Mkasa wa kusisimua wa Rojaz katika kipindi cha Sitasahau cha Radio Free Africa

shikamkono01

JF-Expert Member
Mar 26, 2016
566
1,783
Sehemu ya 1.

Naitwa Rojaz na nimezaliwa kwa wazazi ambao baba na mama matamanio yao ni kuona watoto wao tunasoma kwa bidii ili kuweza kufikia malengo yetu na ndoto ambazo wao kama wazazi wanaziota juu yetu,natumaini ni ndoto ya kila mzazi kwa mtoto wake,hakuna mzazi anayesomesha mtoto na asitamani kuona anapata mafanikio katika masomo yake,kiufupi mimi nilikuwa ni mmoja kati ya watoto 6 katika familia yetu nikiwa ni mtoto wa tatu kuzaliwa.

Na nimejaaliwa kusoma mpaka kidato cha nne na sikufanikiwa kufanya vizuri katika matokeo yangu ya mwisho, ukiniuliza sababu ya matokeo yangu kuwa mabaya kiukweli sikuwa na jibu la moja kwa moja ila kiukweli hakukuwa na ugumu huo ila naweza kusema ni mimi mwenyewe kwa uzembe wangu na uzembe wa wanafunzi baadhi mnapokuwepo shuleni kutotambua nini kilichowaleta pale. Kuna wengine ambao wanatilia mkazo masomo yao matunda yake waliyaona na wale wakina wenzangu mie akili tunaielekeza katika michezo isiyo na tija, naeleza haya usidhani nilidharau elimu kwakuwa labda nilitokea katika familia bora, familia yetu ina uwezo wa kiuchumi la hasha kwani hata elimu yangu tokea kidato cha kwanza ni harambee ndio ilikuwa inatawala katika upatikanaji wa ada yangu, mara kachangia shangazi, mara mamdogo au mwana familia yoyote anayeonekana ana nafuu ya kipato kwa wakati huo. Kiufupi nilikulia katika familia duni.

Tulikuwa tumezaliwa watoto wengi na kila mtoto alikuwa na mahitaji yake kwa wakati husika. Sasa maisha ya mtaani bada ya kumaliza mchakato wa masomo tena ukiwa matokeo ambayo sio rafiki chamoto hujakiona, changamoto nyingi zinakuwa zinajitokeza na hapo unatakiwa kujiongeza ili kuweza kujikimu wewe na wanaokuzunguka ilimradi mkono uende kinywani. Katika kusaka tonge nikaanza kujichanganya kwa kuanza kutembea na mafundi hawa mafundi ujenzi nikiwa kama saidia fundi (kibarua msaidizi) na haikuwa kwa mafundi tu kwani pale mtaani kila aina ya kazi iwe kuchimba shimo,kukusanya mchanga (wakati wa mvua ule mchanga unaoletwa na maji), kubeba tofali, kusaidia mtu anayetaka kuhama na kadhalika mie kwangu ilikuwa twende kazi yaani kwa upande wangu maisha yalikuwa ni magumu sana sana sana na msalie Mtume yangu ni kujipenyeza katika harakati hizi, (nakuhusia ewe kijana ambaye umepata neema ya kupata nafasi ya kusoma chonde chonde usiichezee bahati hiyo uko mbele ni kugumu sana,soma kwa bidii maisha sio marahisi), maisha ya kukaa nyumbani yalikuwa na maneno maneno mengi yenye kuumiza roho, ukishamaliza shule hata andazi upewaji wake hauwezi kuwa kama mwanafunzi kwani ukigewa ujue utasindikizwa na neno la masimango hivyo sikuipenda hali hiyo nikawa najibidiisha katika videiwaka hivyo ili kuweza kupata mahitaji.

Siku zilisogea, maisha nayo yakawa yakienda yakibadilika kwani kama unavyojua siku hazigandi mahitaji yanaongezeka, vitu vinapanda bei na maisha yanavyosogea kwangu ndivyo maisha yakazidi kuwa magumu sana kwani ni jasho lako ndilo litakaloamua mustakbali wako.

Pale nyumbani tulikuwa tunaishi kifamilia na mama yangu yeye alikuwa anajishughulisha kwa kufanya biashara, alikuwa anafanya biashara za sokoni (mchuuzi mdogo mdogo) na baba yangu yeye kwa muda mwingi alikuwa yupo tu nyumbani (misheni town) na sana alikuwa kama dalali kimtindo ingawa haukuwa ule udalali wa moja kwa moja yaani kama kuna chumba yeye anadalalia kupata mpangaji na anapewa kamisheni au mtu ana mali yake anauza au anatafuta kitu yeye anamsaidia kuweza kufanikisha jambo husika.

Kwahiyo egemeo kubwa la familia lilikuwa ni mama,mama yeye alikuwa anaenda sokoni uko akaemee ndio akirejea watu wanapata afadhali, siku zilisogea na kusogea mama yangu pekee aliendelea kuwa mkombozi wangu kwani hata nikiwa nimepungukiwa nauli alikuwa ananipa lakini alikuwa ananambia akinikumbushia kwa kusema "Nilikupa nafasi ya kusoma ukachezea unaona unavyopata tabu? Yaani wewe unaniomba mimi nauli? Utagewa nauli hadi lini?"

Lakini pamoja na maneno yote mama yangu mpenzi alikuwa ananipa mtoto wake
Ikafika wakati mama yangu mpendwa akapata maradhi,akaumwa sana, aliumwa sana yule mama na kama nilivyotangulia kueleza awali mama ndio alikuwa nguvukazi na wakati alipopata maradhi akawa yupo kitandani tu na baba yetu ndio hivi mara apate pesa, mara siku asikutane nayo yaani utokaji wake haukuwa na uhakika wa kurudi na kitu yaani ni bahati nasibu tu, mama alikuwa ana utaratibu wa kudunduliza pesa kama akiba kwa ajili ya maendeleo na kutokana na changamoto iliyojitokeza zikaanza kutumika kwa ajili ya kumuuguza yeye na kutatua changamoto za nyumbani kwani pia nilikua na ndugu zangu ambao walikuwa wanasoma.

Maisha yalikuwa magumu sana huku mimi nikizidi kupambana ili kuweza kujikwamua na umaskini uliokuwa umetuzunguka. Dah! Majira na nyakati
yalikuwa yamefika, mama yangu kipenzi, mama yangu nimpendae, mboni ya jicho langu akaaga dunia!

Tulifanya mazishi kuweza kumpumzisha mama yetu kipenzi katika nyumba yake ya milele, kiukweli huu ulikuwa msiba mzito sana kwetu kwa sababu hakuna asiyejua kuanzia majirani hadi ndugu wa karibu kuhusu nafasi ya mama yetu katika familia, mama alikuwa kinara, alikuwa mpambanaji katika familia yetu kwahiyo kuondoka kwake woga ulituvaa miilini mwetu kwa namna ya kuikabili kesho yetu yaani hasa mimi nikajiuliza tutafanyaje?

Hii kauli hata wadogo zangu waliweza kuitamka na kujiuliza tutaishi na kusoma vipi? Lakini maisha lazima yaendelee na tukakamilisha kipindi cha maombolezi ya mama yetu kipenzi.

Siku zikasonga nikiwa nayakumbuka mengi ambayo mama alikuwa akinishauri alikuwa akiniambia
"Rojaz soma mimi leo nipo kesho sipo, kesho baba yako yupo kesho hayupo mkombozi wako ni elimu, tizama ndugu zako wanasoma, hivi vipesa ninavyokupa visikubweteshe kesho nitakopokuwa sipo utapata tabu mwanangu, dunia hii ni ngumu sana ukiwa hauna cha kufanya dunia ni ngumu sana naomba ulitambue hilo",


Nazikumbuka hizi kauli kwani uwa zinanijia sana,zinanijia pale nina shida, pale napokuwa sina kazi yakuweza kunipatia riziki, unajua sie masaidia fundi ni pale fundi apate kazi ndio akwambie njoo, kama hajapata nawe ujue imekula kwako!

Kaka yangu mkubwa alikuwa ana rafiki yake ambaye ni dereva taksi, nakumbuka nilimfata kaka na kumwambia, "kaka huku kwenye ujenzi ni pagumu sana, kaka kama unaweza hata kuniunganisha kwa rafiki yako niweze kukaa hata kijiweni naweza kupata chochote kitu"

Kaka yangu alicheka na akanambia
"sasa wewe ukakae katika kijiwe wakati gari huijui, yaani hujui chochote kuhusu gari pale sio wanakaa tu, wanakaa watu wenye idea na hivyo vitu yaani ukakae kijiweni na haujui lolote? Au unatakaje? Unatakaje mdogo wangu?"
Nikamwambia, "nataka kujua hiyo gari sasa ndio maana nataka kukaa na wenye magari". Akasema, "Ntaongea naye na atakaporidhia utaambatana nae lakini ngoja nizungumze nae kwanza".

Siku zikapita toka nimueleze kaka kuhusu hili jambo na nilikuwa nikimkumbusha mara kwa mara yeye alikuwa akinijibu kuwa amesahau lakini nashukuru siku moja niliwakuta wote wawili kaka na rafiki yake wakiwa pamoja nikamwambia kaka
"Kaka naomba umwambie hapahapa maana uwa unasahau naomba umwambie sasa hivi", nashukuru Mungu kaka alimwambia huyu rafiki yake ambaye anaitwa John, naye akajibu, "Hakuna shaka kama yeye anapenda hata kama hajui chochote atajua tu, wengi walifika pale hawajui chochote kuhusu gari na sasa wanajua, atakuwa akitazama tunavyofanya na tutamfundisha atajua"

Maisha yakasogea na nilifurahi sana kwa ombi langu hili kukubaliwa, nilianza kwenda pale kijiweni na kwa nyakati hizi biashara ya taksi ilikuwa na mzunguko sana, wateja walikuwa wengi kwani kulikuwa hakuna mambo mengi kama mabodaboda au hizi Uber yaani taksi ndio ulikuwa mpango mzima.

Basi nikafika kijiweni nikakutana na John na alinambia wewe utajumuika nami katika safari iwapo mteja atakuwa ameridhia, utakaa unatazama namna ninavyopiga gia na pia siku za Jumapili John alikuwa hafanyi kazi hivyo alikuwa ananichukua na kwenda katika uwanja wa wazi na kunifundisha gari na kwa sababu mimi nilikuwa na nia na ninapenda kwangu haikuwa ngumu kujua tena kaka John alinipa maneno ya hamasa sana
"Sio ngumu mdogo wangu weka nia tu kuna wenzako wengi wametoka vijijini uko leo wanawaendesha mabosi na maisha yao yanasonga, wanakula vichwa kwahiyo wewe pambana bwana, pambana mdogo wangu".

Kweli nikapambana hadi ikawa tena kwenye vile vibarua vya saidia fundi siendi nikawa napenda gari napenda gari kweli kweli, ikifika asubuhi mie wa kwanza kijiweni utasema kama vile mie ndio nimekabidhiwa taksi kumbe bado deiwaka, namsubiri bro John basi mishemishe zinaendelea.

Taratibu nikawa najenga imani kwa John na John akanambia sasa siku mojamoja nitakuwa nakupa nawe uwe unakula vichwa, yaani siku ambazo anakuwa yuko sehemu ametulia ananiachia chombo nakula vichwa, yaani alikuwa ametokea kunikubali sana nami nikawa napiga mishe kila kaka John anaponikabidhi chombo, sasa nikawa dereva namudu kukiongoza chombo maana kijiweni tena John awepo au asiwepo mi naburuza tu, maisha ya udereva yakaendelea na bro John akawa ananitoa toa mara buku tatu, mbili hadi tano, kwa kipindi iko ilikuwa ni kubwa, elfu tatu kwangu ni kubwa tena ukitilia maanani natokea nyumbani akinipa elfu tatu, akinipa elfu mbili niliona safi sana kwa sababu nikitu nilishaanza kukipenda.

Huyu John kwa muda mchache niliokaa nae nilimsoma nilimgundua ni mtu anayependa sana mabinti (mtu wa totozi) yaani yeye ikifika jioni tu kile kigiza cha kwanza tu anapotea kijiweni anaenda kujificha na binti aliyemteua siku hiyo. John alikuwa mwenyeji sana katika nyumba za wageni na ukitilia maanani alikuwa na wateja sana katika biashara yake ya taksi yaani kwa watu wa taksi saa 1 hadi saa 2 usiku ndio kunakuwa kumekucha lakini yeye hauwezi kumkuta muda huo anakuwa maeneo yake yakujidai kwani muda huo kibunda kishanona hapo ananiambia dogo nishaondoka kwenda kujipumzisha na shemeji yako, kiufupi alikuwa mzee wa bandua bandika.

Kwa hiyo muda mwingi alikuwa ananiachia funguo sababu alikuwa ameshaniamini kama deiwaka wake nami nikawa napiga kazi hadi mida flani nampigia bro nshamaliza naye ananielekeza alipo namkabidhi chombo narudi nyumbani
Siku moja John akanambia "mdogo wangu sasa wewe umeiva, umekwisha iva inabidi tufanye mpango upate leseni usije kukutwa barabarani huna chochote hii ni hatari kwakuwa ushakuwa uko vizuri katika uendeshaji, lakini pia uweze kujua sheria za barabarani"

Kwahiyo nikafanyiwa mpango wa kupata leseni na John akanitimizia nikapata leseni sasa nikawa kamili gado kama wasemavyo watoto wamjini! Na akanambia sasa upo kamili na hata akitokea tajiri anaweza kukukabidhi gari ukawa unapeleka hesabu, uko vizuri na hii ukiichukulia serious itakutoa dogo" Nikamwambia
"Asante bro kwa wema wako nakuahidi sitakuangusha na hata hizi dakika chache unazonipa naamini kijiweni michongo ni mingi ntatoka tu"

Aliendelea kunielezea "Hapa kijiweni kweli kazi ni nyingi tena waweza akatokea mtu akazingua na tajiri akatafuta dereva anaweza akakukabidhi wewe chombo, komaa dogo hao wengi unaowaona kijiweni si kama wewe tu wamekabidhiwa rasmi vyombo bali madeiwaka we kuwa mvumilivu tu".

Kiukweli alinipenda kwakuwa mimi nilikuwa mchangamfu, mwepesi kuelewa jambo ninaloelekezwa, kazi nilitokea kuipenda na zaidi sikuwa muongo yaani zile za kumdanganya labda nimebeba mteja alafu nimwambie sijabeba au nimebeba ila nikawasilisha pesa pungufu kiukweli sikuwa na utundu huo, kwahiyo ndio sababu bro John akaniamini sana.

