Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHIS SYKES (1924 -1968)

Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika na Mohamed Said

Pitio la Kitabu

Kitabu hiki kilipochapwa kwa mara ya kwanza 1998 kwa Kiingereza nchini Uingereza na kilipoanza kuzagaa katika maktaba na maduka ya vitabu mjini London yanayouza vitabu kuhusu Afrika Watanzania wengi waliokuwa Uingereza walisisimuliwa na yale yaliyokuwa ndani ya kitabu hiki. Kubwa zaidi ilikuwa kule kufunuliwa kwa mara ya kwanza kuwa kumbe TANU chimbuko lake si Julius Nyerere bali ni marehemu Abdulwahid Sykes. Hii ilikuwa habari mpya kwa wengi hasa ikizingatiwa kuwa Nyerere mwenyewe hakuwahi kumtaja Abdulwahid Sykes kama mwenzake katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Hili lilikuwa la kwanza. Kitu cha pili kilichosisimua wasomaji ni kuwa mwandishi kwa kutulia kabisa alionyesha bila woga na kutafuna maneno kuwa TANU kilikuwa chama kilichojengwa katika migongo ya Waislam. Hili alilishaijisha kwa kueleza wazalendo waliokuwa bara ambao kwa umoja wao na wengi wao wakiwa Waislam walipambana na ukoloni wa Kiingereza.

Kubwa zaidi la kusisimua ilikuwa kitabu kilieleza bila kupepesa macho au kutafuna maneno njama alizofanya Nyerere kwanza kumfuta Abdulwahid Sykes katika historia yake binafsi, TANU na katika harakati za kudai uhuru. Lakini kilichotibua sege la nyuki ni pale katika kuhitimisha kitabu mwandishi alipoweka wazi mipango ya Nyerere akishirikiana na Kanisa Katoliki baada ya uhuru kupatikana kupanga njama za kuzuia maendeleo ya Waislam. Katika kipande hiki msomaji atakutana na Mufti Sheikh Hassan bin Amir aliyekuwa mufti wa Tanganyika na Zanzibar na mwanasiasa shupavu. Msomaji ataziona juhudi za Sheikh Hassan bin Amir katika kupambana na njama za Nyerere na Kanisa Katoliki na nini kilimfika msomi huyu maarufu wa Kiislam. Kwa wakati ule Nyerere akiwa hai ilihitaji ujasiri mkubwa kwa yeyote yule kusema au kuandika hayo.

Nakala za kitabu zilifika Tanzania na kila aliyesoma alipatwa na mshtuko mkubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na nje yake. Kitabu kiliwaudhi wapenzi wa Nyerere na wapo waliomwendea kwa kutaka afanye jambo kukomesha "uongo" wa mwandishi. Wengine hawakuamini kuwa huyo anayejiita Mohamed Said kama kweli yupo. Wengine walitaka kujua kama kweli akina Sykes na baba yao ndio waasisi wa vyama vya Waafrika katika Tanganyika katika 1929 hadi 1954 TANU ilipoasisiwa. Hii ilikuwa bahari kubwa kwa wapenzi wa Nyerere ambao wasingeweza kuogelea bila ya msaada wake Baba wa Taifa. Mawimbi ya bahari hii yalikuwa marefu na yakija kwa kasi. Juu ya haya yote Waswahili wana msemo "penye ukweli uongo hujitenga." Nyerere asingeweza kuthubutu kukana mchango wa marehemu Abdulwahid kwake yeye binafsi na kwa TANU. Abdulwahid ndiye aliyempokoea Dar es Salaam ile ya miaka ya 1950 na akamjulisha kwa wenyeji wa mji. Wapenzi wa Nyerere hadi leo ukiwauliza Nyerere alisema nini kuhusu ukweli kuwa si yeye aliyeasisi TANU wamekuwa kimya.

Msomi maarufu wa Chuo Kikuu cha Cambridge John Illife ambae ameandika sana historia ya Tanganyika alikasirishwa na msimamo wa mwandishi khasa pale aliposema kuwa inastaajabisha kuwa Illife ingawa alitegemea nyaraka za akina Sykes katika kuandika historia ya African Association inastaajabisha hakuona umuhimu wa kutaka kumhoji marehemu Abduwahid aliyekuwa katibu na rais wake kati ya 1951 hadi 1953. Akiandika pitio la kitabu hiki katika Cambridge Journal of African History Illife alimshambulia mwandishi katika njia ambayo haikuwa staili yake msomi mkubwa kama yeye. Illife alikuwa ameghadhibishwa kwa kuambiwa katika kitabu kuwa alimzuia mwanafunzi wake katika Idara ya Historia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka wa 1969, Daisy Sykes ambae alikuwa binti ya Abdulwahid asiandike maisha ya baba yake. Daisy wakati huo msichana mdogo alikuwa amekasirishwa na jinsi TANU na magazeti yake yote, "The Nationalist" chini ya uhariri wa Benjamin Mkapa na "Uhuru" yalivyoshindwa kumwandika baba yake kwa hadhi aliyostahili. Magazeti hayo yaliripoti kifo cha Abdulwahid Sykes kwa kuwa Nyerere alikwenda mazikoni. Hapakuwa na jingine. Brendon Grimshaw ambae alikuwa Mhariri Mkuu wa "The Tanganyika Standard" na akimfahamu vyema Abdulwahid ndiye aliyendika tanzia ya maana katika "Sunday News" akasema kuwa Nyerere asingelifika pale alipofika kama si kwa msaada wa Abdulwahid Sykes na ni juhudi za ukoo wa Kleist ndiyo uliowezesha watu wa Tanganuyika kuwa na chama cha siasa. "The Standard" na "Sunday News" wakati ule lilikuwa gazeti huru halikuwa na hofu ya Nyerere. Hii ilikuwa mwaka 1968.

Kilipotoka kitabu hiki mwaka 1998 walikuwepo watu walioona ukweli wa kuwa historia ya TANU bado haijaandikwa na kuna baadhi ya shutuma zilizoelekezwa kwake Nyerere ni muhimu yeye mwenyewe akazijibu akiwa hai kwa faida ya jamii isijesemwa kuwa kasingiziwa, walimsubiri afe ndipo wamzushie la kumzushia. Mmoja wi wa kundi hili la pili alikuwa marehemu Prof. Haroub Othman. Yeye alimkabili Nyerere uso kwa macho na kumuomba atoe majibu kujibu shutuma za waandishi wawili. Kwanza ajibu shutuma za Sheikh Ali Muhsin Barwani aliiyekuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (Hizbu) katika kitabu chake "Conflict and Harmony in Zanzibar" na kitabu cha Mohamed Said "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (19241968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika." Sheikh Ali Muhsin akimtuhumu Nyerere kwa kupeleka mamluki Zanzibar kuipindua serikali ya wananchi na Mohamed Said akimtuhumu kwa chuki dhidi ya Waislam na kupotosha historia ya uhuru wa Tangnayika. Prof. Haroub alimshauri Nyerere kuwa njia nzuri ya kuiweka historia yake na uhusiano wake na Waislam sawa ni kwa yeye kuandika historia ya maisha yake. Hadi Nyerere anaingia kaburini hiili halikufanyika.

Kitabu hiki ni muhimu kwa Waislam na wananchi wote kwa ujumla kukisoma na kuwahimiza watoto wao nao wakisome wapate kujifahamu na kufahamu changamoto za udini na chanzo chake. Ndani ya kitabu hiki mwandishi amejitahidi kukusanya mashujaa waliotupwa waliopigania uhuru wa Tanganyika hata kabla hawajasikia jina la Nyerere wala kuona sura yake, wazalendo kama Hassan Suleiman na Juma Ponda wa Dodoma. Wazalendo waliohutubia mikutano ya hadhara na kuhamasisha watu kudai uhuru hata Nyerere hawamjui kama Titi Mohamed na wengine wengi kutoka katika majimbo ya Tanganyika. Ukikianza kitabu hiki huwezi kukiweka chini hadi umefika mwisho.

Kitabu hiki kinapatikana Ibn Hazim Bookshop Mtoro na Manyema na Tanzania Publishing House, Samora Avenue.


Its an interesting book.I recommend it..... kuna mengi tunayopaswa kuyajua!
 
Heshima kwako Mohamed said,

Mzee wangu hii si mara ya kwanza kusoma habari za Abdulwahid Sykes hapa jamvini,mwaka jana ulikuja na hoja kama hii ikapigwa ban na mod kwasababu mjadala ulijikita zaidi kwenye udini sijui kama na hii itachukua mkondo kama ule wa mwanzo ni mapema mno kutabiri ingawa tayari nahisi kaharufu ka udini.


Binafsi nimekisoma hiki kitabu with an open mind na nikajifunza kitu au vitu - historia ( ambayo ina uwezekano kupotoshwa pia)

Mtu atakayekisoma au kujadili maudhui kwa mrengo wa kidini basi kuna uwezekano mkubwa sana wa kupotosha mambo mengi.I hope mwenzetu aliyeweka mada hapa hana lengo la upotoshaji bali kuelimisha zaidi.
 
Lengo kubwa hapa ni kutafakari na kuchanganua jinsi gani nchi yetu ipambane na changamoto zinazoikabili.

Silielewi dhumuni la mwanzilishi wa thread hii kama lengo ni sisi kumfaham bw. Sykes. Tukishamjua then? Au kueleza ya kwamba Nyerere alikwamisha maendeleo ya watu wa dini yake? Ingawaje hajasema aliyakwamishaje? Na nini kifanyike baada ya kuyatambua hayo!?.
 
Madhumuni ni kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika ambayo marehemu Abdulwahid Sykes alihusika sana khasa katika kuunda TANU. Historia ya TANU imeandikwa na Kivukoni College lakini kwa hakika kwa sisi watoto wa Dar es Salaam ukisoma unaona hiyo ni historia nyingine siyo ya TANU ile ambayo tukiona baba na mama zetu wakiichangia sumni sumni ili Nyerere aende UNO.

Kwa mukhtahasari kusudio ni kurekebisha pale palipokosewa.

Kuhusu vipi Nyerere alifanya khiyana ya kukwamisha maendeleo ya Waislam nimeeleza kwa kirefu mno katika kitabu na kusema kweli ndiyo moyo wa kazi ile.

Ukisoma kitabu utapata majibu ya maswali ulouliza.
 
Ikiwa pako unaona pamepotoshwa sema na Insha Allah nitapitia upya nyaraka kutafuta ukweli.

Kazi yeyote ya binadamu lazima iwe na makosa.

Hili halina wasiwasi.
 
Ahsante nami nitakitafuta kwa udi na uvumba, SHUKRAN ULAMAA KWA IHSAAN YAKO KUTUJUZA HAYO, NITAKITAFUTA Inshallah.
 
Well well well..................angalau nitawasoma tena akina Lole Gwakisa et al....wamepotea sana.........

Mkuu MS karibu tena jamvini.........naona umerudi na gia ile ile...........
 
Mimi naona kuna watu wanataka kutumia historia kuendeleza ajenda zao za siri hapa. Naamini kabisa hawa WAISLAMU kama akina Abdulwahid Sykes na wenzake wengi walikuwa na uchungu wa kweli wa kutaka UHURU, na hawakuwa wakipigania uhuru wa WAISLAMU bali uhuru wa TAnganyika yote. Ndio maana hata alipokuja mpigania uhuru mwingine aliyekuwa sio MUISLAMU wao hawakuona tofauti, kwakuwa ajenda ilikuwa ni UHURU na sio UISLAMU.

Sasa ni wazi kabisa kuwa kuna baadhi ya watu wamepumbazwa na fikra za UDINI na sasa wanataka kutumia majina na mashujaa wetu wapigania uhuru kukuza UDINI ili ajenda zao za siri zifanikiwe. Mohamedi na wenzako acheni fikra za UDINI.....tuijenge nchi yetu hii iwe kama hao waliopigania uhuru walivyopenda iwe. Hii ndio njia pekee nzuri ya kuwaenzi hao mababu zetu na sio kulia lia na UDINI.
 
MOHAMED SAID!!! Sielewi unataka kuwaambia nini watanzania maana hueleweki. Hivi Nyerere kukiongoza TANU na kuongoza kudai uhuru unataka kutuambia waislamu wa kipindi hicho pamoja na wingi wao walihongwa na nyerere ili wamchague awe kiongozi na hatimaye kuwa Rais wa kwanza wa Tanzania.

Unasema amedidimiza elimu ya waislam, kwanza hujatuambia kipindi cha hao wakina sykes shule za waislamu zilikuwa ngapi na za wakristo zilikuwa ngapi then useme nyerere alitaifisha shule za waislam na kuwapa wakristo.

