nakumbuka mama anajifuta machozi baada ya kupokea kipondo kutoka kwa mzee hapo mzee kashalewa, akimaliza kumpiga anaamua aondoke, sikumbuki muda sahih ila giza ilkuwa kubwa nikamuambia mama nahitaji kwenda chooni kukojoa.

Akawasha chemli na palikuwa kuna kimvua kimetoka kunyesha, sasa tumetoka nje maana choo kipo nje hatua kadhaa kutoka nyumba, ni vile vyoo vya shimo. Basi kipindi tunatoka wale mbwa wa jirani wakamuona sijui walifikiri nini! Walikuja ghafla wakiwa wanataka kuja kuninga’ta mama akanibeba wale mbwa walikuwa wawili wakamvaa kwenye mguu wakaanza kumnga’ta basi nikaanza kupiga kelele na mama akipiga kelele.

Jirani wa nyumba ya pembeni akawa anaongea dirishani we toka. Tukaanza kuona majirani wanatoka mbwa wakakimbia ila damu alishaanza kuvuja bimkubwa.

Ikabidi usiku ule majran waje kugonga kumbe mzee hayupo, wakambeba mpaka hosptali.

Kwa kweli siku ile huwa haifutiki kabisa kwenye maisha yangu, sasa nimekua mkubwa nilipokuwa mtoto nilikuwa nikiongea nitakusaidia mama nikiwa mkubwa. Hakika nadhiri ile sijaacha, hata kama nikipata elf5 namtumia mama 2500 unaona jinsi anavyoshukuru, wale ambao wanawatumia wazazi wao watakuwa wanaelewa hii hali na jinsi unavyojhisi.

MAMA NI TUNU YENYE THAMANI.

Embu share kisa chako na mama yako tuwaenzi mama zetu?
 
NA WALE WANAO TUPA WATOTO WAO WA KUWAZAA..?WALE WALIO TUPWA NA WAO WASEMAJE HUKO WALIKO WENGINE WALILIWA NA MBWA BAADA YA KUTUPWA..

WEWE SHUKURU TU MUNGU UMEZALIWA SALAMA ....MAMBO YA NANI KAMA MAMA HUWA SIYAELEWI.

MAMA NA BABA WA UKWELI NI YESU TU,

JE NANI KAMA YESU??

MUNGU WAPE PUMZIKO LA MILELE WANAO TUPWA MAJALALANI NA MAMA ZAO

ASANTE YESU KWA KUNIFANYA NIMEZALIWA BILA SHIDA WEWE NDIE ULIE NILINDA KWA NEEMA TU BADO NIKO HAI
 
NA WALE WANAO TUPA WATOTO WAO WA KUWAZAA..? WEWE SHUKURU TU KWA KUPATA HUYO MAMA YAKO TU....MAMBO YA NANI KAMA MAMA HUWA SIYAELEWI.

MAMA NA BABA WA UKWELI NI YESU TU,

JE NANI KAMA YESU??

MUNGU WAPE PUMZIKO LA MILELE WANAO TUPWA MAJALALANI NA MAMA ZAO

ASANTE YESU KWA KUNIFANYA NIMEZALIWA BILA SHIDA WEWE NDIE ULIE NILINDA KWA NEEMA TU BADO NIKO HAI
Katika wanawake 100 utapata mmoja aliyetupa mtoto.
Sisi wanaume ni kawaida kutelekeza watoto hilo linajulikana labda tu ulete ubishi
 
NA WALE WANAO TUPA WATOTO WAO WA KUWAZAA..? NA WANYEWE WASEMAJE HUKO WALIKO WENGINE HULIWA NA MBWA BAADA YA KUTUPWA.. WEWE SHUKURU TU KWA KUPATA HUYO MAMA YAKO TU....MAMBO YA NANI KAMA MAMA HUWA SIYAELEWI.

MAMA NA BABA WA UKWELI NI YESU TU,

JE NANI KAMA YESU??

MUNGU WAPE PUMZIKO LA MILELE WANAO TUPWA MAJALALANI NA MAMA ZAO

ASANTE YESU KWA KUNIFANYA NIMEZALIWA BILA SHIDA WEWE NDIE ULIE NILINDA KWA NEEMA TU BADO NIKO HAI
Kwani yesu ndio aliyekuzaa? Mkuu Embu soma vzuri dini isikufanye kuwa mpumbavu kiasi hicho!
 
Katika wanawake 100 utapata mmoja aliyetupa mtoto.
Sisi wanaume ni kawaida kutelekeza watoto hilo linajulikana labda tu ulete ubishi
HIZO TAKWIMU WEWE UMEZIPATA WAPI... NCHI HII KUBWA

MDA HUU TUNAO ONGEA KUNA WATU MAENEO TOFAUTI WAPO KUTUPA WATOTO.

NA HATA UNAVYOSEMA KATI YA WANAWAKE 100 UTAPATA MMOJA ANAE TUPA MTOTO

SWALI KWAKO JE UNGETUPWA WEWE UNGEKUJA NA UZI WAKO HAPA WA MAMA NI DHAHABU

NDIO MAANA NAKUAMBIA UKIONA UMEZALIWA SALAMA KATIKA DUNIA HII WEWE MSHUKULU MUNGU TU.
 
Salaama?
Leo nilkuwa napitia picha za zamani, nikakutana na picha ambayo ilinifanya nilie kwa furaha, mwanamke shupavu, aliyejaa tabasamu usoni akiwa na beseni lake nyuma akiwa amebeba mtoto aliyefungwa na kanga. Hakika nimekumbuka mbali sana.

Mimi kipindi nakua mzee wangu alikuwa mlevi sana, stori moja ambayo naikumbuka yenye historia kubwa ni siku moja nilipotaka kwenda chooni.

sasa pale tulipokuwa tukiishi pembeni kulikuwa na nyumba ya jiran ilikuwa na mbwa lakini mbwa wale walikuwa hawana matunzo wanarandaranda tu, usiku huo nakumbuka mama anajifuta machozi baada ya kupokea kipondo kutoka kwa mzee hapo mzee kashalewa, akimaliza kumpiga anaamua aondoke, sikumbuki muda sahih ila giza ilkuwa kubwa nikamuambia mama nahitaji kwenda chooni kukojoa.

Akawasha chemli na palikuwa kuna kimvua kimetoka kunyesha, sasa tumetoka nje maana choo kipo nje hatua kadhaa kutoka nyumba, ni vile vyoo vya shimo. Basi kipindi tunatoka wale mbwa wa jirani wakamuona sijui walifikiri nini! Walikuja ghafla wakiwa wanataka kuja kuninga’ta mama akanibeba wale mbwa walikuwa wawili wakamvaa kwenye mguu wakaanza kumnga’ta basi nikaanza kupiga kelele na mama akipiga kelele.

Jirani wa nyumba ya pembeni akawa anaongea dirishani we toka. Tukaanza kuona majirani wanatoka mbwa wakakimbia ila damu alishaanza kuvuja bimkubwa.

Ikabidi usiku ule majran waje kugonga kumbe mzee hayupo, wakambeba mpaka hosptali.

Kwa kweli siku ile huwa haifutiki kabisa kwenye maisha yangu, sasa nimekua mkubwa nilipokuwa mtoto nilikuwa nikiongea nitakusaidia mama nikiwa mkubwa. Hakika nadhiri ile sijaacha, hata kama nikipata elf5 namtumia mama 2500 unaona jinsi anavyoshukuru, wale ambao wanawatumia wazazi wao watakuwa wanaelewa hii hali na jinsi unavyojhisi.

MAMA NI TUNU YENYE THAMANI.

