Elungata
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 40,204
- 33,229
Leo tunatambiana Mkuu wa Majeshi kaonekana Ngerengere, tunapigana vijembe vya udaku wa afya yake na tetesi za yeye "kutoweka".
Hatulizungumzii hata kidogo tukio lenyewe kubwa pale Ngerengere.
Hatujiulizi Tanzania tumekosa fedha za kujenga na kuboresha kikosi chetu cha anga mpaka tuende Uchina kuomba msaada na kufadhiliwa?
Yaani hatuna dola za kimarekani Milioni mia moja popote? ni heri hata masalia ya Escrow na EPA yangetumika hapo Ngerengere au pale Kigamboni kuliko kuonyesha utegemezi wa hali ya juu kwa China.
Wanatukopesha kujenga Bandari, mitambo ya gesi, reli, barabara, kujenga majengo, matumizi ya serikali, zana za kijeshi na sasa kambi nzima ya jeshi?
Tutalipaje hili deni? Tutalipaje hizi fadhila?
Mlizusha ya CDF Sasa mmeumbuka hamtaki watu wahoji hiyo tabia ya kutunga na kusambaza tuhuma ili kujipatia mtaji wa kisiasa ... Aibu zenu..... Njia ya mwongo ni fupi sana ......
Nashukuru Mkuu kwa kunifumbua macho nikuulize swali lingine.
Je kwa Maliasili tulizonazo ambazo zingine hazipatikani sehemu nyingine Duniani isipokua Nchini kwetu tumeshindwa kua Taifa lisilotegemea Misaada na Mikopo?
Kwa nijuavyo mimi na nilivyojifunza Shuleni ni kua asilimia kubwa ya Mataifa ya Ulaya hasa yaliyokua na Makoloni Bara la Africa yaliendelea kiviwanda kutokana na Malighafi walizochuma toka kwetu.
Sisi tumeshindwa nini japo kua hata na Viwanda vya kati ili tuepu..
hata hivyo naamini miaka 100 toka sasa uwezo huo tutakua nao wa kutumia rasilimali zetu kufikia maendeleo....hata marekani wamechukua miaka 350 kufika hapo walipo
Yaani uwanja wa jeshi mnaipa jeshi la nchi nyingine liwajengeee?
Kiukweli hii nchi Mungu pekee ndio anatushikiria na sio tofauti na hapo
Walisemaje Kuhusu CDF? Nakumbuka yule kijana alidai "CDF Kala chakula chenye sumu na akakimbizwa hospitali kwa matibabu". Tunajuaje kama "kurudi" kwake "hajatokea hospitali matibabuni?". Kwani alisema ameaga dunia? Ikumbukwe kuwa taarifa rasmi ilidai kaenda ziara ya siku 9 Lakini ameonekana baada ya mwezi (almost).
Yaani uwanja wa jeshi mnaipa jeshi la nchi nyingine liwajengeee?
Kiukweli hii nchi Mungu pekee ndio anatushikiria na sio tofauti na hapo
bora uwe ukoroniwe na mmarekani kuliko mchina huyu wa siku hizi.
hadi inzi watachukuliwa
Mbona islaeri wanatengeneza military base za marekani??
marekani amekoloniwa na china kama hujui,,,,china inaidai marekani pesa ndefu sana,,,pia wanahold bond za marekani wakiziachilia uchumi wa marekani utaadhirika vibaya
Rev unafahamu wachina ndio waliwafunza wanajeshi wetu wa anga na zile ndege za mwanzo zilitoka kwao, huo ulikuwa ule mlolongo wa mikataba kama vile ya kiwanda cha Urafiki etc. Wao ndio walijenga Ngerengere kama kambi ya anga. sifahamu details za mikataba yao, pia ukumbuke ndio waliweza kutupa uwezo wa kujenga reli ya uhuru. Huyu Jambazi sugu mwenye kuleta mvua kutoka malasyia sijui atafanya nini zaidi ya wizi wa kukata na shoka.We need to manage our resources and make our choices strategically in order to safe guard the inheritance for our children.
Kuhusu tutalipaje huo ni ujinga wa JK et al, yeye ndiye chimbuko la kuendeleza ule mlolongo wa marais wasioweza kuongoza kama vile Mwinyi. I urge Tanzanians who are educated to go back home and claim their right to see Tanzanians are lead to prosperity, not these thieves from Chadema and Ukawa.
Nashukuru Mkuu kwa kunifumbua macho nikuulize swali lingine.
Je kwa Maliasili tulizonazo ambazo zingine hazipatikani sehemu nyingine Duniani isipokua Nchini kwetu tumeshindwa kua Taifa lisilotegemea Misaada na Mikopo?
Kwa nijuavyo mimi na nilivyojifunza Shuleni ni kua asilimia kubwa ya Mataifa ya Ulaya hasa yaliyokua na Makoloni Bara la Africa yaliendelea kiviwanda kutokana na Malighafi walizochuma toka kwetu.
Sisi tumeshindwa nini japo kua hata na Viwanda vya kati ili tuepuh
hakuna nchi yenye rasilimali duniani kama russia,,lakini kama unakosa capital na technology huwezi utilize rasilimali zakO.
katika link mojawapo hapo juu,umeona uingereza wanajengewa kinu cha nyuklia na mchina,,,,wao waingereza wana technology lakini pesa za kuufanya mradi hawana ndo maana wakampa mchina ajenge...
sasa tuseme uingereza nao hawana rasilimali?,kama uingereza anakosa pesa ya kufund mradi na mpaka anaipa china project,,itakua Tanzania?..
Recolonization