Kili Music Awards 2011

Hajashinda mkuu,mi mwenyewe nilijua ndo utashinda wimbo huo wa ISHA na mamaye RUKIA lakini eti wamempa mzoefu Mzee Yusuph na JAHAZI yake....lol
Lakini kina Mzee Yusuph wana tuzo nyingi, hawa wachanga watahamasika na nini???

Mie basi tena!
 
Diamond anapafom sasa....hapo kwenye wimbo wa asili wameniacha hoi, nilikuwa sijui ndio nimejua leo kuwa Mpoki ana wimbo!!
 
KUMRADHI: Stage imeandaliwa OVYO KABISA. Inauma kusema hivi, lighting upuuzi mtupu, hivi kweli Kilimanjaro wanakosa kurekebisha vitu vidogo kama hivi? Tuzo utadhani ni ngazi ya kata kumbe za kitaifa!?!
 
Mpoki kushinda kumestua watu wengi na tunaendelea kuquestion integrity ya tuzo zenyewe. Lakini wabongo ndio walivyo ukiwapa nafasi ya kuamua lazima wakupe surprise!

Mtu anaimba mziki for funny anawashinda wanaoimba kama kazi na fani yao hata ubora wa video na majina katika tasnia yenyewe, mimbo yenyewe inayoshindanishwa ni utata pia
 
Wimbo bora wa RnB ulioshinda ni;

Nikikupata-Ben Paul................Mmmhhhhhh.Kawashinda Linah(Atatamani) na Z-Anto(Kisiwa cha Malavidavi)........

Halafu wasanii hawajui hata kuvaa kwenye matukia kama haya
 
lakini mpoki mwenyewe kasema kuwa anajiona kama mwanamke ambaye hakuwa mjamzito halafu ghafla akajifungua. kwahiyo ukitafsiri haya maneno ya mpoki mwenyewe utaona kuwa hata yy mwenyewe anajua hakushitali ila kuna ujanja ujanja wanafanya akina ruge hapo.

Wanamuziki werevu walishasanuka mapemaaaa! hata hivyo mafanikio ya msanii wa TZ hayawezi kupimwa kwa Tuzo za kipumbavu kama hizi za kilimanjaro Beer! Never!
 
Artistes JCB, Fid Q, Chidi BenzLanguage Swahili
Writer Jacob Makalla
Year 2010
Intro
ahhh...ahhhh
ohhh yeahhh..(shhhh!).. it\'s the remix
(shhhh!)...JCB....(ahhhh!).....Murder..!
(Tongwe Records Babyyyy)
Verse 1 (JCB)
Damu ilitapakaa baada ya ule mlio kulia PAAA,
Watu wote walisambaa hata walevi wa kwenye bar,
Sio polisi sio baunsa iliye kaa utashanga kwa nini mshkaji alizidi kumimina kwa kujiamini,
Amini usiamini akabaki tu na mimi,
Akanishikia bunduki kwa chini,
Akadai eti nimpe madini lasivyo ananipiga risasi kama sabini,
Anasura kama idi amini akarudi karibu atua tatu mpaka kabatini,
Akatamka HEYOO! nipo kazini nimetumwa mzigo au ujithamini,
Akanikanyaga kwa chini kikorofi bunduki tena akaikoki
Akasema kama simuonyeshi leo sio koki,jinsi alivyo akilenge ye akosi mikosi,
Kavaa koti jeusi jasusi,
Mikono nikaweka juu kuepuka nukx huku natukana mengi matusi...
Chorus X2
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa
Verse 2 (Fid Q)
Wanasema hugeuka mnyama sana anaposaka pesa
Cha ajabu anavuta bangi lakini hawazii magangstar
Hampaki rangi donkey ili ageuke kuwa zebra
Ndo maana kabla hajaikoki, JCB ali-surrender
Akajifanya hayuko na mie ili niipigie defender

.............
 
Wasanii wajifunze kwa akina Juma Kaseja na Nsajnigwa Shadrack..........Wamevaa vizuri sana,si kama huyo Ben Paul
 
Kili Music Awards 2011 Ni M'BORONGO WA NGUVU!!!, BURRREEE KABISA. Yanahitajika mageuzi ya ukweli ili kunusuru muziki wa Tanzania. Kwa Kwa "SHANGAZI" ya Mpoki kuwa wimbo bora wa Kiswahili !! ...halafu na makifi juu ...Tuendako si kwenyewe. Period
 
Back
Top Bottom