Embu share kisa chako na mama yako tuwaenzi mama zetu?
Mama ni Dunia ya kwanza ya mtoto tangu anapozaliww hukua katika mikono yake, ananyonya kweny kifua chake na analala kwenye mikono yake, mama halali mpaka mtoto alale, mama ni furaha ya mtoto alalapo na aamkapo humuona mama karibu yak, mama ni mlinzi wa mtoto katika hatari humkinga mtoto asiumie lakini yupo radhi aumie yeye, mama ni sadaka kwa mtoto tangu kutungwa kwa mimba mpaka kuzaa n kujitoa sadaka kwaajili ya maisha ya mtoto, yupo radhi akose mtoto apate.... Mama ni upendo wa kwanza na wakweli kwa mtoto....nilitoka mama ndio nilielewa upendo wake upoje, hulali mpaka mtoto alale na kipindi ukitoka kujfungua mwili unakuwa mchovu sana Kuna kausingz kazito balaa lakin hutalala kama mtt hajalala na n wanasumbua sana kutwa kulia. wanaposema uchungu wa mwana aujuae mzazi ni kweli.. mtoto ni anauma sana zaid ya sana... Mwenyez mungu awafanyie wepesi waliopoteza watt maana maumv yake hayana kipimo... Mliobahatika mama zenu wapo hai wapendeni sana msiwasahau
 
Hakika huu ujumbe mzuri sana.

MAMA NI THAMANI KUBWA ISIYOLINGANA NA CHOCHOTE.
 
HIZO TAKWIMU WEWE UMEZIPATA WAPI... NCHI HII KUBWA

MDA HUU TUNAO ONGEA KUNA WATU MAENEO TOFAUTI WAPO KUTUPA WATOTO.

NA HATA UNAVYOSEMA KATI YA WANAWAKE 100 UTAPATA MMOJA ANAE TUPA MTOTO

SWALI KWAKO JE UNGETUPWA WEWE UNGEKUJA NA UZI WAKO HAPA WA MAMA NI DHAHABU

NDIO MAANA NAKUAMBIA UKIONA UMEZALIWA SALAMA KATIKA DUNIA HII WEWE MSHUKULU MUNGU TU.
Wewe hizo takwimu umezipata wapi Embu weka takwimu hapa tuzione?

MAMA NI TUNU KUBWA.
 
Dah kweli Mkuu ila unajua kwann dingi Yako alikuwa mlevi at first place?Inawezekana ni kutokana na mdomo wa Maza Ako,any way we don't know shit that's why tutaendelea ku under estimate madingi zetu.
Kwakweli kwa kipigo alichokuwa akipitia mama na kufanya kazi mzee haonekani hata siku tatu hili nalikataa.
Bado na kupigwa kote aliendelea kumpikia baba chakula, na hata akirudi kalewa hajiwezi anamtengenezea uji wa ndimu na kumpaka kwenye unyanyo ili kuondoa pombe haraka.

Hakika nikipata mwanamke Mwenye sifa kama za mama yangu nitaoa.
 
Ni kanuni yako mkuu uliyojiwekea au ndio uhalisia?

Ndo uhalisia

Tambua inatumika nguvu kubwa sana kuishusha hadhi na nguvu ya mwanaume kwa sasa ila kiasili mwanaume ana wajibu wa kuhusika na kila kitu duniani kasoro kubeba mimba na kuzaa!
 
Wewe hizo takwimu umezipata wapi Embu weka takwimu hapa tuzione?

MAMA NI TUNU KUBWA.
TUNU KWAKO MKUU... LAKINI KWA WALE WALIO TUPWA AU KUTOLEWA MIMBA KAMA TUNGEKUWA TUNAWEZA KUWARUDISHA WASINGE KUELEWA WANGEKUPIGA SHABA

WEWE SHUKULU MUNGU TU UMEZALIWA SALAMA SIO KWA UJANJA WA HUYO MAMA YAKO.
 
Pole sana mkuu.
Nasubir takwimu
 
Back
Top Bottom