Marekani inafundisha Wanajeshi wa Kiafrika kufanya Mapinduzi nchini mwao? Walioongoza mapinduzi Guinea na Burkina Faso ni zao lao

w0rM

Member
May 3, 2011
68
164
Katika majibizano makali mnamo Machi 23, 2023, Congressman Matt Gaetz alimuhoji kiundani Kamanda wa Kamandi ya U.S. Afrika, Jenerali Michael Langley kuhusu Dola za Walipa Kodi wa Marekani zilizotumika kuwafunza Viongozi wa Kijeshi wa Mapinduzi barani Afrika

Mnamo Januari 2022, Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba alifanya Mapinduzi nchini Burkina Faso, na kumuondoa madarakani Rais Roch Marc Christian Kaboré. Damiba ni Mwanajeshi aliyefunzwa sana ambaye kulingana na Kamandi ya U.S Afrika, ameshiriki katika mazoezi yasiyopungua 6 ya U.S.

Mamady Doumbouya ni Mwanajeshi mwingine Mwafrika mwenye mafunzo ya hali ya juu ambaye aliongoza Kitengo cha Kikosi maalum cha Guinea kilichoanza mazoezi na Green Berets ya Marekani miezi michache kabla ya kuvamia Ikulu ya Rais na kumpindua Rais wa nchi hiyo, Alpha Condé mnamo Septemba 2021.

Jenerali Langley alikiri katika Kikao hicho kwamba wote wawili Damiba na Doubouya walikuwa wamefunzwa na Jeshi la Marekani, lakini alieleza kuwa wanawafundisha Askari maadili ya msingi ikiwa ni pamoja na Demokrasia, na kwamba ni karibu asilimia moja tu ya askari Elfu 50 waliopata mafunzo wameshiriki katika majaribio ya mapinduzi

Wanajeshi 500 ni wengi mno, achilia mbali moja, na angalau mapinduzi mawili yaliyojaribiwa na Wanajeshi waliofunzwa wa Marekani yamefaulu.

Tangu mwaka 2005, Marekani imeingiza mabilioni ya dola barani Afrika kwa ajili ya operesheni za kukabiliana na ugaidi ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya anga, uvamizi na kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Kiafrika wasiopungua elfu 50. Katika wakati huo huo, mashambulizi ya kigaidi na mashirika ya kigaidi yameongezeka sana.


Pia soma: US Naval Bases In Africa (AFRICOM): Sababu, Pingamizi, Faida na Hasara

- Marekani yaanza mazoezi yake makubwa zaidi ya kijeshi Afrika Mashariki
 
Back
Top Bottom