Kikwete na Davos, Kagame na LA Times!

Nilikuwa namjibu Mzizimkavu.
Utakaa mtandaoni kulaumu, hiyo haitasaidia. Nia yangu ni kujaribu kutafakari jinsi Rwanda na Tanzania zinavyopata misaada kutoka nje. Rwanda asilimia ya misaada inayopata (as a percentage of GDP) ni zaidi kidogo ya Tanzania.

Sasa kwanini Kagame azungumziwe humu kama ni rais asiyependa misaada wakati kibakuli anatembeza kama hana akili nzuri?

Not True, as per GDP may be fine, but i don't remember well how? The fact is, Tanzania ni nchi ya tatu Duniani kwa kuombaomba. Rwanda is not in that shame list. So where do you get the gravity to come up with such wrong premises to jump to that obvious wrong conclusion? Au wewe in Jakaya Mrisho Kiwete?
 
rwanda kupunguza umaskini kwa kutegemea mauzo ya kahawa a big joke!rwanda ndio muuzaji mkubwa wa madini haramu toka congo km hamjui
 
[Yaani niache kujipodoa nikae chini kusoma insha. Babu usituchoshe eeh. Kama vipi jaribu kuifupisha hiyo habari yako vinginevyo hupati mchango wangu ng'oooo...... }

  • na hili ndo tatizo la watanzania kushindwa kusoma habari yote ukapata kile kinachohusu maada. kiukweli nimeisoma sana hii habari na inatoa picha kamili ya viongozi wetu wa afrika akiwemo mtalii wetu jk. labda tumwombe Mungu atupe kiongozi mwenye maamzi magumu! ]
 
makala ni nzuri sana,tuache utegemezi,rasilimali nyingi tunazo tuzitumie jamani.ONE OF THE MOST GREATFUL ARTICLE
 
Yaani niache kujipodoa nikae chini kusoma insha. Babu usituchoshe eeh. Kama vipi jaribu kuifupisha hiyo habari yako vinginevyo hupati mchango wangu ng'oooo......
Hee we dada utamu, hiyo ndo tabia pia ya rais wako, hapendi kusoma vitu kabisa, mamikataba yakiisha kuwa na mapeji mengi tu huwa hola hasomi yeye anasaini tu, anyway usije ukawa ndo Dada MWanaasha, so like father like son.
 
Kwanza kabisa (nataka twende poin by point) si kweli kuwa Tanzania inapokea misaada mingi zaidi ya Rwanda.

Kwa taarifa yako Tanzania ni nchi ya 3 kwa kuomba omba duniani, ya kwanza ni Afganistan na ya pili ni Iraq then sisi, so Rwanda kwa takwimu hizo haipo and for your infor hata kwenye 10 bora ya kuomba omba Rwanda haipo.
 
Johnson Mbwambo

SIKU hizi nina muda wa kutosha kufuatilia majadiliano mbalimbali katika tovuti kadhaa kubwa duniani zinazozungumzia masuala ya Afrika na watawala wetu.

Baadhi ya mijadala hiyo ya mitandaoni iliyonivutia, hivi karibuni, ni ile iliyomhusu Rais wetu, Jakaya Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda.


Mjadala kuhusu Kikwete ulihusu kile alichokizungumza kwenye mkutano wa hivi karibuni wa uchumi uliofanyika huko Davos, Uswisi na ule wa Kagame ulihusu habari zilizoandikwa kwenye gazeti la
Los Angeles Times la huko Marekani kuhusu Rwanda.


Kwenye mjadala kuhusu alichokisema Kikwete huko Davos, wachangiaji wengi walimlaumu kwa mchango wake ‘mwepesi’ kuhusu nini hasa kinacholitatiza bara la Afrika lishindwe kuendelea, na hivyo kuendelea kutegemea misaada ya nchi tajiri duniani.


Katika mkutano huo wa Davos, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, aliwaomba marais wa Afrika waliohudhuria mkutano huo kuueleza mkutano ni kwa nini hali hiyo inaendelea kulikumba bara lao.

