Kilio cha Mlalahoi: Kupanda kwa bei ya umeme wanasiasa mko wapi?

Hiyo tax ni kubwa mno, wanapeleka wapi hela yote hiyo..
Tatizo la wabongo wanaona hili na watakaa kimya tu watalalamikiana wenyewe kwa wenyewe kitaishia hapo, nchi za watu wanagoma ujinga kama huu hadi mambi yanarekebishwa, hawa jamaa mnawalipa hela nyingi sana za bure afu hamna wanachofanya zaidi ya kujilipa wenyewe, Ukianza utasikia wabongo wanajibu ohh nchi yetu ya amani, ohh wanawake na watoto wataumia, utadhani umewambia unashika mtutu kwenda vitani, swala ni kuandamana kugoma ujinga huu... Bongo viongozi wanawapeleka watu ka mazezeta kabisa, na wanavoona mnawaogopa wanakula bata tu


Mkuu umesema ukweli! Nchi zingine watu huandamana ata kupanda kwa bei ya mkate na maziwa tu! Leo Hii Umeme umepanda bei karibu Mara mbili na watu wako kimya tu! Tena wamejazana kujadili thread za ujinga za kesi ya ZZK na kusahau kabisa Hii kadhia ya Umeme!

Ni hatari sn! Vitu vitapanda bei sasaivi na maisha yatakua magumu sn! Na ndio maana maofisini rushwa na ubadhilifu na ukosefu Wa maadili havitoisha. Yani Hii ni kuanzia chini mpaka juu na ni sekta binafsi Na ata za serikalini! Mtu unalazimishwa upokee rushwa au uwe mwizi ofisini au usiwajibike ofisini kutokana na ugumu Wa maisha na kipato kidogo na pia tusisahau viwandani Km bidhaa zao hazitopanda bei basi bidhaa zisizokizi viwango zitakua nyingi sn na kuathiri afya ya mtumiaji! Yani Hali ni mbaya sn!
 
Mi leo hii nimenunua Unit 22.4 kwa Tsh. 15,000/=

Na mwezi wa 12 nilinunua Unit 38 na mwezi wa 11 nilinunua unit 31

Bila shaka ni wakati mwingine wa kufikiri sana na kuhitaji mabadiliko ya kweli.
Ccm haifa kuwepo madarakani kamwe!

Mkuu Ebu tuangalie huu mchanganuo!

Kwa mtu anaekaa Ubungo Dar anaelipwa mshahara kima cha chini!

Kodi ya nyumba vyumba viwili 80000 per month
Umeme 40000 per month
Maji 60000 per month
Simu 30000 per month
Usafiri 45000 per month
Kula 210000 per month
Ziada 30000 per month

Jumla ni 495000.

Je kwa mtu anaelipwa kima cha china kutokana Na ghalama zinavyopanda hivi ataweza kuishi huko bongo?

Au ndo atakua mla fushwa sn na mwizi ofisini?
Tutafakari Jamani!
 
hapa hesabu ya haraka serikali inachukua 1800 kodi kwa umeme huu ambao utautumia si zaid ya siku 2, kwaiyo ukifanya kwa mwezi ni sh.ngap?

kodi saiv kama utakua unatumia sh.elf 10 kwa matumiz ya kawaida serikal inachukua sh.2800
 
Mliacha ya msingi mkajadili migogoro ya chadema hiyo ndo zawadi ya krismasi na heri ya mwaka mpya kutoka serikali ya maccm

Nyambafu.......ninyi ndo kila uchwao mnashindia kwa waganda eti cdm ife leo unaona they have an impact to ur life mpaka wapaze sauti kwenye hili la umeme.........acheni unafiki watz
 
Mbona sijaelewa ? Total unit cost + Tax + Fixed amount +Tax. Tufahamisheni hii total cost na fixed cost ni nini ?
Fixed amount ni service charge ambayo hulipwa Mara moja kwa mwezi, total cost ni Jumla ya hela baada ya kujumlisha tax, fixed, unit cost.
kifupi ni kwamba cost ya hizo uni 8.7 ni elfu mbili Kama ilivyoonyeshwa kwenye list
 
Nguzo ulinunua, nyaya ulinunua, meter ulinunua na umeme unanunua. Je fixed cost unalipia nini?
 
naombeni kujuzwa vile wanavyosema kwa unit 70 gharama ni sh 100, ni vp wanafanya mahesabu ? nikiangalia hapo naona wamekata sh 307 kwa unit.
 
Hii ni mbaya sana kwakweli umeme haununuliki tena!

sasa watanzania tunaanza vp kuligomea hili coz jinsi tunavyosubiri na kuendelea kunung'unika bila kuliweka bayana tunazidi kuumia!
Hebu bac tuweke mikakati ya kugomea hili tupeane maazimio hapa kila mtu kule alipo aweze kufanya kitu.
 
Hii ni mbaya sana kwakweli umeme haununuliki tena!

sasa watanzania tunaanza vp kuligomea hili coz jinsi tunavyosubiri na kuendelea kunung'unika bila kuliweka bayana tunazidi kuumia!
Hebu bac tuweke mikakati ya kugomea hili tupeane maazimio hapa kila mtu kule alipo aweze kufanya kitu.

mi naanza kwa kutumia kuni na koroboi .nawaandikia tanesco waje watoe mita yao
 
naombeni kujuzwa vile wanavyosema kwa unit 70 gharama ni sh 100, ni vp wanafanya mahesabu ? nikiangalia hapo naona wamekata sh 307 kwa unit.

Hakuna chakuuliza hapo boss, invoice ndo hiyo japo juu hakuna chakuongeza! kabla ya kubadili ghara ilikua hiyo elfu 10 unapata unir 19.7 kwa mteja wa daraja hilo hapo juu pamoja na kodi zote ambayo nayo bado ni ghali sana!
 
Nimenunua umeme asubuhi hii. ni kweli kitu 8.7kWhrTUJADILIANE HATUA YA HARAKA YA KUCHUKUA SI KUKAA KIMYA. CCM HOYEE!!!!!!!!!!!1
 
Hii risiti amefuta namba ya mbele 2 ni 28 units hv umept faida gani kwa huu UZUSHI
 
kidogo ni shangae jamaa ubandike lisiti yenye utambulisho wako? ,lakini naona na wewe umejiongeza jina, id, metre no, refrence no vyote kwanza uliviondoa.
 
jamani hii ndo gharama za amani tuendelee kuipenda amani kwa kutoandamana na kuisifia ccm
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom