Kisa cha Kweli: Sitasahau nilivyopendwa na mchawi nikaishia kurogwa

Inaendelea! Sehemu ya 2

Niliendelea na ratiba zingine za shule kama kawaida. Ilipofika mchana saa sita nilirudi nyumbani kupata chakula cha mchana, kisha nikarudi tena shule kwa ajili ya vipindi vya jioni. Wakati wa kutawanyishwa jioni ulipofika nilirudi nyumbani kama kawaida, nilienda moja kwa moja hadi chumbani nikabadilisha nguo kisha nikatoka kwa ajili ya kwenda kucheza mpira. Wakati nikiwa ninatoka nilikutana na mtoto wa mama mdogo ambaye tulikuwa tunaishi nae pale nyumbani akanambia.

"Babu anakuita kule" alisema huku akinionyesha kwenye nyumba ya nyasi ambayo ilikuwa nyuma ya nyumba kubwa. Nilienda moja kwa moja hadi ndani ya nyumba. Nilivyoingia nilikuta ndani kulikuwa na watu watatu. Kulikuwa na Babu, mjomba Elias (yule aliyechanjwa chale usiku uliopita na mzee mmoja aliyekuwa amevaa kibagarashia ambaye sikumtambua. Niliwasalimia, nikamaliza nikauliza " Babu Elikana ameniambia unaniita" Babu aliniambia kaa hapo chini. Nilikaa chini nikatega sikio kuwasikiliza.

Kumbe yule mzee mwenye kibagarashia alikuwa ni mganga wa kienyeji. Baada ya mjomba kuchanjwa chale Babu alimpeleka kwa mganga kuangaliwa kama kutakuwa na shida yoyote. Kule kwa mganga waliaguliwa, halafu yule mganga akawaaambia Babu na mjomba nimeona kuna mtoto hapo kwako wachawi walimfanyia jambo jana. Sasa hilo jambo ambalo mganga aliwaambia nimefanyiwa ndio ilikuwa sababu ya mimi kuitwa pale.Babu aliniangalia machoni halafu kwa sauti ya upole sana akaniuliza

"mwanangu naomba utuambie ukweli jana usiku uliona nini" . Hii haikuwa kawaida ya Babu kumuona akiwa anaongea kwa upole kiasi kile. Licha ya kwamba alikuwa ni mtu mwenye upendo na watoto, wajukuu na ndugu wengine lakini Babu pia alikuwa ni mtata sana. Jambo la kukaripia na kuchapa viboko ilikuwa kama mlevi kugugumia chupa ya konyagi, hakujiuliza mara mbili. Alikuwa ni mkali asiyependa masihara hata kidogo, mpaka alikuwa amebatizwa jina akawa anaitwa "serikali" kwa lafudhi ya kisukuma "serekale". Hivyo aliponiuliza hivyo nilijua hilo ni ombi kwa mara ya kwanza tu, lakini nisipotoa majibu anayoyataka kinachofuata ni mkong'oto. Nilijiandaa kujibu lile swali aliloniuliza lakini moyo uliogopa sana mapigo ya moyo yakawa yanaenda kwa kasi.

Hali hii ilinishangaza kidogo kwani ni mara ya pili sasa kila nikitaka kuongelea hilo jambo, nakuwa naogopa sana. Nilitamani kujibu lakini uoga ulinizidi nikabaki kutoa macho na kujiumauma mdomo.

"Mr the dragon hebu nijibu mwanangu kuna kitu chochote uliona jana" aliuliza tena babu.

Nilitaka kukubali lakini bado nafsi yangu iliogopa na kugoma kabisa, hadi nikaanza kutetemeka kwa hofu. Nilishindwa hata kukubali angalau kwa kutikisa kichwa. Mganga yule alinikodolea macho kama ananichunguza kwa makini, halafu akasema.

"Mzee Manumbu nafikiri wewe mwenyewe umeona, nilikwambia huyu hawezi akasema lolote hata umwekee bunduki, si unaona anavyotetemeka, Kuna kitu amefanyiwa huyu" aliniangalia kidogo kisha akaendelea

"Nafikiri cha msingi tuharakishe twende nae kwangu, tukalifanyie utaratibu hili jambo kabla mambo hayajawa mabaya".

Baada ya pale niliamriwa niondoke pale niende nikamuite mama yangu. Niliondoka nikaenda hadi kwenye nyumba nyingine yenye jiko ambapo pembeni yake kuna mti wa "mhare" na ndio sehemu wanawake walipendelea kukaa. Nilimkuta mama amekaa nikampa maelekezo kwamba anaitwa kisha nikaondoka zangu kwenda kucheza. Kuna muda nilikuwa napata wasiwasi lakini kuna muda pia niliona kawaida tu. Nadhani ni kwa sababu ya akili zile za kitoto. Mpira tulikuwa tunacheza barabarani umbali kama wa mita miamoja na hamsini kutoka nyumbani. Baadae nilikuja kuitwa niende nyumbani mama ananiita.

Nilikimbia kwenda nyumbani kumsikiliza mama. Nilikuwa nimeshapata hisia ananiita juu ya suala hilohilo. Nilipofika swali la kwanza kuulizwa lilikuwa

"eti mwanangu jana usiku kuna kitu uliona" . Nilitaka kujibu lakini nilipatwa na hofu nikaishia tu kujibu "sijaona chochote mama". Mama aliniangalia kwa huruma kisha akasema

"Eti babu yako analazimisha uende kwa mganga ukaangaliwe" sikujibu chochote nilikaa kimya tu. Kiukweli nafsi ilikuwa inaniuma sana kwa kumficha ukweli mama yangu. Lakini ningefanya nini wakati kila nikitaka kuongea moyo unaingiwa baridi kama la Antarctica. Najua mtu mwingine anaweza ajiulize hofu tu ndio ilifanya ushindwe kuongea, mimi mhusika ndio najua jinsi nilivyokuwa najisikia.

"Hebu twende huku" aliniambia mama huku akinivuta kuelekea kwenye nyumba kubwa. Tulienda moja kwa moja hadi ndani ya chumba alichokuwa analala mama yangu. Tulipofika mama akaniambia

"Hata nisipokuwepo, babu yako akikwambia muende kwa mganga ukatae kabisa, jifunze kumtegemea Mungu kwenye maisha yako"

Nilishangazwa kidogo na kauli ile ya mama, maana kwa jinsi babu alivyokuwa mtata sidhani kama ningeweza kumgomea endapo angeamua jambo lake. Nilijua hata mimi hajanichukua kwa lazima kwenda kwa mganga kwa sababu ya babu alimpenda sana mama yangu hivyo hakutaka kulazimisha. Mama yangu alikuwa ni kipenzi cha babu yangu inawezekana kuliko watoto wote wa huyo mzee. Hili jambo hata watoto wengine walikuwa wanalijua. Inawezekana kwa sababu mama yangu alikuwa ni kitindamimba wa mke wake wa kwanza kuoa, ambaye alifariki akamwacha mama yangu bado ananyonya.

Lakini kuhusu suala la kumtegemea Mungu sikushangazwa sana na hilo, pamoja na akili yangu ya kitoto lakini nilitegemea hilo kutoka kwa mama yangu. Kwa sababu mama yangu alikuwa ni mtu wa dini msabato aliyeishika imani haswa. Sio wale wasabato wa kusubili jumamosi ndio wavae suruali nyeusi, shati jeupe na tai nyeusi huku wakikung'uta biblia iliyojaa vumbi ndio waende kanisani. Yeye kusali na kusoma neno ilikuwa ni jadi yake. Baada ya hapo aliniambia nifumbe macho akapiga ombi moja refu la uchungu sana lililoishia na sala ya bwana. Kisha akasema kauli moja tu

"MUNGU ATATENDA"

Itaendelea kesho mida kama hii

NB: huu ulikuwa ni utangulizi tu kesho ndio tutalianza sakata lenyewe. Kuanzia nilivyolazimishwa kuwa kwenye mahusiano na mchawi hadi alivyoniroga.

Usiku mwema.
Hata usiendeleze ..cjasoma kabisa nilishuka mpaka chini kuona itaendelea nikajua walele wale nisome rubbish mtu anawaza Kichwani mwake usjichoshe kuendeleza.woi
 
Hata usiendeleze ..cjasoma kabisa nilishuka mpaka chini kuona itaendelea nikajua walele wale nisome rubbish mtu anawaza Kichwani mwake usjichoshe kuendeleza.woi
Hakuna aliyekuita, anayekuomba wala kukulazimisha kusoma.

Hutaki kusoma unaacha, hakuna anayekuomba kusoma. Na story itaendelea hadi mwisho na hakuna chochote utafanya.

You're not that important.
 
Tunaendelea sehemu ya nne!

Baada ya kugundua nilikuwa nimepakwa dawa, ambazo zilikuwa za unga unga za rangi nyeusi na nyekundu. Wazo la kwanza nilifikiria kuoga kuziondoa zile dawa, Lakini kwa sababu bafu lilikuwa ni la nje niliogopa kutoka nje, ningepata wapi ujasiri kwa mazingaombwe ambayo nimekuwa nikiyashuhudia. Nikapata wazo nijifute tu na kitambaa, nikachukua kitambaa nikakilowesha maji nikaanza kujifuta mle mle chumbani. Baada ya pale nikaona sikuwa na jambo lingine la kufanya zaidi ya kusali kuomba msaada wa Mwenyezi Mungu, yeye ndio kimbilio la wanyonge. Nilipiga magoti nikasali, nikamaliza nikazima kibatari nikarudi kitandani kulala. Usiku ule sikupata usingizi kabisa, ulikuwa ni usiku wenye mchanganyiko wa hisia za hasira, uoga na fadhaa. Wazo ambalo liliisumbua akili yangu niliamini kabisa ile ndoto ina uhusiano na hili tukio. Nilikumbuka kanisani tulifundishwa Mungu wakati mwingine huwapa ujumbe watu wake kupitia ndoto. Ndivyo alivyofanya kwa Yusufu, Daniel na baba wa imani Ibrahim. Niliamini ile ndoto itakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na tukio lile. Nilipata mawazo matatu juu ya nini nifanye

Wazo la kwanza nilifikiri kesho yake asubuhi nirudi nyumbani nikawaambie wazaz wangu juu ya tukio lile lililotokea.

Wazo la pili nilifikiri niongeze bidii ya kusali halafu nisubiri hadi weekend nikirudi nyumbani, niwaambie baba na mama.

Wazo la tatu nilifikiri nimtafute msichana yule niliyemuota amenibeba kwenye baiskeli (tumpe sasa jina la Vumilia). Niliamini huyu kuna kitu atakuwa anakijua.

Nilichakata mawazo yote nikaona niende na wazo la kusubiri hadi weekend ndio niende nyumbani huku nikiongeza maombi. Mama yangu ni msabato kupita maelezo, na nimelelewa katika maadili ya kuishika imani hivyo niliamini Mungu atatenda. Kwa ufupi nitumie hii fursa kuwakumbusha hata wazazi mnaosoma hiki kisa, muwalee watoto wenu katika njia ipasayo nao hawataiacha hata watakapokuwa wazee, Mithali 22:6 . Sio mnafanya umalaya, kuvaa vinguo vifupi na kupost picha mkivuta shisha mbele ya macho ya watoto wenu. Mkijidanganya ndio usomi na usasa, kumbe ni ushamba na kukosa elimu. Siku hiyo pia nilikumbuka fungu la Hesabu 23:23 hapana uchawi juu ya Yakobo wala, wala uganga juu ya Israeli. Niliamini Mungu atatenda!

Anyway sipo hapa kwa ajili ya mahubiri! Tuendelee na kisa chetu!

Wazo la kwanza nililikataa kwa sababu niliona kuharakisha kuwaambia lingewapanikisha wazazi wangu, na sikupenda hali hiyo. Nilimpenda sana mama na baba yangu hivyo nisingependa kuwaona wamefadhaika kwa sababu yangu.

Wazo la kumuuliza Vumilia niliona ni gumu kwa sababu ningemuulizaje mambo mazito kama yale kwa kigezo kipi na uthibitisho gani. Ingekuwa ni sawa nakusema namtuhumu yeye ni mchawi! Nisingeweza kufanya hivyo!

Nilipiga chini hilo wazo!

Asubuhi kulipopambazuka nilioga na kujiandaa kwenda shule kama kawaida. Sikumwambia yeyote juu ya kilichotokea na nilijitahidi sana kuficha zile chale zisije zikagundulika. Tulitoka ndani wote watatu na kuanza kutembea mdogo mdogo kuelekea shule. Tulikuwa tunatembea umbali wa kama nusu saa hadi kufika shule. Tulifika shule na kuendelea na ratiba zingine kama kawaida, japo kimawazo nilikuwa mbali sana. Zaidi zaidi nilikuwa napata hisia za uoga sana. Darasani vumilia alikuwemo nilitamani niamke kwenda kumuuliza, lakini nilikosa courage ya kuamua. Muda sio mrefu iligongwa kengele ya mpumziko mida ya saa nne. Wanafunzi wakatoka nje kupumzika, wenye pesa walienda canteen kunywa chai na maandazi.

Japo baba alikuwa ananipa pesa ya kunywa chai kila siku. Lakini siku hiyo sikuwa na mzuka hata wa kuinywa chai yenyewe. Nilitoka nikajitenga nikaenda kupanda kwenye jiwe moja refu, linalopatikana pale shule nikakaa angalau kupata vitamin D. Wakati nikiwa nimekaa pale ghafla nilimuona Vumilia akija na sahani yenye maandazi kwenye sahani mkono mmoja, mkono mwingine amebeba vikombe viwili vya Chai. Nilitamani nimkwepe lakini nikasema hapana ngoja nione atakuwa na jipya gani, nikajiapiza sitakunywa chai yake. Vumilia kiukweli alikuwa ni msichana aliyekuwa anavutia kwa kiasi chake, si haba. Ni msichana ambaye nisingekuwa kumuogopa bibi yake na undugu wa uongo na kweli uliopo kati yetu basi ningetamani kuwa naye. Alifika pale akaniambia nishuke chini nimpokee, mtoto wa watu sikuwa na hiyana nilishuka na kutii amri bila kuuliza kama niko jeshini. Alinikabidhi kikombe kimoja akaniambia "karibu chai"

"Asante leo sijisikii kula kabisa" nilijibu
"Hujisikii kwani umekula wapi, au unaogopa nitakuwekea dawa unipende"

Nilijichekesha kwa lengo la kupotezea!

Baada ya kukataa hakunibembeleza tena, alianza kunywa chai huku nikimkodolea macho hadi akamaliza. Alipomaliza aliniangalia kwa macho ya huruma kidogo kisha akasema

"Kuna kitu nataka nikwambie"
"Kitu gani" nilijibu haraka kwa pupa
"Mbona una haraka hivyo, uko sawa Kweli"
"Niko sawa we niambie tu"

Alikaa kimya kidogo baadae akaanza kuimba wimbo fulani kwa sauti ya chini, dizaini kama ananichora hivi

Aisee! Alivyoimba palepale kuna kitu nilikumbuka!

Huo wimbo ndio wimbo ambao wale wachawi walikuwa wanauimba siku ile nilipotoka ndani usiku. Kipindi nikiwa darasa la tatu 2005.

Daktari Ben Carson katika kitabu chake cha Think Big aliwahi kusema ubongo wa binadamu una seli zaidi ya bilioni moja. Seli hizi ni nyingi sana kiasi kwamba zinaupa ubongo uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu nyingi kwenye maisha. Kuna jambo linaweza kuwa lilitokea miaka mingi pengine ukiwa bado mtoto ukadhani umeshalisahau, lakini siku ikitokea "stimuli" fulani kuhusiana na lile tukio, utakumbuka kila kitu kama unaangalia runinga. Maneno hayo ya huyo daktari yalithibitika kwangu siku hiyo!

Nilikumbuka haswa ule wimbo niliusikia ukiimbwa siku ile. Kumbukumbu zangu zilinichukua hadi usiku ule nikiwaona wanawake kwa wanaume wakiwa wameshika myoto na wamevaa nguo nyeusi wakiimba na kunengua.Baada ya kumbukumbu hiyo kwa Vumilia Sikutaka kuuliza chochote kwa sababu yeye mwenyewe Vumilia aliwahi kuniambia alikuwepo siku ya tukio. Alivyoona sijaongea chochote aliniuliza

" Jana usiku ulikuwa wapi?"
Nilichanganyikiwa kidogo na lile swali, wakati mwingine nilijiona geneous kwa kudhani toka mwanzo ni lazima kuna kitu Vumilia atakuwa anafahamu.

" Nilikuwa getto tu kwani kuna nini" nilijifanya sielewi
"Sema ukweli mr the dragon jana hujachanjwa chale wewe Kweli?"

Nilishtushwa na taarifa ile ni kama nilikuwa siamini kama Vumilia kweli anajua kuhusiana na tukio lile.

"Hamna" nilikanusha

"Mmmh! Labda lakini kama unanidanganya na tayari umeshachanjwa chale, jua unajidanganya mwenyewe" alikaa kimya kidogo kisha akaendelea

" Ndio unajidanganya mwenyewe! Maana kama umeshachanjwa chale tayari wewe ni nusu mfu nusu hai! Usipoharakisha kutafuta tiba utaitwa marehemu na mimi nipo hapa kwa ajili ya kukusaidia"

"Nimechanjwa" nilikurupuka kujibu pasipo kujiuliza kama ni jambo sahihi au sio sahihi kujibu vile. Uoga ulikuwa umenitawala isivyo kawaida

"Sasa na ulivyokuwa unanificha,ulitegemea nini"

"Naomba unisaidie unajua ni kama nimechanganyikiwa tokea nilivyogundua hilo usiku wa jana nimechanjwa"

Nilivyomwambia hivyo alivuta pumzi ndefu kama mtu aliyekuwa ananionea huruma.

"Kuna kitu nataka nikwambie ila usiogope, unahitaji kuwa jasiri" alikaa kimya kisha akaendelea!

"Kama umeshachanjwa chale mpaka hapo maisha yako, yako mikononi mwa wachawi waliokuchanja, Wewe unaonekana mizimu ya ukoo wa kwenu ina nguvu sana lakini pia umezaliwa na nguvu fulani za asili"

"Kwa nini"

"Unajua wachawi kabla hawajamloga mtu ni lazima waijue kwanza nguvu yake inayomlinda hasa kimizimu. Maana ili mchawi akuloge kwanza kabisa huwa kuna makubaliano baina yake na mizimu yako yaani ya upande wa baba yako pamoja na mama yako, makubaliano yakishindikana haulogeki kamwe, labda atakutesa tu ila hawezi kukuua. Ukionekana mizimu ya kwenu ni mikali na makubalino hayawezi kuwepo ni lazima kuna tambiko lifanyike likihusisha kafara ya kondoo mweusi ili kuua nguvu zako. Sasa kilichofanyika jana wachawi wamekuja kukuchukua usiku wakakupeleka hadi kwenye makaburi ya ukoo wenu upande wa baba yako. Wakafanya tambiko lao, ambalo ndio lilihusisha wewe kuchanjwa chale. Baada ya kumaliza ndio wakakurudisha. Na tambiko hilo likishafanyika unakuwa hauna nguvu tena inayokulinda kimizimu hivyo mchawi kukuloga ni kazi nyepesi zaidi ya kusukuma mlevi. Hivyo nguvu zote zilizokuwa zinakulinda wewe zimeshaondolewa na sio muda mrefu wataanza kukushughulikia na nina uhakika usipofanya jitihada kutatua hiyo shida wiki moja humalizi"

Mpaka hapo nilikuwa nimechanganyikiwa kijasho chembamba kilikuwa kinanitoka. Swali ambalo nilijiuliza ni kwa nini wanataka kuniua, nimewakosea nini na wamejuaje yalipo makaburi ya ukoo wa baba yangu ilhali ni kijiji kingine kabisa japo ni jirani.

"Kwa nini sasa wanataka kuniua nimewakosea nini"

"Hata mimi sijajua bado lakini huwezi amini wanaotaka kukufanyia hivyo ni ndugu zako kabisa"

"Heeeeh! Wakina nani hao?"

"Utawajua tu tena utajionea kwa macho yako mwenyewe"

Nilimuuliza tena

"Wamejuaje yalipo makaburi ya ukoo wetu"

"Wachawi ni shirika kubwa lenye ushirikiano mkubwa, hakuna ukoo usio na wachawi. Na huwa wanasaidiana kutimiza mambo yao" alinijibu

"Sasa naomba unisaidie" niliomba kwa unyenyekevu

"Nitakusaidia ila mpaka ukubali sharti langu"

"Sharti gani"

"Uwe mpenzi wangu kuanzia leo na ukubali kuja kunioa"

Ulikuwa ni uamuzi mgumu kuufanya lakini kwa sababu niliogopa sana. Niliamua kukubali bila kufikiria mara mbili. Niliona ngoja kwanza nipambane na kifo baadae ndio nipambane na mapenzi.

"Asante kwa kukubali, Mr the dragon nimefanya hivi kwa vile nakupenda tu, nakupenda tokea tukiwa wadogo. Na ujue mimi ni miongoni mwa watu wachache ambao wanaweza kukuonyesha njia ya kukusaidia. Nasema hivyo kwa sababu mimi naijua siri iliyoko kwenye mwili wako ambayo bila hiyo siri kuifumbua hakuna mtu anaweza kukusaidia"

"Siri gani"

"Kuhusu hiyo siri nitakwambia muda mwingine, tupambanie maisha yako kwanza, usiku nitakuja kukuchukua twende sehemu ila unahitaji uwe jasiri. Tukishamaliza hili suala sitegemei utaniacha" alisema Vumilia

Baada ya mazungumza hayo tulielekea darasani sikuamini kama nilikuwa katikati ya bonde la kifo na uzima. Ni kama nilikuwa nimechanganyikiwa nikimkumbuka mama yangu, baba yangu, kaka, dada na marafiki zangu halafu lisipofanyika jambo ndani ya wiki moja nitakuwa nimewaacha wote. Sikupata hata mood ya kuendelea kukaa darasani nilichukua begi langu nikatorokea porini na kuanza kutembea mdogo mdogo kuelekea getto. Njiani machozi yalinibubujika mashavuni. Wakati mwingine niliiangalia ardhi na kutabasamu mwenyewe yaani mimi huyu mr the Dragon kijana barobaro wa shule ndani ya wiki hii nitakuwa nimefukiwa na hii ardhi ninayoikanyaga. Ama kweli dunia ni uwanja wa fujo kila mtu atafanya fujo zake na kuondoka!

Lakini pia niliyawaza maneno aliyoniambia Vumilia kwamba kuna ndugu zangu ndio wanataka kuniua, nilijiuliza ndugu gani huyo lakini sikupata jibu. Nilijiapiza sitomsamehe kamwe kama nitapona.

Itaendelea baadae kidogo ngoja nipate lunch!
Yamoto
JamiiForums610052602.gif
 
Inaendelea sehemu ya tano.

Nilitembea moja kwa moja hadi getto, nikafika nikajilaza kichwa kilikuwa kina mawazo mengi sana. Naamini watu wengi ambao nilikutana nao njiani inawezekana walibaini siko sawa. Nilikaa sikuwa hata na nguvu ya kupika, nilikuwa nawaza tu. Baadae washkaji tuliokuwa tunakaa nao getto walirudi kutoka shule ilikuwa mida ya saa tisa hivi. Jamaa walilalamika kwa nini nimewahi kurudi kutoka shule lakini sijapika,nikawaambia naumwa. Jamaa walipika ugali dagaa nikala kidogo kwa kujilazimisha. Baadaye nikaona nimfate Vumilia getto kwake ili twende alikokuwa anasema, niliona siwezi kusubiri wakati niko kwenye mdomo wa Simba.

Uzuri alipokuwa anakaa haikuwa mbali sana, nilitembea kwa dakika kadhaa chache nikawa nimefika. Nilibisha hodi akafungua mlango nikaingia ndani. Nilivyoingia, nikaketi chini kwenye godoro lililopo chumbani kwake, nikawa namtazama. Nilimuona kama mtu aliyekuwa amebaki kama tumaini langu la mwisho. Moja kwa moja, nikamwambia twende ulikokuwa unasema. Alikataa akasema nitakuja kukuchukua mwenyewe usiwe na haraka. Nilimbembeleza lakini alikataa katakata akasema atakuja baadae usiku. Niliamua kurudi getto, nikafika nikalala nikimsubiri aje anichukue. Ilifika hadi usiku saa tatu alikuwa hajaja, nikajikuta nimepitiwa na usingizi. Baadae nilishtuka usingizini, kuna mtu alikuwa kama ananivuta mkono. Niliangalia na kumkuta alikuwa mtu ambaye amevaa nguo nyeusi tii, nilipiga kelele kwa nguvu hadi mshikaji wangu mmoja aliyekuwa amelala akashtuka kutoka usingizini. Mshikaji mwingine alikuwa mezani amewasha kibatari anapiga kitabu naye aliniangalia, akaniuliza.

"Vipi unaota?"

Nilimtazama Yule mtu na kugundua alikuwa ni Vumilia. Usoni alikuwa amepaka dawa nyeupe za unga unga. Alinifanyia ishara ya kuniambia nikae kimya. Kilichonishangaza licha ya kwamba Vumilia alikuwa pembeni kidogo tu ya jamaa anayesoma mezani lakini mshikaji alionyesha haoni chochote. Ilikuwa ni kama mimi tu ndiye niliyekuwa namuona. Alinifanyia ishara nisimame, niliwaza kidogo kuona kama nachokifanya ni sahihi. Ghafla kuna wazo lilikuja kichwani likaniambia hivi kwa nini nimemuamini Vumilia ghafla, je kama ndio yeye anataka kunichukua kunipeleka kwa wachawi wenzie wakanimalize, si ndio naenda kufa kirahisi rahisi tena kwa kujipeleka mwenyewe. Wazo hili lilianza kama utani lakini lilinishawishi, nikajikuta natikisa kichwa kuashiria kwamba nimekataa na sikuwa tayari twende naye. Ni kama vile aliyasoma mawazo yangu.

"Vipi umeogopa, au unadhani nataka nikufanyie kitu kibaya, kumbuka nilikuambia uwe jasiri" aliniuliza kwa sauti kubwa

Nilipigwa butwaa na kumuangalia mshikaji aliyekuwa anasoma, lakini macho alikuwa amekodolea kwenye kitabu, ni wazi hakusikia chochote. Nilishangaa nikajisemea moyoni ama kweli duniani kuna mengi. Nilikaa kimya kwa kuogopa nikijibu jamaa angesikia na kuanza kuwaza tofauti.

"Sikia nikwambie mr the dragon, hata hapa nimefanya ustaarabu tu. Ningeamua ningekuchukua kimya kimya hadi ninakotaka kukupeleka bila wewe kujua. Hujiulizi jana umepelekwa makaburini na kuchanjwa bila kujitambua, sasa nikitaka kukupeleka unadhani nitashindwa. Kama hauamini subiri"

Aliongea vile na kuanza kurudi kinyumenyume hadi kwenye kona moja ya chumba na kupotea. Sijui kilitokea nini lakini nilijikuta nashikwa na usingizi mzito ghafla na nilipokuja kushtuka nilijikuta nilikuwa nje ya ile nyumba, Vumilia akiwa pembeni yangu amenishika mkono.

"Umeamini sasa kwamba naweza kukupeleka popote. Sikiliza Mimi napambania maisha yako kwa hiyo fuata kila nitakachokwambia"

Mpaka hapo sikuwa na ujanja zaidi ya kutii amri, niliamua sasa liwalo na liwe. Vumilia alinitangulia na kuniamuru nimfate kwa nyuma. Alianza kutembea kwa miguu halafu mimi nikawa namfata kwa nyuma. Tulitembea kwa mwendo wa dakika chache tukawa tumeshafika kijijini kwetu. Yalikuwa ni maajabu yaani sehemu ambayo huwa tunatembea sio chini ya masaa mawili na nusu tulitembea kwa dakika zisizozidi kumi na tano.

Tulipofika kwenye kijiji chetu alininong'oneza "tunaenda kwa mzee Nkelebe"

Mzee Nkelebe alikuwa ni mganga maarufu wa kienyeji pale kwenye kijiji chetu.

Tulipiga hatua ndani ya dakika chache tulikuwa tumeshafika.

Itaendelea kesho asubuhi!

Leo nimeandika kwa kifupi kuonyesha bado tuko pamoja maana watu washaanza kupata wasiwasi, kwamba sitamalizia. Jamani niko hapa mwanzo mwisho.

Na kesho ni weekend nina muda mwingi wa kuandika kwa hiyo ni bandika bandua.

Usingizi nipumzike. Good night
 
Hakuna aliyekuita, anayekuomba wala kukulazimisha kusoma.

Hutaki kusoma unaacha, hakuna anayekuomba kusoma. Na story itaendelea hadi mwisho na hakuna chochote utafanya.

You're not that important.
Mtu anayeandika story yake na kushare huwa namkubali sana. Kwasababu
1. Ametumia muda wake kuandika. Watu hufikiri hauna kazi, wewe ni kuandika na kuweka tu na wengine wanalazimisha
2. Unasoma bure
Ndiyo maana nikikuta nasoma, nisipokuta siwezi kulalamika maana kwa jicho la tatu nilitakiwa nikupe hela ndiyo maana watu wanaweka Youtube. Kuna wale hufikiri kama story anatoa Mello, watakulazimisha.
Big up sana
 
Back
Top Bottom