Kilio cha Mlalahoi: Kupanda kwa bei ya umeme wanasiasa mko wapi?

na bado huu mwaka utakuwa mgumu sana kimaisha kwa mfumo huu wa upandishaji holela wa vitu vinavyodrive sector zote kama umeme kwa sababu bidhaa zitapanda bei maradufu, huduma karibu zote zitapanda bei, juzi tu nilikuwa naangalia kipindi cha eatv kinaitwa kurasa wanaomiliki salon wanalalamika na kudai kwa unit kidogo wanazopata kwa sasa baada ya kulipia umeme nao watapandisha bei zao za salon. na mimi nafikiri ni wakati wa kuingia barabarani na kupinga kwa nguvu zote bei hizi mpya za umeme la sivyo cha moto tutakiona. kinachoniuma zaidi kauli za mawaziri kipindi gesi imegundulika tuliambiwa ndo itakuwa mkombozi kwa kuwa umeme utakuwa ni wa uhakika na nafuu, lakini mpaka sasa mgao bado upo na umeme umepanda maradufu. hii ndo Tanzania.
 
Watz tuna matatzo wakati wanatangaza mlihic wanatania au? Mi sioni haja ya kulalamika i saw it coming.
Hii tabia ya kusubir mambo yafike mbal ndo tulalamike sio sahih. Pale pale wakitangz inabid kuwakalia kooni.
 
Sasa ulitaka usilipe service charge? umeshafikiria gharama za usafiri na muda ulizopunguziwa kwenda kulipia bill yako TANESCO kila mwezi?

Hivi kumbe ndio maana Service Charge?

[pole sana hakika hujuhi kitu kuhusu Umeme, Waulize wenzio nini maana Service Charge.
 
Elfu kumi mwisho wa mwezi wakupe unit 28? Ondoa mawazo mgando wewe.

Yupo sahihii kiasi maana nimenunua mwingine hapa bila ya service charge nimepata 26.8 Units.

Kifupi ni majanga, tutegemee kila kitu kupanda kuanzia Vinywaji baridi mpaka saloon, kifupi sector yeyote inayotegemea Umeme lazima gharama za uendeshaji zipande.
 
Hii risiti amefuta namba ya mbele 2 ni 28 units hv umept faida gani kwa huu UZUSHI


Pole kwa ulimbukeni, na jitahidi usile ugali wa shikamoo..haujui hata umeme wa ten thou ulikua ni 18 units, wewe unakazana kusema amefuta 2 hapo kwenye receipt..poor you, mwambie baba akufukuze nyumbani
ukajitegemee pengine utajua bei za vitu..
 
Nguzo ulinunua, nyaya ulinunua, meter ulinunua na umeme unanunua. Je fixed cost unalipia nini?

na ukicheki kwenye makato ya mwisho wa mwezi,hiyo fixed cost nayo inalipiwa VAT na bado kule kwenye units unalipia VAT pia.Labda wataalam wa kodi mje mnielimishe kuhusu hili.Sielewi ni kwa nini fixed cost ambazo ni pesa za Tanesco zisizokuwa na return yoyote kwangu nizilipie VAT mimi.Hizi fixed costs hatuzielewi kwa kweli.Kwa nini ziwekewe VAT,kuna biashara gani ya faida kwangu mie mtumiaji wa nyumbani hadi uniumize na VAT wakati kuna maeneo kibao nalipia VAT ?halafu hapo hapo mwekezaji asiye mtanzania anasamehewa hizi kodi wakati yeye anatengeneza profit in terms of billions of dollars kwa manufaa yake binafsi na ukoo wake na nchi yake!Zamani nilikuwa nikiwashangaa mataifa ya Afrika magharibi kwa jinsi watu wasivyoheshimu mamlaka za nchi na kupindua serikali huku wakiwaburuza uchi mitaani marais wao akina Samuel Doe,William Tolbert n.k lakini leo sitashangaa mambo ya aina hii yakitokea nchini.Unyonyaji wa wananchi wa Tz,unakaribia provocation ambayo ni wachache wataendelea na uvumilivu.Tunahatarisha amani ya nchi kwa kuwanyonya maskini kupita ukomo.Viongozi wa nchi hii wamekaribia kujisahau kule kwa hatari kama alivyojisahau yule mfalme wa Ufaransa ambaye mkewe aliwashangaa watu kwenda ikulu kuomba mkate.Mnaofahamu habari hii mnaelewa nini kilitokea!
 
Kweli dada yng unabisha tu au unatetea kitu ili mladi umetetea!!

Ivi wewe hujui kwa kupanda bei Umeme bidhaa zote kasoro mazao ya shambani zitapanda bei? Vile vitu tulivyokua tunanunua Mia tano vitapanda mpk Mia 800 buku!

Kupanda kwa Umeme sio Km kutaathili matumizi ya Umeme majumbani la hasha! Kutaathili mahitaji ya kila siku ya mwananchi! Huo Umeme ata nikitumia taa moja sio mbaya! Ata Km nikitiza taarifa ya Habari sio mbaya! Aya Km nikinywa Maji ya moto sio mbaya! Ata nisiposaga juice sio mbaya! Na pasi Je? Au niende Job sio nadhifu? Hayo ni mambo mtu waweza jinyima!

Lakini kwa swala la mahitaji muhimu ya binadamu vitu vitapanda bei kutokana na ghalama za uzalishaji kuongezeka hasha nishati ya Umeme!

=Mradi.

Hata mazao ya shambani yatapanda. Hilo kumbuka.

Bado sioni sababu kwanini tulie tulie kila siku. Tunataka umeme lazima tujuwe una gharama zake.

Ngojeni gas ianze kuchimbwa kwa wingi tupate umeme nafuu au vipato viongezeke.

La sivyo, tutumie fursa hii kupata vyanzo mbadala vya umeme. Nyinyi wakati mnapiga kelele, wenzenu tayari wameshaanza kuleta vifaa vya umeme mbadala. Sisis tunangoja nini?:

Soma zaidi: Can This Lantern Put An End To Energy Poverty?
 
electricppp.gif


Tanzania kwa sasa tupo hapo karibia na UK.
 
Hatari sana, Mangi shop mtaani kwetu kapandisha bidhaa bei nilivomuuluza kw nn? Anasema umeme umepanda, kaaaaaazi kwelikweli, mafuta yakipanda bidhaa bei juu, nauli zikipanda bidhaa bei juu,Leo hii umeme, bidhaa bei juu, lol Mungu ibariki nchi Yang Tanzania
 
i think monopoly of tanesco in electricity should end now other big companies should be given right to generate,circulate and sell their own electricity
 
Ivi Serikali ya sisiem wala haina huruma na mpiga kura wake!!!!!!!?????
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom