masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,906
- 13,211
Lalamikeni sana wakati mkiendesha magari yenu katika barabara zilizojengwa kwa msaada toka Japan, mnatibiwa katika hospitali za misaada toka Ulaya, mnasomesha watoto wenu katika shule za misaada toka EU!!Leo tunatambiana Mkuu wa Majeshi kaonekana Ngerengere, tunapigana vijembe vya udaku wa afya yake na tetesi za yeye "kutoweka".
Hatulizungumzii hata kidogo tukio lenyewe kubwa pale Ngerengere.
Hatujiulizi Tanzania tumekosa fedha za kujenga na kuboresha kikosi chetu cha anga mpaka tuende Uchina kuomba msaada na kufadhiliwa?
Yaani hatuna dola za kimarekani Milioni mia moja popote? ni heri hata masalia ya Escrow na EPA yangetumika hapo Ngerengere au pale Kigamboni kuliko kuonyesha utegemezi wa hali ya juu kwa China.
Wanatukopesha kujenga Bandari, mitambo ya gesi, reli, barabara, kujenga majengo, matumizi ya serikali, zana za kijeshi na sasa kambi nzima ya jeshi?
Tutalipaje hili deni? Tutalipaje hizi fadhila?
Na bado watu wana ruka ruka na kufurahi kama wenda wazimu kwani wameahidiwa shule bure toka chekechea hadi chuo kikuu!
Boda boda na mama ntilie hawatalipa kodi yoyote hadi kufa!
Na watapanga bidhaa zao hadi milango ya Ikulu!
Wafanyakazi hakuna kulipa kodi !
Hii ndo Tanzania yetu ya wananchi wanaopenda vya bure bila kulipa kodi.