Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

Mohamed said, kama ni marketing strategy me i salute you, hii historia ya "wazee wenu kumchangia Nyerere thumni thumni ili aende UNO"haipo kabisa has given me food for thought.

Nimejaribu kugoogle hicho kitabu, i see it but naona maybe wamerun out of copies. Sasa a bit of help please hivyo zurich au london where can i get this book au naweza kiagiza wapi ili nikipate at least within a week
 
Kitabu kinauzwa Ibn Hazm Msikiti wa Mtoro na Tanzania Publishing House, Samora Avenue.
Ama kuwa ni ujanja wa kuuza kwa kweli si nia yangu iliyonisukuma kupata fedha.

Kubwa ilikuwa kutoa shukurani kwa wazee wetu wengi wao wametangulia mbele ya haki kuwa
hatukuwatupa mkono.

Sisi watoto wao tumejitahidi kwa kadri Allah alivyotuwezesha kuihifadhi historia yao kwa
manufaa ya kizazi kijacho.
 
Kinauzwa Shilingi ngapi, japo kama unafanya marketing na unashindwa kuweka bei ya bidhaa yako, utanishawishi vipi juu ya usahihi wa kitabu. nitajitahidi nikisome with an open mind.

Shillingi ngapi kinauzwa??
 
Mohamed Said,

Mbona umekazana sana na hizi historia za uislamu na uhuru as if to say waislamu peke yao ndio walianza hili varangati la uhuru. Ina maana na wakirsto nao wakianza kuelezea jitihada za makanisa kuleta uhuru itakuaje, by 'commonsense' some western missionaries were also not happy about colonizing countries in Africa. Point hapa ni kwamba tukisema tupekue wapiganaji wote tutakuta na wachungaji pia ambao walikua wakihutubia kutokubali ukoloni na sidhani kama na wao wapo mentioned katika vitabu vingi vya historia je hilo nalo unalionaje? au labda unataka kusema hakukuwa na wakristo wapiganaji wakati huo ambao hawajanukuliwa na historia.

Ukizungumzia dar au pwani utakuta majina ya waislamu wengi wapiganaji, lakini ukiingia bara utakutana na majina mengi pia ya wakristo ambao hawajatajwa kabisa katika historia na wao pia walikuwa na michango yao.

Halafu mbona mnapenda kujipa sifa sana za kupigania ukombozi au kuipatia Tanganyika uhuru kwa kuangalia historia ya upande mmoja, je mtu wa calibre yako (ya juu in my opinion) unashindwa ku-delve deeper into both sides of the coin historically hili utoe ukweli na jitihada zilizo hitajika kuipatia Tanganyika Uhuru. Nauliza hivi kwa sababu hata wazungu nao walishajua kuna baadhi ya makoloni ilibidi yarudi from early 1910's and by the 30's they knew it was inevitable especially with the indepence momentum that was growing very much in the 'gold cost' led by Dr.Azikiwe and other west African scholars.

Hii ndio ilikuwa the thinking in the west some colonies had to go but they tried hard to maintain the trophy ones like India, Zimbabwe and Kenya. Na hii ndio sababu ya kuanza kuwapeleka wa Africa kusoma makwao kwakujua endapo uhuru utakapo daiwa tutakuwa na baadhi ya watu wa kutuendesha. Sasa hizi hadithi zako za kusema sijui waisalamu ndio walioleta uhuru na porojo embu kidogo ungezipunguza kwa sababu makoloni yaliyo kuwa na faida trust me uhuru wao aukuja bila ya damu na fujo.

Historia ya Tanganyika na mkoloni wa mwisho aikuwa na ugumu sana kwetu, kwa sababu hawakufikia kiwango cha kusema wame invest as much as they did in other countries so Tanganyika was not a trophy colony. Not to mention they were having trouble finding people to govern the whole colony therefore any little fuss uhuru ungepatikana tu sioni sababu ya kumtukuza 'Nyerere' wala waislamu for that matter.

Huwezi fananisha pilika za 'Kenyatta' na 'Nyerere' kupatikana kwa uhuru. Vilevile kwa upande wa wazungu after the 'suez canal' crisis they had already given up maintaning most unprofitable colonies Tanzania being one of the main one, they hadnt done much then and it was a colony they only got to acquire by chance after the first world war.

Ukitaka kuelezea historia kabla ujapotosha wasomaji wako ebu kwanza weka na ugumu uliokuwepo kipindi hicho na wafungwa wote waliofungwa na si kusema waislamu tu, or else ni kujionyesha uislamu kwako huko mbele kuliko uzalendo wa tiafa lako you claim to care about.
 
........Sasa ni wazi kabisa kuwa kuna baadhi ya watu wamepumbazwa na fikra za UDINI na sasa wanataka kutumia majina na mashujaa wetu wapigania uhuru kukuza UDINI ili ajenda zao za siri zifanikiwe. Mohamedi na wenzako acheni fikra za UDINI.....tuijenge nchi yetu hii iwe kama hao waliopigania uhuru walivyopenda iwe. Hii ndio njia pekee nzuri ya kuwaenzi hao mababu zetu na sio kulia lia na UDINI.

Umekisoma hicho kitabu hata ukatoa comments hizo hapo juu? Soma halafu ueleze ni page gani na gani mwandishi amemaanisha udini.
 
Hapana udini.

Kitabu ni kitabu kama vitabu vingine.

Ukisoma utajifunza mengi na hapo kama utaona kuna udini basi utasema utakacho.

Usitishwe na neno "Uislam" kama lilivyokuwa likimtisha Julius Nyerere kiasi cha kuogopa kuwataja Waislam waliokuwa katika harakati za kudai uhuru.
 
MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHIS SYKES (1924 -1968)

Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika na Mohamed Said

Pitio la Kitabu

Kitabu hiki kilipochapwa kwa mara ya kwanza 1998 kwa Kiingereza nchini Uingereza na kilipoanza kuzagaa katika maktaba na maduka ya vitabu mjini London yanayouza vitabu kuhusu Afrika Watanzania wengi waliokuwa Uingereza walisisimuliwa na yale yaliyokuwa ndani ya kitabu hiki. Kubwa zaidi ilikuwa kule kufunuliwa kwa mara ya kwanza kuwa kumbe TANU chimbuko lake si Julius Nyerere bali ni marehemu Abdulwahid Sykes. Hii ilikuwa habari mpya kwa wengi hasa ikizingatiwa kuwa Nyerere mwenyewe hakuwahi kumtaja Abdulwahid Sykes kama mwenzake katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Hili lilikuwa la kwanza. Kitu cha pili kilichosisimua wasomaji ni kuwa mwandishi kwa kutulia kabisa alionyesha bila woga na kutafuna maneno kuwa TANU kilikuwa chama kilichojengwa katika migongo ya Waislam. Hili alilishaijisha kwa kueleza wazalendo waliokuwa bara ambao kwa umoja wao na wengi wao wakiwa Waislam walipambana na ukoloni wa Kiingereza.

Kubwa zaidi la kusisimua ilikuwa kitabu kilieleza bila kupepesa macho au kutafuna maneno njama alizofanya Nyerere kwanza kumfuta Abdulwahid Sykes katika historia yake binafsi, TANU na katika harakati za kudai uhuru. Lakini kilichotibua sege la nyuki ni pale katika kuhitimisha kitabu mwandishi alipoweka wazi mipango ya Nyerere akishirikiana na Kanisa Katoliki baada ya uhuru kupatikana kupanga njama za kuzuia maendeleo ya Waislam. Katika kipande hiki msomaji atakutana na Mufti Sheikh Hassan bin Amir aliyekuwa mufti wa Tanganyika na Zanzibar na mwanasiasa shupavu. Msomaji ataziona juhudi za Sheikh Hassan bin Amir katika kupambana na njama za Nyerere na Kanisa Katoliki na nini kilimfika msomi huyu maarufu wa Kiislam. Kwa wakati ule Nyerere akiwa hai ilihitaji ujasiri mkubwa kwa yeyote yule kusema au kuandika hayo.

Nakala za kitabu zilifika Tanzania na kila aliyesoma alipatwa na mshtuko mkubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na nje yake. Kitabu kiliwaudhi wapenzi wa Nyerere na wapo waliomwendea kwa kutaka afanye jambo kukomesha uongo wa mwandishi. Wengine hawakuamini kuwa huyo anayejiita Mohamed Said kama kweli yupo. Wengine walitaka kujua kama kweli akina Sykes na baba yao ndio waasisi wa vyama vya Waafrika katika Tanganyika katika 1929 hadi 1954 TANU ilipoasisiwa. Hii ilikuwa bahari kubwa kwa wapenzi wa Nyerere ambao wasingeweza kuogelea bila ya msaada wake Baba wa Taifa. Mawimbi ya bahari hii yalikuwa marefu na yakija kwa kasi. Juu ya haya yote Waswahili wana msemo penye ukweli uongo hujitenga. Nyerere asingeweza kuthubutu kukana mchango wa marehemu Abdulwahid kwake yeye binafsi na kwa TANU. Abdulwahid ndiye aliyempokoea Dar es Salaam ile ya miaka ya 1950 na akamjulisha kwa wenyeji wa mji. Wapenzi wa Nyerere hadi leo ukiwauliza Nyerere alisema nini kuhusu ukweli kuwa si yeye aliyeasisi TANU wamekuwa kimya.