Lazima tujiulize, TAA kilianzishwa muda mrefu miaka ya 1920s kama sikosei na wengi wa wanachama wake walikuwa waislamu, hivi kwa muda wote huo hawakujua tanganyika ilikuwa chini ya ukoloni mpaka wakashindwa kudai uhuru mpaka wakamsubiri nyerere kukibadilisha TAA na kuwa TANU? ambapo <b><font color="blue">ilimchukua nyerere miaka 7 kutoka 1954 - 1961 kuiletea tanganyika uhuru

Acheni kupotosha watu, udini hauwasaidii watanzania. mawazo yako ni mgando. SASA HIVI TUNATAKIWA KUIJENGE TANZANIA MPYA KWA KUPAMBANA NA MAFISADI NA KUTETEA RASILIMALI ZA NCHI YETU ILI ZIJE ZISAIDIE VIZAZI NA VIZAZI VYA TANZANIA IJAYO WATU TUNATAKA KATIBA MPYA ITAKAYOKIDHI MAHITAJI YETU YA SASA NA MIAKA 100 IJAYO CHA KUSHANGAZA WEWE UNATAKA UTUREJESHE ETI KWENYE HISTORIA ILIYOSAHAULIKA. NATAKA NIKWAMBIE HAITUSAIDII KWANI HILO SI TATIZO LINALOTUTATIZA KWA SASA MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE ASLAAM ALEYKUM!!!!
Mfukuzi, nashauri tukinunue kitabu tukisome ndipo tumshukie Mohamed Said. Nategemea nitayakuta pia majina ya wapigania uhuru wengi tuu ambao hawakutajwa tajwa kama kina Bagdelah, Makange, Kunambi, Kaaya , Rupia etc. Vinginevyo its another crap ya ajenda za udini!.

Binafsi niliwahi sikiliza simulizi moja ya Julius na Maria, toka kwa mjane wa Abdul Wahid enzi hizo akiishi pale Upanga opp. Califonia Dreamer, 'haziandishiki'!.
 
Paragraph yako ya kwanza umeeleza harakati kwa uzuri usio kifano.

Kitabu changu sasa kinaeleza nani alileta udini huu ambao sasa tunaueleza.

Kwa hakika mimi ningependa sana ukisome kitabu kwanza na uangalie mambo
yalivyoanza kubadilika mara tu uhuru ulipopatikana 1961.

Nina hakika utashangazwa kujua kuwa baada ya uhuru wapiganaji wote na wengi
wao wakiwa Waislam wakafutwa katika historia.

Mfano mdogo tu ni kuwa ilipoandikwa historia ya TANU na Chuo Cha Kivukoni jina
la Abdulwahid Sykes na wazalendo wengine kama Kiyate Mshume, Jumbe Tambaza,
Mufti Sheikh Hassan bin Amir hayakuwapo.

Jina lilikuwa moja tu la Julius Nyerere. Vipi utamuacha Abdu wakati mikutano ya siri ya
kuunda TANU ikifanyika nyumbani kwake Mtaa wa Aggrey na Sikukuu? Vipi utamuacha
Mshume Kiyate na wenzake na hao ndio walikuwa wafadhili wakuu wa harakati za kupigania
uhuru?

Siku nilipokwenda Tabora kumhoji Bilal Rehani Waikela mmoja wa waasisi wa TANU
Western Province alifurahi pasi na kiasi na aliniombea dua kazi yangu ifanikiwe.

Halikadhalika nilipokwenda kumhoji marehemu Dossa Aziz pale nyumbani kwake Mlandizi
furaha yake ilikuwa kubwa kiasi alitaka kuchinja mbuzi.

Wote waliokuwa katika harakati hawakuwa wamefurahi kuona historia ya uhuru wa Tanganyika
imeelekezwa kwa Nyerere peke yake ilhali harakati zilianza kabla yake toka 1929 na akina Kleist
Sykes (baba yake Abdu) na wenzake kama akina Mzee bin Sudi na Ibrahim Hamisi na wengineo.

Nakushauri usome kitabu na kama utakuta hicho unachoona "udini" lilete jambo hilo hapa ukumbini
tulijadili kwa pamoja.

Kwa hakika nia yangu ni kueleza kile ambacho wengi hawakuwa wanakijua.
 
Well well well..................angalau nitawasoma tena akina Lole Gwakisa et al....wamepotea sana.........

Mkuu MS karibu tena jamvini.........naona umerudi na gia ile ile...........

Nina kitabu kingine njiani chaja Insha Allah "Broken Dreams" mambo kati ya 1940 hadi leo. Utawaona wazee wetu walivyoteswa na ukoloni.

Vuta subra.

Nasikitika nimeandika Kiingereza na hili litaathir usomaji hadi ipatikane tafasiri yake.
 
Sheikh Mohamed,

Hawa wazee wetu wakiisalamu unaojaribu kuwatetea walikuwa wanatafuta uhuru wa waislamu au wa Tanganyika toka ukoloni wa Muingereza? Je Muingereza alikuwa anatawala Waisalamu tu au vinginevyo?

Niwie radhi kwa hilo na nakubaliana nawe kuwa historia yetu kama nchi haiko sawia kwa kuwa kun mengi tumefichwa,lakini kwa nini wewe mkazio wako uko kwenye Waislamu tu? Je hakuna watu wanye imani zingine (si lazima ukristo) ambao wamesahaulika? Nini nia yako hasa?
 
Ukisoma kitabu utapata majibu yote ulouliza.

Hakika kitabu hiki kimeleta mjadala mkubwa sana Ulaya na Marekani katika Vyuo Vikuu
vinavyosomesha historia ya Afrika.

Nao swali lao kuu ni kwa nini Nyerere aliiogopa historia ya uhuru wa Tanganyika na nafasi ya
Waislam katika kudai uhuru?
 
Mfukuzi, nashauri tukinunue kitabu tukisome ndipo tumshukie Mohamed Said. Nategemea nitayakuta pia majina ya wapigania uhuru wengi tuu ambao hawakutajwa tajwa kama kina Bagdelah, Makange, Kunambi, Kaaya , Rupia etc. Vinginevyo its another crap ya ajenda za udini!.

Binafsi niliwahi sikiliza simulizi moja ya Julius na Maria, toka kwa mjane wa Abdul Wahid enzi hizo akiishi pale Upanga opp. Califonia Dreamer, 'haziandishiki'!.

Ni wazo la busara kukinunua na kusoma hiki kitabu tuone kuna nini ndani,from there we can say something,lakini ni wazo la busara zaidi kutafuta hizi habari tok avyanzo vingine mbadala nje ya vile vilivyotumika kuandika kitabu hiki.

By the way Kaka naku-PM kuna ishu nataka kukuuliza.
 
Fact is TANGANYKA was not for Moslems alone...it was for Tanganyikans....kwa hiyo tuwashukuru Watanganyika wote waliojitolea kutupigania uhuru wetu wawe Waislamu au vinginevyo...OTHERWISE tuuze vitabu tushibe matumbo
 
Ukisoma kitabu utapata majibu yote ulouliza.

Hakika kitabu hiki kimeleta mjadala mkubwa sana Ulaya na Marekani katika Vyuo Vikuu
vinavyosomesha historia ya Afrika.


Nao swali lao kuu ni kwa nini Nyerere aliiogopa historia ya uhuru wa Tanganyika na nafasi ya
Waislam katika kudai uhuru?

Lazima kuzuke mjadala wa kutushangaa Watanganyika kuwa tunawaza udini badala ya utaifa
 
Swala nadhani wala si kutaka kujua aliyeanzisha TAA au TANU ni nani. Swala ni kufahamu na kuheshimu kila zuri lililofanywa na KILA waasisi na walioviendeleza vyama hivi. Ndio maana leo haumjui mzee James Mapalala lakini unamjua Ibrahim Lipumba na Maalim Seif(CUF).

Ndio maana leo haumjui Mzee Edwin Mtei lakini unawajua na kuwathamini Dk Slaa na Mbowe jr(CHADEMA). Tuwe na positive thinking behaviour jamani na tuondoe mawazo ya udini. Kuchochea udini hakutoweza kututoa kwenye lindi la u maskini tulionao. Umaskini utaondoshwa na kuacha porojo na kufanya kazi kwa bidii,ku plan kila kitu unachofanya,kupima matokeo na kurekebisha pale ulipokosea kwa ajili ya kupata matokeo mazuri baadae.

Ndio maana hata leo kuna matajiri wakubwa duniani ambao si wakristo wala si waislamu!. Haujajiuliza tu kwa nini?.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom