tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,859
- 18,282
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Kijana mmoja kutoka Arusha ajulikanaye kwa jina la Idrisa Baltazari (30) amefanikiwa kumuua mpenzi wa mama yake aitwaye Manzi Yambayamba (34) kwa sababu za wivu wa kimapenzi.
Habari kamili kutoka eneo la tukio zinadai kuwa kijana huyu pia alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mama yake na kwamba yeye ndiye aliyemuanza mama kabla Yambayamba hajaja kuingilia penzi lao. Kijana alipoona mama yake anaegemea zaidi kwa mpenzi wake mpya ndipo akachukua jukumu la kumuua ili asiendelee kuwa kikwazo kwake.
Chanzo: Mwananchi
MAONI YANGU
Kisa hiki kimenikumbusha mama wa msanii maarufu wa bongofleva nchini Tanzania ambaye ameolewa na mwanaume mwenye umri mdogo unaokaribiana na umri wa msanii huyo. Wakati mwingine akina mama wanawaangusha sana watoto wao, kitendo kinachoweza kusababisha wivu wa kimapenzi, hasa pale wanapoona wanakaribiana umri na mwanaume anayetoka na mama yao. Hapo ndipo wivu wa mapenzi huanzia kwani huwezi kujua uhusiano wa ziada uliopo kati ya mama na mwanaye.
Natoa wito kwa wanaume wanaowachukua wanawake wazee kujithathmini kwanza kabla ya kuchukua maamuzi ya kuoana au kudumisha penzi lao kwani suala hili limekuwa chanzo cha mauaji ya kizembe kwa sababu ya wivu wa kimapenzi unaoweza kuzuilika.
Nawasilisha.