Msomi maarufu wa Chuo Kikuu cha Cambridge John Illife ambae ameandika sana historia ya Tanganyika alikasirishwa na msimamo wa mwandishi khasa pale aliposema kuwa inastaajabisha kuwa Illife ingawa alitegemea nyaraka za akina Sykes katika kuandika historia ya African Association inastaajabisha hakuona umuhimu wa kutaka kumhoji marehemu Abduwahid aliyekuwa katibu na rais wake kati ya 1951 hadi 1953. Akiandika pitio la kitabu hiki katika Cambridge Journal of African History Illife alimshambulia mwandishi katika njia ambayo haikuwa staili yake msomi mkubwa kama yeye. Illife alikuwa ameghadhibishwa kwa kuambiwa katika kitabu kuwa alimzuia mwanafunzi wake katika Idara ya Historia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka wa 1969, Daisy Sykes ambae alikuwa binti ya Abdulwahid asiandike maisha ya baba yake. Daisy wakati huo msichana mdogo alikuwa amekasirishwa na jinsi TANU na magazeti yake yote, The Nationalist chini ya uhariri wa Benjamin Mkapa na Uhuru yalivyoshindwa kumwandika baba yake kwa hadhi aliyostahili. Magazeti hayo yaliripoti kifo cha Abdulwahid Sykes kwa kuwa Nyerere alikwenda mazikoni. Hapakuwa na jingine. Brendon Grimshaw ambae alikuwa Mhariri Mkuu wa The Tanganyika Standard na akimfahamu vyema Abdulwahid ndiye aliyendika tanzia ya maana katika Sunday News akasema kuwa Nyerere asingelifika pale alipofika kama si kwa msaada wa Abdulwahid Sykes na ni juhudi za ukoo wa Kleist ndiyo uliowezesha watu wa Tanganuyika kuwa na chama cha siasa. The Standard na Sunday News wakati ule lilikuwa gazeti huru halikuwa na hofu ya Nyerere. Hii ilikuwa mwaka 1968.

Kilipotoka kitabu hiki mwaka 1998 walikuwepo watu walioona ukweli wa kuwa historia ya TANU bado haijaandikwa na kuna baadhi ya shutuma zilizoelekezwa kwake Nyerere ni muhimu yeye mwenyewe akazijibu akiwa hai kwa faida ya jamii isijesemwa kuwa kasingiziwa, walimsubiri afe ndipo wamzushie la kumzushia. Mmoja wi wa kundi hili la pili alikuwa marehemu Prof. Haroub Othman. Yeye alimkabili Nyerere uso kwa macho na kumuomba atoe majibu kujibu shutuma za waandishi wawili. Kwanza ajibu shutuma za Sheikh Ali Muhsin Barwani aliiyekuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (Hizbu) katika kitabu chake Conflict and Harmony in Zanzibar na kitabu cha Mohamed Said The Life and Times of Abdulwahid Sykes (19241968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika. Sheikh Ali Muhsin akimtuhumu Nyerere kwa kupeleka mamluki Zanzibar kuipindua serikali ya wananchi na Mohamed Said akimtuhumu kwa chuki dhidi ya Waislam na kupotosha historia ya uhuru wa Tangnayika. Prof. Haroub alimshauri Nyerere kuwa njia nzuri ya kuiweka historia yake na uhusiano wake na Waislam sawa ni kwa yeye kuandika historia ya maisha yake. Hadi Nyerere anaingia kaburini hiili halikufanyika.

Kitabu hiki ni muhimu kwa Waislam na wananchi wote kwa ujumla kukisoma na kuwahimiza watoto wao nao wakisome wapate kujifahamu na kufahamu changamoto za udini na chanzo chake. Ndani ya kitabu hiki mwandishi amejitahidi kukusanya mashujaa waliotupwa waliopigania uhuru wa Tanganyika hata kabla hawajasikia jina la Nyerere wala kuona sura yake, wazalendo kama Hassan Suleiman na Juma Ponda wa Dodoma. Wazalendo waliohutubia mikutano ya hadhara na kuhamasisha watu kudai uhuru hata Nyerere hawamjui kama Titi Mohamed na wengine wengi kutoka katika majimbo ya Tanganyika. Ukikianza kitabu hiki huwezi kukiweka chini hadi umefika mwisho.

Kitabu hiki kinapatikana Ibn Hazim Bookshop Mtoro na Manyema na Tanzania Publishing House, Samora Avenue.
we as a tanganyikan we've so manythings to do, and not to deal with this type of blah blah in the image of history, what if yes Mr ABDULWAHIS SYKES was the one of TANU's founder to the todays tanganyikan pipo?

Have we try to think before, what is the most benefts of ABDULWAHIS SYKES to the pipo of tanganyika with the life thy live now?
 
Nimekazana na historia ya Waislam na harakati za kudai uhuru kwa kuwa walioandika historia waliwapuuza wazee wetu. Kama nisingeandika kitabu hiki historia ya kweli ya kudai uhuru ingepotea.

Mimi najiuliza siku zote hivi kwa nini Wakristo wanaumwa sana na historia hii kuanzia Julius Nyerere hadi Wakristo wa kawaida?

Katika kumbukumbu ya Vita Vya Maji Maji majina yote ya Waislam walionyongwa na Wajerumani yamefutwa. Ali Songea Mbano haitwi kwa majina yake yote anaitwa "Songea Mbano."

