Kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab auawa na majeshi ya Marekani nchini Somalia

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
12,900
15,329
Majeshi ya Marekani yamefanikiwa kumuua kiongozi muhimu wa kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab nchini Somalia.

Kikundi hicho cha kigaidi kina mafungamano na kikundi cha kigaidi cha Al Qaeda ambaye kiongozi wake mkuu Bw. Osama bin Laden naye aliuawa nchini Pakistan na vikosi vya vya jeshi maalumu la Navy SEALS la Marekani.

====

Majeshi ya Marekani yamlenga kiongozi wa al-Shabaab katika shambulizi la Somalia​

VoaswahiliOct 3, 2022

20221003171916_-995608025_7993260188869145762_640_359_85_webp.webp


Kwa kushirikiana na Serikali Kuu ya Somalia, Kikosi cha Kamandi ya Marekani Afrika kimefanya shambulizi la anga dhidi ya mtandao wa wapiganaji wa al-Shabaab nchini Somalia Oktoba 1. Shambulizi hilo limefanyika karibu na Jilib, takriban kilomita 370 kusini magharibi mwa Mogadishu.

Tathmini ya awali ya kamandi hiyo ni kuwa shambulizi hilo limemuua kiongozi wa al-Shabaab na hakuna raia aliyeuawa au kujeruhiwa.

Kamandi ya Marekani Afrika inachukua tahadhari kubwa kuepusha vifo vya raia. Kuwalinda raia wasio na hatia ambao ni sehemu muhimu ya operesheni za kikosi hiki kuhakikisha usalama zaidi na utulivu Afrika.

Al-Shabaab ni mtandao mkubwa kabisa na wenye harakati zaidi za al-Qaeda duniani na imethibitisha nia yake na uwezo wake wa kuyashambulia majeshi ya Marekani na inatishia maslahi ya usalama wa Markeani.

Kamandi ya Marekani Afrika, kikiwa na washirika wake, inaendelea kuchukua hatua kuzuia kikundi hiki cha kigaidi kiovu kupanga na kutekeleza mashambulizi kwa raia.

Somalia itaendelea kuwa ni kituo muhimu kwa mazingira salama ya Afrika Mashariki. Majeshi ya Kamandi ya Marekani Afrika yataendelea kufundisha, kushauri na kutoa vifaa kwa majeshi ya washirika kuwapa nyenzo za kuidhoofisha al-Shabaab.

Kamandi ya Marekani Afrika itaendelea kutathmini matokeo ya operesheni hii na itatoa taarifa ya ziada kama itkavyohitajika. Maelezo kamili kuhusu pande zilizohusika na vifaa vilivyotumika havitatajwa kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa operesheni zake.

Kamandi ya Marekani Afrika, yenye makao yake makuu Stuttgart, Ujerumani, na washirika wake, inapambana na watenda uovu na vitisho vya kimataifa, inakabiliana na majanga, na kuimarisha majeshi ya usalama kwa ajili ya kusukuma mbele maslahi ya taifa la Marekani na kuhamasisha usalama wa kanda, utulivu na mafanikio.
 
Hana jina kiongozi wa Al shabaab!!?..umoja wa mahakama za kiislam uliituliza nchi,mkawapiga,mkaleta alshabaab
 
Wanawake bwana wamechonganisha watu Ukraine wao wamejificha huku wanaua wagambo.amerika ni Pepo.
 
Back
Top Bottom