Ufaulu Darasa la Saba

Nimepitia matokeo ya darasa la Saba shule za serikali zinazofundisha Kwa mtaala wa kiingereza zimekuwa zikifanya vizuri, Sasa kama watoto lugha ya kiingereza wanaielewa kwa urahisi kwanini tusitumie huu mtaala Kwa shule zote?
Matokeo yametoka?
 
Nimepitia matokeo ya Darasa la Saba shule za serikali zinazofundisha Kwa mtaala wa Kiingereza zimekuwa zikifanya vizuri, Sasa kama watoto lugha ya Kiingereza wanaielewa kwa urahisi kwanini tusitumie huu mtaala Kwa shule zote?
Hizi shule zipo facilitated sana
 
Malengo ya Mwl. Nyerere kutumia kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ilikuwa kuwesha watanzania (Elimu msingi) kuwa mahili kuongea kiswahili, umoja na kuondoa ukabila, Sasa hili nadhani limeshafanikiwa Kwa asilimia miamoja, Sasa nawashagaa watunga sera, mitaaala kuendelea kushikilia kutumia lugha ya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia (shule za msingi za serikali) wakati huohuo shule za binafsi zitumia lugha ya kiingireza( English medium) Kwa jicho lingene nikama kutengeneza Tabaka ndani ya nchi Moja. Jambo alilopinga Mwl. Nyerere. Maoni yangu ndani ya huu mtaala mpya shule za serikali zingebadili lugha ya kufundishia kuwa English kwakuwa walimu wapo, kiswahili kubaki ni somo la kujifunza kama wanvyofanya shule binafsi.
 
Back
Top Bottom