Hebu soma kisa hiki hapa chini:

Nje kidogo ya mji wa Songea kuna kitongoji kinaitwa Mahenge, hapo kuna sehemu ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji. Jambo kubwa la mahala hapo ni kaburi kubwa la halaiki ambamo askari zaidi ya sitini na… (sitini na saba) walizikwa kwa pamoja. Na kando ya kaburi hilo la pamoja kuna kaburi la Ally Songea Mbano ambae yeye alizikwa peke yake.

Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam. Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho. Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.

Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

Nilimuuliza muhudu kulikoni? Akasema, "Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi. Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka. Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatizwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Ally Songea Mbano. Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa peke yake.

Ukiingia ndani ya kinyumba cha ghorofa, unaanza kuona picha za mashujaa wa Maji Maji wakiwa wamevaa mavazi ya vita mithili ya mahujaji wanavyovaa Ihraam wakati wa hija. Kinachoongezeka kwao ni vilemba kichwani. Chini ya kila picha kuna jina la aliyekuwa kwenye picha ile. Ukipanda gorofani utaona silaha za kiajadi kama mikuki, pinde, ngao n.k. Kinachosisimua zaidi ni mavazi ya vita. Mavazi ya vita ya askari wa Maji Maji wengi walivaa kanzu za Kiislaam na vilemba. Jambo jingine linalosisimua ni kile ambacho watu wa kituo hicho wameandika "rosary" hili ni jina la Kikristo, hasa la Kikatoliki, ni zile shanga ambazo huning'inia msalaba lakini unapotazama hicho kilichoitwa "rosary" utaona si "rosary," bali ni tasbihi hasa ya Kiislaam yenye kupangika hasa shanga zake, 33, 33, 34. Maneno yaliyoandikwa kuelezea "rosary" hizo ambazo ni tasbihi ni:

"Hizi ni rosary ambazo wapiganaji wa majimaji walikuwa wakitumia KUTAMBIKA kabla ya kwenda vitani kwa kuamini kwamba zitawakinga na risasi."

Ukweli ni kwamba hawa askari wa Maji Maji wengi walikuwa ni Waislaam hivyo hawakuwa WAKITAMBIKA bali walikuwa wakitumia tasbihi hizo kufanya dhikri kwa Allah kabla ya kwenda vitani. Midhali sisi Waislaam hatujawa tayari kuandika historia yetu kama Waislaam wanaotuandikia watapotosha na kupindisha na kutuzulia wanavyotaka. Hapo gorofani kuna jambo jingine la kusisimua. Kuna magudulia na makopo. Wameandika kuwa, haya ndio makopo ambayo askari wa Maji Maji walikuwa wakiyatumia KUNAWA kabla ya kwenda vitani [kushika udhu na sio kunawa] pia kwa kuamini kuwa maji hayo yatawakinga. Muhudumu alitueleza kuwa kumbukumbu nzuri na za kuaminika ziko Jimbo Kuu la Wakatoliki Peramiho.

Tulikwenda jimboni lakini hatufanikiwa kwa sababu za ki-urasimu tu.T ulitakiwa tupate kibali cha Askofu Mkuu. Hatukukipata. Kwa yale tuliyoyaona na kuyashudia yafuatayo:

i. Vita vya Maji Maji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao. La. Vilikuwa ni vita vya Waislaam wakipigana na Wakristo wa Kijerumani waliovamia maeneo asilia ya Waislaam kwa lengo la kuuwa Uislam na kusimamisha Kanisa kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya Maji Maji ni mazingira ya Kiislaam, kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa Kijerumani ila katika miji ya Waislaam kama Kilwa, Bagamoyo n.k. Kwa nini wauliwe maeneo ya Waislaam tu? Walifuata nini huko?

ii. Kuna upotoshaji mkubwa sana wa historia ya vita vya Maji Maji. Vinaoneshwa kama ni vita vya wazalendo wakipigana na wakoloni wa Kijerumani, wakati ukweli si hivyo. Ukweli ni kwamba vita vya Maji Maji vilikuwa ni vita baina ya Waislaam na Wakrito wa Kijerumani, Waafrika Wakristo wa Songea walijiunga na Wakristo wenzao wa Kijerumani dhidi ya Waafrika wenzao wa Kiislam.

iii. Wakristo wameitafiti hakika hii na wakaijua kisha wameificha kwa maslahi yao.

MWISHO

Kuna haja ya wasomi wetu wa Kiislaam kufanya juhudi za makusudi za utafiti wa historia yetu ili kukifanya kizazi hiki cha Kiislaam kujitambua zaidi na kujenga ujasiri. Taasisi za Kiislaam na watu binafsi [matajiri] wawawezeshe kiuchumi wasomi hawa kufanya kazi hii.

Mwaka 2008 nimetembelea Kilwa Kisiwani, huko nikamkuta Mzungu wa Kifaransa akiandika historia ya Kilwa Kisiwani akiitwa Thiery, ameweka kambi na majenereta ya umeme, solar power na makompyuta. Kazi nyingine kubwa alokuwa akifanya ni kukarabati yale magofu ambayo mengi ni misikiti na majumba ya mawe ya wafalme wa kale. Kilwa Kisiwani ni moja kati ya dola kubwa za Kiislaam katika mwambao wa Afrika Mashariki, ndio dola ya mwanzo kuwa na sarafu yake ambayo iliandikwa jina la Allah.

Tuliposoma kazi ile ya yule Thiery Mfaransa tayari alikwisha ipotosha kwa kiasi kikubwa. Sikuwa na la kumfanya. Kizazi cha vijana wa Kiislaam hakitopata historia ya kweli ya Kiislaam kama tutawaacha akina Thiery waandike na hivyo vijana wetu hawatajitambua na hawatokuwa na ujasiri katika Uislam wao."

Ni mambo kama haya ya udanganyifu na hila ya kubadilisha historia ndiyo yanawasukuma wasomi wa Kiislam leo kuangalia nyuma na kurekebisha pale palipopotoshwa.
 
Kitabu kinauzwa Tanzania Publishing House bei yake 13,000.00.

Tujadiliane kwa heshima tu hapana haja ya kuhamakiana.

Kauli njema ni tunu na humfanya mtu akapendeka.
 
Ishu siyo historia tu kuna kitu ambacho waliokitunga wanakitaka. Badala ya kuzunguka na kupotezeana muda wangesema wanataka nini,

Ili kuthibitisha hoja yake mwandishi katika kitabu chake anawataja waislam tu na kuwaacha wale wasiowaislam ingawa mchango wao wa siasa ulikuwa mkubwa.

Mfano mmoja mndogo ni pale anapomtaja Ali Ponda wa pale Dodoma na kumuacha Edward Mwangosi ambaye alitoa mchango mkubwa sana toka enzi za TAA mpaka TANU!!
 
Nimekazana na historia ya Waislam na harakati za kudai uhuru kwa kuwa walioandika historia waliwapuuza wazee wetu. Kama nisingeandika kitabu hiki historia ya kweli ya kudai uhuru ingepotea.

Mimi najiuliza siku zote hivi kwa nini Wakristo wanaumwa sana na historia hii kuanzia Julius Nyerere hadi Wakristo wa kawaida?

Katika kumbukumbu ya Vita Vya Maji Maji majina yote ya Waislam walionyongwa na Wajerumani yamefutwa. Ali Songea Mbano haitwi kwa majina yake yote anaitwa "Songea Mbano."

Hebu soma kisa hiki hapa chini:

"Nje kidogo ya mji wa Songea kuna kitongoji kinaitwa Mahenge, hapo kuna sehemu ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji. Jambo kubwa la mahala hapo ni kaburi kubwa la halaiki ambamo askari zaidi ya sitini na… (sitini na saba) walizikwa kwa pamoja. Na kando ya kaburi hilo la pamoja kuna kaburi la Ally Songea Mbano ambae yeye alizikwa peke yake.

Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam. Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho. Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.

Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

Nilimuuliza muhudu kulikoni? Akasema, “Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi. Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka. Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Ally Songea Mbano. Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa peke yake.

Ukiingia ndani ya kinyumba cha ghorofa, unaanza kuona picha za mashujaa wa Maji Maji wakiwa wamevaa mavazi ya vita mithili ya mahujaji wanavyovaa Ihraam wakati wa hija. Kinachoongezeka kwao ni vilemba kichwani. Chini ya kila picha kuna jina la aliyekuwa kwenye picha ile. Ukipanda gorofani utaona silaha za kiajadi kama mikuki, pinde, ngao n.k. Kinachosisimua zaidi ni mavazi ya vita. Mavazi ya vita ya askari wa Maji Maji wengi walivaa kanzu za Kiislaam na vilemba. Jambo jingine linalosisimua ni kile ambacho watu wa kituo hicho wameandika ”rosary” hili ni jina la Kikristo, hasa la Kikatoliki, ni zile shanga ambazo huning’inia msalaba lakini unapotazama hicho kilichoitwa “rosary” utaona si “rosary,” bali ni tasbihi hasa ya Kiislaam yenye kupangika hasa shanga zake, 33, 33, 34. Maneno yaliyoandikwa kuelezea “rosary” hizo ambazo ni tasbihi ni:

“Hizi ni rosary ambazo wapiganaji wa majimaji walikuwa wakitumia KUTAMBIKA kabla ya kwenda vitani kwa kuamini kwamba zitawakinga na risasi.”

Ukweli ni kwamba hawa askari wa Maji Maji wengi walikuwa ni Waislaam hivyo hawakuwa WAKITAMBIKA bali walikuwa wakitumia tasbihi hizo kufanya dhikri kwa Allah kabla ya kwenda vitani. Midhali sisi Waislaam hatujawa tayari kuandika historia yetu kama Waislaam wanaotuandikia watapotosha na kupindisha na kutuzulia wanavyotaka. Hapo gorofani kuna jambo jingine la kusisimua. Kuna magudulia na makopo. Wameandika kuwa, haya ndio makopo ambayo askari wa Maji Maji walikuwa wakiyatumia KUNAWA kabla ya kwenda vitani [kushika udhu na sio kunawa] pia kwa kuamini kuwa maji hayo yatawakinga. Muhudumu alitueleza kuwa kumbukumbu nzuri na za kuaminika ziko Jimbo Kuu la Wakatoliki Peramiho.

Tulikwenda jimboni lakini hatufanikiwa kwa sababu za ki-urasimu tu.T ulitakiwa tupate kibali cha Askofu Mkuu. Hatukukipata. Kwa yale tuliyoyaona na kuyashudia yafuatayo:

i. Vita vya Maji Maji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao. La. Vilikuwa ni vita vya Waislaam wakipigana na Wakristo wa Kijerumani waliovamia maeneo asilia ya Waislaam kwa lengo la kuuwa Uislam na kusimamisha Kanisa kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya Maji Maji ni mazingira ya Kiislaam, kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa Kijerumani ila katika miji ya Waislaam kama Kilwa, Bagamoyo n.k. Kwa nini wauliwe maeneo ya Waislaam tu? Walifuata nini huko?

ii. Kuna upotoshaji mkubwa sana wa historia ya vita vya Maji Maji. Vinaoneshwa kama ni vita vya wazalendo wakipigana na wakoloni wa Kijerumani, wakati ukweli si hivyo. Ukweli ni kwamba vita vya Maji Maji vilikuwa ni vita baina ya Waislaam na Wakrito wa Kijerumani, Waafrika Wakristo wa Songea walijiunga na Wakristo wenzao wa Kijerumani dhidi ya Waafrika wenzao wa Kiislam.

iii. Wakristo wameitafiti hakika hii na wakaijua kisha wameificha kwa maslahi yao.

MWISHO

Kuna haja ya wasomi wetu wa Kiislaam kufanya juhudi za makusudi za utafiti wa historia yetu ili kukifanya kizazi hiki cha Kiislaam kujitambua zaidi na kujenga ujasiri. Taasisi za Kiislaam na watu binafsi [matajiri] wawawezeshe kiuchumi wasomi hawa kufanya kazi hii.

Mwaka 2008 nimetembelea Kilwa Kisiwani, huko nikamkuta Mzungu wa Kifaransa akiandika historia ya Kilwa Kisiwani akiitwa Thiery, ameweka kambi na majenereta ya umeme, solar power na makompyuta. Kazi nyingine kubwa alokuwa akifanya ni kukarabati yale magofu ambayo mengi ni misikiti na majumba ya mawe ya wafalme wa kale. Kilwa Kisiwani ni moja kati ya dola kubwa za Kiislaam katika mwambao wa Afrika Mashariki, ndio dola ya mwanzo kuwa na sarafu yake ambayo iliandikwa jina la Allah.

Tuliposoma kazi ile ya yule Thiery Mfaransa tayari alikwisha ipotosha kwa kiasi kikubwa. Sikuwa na la kumfanya. Kizazi cha vijana wa Kiislaam hakitopata historia ya kweli ya Kiislaam kama tutawaacha akina Thiery waandike na hivyo vijana wetu hawatajitambua na hawatokuwa na ujasiri katika Uislam wao."

Ni mambo kama haya ya udanganyifu na hila ya kubadilisha historia ndiyo yanawasukuma wasomi wa Kiislam leo kuangalia nyuma na kurekebisha pale palipopotoshwa.

yaani niliposoma toka mwanzo nilisoma with an open mind kuwa nia yako ilikuwa ni kuenzi wale wote ambao hawakutajwa kwenye historia coz it is true historia ya nchi haiwezi kumzunguka mtu mmoja ni lazima alikuwa na wasaidizi. Ila niliposoma hii post yako ya mwisho imenipa alama ya kuuliza kidogo kuhusu nia ya maelezo yako.

Mimi naomba utumie uhuru wako wa kujielezea utuandikie hasa nia yako ni plain Black and white yaani usizunguke coz watanzania sasa tuna matatizo mengi sidhani kama ni haki kutuongezea vitu vya kufikiri.

Samahani kama nimekukwaza ila hayo ndio maoni yangu
 
Mawazo yangu yamo katika kitabu hiki nilichoandika sasa takriban miaka 13.

Wengi wamenisoma na wamenielewa. Walioukuwa wanataka kujua zaidi wamenialika katika vyuo vyao na wamenisikiliza.

Ukipenda soma kitabu na kama wengine bila shaka utanielewa.
 
