Mhache
JF-Expert Member
- Jun 20, 2008
- 345
- 24
Leo wanafunzi wa darasa la saba wapatao zaidi ya milioni moja wanafanya mtihani wa kumaliza shule. Hii ni hatua muhimu sana kwao. Matokeo ya mtihani huo ndio utakaowapa wahitimu hao mwelekeo wa maisha. Kwani wapo watakaoendelea na masomo na wapo watakao rudi majumbani mwao bila chochote.
Mimi kama mdau wa elimu ninawatakia mtihani mwema na wenye mafanikio mema. Yapo mambo ambayo yasipoangaliwa yanaweza kuwaharibia matokeo yao. Mojawapo ni kufutiwa matokeo kutokana na kuonyeshwa nitihani na walimu wao au wasimamizi wa mitihani hiyo. Ninaomba walimu na wasimamizi wa mitihani hiyo wafuate sheria na taratibu wasije kuwaharibia watoto wetu matokeo yao. Na watakaobainika wachukuliwe hatua kali za kisheria.