Elections 2010 Kipindi cha Dk Slaa kilichokuwa kirudiwe chaahirishwa

Yaani nafarijika sana kuona wana mageuzi wenzangu hapa... Slaa for President, warudie wasirudie kipindi kipo online tayari. UPINZANI JUU
 
Mfa maji haachi kutapatapa! CCM inchungulia kaburi lakini kuingia kaburini inabidi tuisukume kwa kura zetu! Bil kuinyima kura itafufuka na tutaendelea kuendeshwa kama mapeazi ya Lushoto na kina Makamba!
Rostam, mtoto wa mhujumu uchumi aliyekimbilia Uganda wakati wa vita ya Sokoine walimfanya mweka hazina wa CCM ya Mwalimu! Hawa jamaa wamemtusi kweli mzee wa watu (Mungu amrehemu). Mhujumu Uchumi anaongoza chama cha Mwalimu! Kha! Inatia kinyaa hii CCM, inanuka ! Halafu sie watanzania sijui tuna grisi badala ya ubongo? Mwalim alitumia utu uzima kumkataa huyu mhuni kwa kumwambia muda wake bado, sie tukatafsiri eti aliambiwa angojee! Alikataliwa kiutu uzima kwamba HAFAI!. Matokeo ya kutosoma busara ya Mwalimu ndiyo haya; mtoto, memsap, marafiki, mahawara na wahuni wanaendesha nchi! Tujisahihishe kwa kumyima kura halafu tukatubu kwenye kaburi Butiama!
 
Jamani jana usiku nilikaa hadi saa tano usiku baada ya kuambiwa kuwa watarusha tena mdahalo wa DK. Slaa ( PhD) bahati mbaya sana ulipowadia wakati wenyewe nikiwa nimekaa na kijitaulo tu na kumlazimisha my wife wangu tuahirishe ratiba ya jana, mara ukapita mstari wenye maneno kuwa, mdahalo huo hautaonyeshwa tena....hakuna apology hakuna extra info, sijui walishikwa na kigugumizi gani au hawa jamaa walienda kuwabembeleza waisurudie tena???

Kufika room nako, wife ameshalala, nimeamka na hasira kibao, hakika CCM siwapi kura yangu, hata kwa damu ya kuku........nawakilisha
 
Hii ndio raha ya kuwa na Rais Kilaza kwani hawezi kubuni mambo yake mwenyewe mpaka apige chabo. Kuna vimjamaa viwili vinadhani vyenyewe ni V.I.Ps wa nchi hii. January na Ridhwan. Kama wao ni wababe wakatafute dawa ya kifafa ya JK!!! Na kama JK atakwenda Jangwani tarehe 30 akianguka haamki tena.

ALWAYS OIL FLOATS ON WATER!!! Wazuie vipindi, wazuie kampeni Dr. Slaa is the president
 
Huwezi kumfunga bondia mwenzako mikono halafu utambe eti umeshinda kwa knock out (KO). si utaonekan mwehu tu??!!
 
AIBU kwa CCM.Msiwalazimishe wananchi nini wachague,uchaguzi ni wao wenyewe na hiyo ndiyo demokrasia.Mnaogopa nini kama kweli mna sera nzuri?Kumbukeni usemi CHEMA CHAJIUZA NA KIBAYA CHAJITEMBEZA.Wakati umefika sasa wa kujua CHEMA ni kipi na KIBAYA ni kipi.Tafadhali waachieni wananchi uhuru wa kuamua.Kutokuonyesha mdahalo wa Dr Slaa wakati ilitangazwa hivyo inaelekea wazi ni njama za CCM.Mnaoggopa nini?Kwanini mnataka kuleta fujo zisizohitajika?Siku zote hoja hujibiwa kwa hoja hivyo basi CCM mnatakiwa kujibu hoja kutoka kwa wapinzani na si kuzuia kurushwa kwa mikutano yao.Kwa kufanya hivyo ni nyie CCM ndiyo mtakuwa mnaleta fujo.Mungu ibariki Tanzania hasa ktk kipindi hiki cha uchaguzi.
 
Back
Top Bottom