Safari ikaendelea maisha yakasogea nikiwa sasa ni dereva kamili wa taksi na nikawa najivunia na kufurahia kazi yangu ya udereva ingawa katika mambo yote bado nilikuwa namtegemea John lakini nilikuwa nimepata ujuzi mkubwa kutoka katika kitu nilichokuwa sikijui kabla, kadri siku zilivyokuwa zinaenda nami nikawa naanza kuzoeleka na kujulikana kwa wateja mmoja mmoja, siku moja tukiwa kijiweni alikuja dada, huyu dada alipofika John akanambia, "Huyu dada ni mtoto wa mwenye hii gari ambayo mimi nimekabidhiwa"

John alinieleza haya kwakuwa huyu dada alitaka kuleta mazoea yaliyopitiliza, yaani ni mara mbili tu ndio nimepata kukutana na huyu dada, mara ya kwanza nikiwa na bro John alipokuwa akipeleka hesabu ya gari kwao kwahiyo John akanitambulisha kwao mimi kuwa ni mdogo wake, siku ya pili ndio hii tunaonana hapa kijiweni lakini ile siku ya kwanza huyu dada alikuwa akiniwekea ishara ambazo mimi sikuzielewa, unajua mimi tangu ninasoma hadi kufikia hatua hii sikuwa na ukaribu wa kivile na akina dada kama hivi yaani kiufupi sikuwa na masuala ya mahusiano na akinadada kwa sababu mazingira ya shule na nyumbani hayakuwa rafiki katika mambo hayo yaani hakukuwa na nafasi ya zile za kikombolela au michezo ya kujificha vichakani.

Huyu binti kwanza alikuwa na mtindo wa kunikonyeza nami nikawa namshangaa tu na haya mambo hakuna aliyekuwa anaona zaidi yangu mimi ile siku ya kwanza tulipoenda kwao na John na siku ya pili ndio hii amekuja hapa kijiweni na alipofika kwanza aliniulizia sisi tukiwa tumegeuza migongo tumekaa hapa kijiweni tumegeukia kwingine mimi na huyu bro. Alikuja moja kwa moja na kuniulizia akitaja jina langu yaani huwezi kuamini jina langu alilishika kwelikweli, siku ya kwanza tu kulisikia akalishika akaulizia, "Yuko wapi Rojaz?"
Wakamuuliza "Rojaz wa John?"
Akajibu "eeh, yuko wapi?

Akaelekezwa mpaka nilipo na dada yule akaja yaani wala hakuwa na woga sijui yuko vipi,akaanza kusema,
"Jamani toka siku ile hata haunitafuti"
Mbele ya John akawa anayatamka maneno hayo "Hunitafuti? Mbona umekuwa hivyo? Au haujui mambo ya mjini? Haya mambo ya mjini we huelewi? Basi mi nikabaki nashangaa shangaa nikiwa nimeweka mikono hivi tukipiga stori na John akaja yaani akanikumbatia kwa kuniwekea mikono yake juu yangu akiwa amenikumbata kutokea nyuma akanambia
"Nimekumiss sana, nimekumiss mno, nyumbani umekuja siku moja tu nimekufahamu haukuja tena,au John amekwambia usije? Nikamwambia "hapana mbona tunakuja sana labda uwa tunapishana wakati sisi tunakuja wewe unakuwa haupo"
Akanambia "kama tunapishana si uniulizie?". Pale ni nyumbani kwetu ulizia flani yuko wapi utaniona, siku hizi tunaenda kwa simu sasa mpaka unione tena wewe huna hata simu nikamjibu "sina simu"

John akawa anamtizama tu, anatutazama tu na si kama alinivuta pembeni ni mbele ya huyu John, akasema "Basi itabidi utafute simu, ntakutafutia simu". Basi yule binti akaondoka zake mi nikiwa nimeshikwa na butwaa, wakati anaondoka akanambia "Mbona hata haunisindikizi?

Wakati ananambia hivyo John akawa ananinng'oneza kitaratibu
"mwache aondoke zake"
Akaendelea kunambia
"Katika vitu ambavyo unatakiwa ukae navyo mbali kimojawapo ni huyu binti, huyu binti achana nae kabisa hii ni hatari unaweza kupigwa risasi ya kichwa,achana nae asikuzoee"
Nilimwambia John "Kaka wala usiwe na wasiwasi na mimi kuhusu yule binti kwani ugumu wa maisha ambao nimeupitia haitaweza kutokea, kwanza sina mahusiano nae na kama ulivyosikia ameniulizia kama nina simu nimemdanganya kuwa sina na hayo anayonieleza akili yangu wala haiko huko na kwakuwa umenisisitiza nitakuwa mtiifu kwako wala sitajihusisha nae, mimi nitakaa kimya"
Akanambia "ndio hivyo unatakiwa ufikirie maisha sasa mambo lazima yaendelee, hawa mabinti wa mabosi watakuja kukuletea matatizo mbeleni achana nao kabisa".

Nikamsikiliza kaka yangu na baada ya muda kanambia "leo usiku kunaweza kukawa kuna dili tunaweza kulifanya na kwa sababu umeshakomaa sasa wewe ni dereva mzuri" Nikamwambia "hakuna shida, kuna abiria?

Kaka John akasema "yes,kuna abiria ila mimi ntaenda kupumzika nina kitu changu(mpenzi) bwana si unajua? Mimi bwana sinywi pombe, mi sio mshabiki sijui wa vitu gani gani lazima nitulie sehemu na mtoto mzuri tule raha, mimi nitakupa mchongo muda ukifika".

Basi nikakaa tayari kwa huo mchongo, akaniachia funguo naye akaondoka zake lakini sehemu alienda mimi sikuijua (sikujua ni guest gani) lakini aliniambia tu kaa tayari, usiku nikaona muda umeenda na kwa sababu nilifanyafanya kazi kwa toka muda ule alionieleza hili swala jioni ilishaingia ilikuwa mida ya saa 11 hivi, nikapigapiga kazi mpaka kwenye majira ya saa 3 usiku nikajiuliza bro yuko wapi? Nikipiga simu yake hapokei, nikajua huyu kashakuwa katika uwanja wake wakujidai tena basi nikajiondokea zangu nyumbani kujipumzikia, gari nikaenda kuipaki palepale tunapoipaki, nikaenda zangu nyumbani nikijua mteja ameaghirisha hilo zoezi, nilipofika nyumbani nikaoga zangu na kula chakula nikijiandaa kwa kulala, wakati nimeshajipumzisha mara simu yangu ikaita na kutizama ni bro John akanambia, "Nakupgia muda mwingi naona namba yako inatumika au ulikuwa unaongea na yule mtoto?

Nikamwambia, "Hapana bro siongei na huyo mtu kwanza nimemwambia sina simu na wewe shahidi ulisikia pale nikimwambia, sina hata namba yake wala namba yangu hana, nafatisha ushauri wako kama ulivyonambia niachane nae nami nafanya hivyo"
Bro akanambia "vizuri, sasa lile dili liko tayari limeshakaa mkao wake,kuna abiria utaenda kumchukua". Nikamuuliza "namfata wapi?"
Akanambia "palepale gari ilipo yeye tayari atafika hapo na atakapofika hapo ataingia kwenye gari na utamsikiliza wapi unapompeleka"
Nikamuuliza "ina maana gari ilipo yeye anapajua? Akanambia "anapajua tena ukichelewa unaweza kushangaa yeye ameshafika kabla yako wewe lakini sitaki wewe umkute jitahidi uanze kufika wewe na ukifika milango ya gari aikute iko wazi, yaani yeye akifika akute milango haijakomewa yeye atafungua na ataingia ndani mtazungumza akiwa ndani ya gari huku ukiwa umewasha gari,ni mteja wetu mzuri, anatoa pesa nzuri kwahiyo wewe kale kichwa".

Basi mimi nikanyanyuka na kujiandaa, nikatoka zangu kuelekea pale tunapolaza gari, ile nimefika tu nafungua gari na kuweka mazingira vizuri garini basi kweli mtu huyu akaja, alionekana ni kijana ila alionekana amenizidi umri kidogo lakini ni rika la kijana, alikuwa anashabihiana kiumri kiasi kama bro John hivi lakini sema yeye alikuwa ni mrefu, akaja akaingia garini na akakaa siti ya nyuma, ujue tena taksi hizi, akanambia, "Naomba endesha twende huku" Nikamwambia "wapi? Akanambia "wewe twende ntakuelekeza,taarifa zangu si John amekupa? Nikamwambia "ndio"
Akasema "sawa sasa twende".

Nikawasha gari tukaanza kuondoka huku yeye akiwa ndio muelekezaji njia mara pita hivi, kata hapa lakini akanambia "wewe ni dereva mzuri sana John amenambia ni dereva mzuri alafu ni mzoefu barabarani sasa tupite short cut"

Kwakuwa nilishakuwa na gari muda mrefu na mzoefu katika njia tofauti tofauti ni kawaida yetu kumsikiliza mteja matakwa yake, nikapita njia alizozitaka basi tukawa tunachanja mbuga, nikamwambiab"Bro kwani tunaelekea wapi?" Akanambia "wewe twende"

Huyu kaka alikuwa amebeba kibegi, kibegi hiki ni vile unaweza kukiweka kwenye mabega si begi kuubwa ni kibegi cha mkanda mmoja ambacho alikuwa kakigeuzia kwa mbele, baada ya muda nikaingia kwenye lami kwani hakukuwa na ujanja tena ni lazima ilikuwa tuipate njia kubwa kutokana na eneo ambalo anakwenda, tuliposhika barabara kubwa kama dakika kumi mbele tuliona kama magari yanakuja upande wetu, unajua tena barabara kubwa magari hayaepukiki, mara yakawa yanapiga honi kwa nguvu, jamaa akanambia "nakuomba ongeza spidi"

Nikamwambia "kwanini niongeze spidi kwani kuna shida gani acha wapite hao" Akanambia "nisikilize mimi hao watu wanatufuata sisi" Nikastuka sana na nikamuuliza "wanatufuata?" Akasema "eeh wanatufuata inabidi uongeze spidi"

Nikamuuliza "wanatufuata kwani tumefanya kosa gani? Akanambia "nisikilize mimi kijana acha ubishi we ongeza spidi tu hao watu wananifata mimi" Ikanibidi nitii nikaongeza spidi na akanambia "hawa watu wakitukamata hawatataka kujua wewe ni nani yaani wote tutapigwa risasi za vichwa na uwe ndio mwisho wetu,ongeza spidi".

Nilitii na kuongeza spidi hatimaye wale watu hatukuwaona tena tukawa tunaelekea njia kama vile nje ya mji akawa ananisisitiza "kazana, kazana"
Na kwa sababu kiasi nilikuwa najua njia za mikato tukawa tunapita hizo tunarudi njia kuu lakini ukiniuliza kwanini alikuwa ananiambia niongeze spidi mimi sijui kabisa kwani hata nilipokuwa nikimuuliza jibu lake kwangu lilikuwa "Haya mambo wewe hayakuhusu, hao watu wananifata mimi"

Nakumbuka kweli nyuma kukawa shwari hakuna watu wanaotufuata, tukafika sehemu moja nje sana ya mji yaani ni mbali sana sikuwahi kupata abiria wa kuja huku kabla, tukafika mpaka uko sasa akanambia "Basi sasa mimi nashuka", Yaani kwa sababu nilikuwa nimeacha vioo wazi ile nataka kusimamisha gari huyu kaka aliruka, yaani alichoropoka kama panya,aliruka na kibegi chake. Nikamwambia "Bro si utaumia" Akasema "sasa basi we geuza uende zako na hakikisha hawa watu haukutani nao na ukikutana nao ujue watakuua"

Nikamuuliza "kwanini bro?" Akasisitiza
"unaporudi tafuta njia yakuweza kuwakwepa wale la sivyo watakuja kukuua hao sio watu wazuri watakuja kukuua amini hivyo"

Mimi mpaka hapo sikujua lolote,sikujua kwanini alikuwa ananiambia maneno hayo, sijui alikuwa amefanya kitu gani, sijui walikuwa wamekoseana nini,nikageuza gari kuanza kurudi wakati huo nikawa nampigia simu bro kumjuza kuwa nimekutana na kitu ambacho kinanitisha, nikawa napiga simu ya bro John na simu yake ikawa haipatikani hewani, simu yake haipatikani na mbaya zaidi hata namba ya simu ya huyu mtu niliyempakiza pia sikuichukua kwa sababu ilikuwa kuachana ni chapchap halafu yupo kama kuna kitu flani ananificha namimi sijui lolote, uoga ulitanda ndani ya moyo wangu,amani ilinipotea kabisa.

Nikageuza gari kinyonge na kuanza kurudi, nikarudi nikiwa na tahadhari maana niliambiwa hawa watu nisikutane nao au wasinione, kumbe hii ilikuwa ni siku mbaya kwangu, ilikuwa siku mbaya, mbaya, mbaya sana, wakati niko barabarani mara ghafla hawa watu sijui walitokea wapi, sijui hata kama walikuwa wanajua kama mimi ninarudi niko barabarani gari moja nyeusi na nyingine yakawa yananifuata kwa kasi, ni lile lile la mwanzo na la pili nayaona yakijia upande wangu kiukweli niliogopa mno, niliongeza spidi lakini hawa watu walikuwa spidi zaidi yangu, yaani ukiniuliza nilikuwa nakimbia nini kiukweli hata mie nilikuwa sijui lakini lazima nikimbie kwani nilisisitizwa kukimbia kwani nikisimama nitapigwa risasi, mimi sijafanya kitu nilimbeba tu huyu abiria na wala sijui lolote.

Kila nilipokuwa nikimpigia bro John nikawa simpati hewani, namba ya huyu mtu sina yaani nimejikuta ninaucheza mziki nisioujua kiukweli sikujua ntakuwa mgeni wa nani mie....

Itaendelea!
 
Karibuni wapendwa story.

,Antonnia ,Bantu Lady ,Kalpana ,Gily ,kaburungu ,Kibunango ,Lastmost ,wao ni wao ,Mpetde ,Santos06 ,To yeye ,niachiemimi ,JBourne59 ,harakati za siri ,Aaliyyah ,Lovelovie ,Semere92 ,mludego ,mwonge ,Smart AJ ,Mwana ,Mwanga Mkali ,sumbai Zeus1, Rashidi Jololo ,barakalyimo ,Iceberg9 ,ERoni ,Dahan ,Mwananchi B ,Watu8 ,liwaya ,Ushimen ,madindigwa ,The email ,Gamaha ,IBRA wa PILI ,Kaka yake ,shetaniKoffi Annan[/USERmacho_mdilikopremji canoonhamachoachila ceez
 
Karibuni wapendwa story.

,Antonnia ,Bantu Lady ,Kalpana ,Gily ,kaburungu ,Kibunango ,Lastmost ,wao ni wao ,Mpetde ,Santos06 ,To yeye ,niachiemimi ,JBourne59 ,harakati za siri ,Aaliyyah ,Lovelovie ,Semere92 ,mludego ,mwonge ,Smart AJ ,Mwana ,Mwanga Mkali ,sumbai Zeus1, Rashidi Jololo ,barakalyimo ,Iceberg9 ,ERoni ,Dahan ,Mwananchi B ,Watu8 ,liwaya ,Ushimen ,madindigwa ,The email ,Gamaha ,IBRA wa PILI ,Kaka yake ,shetaniKoffi Annan[/USERmacho_mdilikopremji canoonhamachoachila ceez
Asante mkuu nimefika!! Ngoja niisome
 
MKASA WA KUSISIMUA WA ROJAZ:
katika kipindi cha sitasahau cha radio free Africa




Part 2


Naendelea kuelezea mikasa niliyokumbana nayo katika harakati zangu za utafutaji na kama nilivyowaelezea awali niko katika harakati za kuwakimbia wale watu ambao hadi wakati huu sijawajua kiundani hawa ni wakina nani,sijui ni majambazi ama ni polisi mi kikubwa nilichoamua ni kukimbia kadri nitakavyoweza ili kuwakwepa hawa watu.

Niliongeza spidi ya lakini hawa watu walikuwa wanakimbia zaidi na hofu ilizidi kunitanda moyoni mwangu,nikawa nawaza peke yangu aliyesababisha yote haya ameshashuka na gari hili siwezi kulitelekeza njiani kwani bro John amenikabidhi mimi je ntaenda kumueleza nini kama ntalitelekeza? Mawazo kiukweli yalinitinga sana na ukitilia maanani namba za simu za bro John zilikuma hazipatikani hewani muda wote huo,mbio za sakafuni huishia ukingoni ikanilazimu kusimamisha gari na wakaniamuru kutelemka garini tena katika eneo lenye giza nene ni mwanga tu wa taa za gari ndizo zilikuwa msaada wa kuweza kuonana,nikatii amri zao ila nikawauliza
"mbona siwafahamu nyinyi ni wakina nani?"

Hiyo ndio ilikuwa sentensi yangu ya kwanza kwao,kabla sijapata jibu mmoja kati ya wale watu alinipiga ngumi moja ya uso, yaani katika maisha yangu toka nizaliwe sijawahi kupigwa ngumi kama ile,watoto wa mjini siku hizi wangeiita Ndoige,ngumi iliniyumbisha na kunipeleka mweleka mpaka chini,kiukweli kila nikitizama hili eneo nilikuwa silielewi hata kidogo kwani ramani ilinipotea nikawa najiuliza peke yangu ni wapi hapa? na ukitilia maanani ule mfukuzano na hawa watu hata sikuelewa niko eneo gani,nakumbuka niliwauliza tena
"Mbona mnanipiga,mbona mnanipiga mimi nimefanya kosa gani?"
Mmoja wao akasema kwa kufoka
"mshkaji ameshatutoroka huu ni uzembe wa hali ya juu sana,hatukutakiwa kufika hapa na kama tungefika mapema tusingefika hapa"

Lakini mwingine akasema "huyu anajua alipo" nikamjibu
"Mimi simjui huyo mtu mnayemtafuta mimi nilimbeba kama abiria tu na mimi nilimpakia akaanza kunambia kuna watu wanamfata"
Mmoja wao akasema "nyamaza,nyamaza wakubwa wanapozungumza,ameelekea wapi huyu mtu?
Nikawajibu mi simjui huyu mtu mimi ni dereva tu na hii gari mi si ya kwangu mi ni Deiwaka tu"
Ghafla nikapigwa ngumi nyingine
"Tumekwambia tulia"

Waliingia kwenye gari wakawa wanasagula sagula sasa kwa sababu mimi sikuwa najua wanachotafuta ila kwakuwa niliambiwa nisizungumze chochote nikawa natizama tu tena nikikumbuka zile ngumi mbili nilizotwangwa nikawa mdogo nisije nikaongweza nyingine zikaweza kuniletea kizaazaa mwilini,taa za gari yangu zikiwa zinawaka,taa za gari nyingine zikiwaka na za gari nyingine pia zikiwaka nikaamrishwa
"Kaa chini,kaa chini,kaa chini"
Sasa kwakuwa nimeona hawa watu idadi yao ni kubwa na mimi nipo peke yangu hata wakiamua kunifanyia vitendo vibaya nani atakayejua? Wakiamua kunipoteza ndugu yangu gani atakayejua? Nililala kifudifudi na nakumbuka kaka mmoja kati yao alikuwa amevaa kiatu kizito kwelikweli kama buti akaja akanishindilia si unajua mtu akikukanyaga kwa nguvu mgongoni nikawa nahangaika akawa ananambia "tena nakwambia utulie,utulie,utulie hapo wakati tunawatafakali"

Mmoja kati ya hawa walioniweka chini ya ulinzi akawa anawaambia wenzake "kwa kupitia huyu kijana tutampata huyu mshkaji wala hakuna haja yakupaniki,huyu huyu atatupeleka mpaka mlangoni kwake"
Lakini mwingine akasema "huyu hajui lolote si unamuona? Hajui chochote na kama angekuwa anajua mi ningeshajua hapa tunapoteza muda tu"
mwingine akasema "huyu ni kijana na tena ni Deiwaka mwenye gari hii atatupa taarifa za huyu mtu,mwenye gari hii atatupa taarifa za huyu mtu,kwahiyo chakufanya hapa tufanyaje?"

Wakawa wanajadili hapa huku mimi nimelazwa kifudifudi,mmoja akasema "tuondoke na hii gari" wakanambia "inuka" yaani ni watu wa milaba minne wameshiba haswa wakaniamrisha kuinuka na kuniuliza "wewe umesema ni Deiwaka haya mwenye hii gari ni nani? " kiukweli sikuweza kuficha nikawaeleza mmiliki wa gari kuwa ni kaka yangu ambaye ananiachia mara kwa mara na sijui chochote,wakaniuliza anaitwa nani? Mi nikawatajia jina lake
"Mpigie simu sasa hivi,taja namba yake"
Nikawajibu "kiukweli huyu mtu hapatikani,nimempigia muda mrefu hapatikani"

Kiukweli naikumbuka sana siku hii,katika harakati zangu zote za kufanya kazi ya udereva sitaisahau hii siku,niliwaambia "mimi sifahamu chochote nawaomba msinifanye jambo baya lolote huyu ni mtu tu nilimbeba kama abiria"
Mmoja wao akanambia "huna sababu ya kujieleza utaondoka mazingira haya kama ulivyo na vitu vyako vyote utaviacha hapa"
Nikaacha kila kilichostahili kuacha na kile kisimu changu nilichokuwa nacho na kwa kutizama mazingira haya jinsi nilivyo na ukitilia maanani ulikuwa ni usiku niliona ni bora nitafute njia ya kutoka kuliko kuendelea kubishana na hawa watu nikaukumbuka msemo wa wahenga mwenye nguvu mpishe nami sikuweza kuendelea kung'ang'nia visivyowezekana,nikaondoka nakujisemea moyoni kama ni gari kaka atashughulikia acha nitoke kuliko kuendea kuwa katika mazingira hatarishi,nilipopewa ruhusa ya kuondoka katika mazingira haya sikujali giza,sikujali ninamjua nani,sikujali naelekea wapi ilikuwa mimi ni kukimbia kutafuta mpenyo wa kuweza kupata msaada,nilikimbia sana na giza hili sikugeuka nyuma nilikimbia hadi nikakutana na mazingira ambayo niliona naweza kupata msaada,nakumbuka nilienda katika nyumba moja na kugonga ili kupata msaada majira haya ya usiku,Tanzania ni nchi nzuri na yenye amani sana,nilibisha hodr na kuomba msaada nikafunguliwa na wenyeji wangu wakaniuliza nilikuwa nimetoka wapi isitoshe usiku ulikuwa mkubwa,nilikuwa natokwa na jasho jingi,wakawa na taharuki na waliendelea kuniuliza maswali kujiridhisha kama ni mtu mwema nami nilijieleza kadri ya uwezo wangu ili niweze kupata msaada,walinambia sijui twende kwa mwenyekiti wa mtaa nikawaambia "naombeni angalau tu nipumzike na huko kwa mwenyekiti tungeenda kutapopambazuka" kwa imani waliniamini na wakanipa msaada na kulipopambazuka nikafanya utaratibu wa kurudi nyumbani huku nikiwa sina simu,sina chochote,sijui kaka yupo wapi na sijui ntakapomueleza atayapokeaje haya ambayo namwambia.

Hatimaye nikafika nyumbani na kuwaeleza ndugu zangu kile kilichotokea,wao wakapigwa na mshangao na kuniuliza "si umeondoka hapa mkiwa mnaongea imekuwaje tena hapatikani? Huyo uliyembeba alikuwa amebeba nini? Maswali yalikuwa lukuki lakini mimi nikawa sina majibu ndipo kaka mkubwa ambaye yeye ndiye alikuwa anafahamiana zaidi na huyo kaka alisema atamtafuta,alitafutwa hapatikani,alifatiliwa mahali ambapo anaishi huyu kaka John ambaye alinifundisha mimi udereva hakupatikana nyumbani kwake kwahyo hata mimi nikawa sina jibu la ya chochote katika kile kilichotokea,simu nimeacha,gari nimeacha na kaka huku anatafutwa hapatikani kwahiyo ishu ni kama inaishia hapo lakini kaka alinambia ni vyema twende kituo cha polisi kutoa hizi taarifa kwa akiba lakini mimi nikamjibu sawa tunaweza kwenda lakini kaka John akisikia tumeenda uko anaweza asipendezwe na kwanini tusizungumze nae kwanza alafu tuweze kujua anatushauri vipi,tunaweza kwenda polisi tunaweza kujikuta tunamuharibia yeye pia na kumbe ni mambo ambayo anayafahamu pia,mimi nilishauri hivyo na hata kaka akasema ni kweli lakini hatuwezi kujua watu hawa ni wakina nani wanaweza kuendelea kukuwinda wakati wewe hauelewi chochote,mambo haya tulizungumza kama familia lakini ilibidi tuwe wapole kumsubiria bro John kujua atakuja kusema nini kuhusiana na hiki kilichotokea nami nimueleze gari yake mazingira ambayo nimeiacha kule kwa wale watu ambao walinikamata.

Tumekaa siku nne toka lile tukio kutokea kwahiyo tukawa katika hali ya ukimya tu na kuruhusu maisha mengine yaendelee,nakumbuka niko tu home kwa sababu hata ile mood ya kufanya kazi ilikuwa imekata kwa changamoto hizi nilizokutana nazo,kaka alikuja (kaka yangu huyu kabisa) akanambia "kuna tatizo,yaani nimepata taarifa ambayo sio nzuri tena sio nzuri hata kwa upande wetu sisi pia"
Sikujua zinamuhusu nani lakini kaka akasema "nasikitika mpaka sasa hivi mshkaji hapatikani,hajulikani wapi alipo"
Nikamwambia kaka "taarifa gani?
Kaka akanambia taarifa ambazo anazo ni kuhusiana na mimi,kaka anasema kuwa leo leo nakuja kukamatwa
"Kuhusu nini? Kaka mbona unanambia mambo ambayo siyaelewi? Kaka akanambia "unatakiwa utulie na unisikilize kila ntakachokisema,ile ishu iliyotokea siku ile,ile ishu iliyotokea usiku ule haijawa nzuri ndio maana nilikwambia twende kituo cha polisi tukatoe taarifa na hata niliuliza kuna mshkaji alinambia nendeni kituo cha polisi mkatoe taarifa mambo kama haya msinyamaze nayo nyumbani"
"Kaka nini kilichotokea kwanini unanitishia maisha?kwanini unambie mambo nusunusu? Akanambia "yule kijana ambaye siku ile alipanda gari yako amepatikana ameuwawa,nikamjibu "kama amepatikana na ameuwawa mimi nahusika vipi hapo? Yaani kwanini uone hii kwangu ni taarifa mbaya? Alishuka akaenda zake mimi najua nini na nani alikwambia hizo taarifa za uongo,nani alikwambia?"

Mimi nilipokea taarifa katika mazingira haya lakini kumbe kaka alikuwa na taarifa zaidi ya hizi alizonieleza kuwa ni kweli yule kaka ambaye nilikuwa nimembeba ambaye sikuwa namfahamu zaidi ya kuambiwa na kaka ambaye alinifundisha udereva kuwa nikambebe na hata nilipotaka namba yake alinambia wewe nenda uko uko garini utamkuta yeye hii gari anaijua,sasa kama amepatwa na matatizo mimi sasa nahusika vipi na matatizo yake?
Mambo kumbe hayakuwa mepesi kama nilivyokuwa nikiyawaza kichwani mwangu au nilipokuwa nawaza yaliponitokea kwamba kaka atafanya utaratibu atapata gari yake,sikuwaza hasa kuhusiana na yule kijana kwanza alishatoka na kukimbilia uko akisema ana mzigo ingawa mimi niliona kipochi sijui mzigo ni mzigo gani,ni kweli mimi nilikuja kufatwa na askari polisi "wewe ni Rojaz?
"Ndio"
"unamfahamu flani?"
Sasa mimi majina ya yule mtu hata siyajui
"Mara ya mwisho wewe ndio ulimchukua kwenye gari yako na hakuonekana na alipoonekana tayari ameshakuwa katika hali ya umauti,tunakuhitaji kituo cha polisi"
" Yaani mimi Deiwaka nisiyekuwa hata na gari jamani,nimepigiwa simu nikambebe abiria leo matatizo ya mtu mnataka kunitwisha mimi kwa sababu gani? Mi sijui chochote"

Unajua katika hali ya taharuki unapopewa taarifa kama hii unaweza sema "mi simjui huyo mi simjui"
"Aah sasa kwani sisi tumesema wewe umetenda? Sisi tunachojua mara ya mwisho ulikuwa nae kwahiyo tutakapokwenda kule kituo cha polisi utaenda kupata maelezo zaidi,bila kutumia nguvu basi fuata utaratibu tunaokueleza" kaka alikuwepo wakati huo akanieleza "ni kweli mdogo wangu haujui chochote,sheria iko hivyo,ni kweli humjui jina lake nawe ni Deiwaka kama unavyosema nami najua hivyo lakini lazima uende kituo cha polisi" nikamwambia kaka "mimi kituo cha polisi siendi,siendi mimi kituo cha polisi" polisi walinizoa mzobe mzobe kunitoa pale wakinambia wananichukua ili kuweza kunihoji ilikuwaje mara ya mwisho,kwanini akutwe na hili jambo ndio walivyonieleza,nilipofika kituoni kile walichoniahidi kule nyumbani kilikuwa tofauti kabisa yaani kwenda kituo cha polisi ni rahisi lakini kuondoka katika hayo mazingira sio rahisi,nikajikuta katika mazingira hayo nikiwa sielewi nini nitafanya,taharuki pia ilitokea kwenye familia yetu lakini aliyenifundisha udereva,yeye ambaye alinituma mimi nikamchukue huyu mtu hajaonekana toka siku ile mpaka mimi nimefight nimerudi nyumbani basi nae atafutwe aelezwe kuhusu hili,hapatikani mpaka sasa hivi!

Kwahiyo mimi nikawa nimeshikiliwa kituo cha polisi "niachieni mimi nirudi zangu nyumbani,niachieni mimi nikaendelee na maisha yangu mimi sijui chochote,mi sijui chochote" habari ya kwamba hujui chochote mpaka ije ithibitishwe kuwa hujui chochote ni lazima hapo wafanye kazi yao inabidi utulie na kaka aliniambia "tulia usiongee sana,usiongee sana haya ni mambo ya kisheria ndio maana tulishauriwa tutoe taarifa kituo cha polisi kwa sababu tutaulizwa kama hayo yaliyotokea mliripoti wapi? Tutajibu nini? Ina maana tuna vitu tunavijua,hakuna muda wa kulaumiana ni kufata taratibu za kisheria zinavyosema,mambo yatakaa sawa"

Kwa upande wangu kilio ndio kilikuwa kimeshika hatamu nikiwaza toka nizaliwe nilikuwa sijawahi wekwa lock up leo nimekutwa na mkosi gani huu,mi ni kijana ambaye naishi kwa amani na wenzangu na nafanya kazi zangu bila ya zengwe lolote lile,sijawahi kupora mtu,sijawahi kumfanyia hila mtu yoyote yule mi napiga mishe zangu najipatia chochote cha kujikimu maishani leo naambiwa "sasa utapumzika hapa" Nini hasa kilichotokea hata mimi nilikuwa natamani kujua kwa sababu sijui chochote na walionikamata pengine wanahisi nina maelezo zaidi nitasema lakini sijui chochote yaani kama wao wanavyojiuliza nami mwenyewe najiuliza sijui chochote,mtu huyu ameuwawa vipi wakati alinambia "hakikisha unatoka katika mikono ya hawa watu,wakikukamata watakuua"unaona na yeye ndio aliniambia "unaona huu mwendo tunaoenda nao? Ukisema ujisalimishe hapa,usimamishe gari tutapigwa risasi za vichwa hatutapata hata nafasi ya kujieleza,utajieleza mbele ya safari" na mimi hofu,taharuki ndicho kilichonikimbiza mpaka nipo hapa kizuiani sina nafasi ya kufanya chochote wala kujitetea kwa loloje.

Itaendelea!
 
MKASA WA KUSISIMUA WA ROJAZ:
katika kipindi cha sitasahau cha radio free Africa



Part 3



Maisha ya pale kituo cha polisi yalikuwa ni ya muda mfupi kwani utaratibu wa kimahakama ukafika na nikatakiwa kupelekwa gerezani wakati suala langu likiendelea kupatiwa ufumbuzi,wakati nikiwa gerezani kuna kaka mmoja tulitokea kujenga ukaribu wa kiurafiki nae na akawa msaada mkubwa kwangu katika mambo mengi yaliyokuwa yakinikabili,siku moja katika maisha yetu ya gerezani nikiwa na huyu kaka alinambia "kila nikikutizama macho yako nakuona ni mtu mwema sana" nikamuuliza "mimi?akaendelea "yaani hata wale watu wabobevu wa kufanya uchunguzi,watu ambao ukijitetea wanaona auhusiki ndio wanakubana lakini nakuona ni mtu mwema kabisa"

Nikamjibu "sijui,lakini mimi sipendi ubaya na mtu na napenda amani katika harakati zangu za kila siku" akaendelea "unajua uwa nawatizama watu wengi sana hapa lakini katika wengi sijaona mtu mwema kama wewe" nikamuuliza "mimi?" Akasema "ndio sijaona mtu kama wewe humu,wewe ni mtu mwema na kama haujajua basi siku moja utakapopata neema ya kutoka hapa utajua kama wewe ni mtu mwema itambue hiyo na iishi hiyo kwa sababu una upekee wako" nikahisi ni maneno ya faraja tu ananambia yakunitia moyo,kunisahaulisha tabu zangu na kunifanya nifurahi na kujiona ni wa pekee hata kama niko katika mazingira magumu na vitu kama lakini aliendelea kuniambia anamaanisha kwa kile anachokiongea,nakumbuka nilimuuliza "kwanini wewe uko hapa? Kwani wewe si mtu mwema?" Akanambia "hata nikikuambia hautaweza kuniamini lakini mimi natofautiana na wewe,angalia macho yangu yalivyo je una uwezo wa kumtambua mtu tabia zake,hisia zake na kile kilichopo ndani yake? Nikamwambia "hapana sina huo uwezo" akanambia "basi mimi ninao huo uwezo ila sikuutumia vizuri nikiwa uraiani,mimi sifanani na wewe,wewe umekuja kwa njia ambazo si za haki yaani umekuja kwa sababu kuna watu wamefanya mambo mabaya wamekuingiza na wewe lakini mimi ni tofauti na wewe" nikamwambia "utofauti wa mimi na wewe ni upi? Akasema "ni stori ndefu sana huwa sipendi kuzungumza lakini kiufupi niko hapa natumikia kile ambacho nilistahili,siku nyingine ntakueleza lakini siko hapa kwa makosa hakuna mtu amenisingizia,maisha yangu ya uraiani mwenendo wangu ndi ulionipeleka mimi kuwa"

Nilitamani kujua alifanya kitu gani kilichopelekea hadi yeye kuwa anastahili kutumikia kifungo anachokitumikia,alinambia "niko hapa gerezani natumikia miaka yangu 30 na mpaka kesi yangu inasomwa nimeshakaa miaka mingi" nikamuuliza "umekaa miaka mingapi?" Akanambia "sikuvunji moyo wakati mwingine kuna kesi uendeshaji wake uwa unachelewa kwani kabla ya kufikia hukumu unaweza kujikuta umekaa hata miaka 5" nikamuuliza "hivi mimi naweza kukaa hapa muda mrefu?" Akanambia "inategemea na jinsi kesi inavyoendeshwa,kadri kesi inavyoendeshwa uenda uchunguzi zaidi ukaitajika hivyo kupelekea kuchukua muda lakini nakuombea sana mdogo wangu kesi yako isichukue muda mrefu na uachiwe huru" huyu kaka tulikuwa tunazungumza sana na kiukweli alinijenga sana katika mazingira yale nakunipa matumaini.
Siku zikiwa zimepita siku moja huyu kaka aliniita na tukawa tunazungumza na alinambia"unajua kama ninao ndugu zangu lakini toka nimepata haya matatizo wamenitelekeza na kunisusa huku,huwezi amini kati yao wakati nikiwa uraiani nilijitolea sana katika kuwasaidia hata katika vitu ambavyo havikuwa na faida kwangu niliwapiga tafu lakini kwakuwa mimi nimekamatwa hakuna hata anayetaka kunisogelea wakihisi pengine nao wanaweza kuhusishwa na mimi lakini licha ya hivyo hata ilipotoka hukumu hakuna aliyesogea,wameniacha" nikamwambia "ni sehemu ya maisha,je hakuna hata mmoja aliyekuja kukuona? Akanambia "ninaye mtu ambaye yeye hajawahi kuniacha,uwa namimi katika mazingira yoyote yale hata niwe ndani na hauwezi amini yeye uniletea mahitaji toka siku siku ile ya kwanza nimekamatwa" nikamuuliza "ni wazazi wako? Ni mtu gani huyo?" Akanambia ni girl friend wake (mchumba wake) ndio ambaye hajawahi kumuacha toka siku ile amekamatwa,nikamwambia kuwa alibahatika kumpata mtu sahihi sana,akanambia anahisi anaweza kuchoka nami nikamjibu kama ana upendo wa kweli hatoweza kuchoka na akanijibu "sijui,nina watoto pia yupo mwanamke ambaye nilipata nae watoto,watoto wangu wana uhitaji sana lakini mimi baba ambaye nilikuwa nikipambana katika njia mbalimbali leo nipo hapa,watoto wangu hawako katika mazingira salama na huyu mwanamke kila anapokuja kuniona aachi kunipa lawama na sasa amekuwa ni mwanamke wakuhangaika hovyo na wanaume,sielewi hatima ya watoto wangu,nilizungumza na ndugu yangu lakini ndio hivyo wameniacha peke yangu" kiukweli maelezo yake yalinisikitisha sana na hasa aliponielezea juu ya wanae maumivu yaliutanda moyo wangu,alinambia kuwa uraiani alikuwa anapambana sana,anapambana kwelikweli kwa ajili ya watoto wake lakini kwakuwa yupo jela hatoweza tena kuwapambania,kiukweli nikazidi kuumia kwa maneno yake nikamwambia "pole sana ndugu yangu,umenigusa sana,najua ukiwa hapa kule nje kila kitu chako kinakuwa kimesimama na kama ulivyonitia moyo kwenye maswaibu yangu nami nakutia moyo,tutatoka siku moja tutatoka" akasema "ni kweli natambua ni kweli"

Siku zikawa zinaenda na tukawa tunashea mengi katika mazungumzo yetu ya kila siku na kuna siku mfungwa mmoja aliniambia naona uko na urafiki na mtu flani (akimtaja yule mfungwa ambaye uwa napigana nae stori)nami nikamjibu ndio kwani amekuwa kama kaka,kama mshkaji na mfariji ndio tunabadilishana mawazo akanambia jamaa ana miaka mingi huyo kwani sote tutatoka na tutamuacha humo humo na akakazia huyo anafia humo humo gerezani,kiukweli sikumtilia maanani kwani kama ni miaka ambayo tayari imeshatamkwa mfano atatumikia miaka 30 si atatumikia miaka husika kwanini aonekane kama atafia huku? Sentensi gani hizi?
Siku zilikwenda na kwenda,safari za kwenda na kurudi mahakamani hazikuisha na mara zote nilizokuwa nikisimamishwa kizimbani nilikuwa naeleza ukweli na lile nililokuwa nalijua tu,sikuwa napindapinda katika maelezo yangu,sikuwa na mengi yakuyaeleza kwakuwa yangu ni machache kwani nilielezea stori toka nimekutana na huyu kaka hadi kufikia kunifundisha udereva,umiliki wake wa gari na hata kuhusu yule abiria ukutanaji nae ulivyokuwa na kama ujuavyo jela nilipata vijiupeo kutoka kwa wabobevu wa sheria ambao walininoa namna ya kuongea kuwa lipi lakuepuka kuliongea,lipi lakulisema na kadhalika maana mahakamani kuna maswali yamitego ni muhimu kusimamia kile unachokiongea na kiwe cha kweli kwani niliamini ukweli ndio utakaoniweka huru!

Nakumbuka siku moja kaka alikuja kunitembelea gerezani na akanambia "mdogo wangu uko katika mazingira mazuri kabisa katika kesi hii na upelelezi unavyoendelea unaonesha hauhusiki kabisa kwahiyo wakati wowote waweza kuachiwa huru,huenda mara ijayo utakapoenda mahakamani yawezekana usirudi tena huku gerezani" nikamuuliza "ni kweli usemayo kaka?" Akasema "ndio" nikajawa na matumaini na furaha sana kwa maelezo haya ya kaka,kuna siku yule kaka mule jela alinambia "naona mwenendo wa kesi yako si mbaya na matumaini ya kutoka yanazidi kuchanua sana hongera sana" nikamwambia "kaka kuna siku ntaenda mahakamani na sitarudi tena huku" akanijibu "ni kweli na mimi nimefatilia huo ni ukweli kabisa,naomba nikuulize najua utatoka na utakapotoka na kwenda uraiani unaweza kunisaidia kitu?" Nikamjibu "ndio" akasema "ntashukuru sana utakaponisaidia katika hili jambo,naomba unisaidie ntakupa maelekezo naomba ukawasalimie watoto wangu" nikamwambia "kaka hakuna shida" akaongezea "na pia ntafurahi sana kama utapata fulsa yakuweza kwenda kumsalimia na mchumba wangu" nikamjibu "nitafanya hivyo pia kaka" akanambia "naomba tuwe ndugu,unajua ndugu sio lazima muwe mmezaliwa tumbo moja,unajua wako ndugu sasa hivi hata wakija nimekuwa siwaamini tena lakini moyo wangu nimejikuta nakuamini sana wewe,sijawahi kukuona enzi nikiwa uraiani tumekuja kukutana gerezani lakini mimi naamini kukutana kwetu Mungu amepanga tena amepanga tukutane katika mazingira kama haya,hivi unajua waweza kukutana na mtu sahihi hata ukiwa gerezani?" Mi nikacheka kwa hayo maneno yake nikamuuliza "mtu sahihi gerezani? Mtu gani awe sahihi mazingira kama haya?" Akanambia "mimi naweza kuwa mtu sahihi sanj kwako na nikawa mtu mwema kwako,jua nimekuona kuwa wewe ni mtu mwema tafadhali nakuomba nawe unirejeshee huo wema ntakaokupa" yale maneno aliyokuwa akinambia sikuwa nayaelewa alikuwa anamaanisha kitu gani,msisitizo wa maneno haya kwangu uliendelea mara kwa mara mpaka siku naenda mahakamani,nakumbuka siku hiyo sasa ndio naenda mahakamani kabla hatujatolewa nje kupandishwa karandinga alinambia "unakumbuka maneno niliyokuwa nikikwambia mara kwa mara ? Unaweza haya maneno ukayafanyia kazi?

Nikamwambia "kaka wala usiwaze kwani undugu si lazima kuzaliwa tumbo moja,tunakutana katika mazingira yoyote alafu tunatokea kuelewana,nakuahidi kaka kama nilivyokwambia nitaenda kuwasalimia watoto na nitaenda kumsalimia mchumba wako,na nikuahidi mimi ni kijana na kama Mungu atanipa neema ya kutoka nitaenda kupambana,nitaenda kupambana na napenda nikuahidi kitu kimoja nitaenda kuwatembelea watoto wako na chochote nitakachobarikiwa sitawasahau kwani najua wewe baba yao uliyekuwa ukipambana kwa ajili yao umekwama humu" akaniuliza "kweli? Kweli unasema? kweli Rojaz unaniahidi kitu kama hiki? Ndio maana niliona,macho yangu yaliona na moyo wangu ukavutika kuzungumza na wewe,wewe ni mtu mwema" kiukweli ninaikumbuka sana siku hiyo kwani alikuja akanikumbatia huku machozi yakindondoka na kunipigapiga mgongoni akanambia "aisante sana mdogo wangu,asante nakutegemea kwani hakuna mtu yoyote ambaye ameweza kuniahidi hivi kama wewe,sijawahi kupata rafiki mwema hivi kwani kuna mshkaji nilikuwa nae hapa karibu kweli lakini toka ametoka hajawahi kurudi tena kunitembelea,hakuwahi hata kwenda kuwatembelea wanangu,Rojaz kumbuka ahadi unayonipa mdogo wangu" nikamwambia "kaka amini ninachokwambia,sitasahau" mimi niliondoka na nikaweka hiyo ahadi kwenye kichwa changu,muda wa kwenda mahakamani ulipofika tukapandishwa kuelekea uko na kesi ilisomwa na mheshimiwa akangurumisha kesi na mwishowe hakimu akatamka kuwa kuanzia muda huo niko huru,kiukweli kutokana na kuwa sikuhusika sikustuka sana kwa uamuzi ule uliotolewa kwani nilijua ni suala la muda tu ili kuweza kuujua ukweli halisi,jela nilikaa kama mwaka mzima hadi kufikia hii siku ya kuachiwa huru na katika kesi iliyokuwa ikinikabili tulikuwa wengi na wengine waliendelea na kesi mbele,ndugu zangu walifusahi sana kwa ndwtgu yao kuwa huru na kujumuika nao tena uraiani,kaka akanambia "sheria zipo kwa ajili ya kutenda haki walimdhuru huyo kijana watabainika tu, sheria itawakamata na kuwahukumu" kwahiyo mimi nilitoka gerezani na kurudi uraiani hakika ilikuwa ni furaha sana kwetu sisi na nilpata somo kubwa kuwa ni vyema kuwa na tahadhari katika shughuli tunazofanya



Itaendelea!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom