Hiki kipindi hurushwa kila Jumapili kuanzia saa 8 mchana. Nimekuwa nikikisikiliza kwa muda sasa, lakini sijatambua lengo kuu hasa la hiki kipindi ni nini. Maana nionavyo ni kama mtangazaji " anawachora" wale wageni wanaoeleza matatizo mule, na "wageni" wanavyojiachia na matatizo yao utafikiri kuna la maana atakalopata humo zaidi ya kupewa pole na watuma sms/ wasikilizaji.
Wajameni, Watanzania tupunguze malalamiko redioni, huu umaskini tulionao haumalizwi kwa kuhojiwa redioni. Tunapaswa kufanya kazi kwa bidii na pia kuwa na nidhamu na matumizi.
Ni hayo tu kwa leo.
Wajameni, Watanzania tupunguze malalamiko redioni, huu umaskini tulionao haumalizwi kwa kuhojiwa redioni. Tunapaswa kufanya kazi kwa bidii na pia kuwa na nidhamu na matumizi.
Ni hayo tu kwa leo.