Walitangulia kujieleza Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Raila Odinga wa Kenya, na ndipo Rais wetu Jakaya Kikwete alipopewa fursa kuzungumza.

Kwa mujibu wa wachangiaji wengi kwenye mitandao hiyo, Zuma na Raila walijitahidi kujieleza vizuri; lakini Rais wetu, Jakaya Kikwete, ‘aliboronga’, na kwamba aliishia tu kujenga dhana kwamba nchi za Afrika haziwezi kuendelea bila ya misaada ya mataifa tajiri!

Baadhi ya wachangiaji kwenye mtandao waliwalaumu wasaidizi wa Rais Kikwete kwamba hawakumuandalia kitu kizito cha kuzungumza

kwenye mkutano huo, na hivyo kumwachia azungumze mwenyewe kutoka kichwani mwake.

Hicho alichokisema Kikwete huko Davos nacho kimewekwa (neno kwa neno) kwenye mitandao na mwananchi mmoja.
Mtazamo huo wa Kikwete huko Davos kwamba Afrika haiwezi kuendelea bila misaada ya mataifa tajiri ndio uliomuudhi Mwingereza

mmoja ambaye alimshutumu rais wetu gazetini; huku akitumia lugha ambayo haipendezi – lugha ambayo unaweza kusema ni sawa na kupiga chini ya mkanda.


Huyo Mwingereza alidai alifanya kazi UNDP hapa Tanzania na anaijua vizuri nchi yetu. Kwa mtazamo wake, Kikwete ni rais dhaifu kiutendaji kuliko wengine wote tuliopata kuwanao.


Alichokisema bwana huyo dhidi ya Kikwete kiliwekwa hata kwenye mtandao wa hapa nchini wa
Jamiiforum, na watu wamekuwa wakisambaziana habari hiyo hapa nchini kwa njia ya intaneti.

Labda niweke wazi mapema kabisa kwamba nami naungana na wale wote wanaotofautiana na Rais Kikwete kuhusu kile alichokizungumza kule Davos.

Si kweli kwamba Afrika haiwezi kuendelea bila kusaidiwa na mataifa tajiri, na si kweli kwamba Afrika haiwezi kulitupilia mbali bakuli la ombaomba ambalo imekuwa ikilitembeza Ulaya na Marekani kwa zaidi ya miaka 50 sasa.


Lakini nisemi pia kwamba sikushangazwa na kauli hiyo ya Kikwete huko Davos; kwani miaka sita au saba hivi ya uongozi wake, imetuthibitishia sote kuwa si muumini wa dhana ya kujitegemea.


Na ndiyo maana alikwenda Davos na kulalamika ili tuonewe huruma na Wazungu kwa kutamka kwamba Waafrika tunaishi maisha ya shida mno
(hand to mouth) na tunahitaji kusaidiwa!


Najua jambo hili kwamba hatuwezi kuendelea bila misaada ya Wazungu linakera baadhi yetu, na ndio maana mimi binafsi sichoki kumtolea mfano Rais Kagame wa Rwanda kama mmoja wa marais Afrika anayethibitisha kwamba nchi inaweza kupata mafanikio katika vita yake dhidi ya umasikini bila misaada ya Wazungu.


Mwezi uliopita niliandika katika safu hii kuhusu mafanikio makubwa ambayo Serikali ya Rwanda imeyapata katika kampeni yake ya kutokomeza nyumba za udongo katika nchi hiyo, na kuwaomba watawala wetu wakajifunze Rwanda kwa Kagame.

Makala hiyo ilipokelewa vyema na wasomaji wangu wengi, lakini wako wachache waliotofautiana nami; huku wengine wakinipinga kwa

kutumia lugha chafu ikiwa ni pamoja na wanaoishi Ughaibuni waliosema eti mimi ni Mtutsi. Mpare na Mtutsi wapi kwa wapi jamani?!

Ni kwa sababu ya hao walionipinga kuhusu Kagame nilifuatilia kwa hamasa kubwa huu mjadala mwingine mitandaoni juu ya kile

kilichoandikwa na gazeti la
Los Angeles Times la Marekani kuhusu Kagame.

Serikali ya Rwanda ilitangaza, hivi karibuni, kwamba imefanikiwa kupunguza umasikini kwa asilimia 12 katika kipindi cha miaka sita iliyopita; yaani imeushusha umasikini kutoka asilimia 57 hadi asilimia 45.

Mafanikio hayo yamechukuliwa kuwa ni ya aina yake duniani; huku gazeti hilo likiyaita
; one of the most stunning poverty drops in the world.


Ni kwa sababu hiyo
, Los Angeles Times lilimtafuta mmoja wa wachumi wanaoheshimika duniani anayeitwa Paul Collier ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Uchumi wa Dunia katika Chuo Kikuu cha Oxford na kumuomba ufafanuzi wake juu ya mafanikio hayo ya haraka ya Rwanda.


Matokeo ya mazungumzo hayo ni kuchapishwa kwa habari hiyo kwenye
Los Angeles Times iliyobeba kichwa kinachosomeka hivi: How did Rwanda cut its poverty so much? Habari hiyo iliwekwa katika mitandao kadhaa na ikawa ndio chanzo cha majadiliano hayo mitandaoni.


Kimsingi, mchumi huyo wa Oxford University anataja sababu mbili kubwa zilizoiwezesha Rwanda kupata mafanikio hayo makubwa ndani ya miaka sita.


Sababu ya kwanza aliyoitaja ni bei nzuri ya kahawa katika soko la dunia, na kwamba Rwanda iliitumia vizuri fursa hiyo.

Paul Collier anaeleza kwamba Serikali ya Rwanda ilielekeza mapesa iliyoyapata kutoka katika mauzo yake ya nje ya kahawa kwenye miradi ya maendeleo vijijini.

Kama hivyo ndivyo, Mtanzania unashindwa kujizuia kujiuliza; sisi Tanzania tulikuwa wapi tusifaidike na bei hiyo nzuri ya kahawa katika soko la dunia?


Lakini si vigumu kulipata jibu la swali hilo hasa katika mazingira ambayo tunaambiwa kuwa kahawa yetu mkoani Kagera inavushwa kila mwaka kuingizwa nchini Uganda, na kwamba ni Uganda ndio inayoiuza nje kwenye soko la dunia!

Lakini sababu ya pili iliyotajwa na Paul Collier ni kwamba Rwanda ina rais mwadilifu na mchapakazi kweli kweli. Kwa maneno yake mwenyewe Collier alitamka hivi: The President (Kagame) runs a tight ship within government built on performance rather than patronage”.

Msomi huyo wa Oxford University pia alimsifu Kagame kwa kujenga utamaduni wa uchapaji kazi nchini Rwanda, na kwa kuwapangia mawaziri wake viwango wanavyopaswa kuvifikia kila mwaka, na wasiovifikia huwajibishwa.


Si hivyo tu, msomi huyo alisema kwamba Rwanda ndio nchi pekee katika bara la Afrika inayokaribia, japo kidogo, njia iliyofikiwa na nchi za Mashariki ya Mbali kupata maendeleo ya haraka. Alisema hivi:


“Basically, President Kagame built a culture of performance at the top of the civil service –minister well paid but given targets. Rwanda is the nearest that Africa gets to an East Asian-style developmental state.”


Hivyo ndivyo mkurugenzi huyo wa Oxford University anavyomwona Kagame na Rwanda yake, na sisi tuliobahatika kuitembelea Rwanda ndivyo pia tunavyomwona Kagame.


Nirudie kusema tena kwamba Kagame ni mfano hai unaothibitisha kwamba Afrika inaweza kuendelea bila ya kutegemea misaada ya Wazungu; kitu ambacho Rais wetu, Jakaya Kikwete, hakiamini; kama alivyotuthibitisha tena kwa kauli yake ile tata kule Davos.


Kwa hiyo, tunachohitaji Afrika ni kuwa na marais wa aina ya Paul Kagame, na si wa aina ya Jakaya Kikwete na wenzake.

Hawa (kina Kikwete na marais wenzake Afrika) ndio wale waliofurahia na kuchekelea, hivi karibuni, kule Addis Ababa, Ethiopia wakati wa uzinduzi wa jengo la makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) lililojengwa na Serikali ya China kama ‘msaada’ kwa Waafrika.

Kina Kikwete na wenzake hawakuona kuwa ni aibu kubwa kwa AU kujengewa hata ofisi zake na China wakati umoja huo umekuwepo kwa miaka zaidi ya 40!

Kama katika historia ya miaka zaidi ya 40 ya umoja huo, wameshindwa hata kujijengea ofisi tu, watamudu nini?
Na wala marais wale wa Afrika hawakutambua hata kuwa kujengewa jengo hilo na Wachina ni aina fulani ya “rushwa”!

Wangelijua kwamba ni aibu na ni ‘rushwa’ ya aina fulani inayotolewa na nchi hiyo inayosomba na kunufaika na maliasili za Afrika; achilia mbali kubwaga bidhaa zake dhaifu kwenye bara hilo, wasingechekelea walivyochekelea wakati wa uzinduzi ule!

Ni rais mmoja tu barani Afrika ambaye hakuchekelea. Yeye aliiona hiyo kuwa ni aibu kubwa kwa bara letu la Afrika na alitamka hivyo.

Rais huyo ni Paul Kagame wa Rwanda, na ndiyo maana sikushangaa
Los Angeles Times likimmwagia sifa kemkem.

Hii ndio simulizi yangu ya leo kuhusu ya Jakaya Kikwete huko Davos na ya Paul Kagame huko Los Angeles (LA), lakini nihitimishe hivi:

Kwa miaka 50 tumekuwa tukipokea misaada kutoka kwa Wazungu lakini tumeshindwa kuitumia kujiletea maendeleo na pia imetufanya tushindwe kujitegemea.


Utegemezi huo umetubwetesha kiasi kwamba (kwa mfano) tukipewa msaada wa boti ya uvuvi, mathalan na Sweden, tutataka pia fedha za kununulia mafuta ya boti hiyo zitoke pia Sweden! Hicho ndicho kiwango cha utegemezi tulichokifikia.


Ndugu zangu, tumebweteshwa mno na misaada ya Wazungu. Ole wetu siku Wazungu watakapoanza kutuchoka. Na siku hizo hazipo mbali; maana tumeshaanza kuziona dalili.
Tafakari.

nduku nakupongeza kwa thread nzuri @least sasa jukwaa linarudi ktk hadhi yake si ya CCM VS CDM,
hapo nipohighlight pamenikuta mimi c zamani sana, ckumuja tukiwa na wafanyakazi wenzangu tulikwenda kupata lunch ktk mgahawa mmja mjini , tulikuwa watatu, mtz ni pekeyangu, mmja mtchad, mwingi mseden,sasa yule msweden alikuwa ameagiza chakula cha kikwao(chakula cha Kiswedish), hivyo kilichuka mda kuandaliwa, na ktk na haraka ya kurudi officn ikabidi aombe kifungwe kama take away, jamaa wa mgahawa wakamwambia bei itabidi iongezeke tofauti na kula palepale, hapo ndipo balaa lilipokuja,jamaa alilalamika, akudhihaki system nzima ya biashara ya tz, mi nilikuwa kimya cna cha kusema, sasa yule mtchad ktk kumpoza akamwambia kuwa achukue kwanza anabahati sana, yupo tz na anapata chakula cha kiswedish, yeye ameshindwa kabisa kupata chakula cha Kitchad, jamaa kwa hasira alimjibu na namnukuu,"What did you say!! thats bullshit................do you know how much money my government............the Swedish government has invested in this country......... and where does that money come from............from our hard working........ Sweden is among the leading donors in Tanzania, got that"

nilichojifunza nikwamba raia wa hao tuanaowaita wafadhili, wameshachoka na pesa zao kupelekwa kwa watu wenye uwezo wa kujihudumia kama Afrika, sasa cjui wachoke mara ngapi, dalili za kuchoka ndio hizo za kuhalalisha ushoga bila hivyo tunakata misaada.............sometimes inafedhehesha sana kuwa mwafrika ............ianuma lakini utafanyaje.
 
Sitakubali. That is not an issue here.
Umeleta hoja kuwa Rwanda haitegemei misaada kama Tanzania.
Naomba ulete data hapa. According to WB, Tanzania ina Poverty head count ratio of 34% right now.
Na Rwanda ina 44.9%.
Misaada kwa tanzania tangu 2007 ni asilimia 13.7 ya total GDP.
Misaada kwa Rwanda ni asilimia 17.9 ya total GDP.

mi nadhani hapa lengo la mleta mada si kulinganisha hali ya utegemezi wa rwanda na tanzania, umasikni wa rwanda na tz, watz tujifunze kutafsiri mada kabla ya kuchangia ili kuepusha malumbano yasiyo ya msingi, tujitahidi kuextract intention ya mtoa mada.........mtoa mada amekusudia kutuambia nini..........hata kama ameteleza kidogo msahihishe with manners....c kumponda kama kaandika ujinga mtupu wakati mtu katumia mda mwingi kukuletea jambo la kukuongezea weledi ktk masuala mbalimbali.

Wale wavivu wa kusoma mada ndefu ndio wanaodhibitisha zana ya mkwele ya kuwa hatuwezi kuendelea bila ya misaada.........maana tunataka virahisi tu................., habu tu watu wa KAZA ROHO UMEZE WEMBE,, sio unajibweteka tu.
 
Not True, as per GDP may be fine, but i don't remember well how? The fact is, Tanzania ni nchi ya tatu Duniani kwa kuombaomba. Rwanda is not in that shame list. So where do you get the gravity to come up with such wrong premises to jump to that obvious wrong conclusion? Au wewe in Jakaya Mrisho Kiwete?
Kama nchi yenye eneo kama la mkoa mmoja wa tanzania, ni ukosefu wa elimu kulinganisha misaada in terms of the total amount.

Kwa mfano, only 6% ya kenya's GDP is foreign aid. Hivyo naweza ku-expect Raila akaongea hayo maneno, kwa sababu out of 40bn$ zinazocirculate Kenya, ni asilimia sita tu ndiyo misaada.
Lakini kwa Rwanda, almost 18% yA FEDHA ZINAZOZUNGUKA NI KUTOKANA NA MISAADA!!... so what gave Kagame the bragginng rights? His country is as dependent as any country in AFRICA.
 
The culture of begging is so ingrained in Tanzanians that they don't even feel embarrassed.

What a shame.

The only thing this country lacks is good leadership.
 
JK heri angempa Lipumba homework ya kumuandalia cha kuongea maana tunapata shida ughaibuni uku maana wote wanajua nasi uwezo wetu ni kama JK.
GDP (purchasing power parity):
$13.46 billion (2011 est.)
country comparison to the world: 140 $12.55 billion (2010 est.)
$11.73 billion (2009 est.)
note: data are in 2011 US dollars





Naona Mkuu sasa chumvi umezidisha, au hiyo ni CIA ya wapi, hebu angalia hapa chini halafu fananisha na upotoshaji wako hapo juu::A S-coffee:

6946685739_856bc505f6_b.jpg


Source:
https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/geos/tz.html
 
Ndugu Kobelo,
Nimeona una point kuhusu Rwanda ingawa unatoa kwa kuwa upande mmoja. Nafikiri issue siyo misaada Bali jinsi ya kuitumia misaada hiyo kuendeleza wananchi kwani mwisho wa siku ndo walipaji. Kwa haraka Rwanda imekuwa kiuchumi kiasi cha kutoka 180usd Mwaka 1994 na 2011 ilifikia USD 600. Imepunguza umaskini kwa 12% sawa na watu million moja kwa muda wa miaka mitano (2006-2011). Tanzania tupo wapi kwa upande huo?
 
Back
Top Bottom