Kikwete wa 10 barani Afrika

Dubo

JF-Expert Member
Aug 16, 2010
322
17
RAIS Jakaya Kikwete ni wa 10 kati ya viongozi 52 wa Afrika kwa kuchapa kazi katika mwaka 2010 kwa mujibu wa jarida la East African.

Katika toleo lake la Desemba 27, 2010 hadi Januari 2 mwaka huu, jarida la East African limetoa orodha yake kulingana na ufanisi wa marais wa Afrika katika nyanja mbalimbali za maendeleo kwa mwaka 2010.
Kwa mujibu wa jarida hilo, aliyeshika nafasi ya kwanza kwa ubora ni Waziri Mkuu wa Mauritius, Navinchandra Ramgoolam, akifuatiwa na Rais wa Jamhuri ya Cape Verde, Pedro Verona Rodriques Pire.

Nafasi ya tatu imeshikwa na Rais wa Botswana, Seretse Ian Khama wakati ile ya nne imeshikwa na Rais wa Ghana, John Evans Atta Mills.

Wengine waliofuata ni Hifikepunye Pohamba wa Namibia (wa tano), Jacob Zuma wa Afrika Kusini (wa sita), James Michel wa Shelisheli (wa saba), Amadou Toure wa Mali (wa nane) na Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone (wa tisa).

Baada ya Jakaya Kikwete wa Tanzania kushika nafasi ya kumi, anayefuata ni Ellen Johnson-Sirleaf wa Liberia (11) na Rupiah Banda wa Zambia (12).

Walioshika nafasi za mkiani ni Robert Mugabe wa Zimbabwe (47), Sheikh Ahmed wa Somalia (48), Idriss Deby Itno wa Chad (49), Teodoro Mbasogo wa Equatorial Guinea (50), Omar Al-Bashir wa Sudan (51) na Isaias Afweriki wa Eritrea aliyeshika nafasi ya mwisho.
 
Hata hiyo nafasi ya tisa haistahili kwani hakuna alichoifanyia tanzania kwa miaka 5 aliyokaa madarakani zaidi ya ufisadi na wizi wa halaiki.
 
Hii yaonyesha kabisa wanaompinga JK wana lao jambo, na hii ni taasisi ya nje ambayo imefanya kazi yake independent kabisaaa
 
Anastahili jamani,tusikatae sababu ya itikadi,ushabiki na mzugo wa kisiasa.
 
kama huyu wetu yuko nafasi ya kumi na hali ya tz ndiyo hii, basi huko kwa walioshika kuanzia ya 11 kuendelea ni sawa na jehanam
 
Orodha sahihi

1. Abdulazizi boutafrika (algeria).

2. Kamati ya uchaguzi ivorikosti (code voire).

3. Utafiti wa east africa.................................................
 
Na tanzania ni nchi ya ngapi kiuchumi Afrika ? Au imepanda/imeporomoka mpaka kuwa ya ngapi kiuchumi ?
Je mfumuko wa bei umeshuka kwa asilimia ngapi ?Au je ni nchi ya ngapi kwa kudhibiti rushwa ?thamani ya pesa ikoje ,hali ya maisha ya wananchi wake nikiwemo mimi na wewe ,majomba,wapwa na wajukuu zetu zikoje,wanakwenda choo mara ngapi kwa wiki ?wakiugua
wanachimba mizizi au wanatibiwa hospitali.

Waambie watupe taarifa kwa maswali hayo hapo juu.
 
Hii yaonyesha kabisa wanaompinga JK wana lao jambo, na hii ni taasisi ya nje ambayo imefanya kazi yake independent kabisaaa

Hao wa nje ndio wana lao jambo, kwa sababu JK amewapa nafasi ya kuja kufanya ufisadi hapa ndio wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa! Ndo maana hawasemi huo wanaodai ni ubora ni upi hasa? Je, maisha bora aliyoahidi 2005 yako wapi?
 
Tusishabikie hizo riport za nje maana hata wakati wa kampeni walikuwa na report nzuri kila kukicha mara uchumi umekuwa, mara shillingi imepanda na vingine vingi, sisi tunaangalia maisha ya kila mtu kwa pamoja na kuzingatia huduma muhumu za jamii je zipo katika hali gani,hawa mafisadi wamefikishwa wapi au wanaendelea kutuibia kama vile wao sio watanzania
 
Hebu angalia na unijuze Rais Ghabo wa Ivory cost ni wa ngapi pia Mwaiki Kibaki na Mseveni wa Uganda
 
Kwa waafrika raiksi mchapakazi, ni yule mwenye uwezo wa kuzungukazunguka duniani akiomba misaada na vyandalua!
 
angalia hao walioshika mkia na ujiulize, hizi ni propaganda za magharibi yani mkwele wa 10??? hahaha mkwele rais bora afrika mashariki?? amemzidi hata odinga, kibaki, kagame!!!

hizi ni tafiti za gazeti la uhuru
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom