Kuelekea Tuzo za Muziki Tanzania (TMA): BASATA yaunda kamati maalumu ili kufanya TMA kuwa na hadhi ya kimataifa

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,313
TAARIFA KWA UMMA

KUANZA KWA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA KAMATI YA KITAIFA YA TUZO ZA MUZIKI TANZANIA (TMA)

Baraza la Sanaa la Taifa linapenda kuufahamisha umma wa Watanzania na wadau wote wa sanaa kuwa Kamati ya Kitaifa ya Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) imeanza rasmi kutekeleza majukumu yake kwa kufanya vikao vya kuweka mikakati ya pamoja itakayowezesha kufikia malengo tarajiwa kuelekea katika utoaji wa Tuzo za Muziki za Mwaka 2023 Tanzania.

Baraza linaufahamisha umma kuwa wanakamati wote wameteuliwa kimkakati ili kuhakikisha kuwa programu ya TMA inakuwa ya kimataifa kutokana na ubobevu wa wanakamati katika masuala ya utawala, masoko, usimamizi wa wasanii, na mawasiliano. Inatarajiwa kuwa sifa hizi za wajumbe zitawezesha kuunganisha TMA na tuzo zingine za kimataifa ndani na nje ya Bara la Afrika kama vile BET na MTV.

Kamati ya Tuzo za Muziki za Mwaka 2023 Tanzania iliyozinduliwa rasmi tarehe 03

Novemba 2023 inaundwa na wanakamati wafuatao ambao ni Watanzania na raia mmoja wa Afrika Kusini:​

i) David Minja (Mwenyekiti)
Ni mtaalamu wa kimataifa wa biashara na masoko. Ana mafanikio makubwa katika historia ya tuzo za muziki Tanzania tangu wakati TMA zikiitwa Kilimanjaro Tanzania Music Awards. Pia, ndiye mwanzilishi wa "TMA Winners Music Tour".
ii) Christine Mosha "Seven" (Makamu Mwenyekiti)
Ni Mkuu wa Masoko na Maendeleo ya Wanamuziki Afrika Mashariki wa Kampuni ya Sony Music Entertainment; Mkurugenzi wa Kampuni ya Rockstar Africa; na Mkuu wa Biashara wa Kituo cha MTV Base Africa (Dar es salaam). Amewahi pia kuwa mtangazaji wa East Africa Radio na TV, na Redio ya Clouds FM.​

iii) Mrisho M. Mrisho (Katibu)
Ni ofisa mwandamizi katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na ana uzoefu katika masuala ya masoko, fedha na biashara. Pia, ni mwanzilishi wa wazo la kurejesha TMA 2021, na alikuwa mratibu wa TMA 2021 na 2022.​

iv) Paul Matthysse "Pfunk" (Mjumbe)
Ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bongo Records na ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika shughuli za sanaa na muziki hapa nchini.
v) Chris Torline (Mjumbe)
Ni raia wa Afrika Kusini na ni kiungo muhimu kati ya TMA na tuzo za kimataifa kama BET na vyombo vya habari vya kimataifa kama MTV.
vi. Natasha Stambuli (Mjumbe)
Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Transs Net inayosimamia uuzaji wa kazi za muziki kidigitali wa Kampuni ya Boomplay.Pia, ni mwanachama wa Akademia ya Tuzo za Grammy.

BASATA linatoa wito kwa wadau wote wa sanaa kuwapa wanakamati ushirikiano wa kutosha pale watakapowafikia ili kuipeleka sekta ya sanaa nchini kwenye anga za kimataifa kwa mustakabali bora wa kiuchumi na kijamii Tanzania.​
Dkt. Kedmon Mapana
KATIBU MTENDAJI

basata.tanzania-20231111-0001.jpg

basata.tanzania-20231111-0002.jpg


basata.tanzania-20231111-0003.jpg
 
Back
Top Bottom