Historia ni elimu, haiwezi kuhifadhiwa kama Hadithi au Mchezo wa kuigiza, maana inachukua mtiririko wa mambo muhimu kwa kipindi kirefu cha matukio yaliyoperekea historia husika. Tofauti na onyesho au filamu ambayo uchukua muda mfupi hivyo utunzwa kama ilvyotolewa na waigizaji; nadhani pia elimu yako ina matatizo, kuwa ukiandika historia uandike hadi nani alikuwa anamkaribisha nyerere jukwaani? kuwa kitabu hicho pia kiandike hadi kibwagizo alichokuwa anatumia kabla ya kumkaribisha mtoa mada, huu ni wuhu.

Historia ya TANU ipo wazi kuwa kuwa ilitokana na TAA na Mwalimu alijiunga na kusaidia kukisajiri na kutengeneza katiba, historia huchua mambo muhimu pekee. Hata Qur'an haikuandikwa hivyo unavyotaka haitwambii nini kilikuwepo kabla ya Mt. SAW.Muhamad wataalam wa Dini ya Ki-kisto pia wanatwambia Biblia haina mambo yote tokea kuzaliwa kwa Yesu hadi kufa kwake, walichukua mambo muhimu tu! Hata wewe tukikwambia uweke CV yako hapa tokea kuzaliwa kwako hivyo ndivyo itakavyo kuwa; akitokea mtu akasema wewe ni muongo eti kwavile hujaandika Darasa la kwanza kuna siku mwalimu alikwambia usome ukashindwa! au kunasiku ulichapwa viboko kwa kuchelewa darasa eti hiyo pia ingelikuwa kwenye CV yako mimi nasema huo ni WUHU hujaongea kama Msomi, umejaa malalamishi bila kujua unachoonge.

Kumbuka kuwa kuna vyama vingi vilidai uhuru wa Tangayika siyo TANU peke yake, Uchagani kulikuwa na Vuguvugu tena walifika hadi umoja wa Mataifa. Kanda ya Ziwa (Nyanza) pia kulikuwa na wakina Boke Munka, TANU ndio iliyoshinda chini ya Uongozi wa Nyerere na kuunda serikali, baadaye Mwalimu alijitoa Serikali ilikuimarisha chama zaidi, na baadae baada ya Uhuru kufuta vyama vingi, hata hivyo vyama vingine kama vingejipanga vikashinda labda leo tusinge ongelea TANU na watu wake!! Lakini msomi yeyote hawezi kupuuza hivyo vyama ngawa wapo nje ya Historia ya mapambano. Kwa utashi wa kuhifadhi historia kipuuzi kama unavyotaka una-maana pia Viongozi wa hivyo vyama walalamike kuwa mbona historia haionyeshi majina yao.

Ajabu sana Kweli Mtaji wa CCM ni Idadi kubwa ya Wajinga waliopo katika nchni yetu ya Tanzania.

Pole sana, ongelea mambo muhimu siyo fikra za kugawa watu na kuturudisha nyuma, mwambie aliyekutuma siyo Nyerere aliyemfanya awe hivyo
 
historia ni elimu, haiwezi kuhifadhiwa kama hadithi au mchezo wa kuigiza, maana inachukua mtiririko wa mambo muhimu kwa kipindi kirefu cha matukio yaliyoperekea historia husika. Tofauti na onyesho au filamu ambayo uchukua muda mfupi hivyo utunzwa kama ilvyotolewa na waigizaji; nadhani pia elimu yako ina matatizo, kuwa ukiandika historia uandike hadi nani alikuwa anamkaribisha nyerere jukwaani? Kuwa kitabu hicho pia kiandike hadi kibwagizo alichokuwa anatumia kabla ya kumkaribisha mtoa mada, huu ni wuhu.

Historia ya tanu ipo wazi kuwa kuwa ilitokana na taa na mwalimu alijiunga na kusaidia kukisajiri na kutengeneza katiba, historia huchua mambo muhimu pekee. Hata qur'an haikuandikwa hivyo unavyotaka haitwambii nini kilikuwepo kabla ya mt. Saw.muhamad wataalam wa dini ya ki-kisto pia wanatwambia biblia haina mambo yote tokea kuzaliwa kwa yesu hadi kufa kwake, walichukua mambo muhimu tu! Hata wewe tukikwambia uweke cv yako hapa tokea kuzaliwa kwako hivyo ndivyo itakavyo kuwa; akitokea mtu akasema wewe ni muongo eti kwavile hujaandika darasa la kwanza kuna siku mwalimu alikwambia usome ukashindwa! Au kunasiku ulichapwa viboko kwa kuchelewa darasa eti hiyo pia ingelikuwa kwenye cv yako mimi nasema huo ni wuhu hujaongea kama msomi, umejaa malalamishi bila kujua unachoonge.

Kumbuka kuwa kuna vyama vingi vilidai uhuru wa tangayika siyo tanu peke yake, uchagani kulikuwa na vuguvugu tena walifika hadi umoja wa mataifa. Kanda ya ziwa (nyanza) pia kulikuwa na wakina boke munka, tanu ndio iliyoshinda chini ya uongozi wa nyerere na kuunda serikali, baadaye mwalimu alijitoa serikali ilikuimarisha chama zaidi, na baadae baada ya uhuru kufuta vyama vingi, hata hivyo vyama vingine kama vingejipanga vikashinda labda leo tusinge ongelea tanu na watu wake!! Lakini msomi yeyote hawezi kupuuza hivyo vyama ngawa wapo nje ya historia ya mapambano. Kwa utashi wa kuhifadhi historia kipuuzi kama unavyotaka una-maana pia viongozi wa hivyo vyama walalamike kuwa mbona historia haionyeshi majina yao.

Ajabu sana kweli mtaji wa ccm ni idadi kubwa ya wajinga waliopo katika nchni yetu ya tanzania.

Pole sana, ongelea mambo muhimu siyo fikra za kugawa watu na kuturudisha nyuma, mwambie aliyekutuma siyo nyerere aliyemfanya awe hivyo
ndugu yangu arafat mbona unaongea kwa jazba sana? Tatizo kubwa una chuki dhidi ya uislam ndio maana unaona kama kero waislam kutajwa kwenye historia. Lakini sio kosa lako ni mfumo kristo uliojikita tanzania, lakini yana mwisho.
 
Hunashindwa nini kutete hoja yako au unategemea nguvu siyo akili, hata mimi ni Muislam lakini sikubaliani na Upuuzi kama huo, soma hizo hoja upambane nazo husiniongelee mimi?
 
Mimi najiuliza siku zote hivi kwa nini Wakristo wanaumwa sana na historia hii kuanzia Julius Nyerere hadi Wakristo wa kawaida?
Tafiti ipi umefanya kujua kuwa Wakristo wanaumwa sana? Au ni fikra zako tu?

Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam.
Ok, hapa unasema robo tatu ya walionyongwa walikuwa waislaam.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam.
Hapa unasema wote walionyongwa walikuwa waislaam. Hapo juu umesema robo tatu, labda sijaelewa, naomba unieleweshe..

Nilimuuliza muhudu kulikoni? Akasema, "Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi. Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka.
Huyo Mjerumani ni mwizi. Kaiba kumbukumbu ya nchi yetu. M.S ana jina lake tumripoti ubalozi wa Ujerumani? Na kwa sababu kaowa binti wa M.S itakuwa rahisi kumpata kupitia huyo binti yake..

Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatizwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Ally Songea Mbano.
Hapa tena unasema wote na siri robo tatu ndiyo walionyongwa.

i. Vita vya Maji Maji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao. La. Vilikuwa ni vita vya Waislaam wakipigana na Wakristo wa Kijerumani waliovamia maeneo asilia ya Waislaam kwa lengo la kuuwa Uislam na kusimamisha Kanisa kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya Maji Maji ni mazingira ya Kiislaam, kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa Kijerumani ila katika miji ya Waislaam kama Kilwa, Bagamoyo n.k. Kwa nini wauliwe maeneo ya Waislaam tu? Walifuata nini huko?
-Ok, ngoja nikubali kuwa walikuwa wanapigania Uislam kwanza na si ardhi yao.
-Then, mkristo mjerumani awaue hawa waislaam na afiche katika kumbukumbu na aonyeshe kuwa ameua wakristo wenzake na si waislaam.. Kwa mtazamo wangu this is illogical.
Wewe uue mkristo afu ufiche kwa kubadilisha majina ya wakristo ulioua, uandike ya kiislaam. Uonekane katika kumbukumbu zako umeua waislaam wenzako.

ii. Kuna upotoshaji mkubwa sana wa historia ya vita vya Maji Maji.
Kweli, nauona huo upotoshaji #sarcasm

iii. Wakristo wameitafiti hakika hii na wakaijua kisha wameificha kwa maslahi yao.
Wakristo wapi? Una majina ya hao Wakristo walioficha hii historia?

MWISHO
Kuna haja ya wasomi wetu wa Kiislaam kufanya juhudi za makusudi za utafiti wa historia yetu ili kukifanya kizazi hiki cha Kiislaam kujitambua zaidi na kujenga ujasiri. Taasisi za Kiislaam na watu binafsi [matajiri] wawawezeshe kiuchumi wasomi hawa kufanya kazi hii.
Mimi, naomba wasomi wote wa dini zote wafanye tafiti kwa maswali kama "where did we come from?". Na Je kweli Mungu yupo? Kuna ushaidi? Vitabu kama biblia na kuran si ushaidi. Vimeandikwa na watu kama sisi tu. Au ni ukoloni tu bado tumeuvaa..
Btw I'm an 80's kid.

These stories are good for the ear, but do not provide solutions to the problems I face daily.
 
Kama vinauzwa Tanzania Publishing House (TPH) naweza kununua kule kwenu tatizo wakituona tu wanatushuku sio wenzao ndio maana hata kwenda mtu unashindwa!
Nyinyi ndio wenzetu hata Quran inasema: "walio karibu na waislam kwa urafiki ni wale wanaojiita Wakristo". ukiona muislam anamtenga mkristo tena kwenye mambo yenye faida huyo atakua haijui Dini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom