Paul Barthélemy Biya’a ndie Rais mzee zaidi barani Afrika

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
80
96
paul_biya05-800x531.jpg

Paul Biya, Rais wa Cameroon tangu mwaka 1982

Jina lake kamili ni Paul Barthélemy Biya’a bi Mvondo.

Alizaliwa Februari 13, 1933 katika kijiji cha cha Mvomeka Nchini Cameroon, kwa sasa ana umri wa miaka 90.

Amekuwa Rais wa Cameroon tangu mwaka 1982 baada ya Rais Ahmadou Ahidjo kujiuzulu ghafla, Biya, akiwa Waziri Mkuu kwa miaka 7, alikuwa mrithi wake wa Kikatiba. Aliapishwa kuwa Rais Novemba 6, 1982.

Biya alichaguliwa tena kuwa Rais katika Chaguzi zilizofanyika mwaka 1984 na 1988, ambapo alikuwa mgombea pekee.

Mwaka 1984 alifanyiwa jaribio la Mapinduzi ambalo halikufanikiwa, kulikuwa na tuhuma kwamba Rais aliyejiuzulu, Ahidjo au wafuasi wake wamehusika na njama hiyo.

Mwaka 1985, katika kongamano la chama cha UNC, Biya alikivunja chama hicho na akaunda chama kingine cha Cameroon People’s Democratic Movement (CPDM) ambacho yeye alijiteua kuwa Kiongozi Mkuu wa Chama.

Ingawa Biya aliunga mkono mabadiliko ya Kidemokrasia alipochukua madaraka kwa mara ya kwanza, alikuja kubadili upepo baada ya jaribio la mapinduzi dhidi yake mwaka 1984. Hata hivyo, Nchi ilifanya uchaguzi wake wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1992.

Alifanikiwa kushinda tena Chaguzi za mwaka 1997 na 2004, akiwa ameongeza muda wa Mihula ya Utawala wa Urais kutoka miaka 5 hadi miaka 7.

Mwaka 2008, akiwa bado ni Rais, aliondoa Ukomo wa Rais kukaa Madarakani ili apate fursa ya kutawala kwa muda anaotaka.

Mwaka 2018 wakati wa Uchaguzi Mkuu, alishinda tena Urais kwa 80% dhidi ya Mgombea wa Upinzani, Maurice Kamto.

February 2022 alitimiza miongo minne Madarakani, ninamaanisha alikuwa ametawala Taifa hilo kwa muda wa miaka 40. Novemba 6 mwaka 2023 alimitiza miaka 41 akiwa Rais wa Taifa hilo.

Hajaishia hapo, Paul Biya anatajwa kuwa atagombea tena Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Kiongozi huyu anashika nafasi ya 7 katika orodha ya Marais 10 wazee zaidi Duniani.

Pia, ndiye Rais wa pili anayetawala kwa muda mrefu akimfuatia Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa Equatorial Guinea anayetawala tangu mwaka 1979.
 
View attachment 2832897

ya Marais 10 wazee zaidi Duniani.

Pia, ndiye Rais wa pili anayetawala kwa muda mrefu akimfuatia Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa Equatorial Guinea anayetawala tangu mwaka 1979.
Huyu si ndiye yule mzee wa kujamba jamba
 
Paul Biya kuna miaka huwa anatawala Cameroon kwa muda mrefu kutoka hotelini Geneva, Uswizi ambapo gharama zake hufikia kadiri ya dola za Kimarekani 40,000 kwa siku.

Mwaka 2008, akiwa bado ni Rais, aliondoa Ukomo wa Rais kukaa Madarakani ili apate fursa ya kutawala kwa muda anaotaka.
Inanikumbusha mwenyekiti wa chama kimoja cha siasa hapa kwetu alifanya hivyo hivyo ili awe mwenyekiti wa milele!
 
View attachment 2832897
Paul Biya, Rais wa Cameroon tangu mwaka 1982

Jina lake kamili ni Paul Barthélemy Biya’a bi Mvondo.

Alizaliwa Februari 13, 1933 katika kijiji cha cha Mvomeka Nchini Cameroon, kwa sasa ana umri wa miaka 90.

Amekuwa Rais wa Cameroon tangu mwaka 1982 baada ya Rais Ahmadou Ahidjo kujiuzulu ghafla, Biya, akiwa Waziri Mkuu kwa miaka 7, alikuwa mrithi wake wa Kikatiba. Aliapishwa kuwa Rais Novemba 6, 1982.

Biya alichaguliwa tena kuwa Rais katika Chaguzi zilizofanyika mwaka 1984 na 1988, ambapo alikuwa mgombea pekee.

Mwaka 1984 alifanyiwa jaribio la Mapinduzi ambalo halikufanikiwa, kulikuwa na tuhuma kwamba Rais aliyejiuzulu, Ahidjo au wafuasi wake wamehusika na njama hiyo.

Mwaka 1985, katika kongamano la chama cha UNC, Biya alikivunja chama hicho na akaunda chama kingine cha Cameroon People’s Democratic Movement (CPDM) ambacho yeye alijiteua kuwa Kiongozi Mkuu wa Chama.

Ingawa Biya aliunga mkono mabadiliko ya Kidemokrasia alipochukua madaraka kwa mara ya kwanza, alikuja kubadili upepo baada ya jaribio la mapinduzi dhidi yake mwaka 1984. Hata hivyo, Nchi ilifanya uchaguzi wake wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1992.

Alifanikiwa kushinda tena Chaguzi za mwaka 1997 na 2004, akiwa ameongeza muda wa Mihula ya Utawala wa Urais kutoka miaka 5 hadi miaka 7.

Mwaka 2008, akiwa bado ni Rais, aliondoa Ukomo wa Rais kukaa Madarakani ili apate fursa ya kutawala kwa muda anaotaka.

Mwaka 2018 wakati wa Uchaguzi Mkuu, alishinda tena Urais kwa 80% dhidi ya Mgombea wa Upinzani, Maurice Kamto.

February 2022 alitimiza miongo minne Madarakani, ninamaanisha alikuwa ametawala Taifa hilo kwa muda wa miaka 40. Novemba 6 mwaka 2023 alimitiza miaka 41 akiwa Rais wa Taifa hilo.

Hajaishia hapo, Paul Biya anatajwa kuwa atagombea tena Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Kiongozi huyu anashika nafasi ya 7 katika orodha ya Marais 10 wazee zaidi Duniani.

Pia, ndiye Rais wa pili anayetawala kwa muda mrefu akimfuatia Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa Equatorial Guinea anayetawala tangu mwaka 1979.

Labda anatafuta apate record ya Dunia. Aingie kwenye kumbukumbu kama mtu wa kipekee.

Kamuzu Banda alitawala mpaka akiwa na umri wa miaka 88. Huyu tayari amekwishampita.
 
Back
Top Bottom