Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,924
- 30,272
- Thread starter
- #81
Ukisoma kitabu utakuta kila kitu chake mle ndani. Ila kwa ufupi katika territorial exams 1941 alitokea mwanafunzi wa kwanza Kitchwele Middle School na akachaguliwa kuingia Makerere College, Uganda.
Kwa nini hakwenda Makerere na badala yake Waingereza wakamtia jeshini (King's African Rifles) kwa mujibu wa sheria utapata katika kitabu.
Huko jeshini wakati wa Vita Kuu ya Pili ndipo alipokuja na wazo la kuasisi TANU. Hii ilikuwa tarehe 25 December 1945 na fikra hii aliandika katika shajara yake (diary).
Baba yangu alisoma darasa moja Al Jamiatul Islamiyya School na marehemu Abdulwahid Sykes (hiyo shule ilijengwa kwa juhudi za baba yake Kleist na wazee wengine hadi leo ipo pale Mtaa wa Lumumba na Aggrey).
Baba yangu anasema ilimchukua Abdu muda mfupi sana kumaliza kusoma mashafu yote na akawa sasa anawasomesha wenzake pamoja na mzee wangu.
Waliomfahamu wanasema Mungu alimjalia akili sana.
Alipata mafanikio makubwa katika KAR huko Burma na akiwa na umri wa miaka 24 alikujakuwa Secretary General wa Dar es Salaam Dockworkers Union mwaka 1949.
Kuna kisa cha kusisimua kuhusu harakati katika za siasa za wafanyakazi katika kipindi hiki.
Lakini sifa yake kubwa ilikuwa ukarimu. Watu wengi wa hali za chini wa Dar es Salaam wanamkumbuka kwa hili.
Maziko ya Abdulwahid hayajapata kutokea kwa wakati ule alipofariki mwaka 1968 alizikwa na umma mkubwa sana.
Nyerere alitembea kwa miguu nyuma ya jeneza la Abdulwahid kutoka nyumbani kwa mama yake Kirk Street
(sasa Mtaa wa Lindi) hadi makaburi ya Kisutu.
Kitabu kitapatikana hapo Kase Bookshop hivi karibuni Insha Allah.
Abdulwahid Sykes alikuwa bingwa wa kusema Kiingereza. Mzee mmoja alinambia kuwa yeye akipenda kumsikiliza Abdu alivyokuwa akikoroga kimombo utasema Mzungu.