Dubo
JF-Expert Member
- Aug 16, 2010
- 322
- 17
RAIS Jakaya Kikwete ni wa 10 kati ya viongozi 52 wa Afrika kwa kuchapa kazi katika mwaka 2010 kwa mujibu wa jarida la East African.
Katika toleo lake la Desemba 27, 2010 hadi Januari 2 mwaka huu, jarida la East African limetoa orodha yake kulingana na ufanisi wa marais wa Afrika katika nyanja mbalimbali za maendeleo kwa mwaka 2010.
Kwa mujibu wa jarida hilo, aliyeshika nafasi ya kwanza kwa ubora ni Waziri Mkuu wa Mauritius, Navinchandra Ramgoolam, akifuatiwa na Rais wa Jamhuri ya Cape Verde, Pedro Verona Rodriques Pire.
Nafasi ya tatu imeshikwa na Rais wa Botswana, Seretse Ian Khama wakati ile ya nne imeshikwa na Rais wa Ghana, John Evans Atta Mills.
Wengine waliofuata ni Hifikepunye Pohamba wa Namibia (wa tano), Jacob Zuma wa Afrika Kusini (wa sita), James Michel wa Shelisheli (wa saba), Amadou Toure wa Mali (wa nane) na Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone (wa tisa).
Baada ya Jakaya Kikwete wa Tanzania kushika nafasi ya kumi, anayefuata ni Ellen Johnson-Sirleaf wa Liberia (11) na Rupiah Banda wa Zambia (12).
Walioshika nafasi za mkiani ni Robert Mugabe wa Zimbabwe (47), Sheikh Ahmed wa Somalia (48), Idriss Deby Itno wa Chad (49), Teodoro Mbasogo wa Equatorial Guinea (50), Omar Al-Bashir wa Sudan (51) na Isaias Afweriki wa Eritrea aliyeshika nafasi ya mwisho.