Elections 2010 Kikwete kufanya mdahalo Ijumaa, aweza kutangaza hali ya hatari Jumapili?

Mazingira ya wizi wa kura yapo.kwenye majumuisho ndiko kunakoibiwa kura na si vituoni kwa taarifa yenu.
Hakika ufisadi ndani ya ccm hautatoka.ijumaa salma kikwete kaja hap songea,njiani alikuwa akimwaga kofia na t shirt kwa kuwarushia dirishani kama mbwa vile wadake wenyewe hukohuko.maeneo yote ya lizaboni hadi mjin alifanya hivyo.watu wa usalama wa taifa walibaki macho tu hawana cha kufanya. Urais wa familia huu nao ni ufisadi mtupu
tusaidiane njia wanazo tumia ilitufafikishie wataka kuwepo wakati wa majumuisho pengine zitafasaidia...
 
Kama alivyosema Dr. Slaa kuyumbishwa kwa nchi kamwe hakuwezi kuletwa na chama pinzani siku zote chama kilichoshika dola ndio kinahatarisha amani ya nchi. Ingekuwa busara kama angehutubia taifa kabla ya uchaguzi maana kufanya hivyo kunaweza kuchukuliwa kwa mtazamo tofauti. Naamini maji yamemzidi sana na walitegemea huu uchaguzi ungekuwa rahisi kwao lakini watu tunaitaji mabadiliko na si tu ilimradi mabadiliko bali tunahitaji kiongozi mbadala anayejua wapi tumetoka, wapi tunakwenda na kwanini tunakwenda huko. JK amekosa washauri wazuri wenye uzalendo wa nchi yao, wanampotosha hawamwelezi ukweli kwa sababu wamemsoma wanajua nini anapenda kusikia. Sasa anatapatapa hajui pa kwenda lakini nguvu ya umma ndio itakayoamua. KURA yako ina nguvu zaidi ya RISASI.
 
Je utakuwa mdahalo kwa maana halisi ya mdahalo? au kuhutubia taifa ?Au vinginevyo? Kama utafanyika ijumaa sawa,lakini kama utafanyika jumapili baada kupiga kura kuna maswali mengi bila majibu.
 
JWTZ, tayari wanafanya maandalizi ya kutangaza hali ya hatari. Na leo asubuhi watakuwa wanajaribu ving'ora vinavyotumika wakati wa kutangaza hali ya hatari. Tangu wakati wa Nyerere haikuwa kutokea kutangazwa hali ya hatari, naona mwaka huu ndo tutaisikia kwa mara ya kwanza.

Mkuu hii ya ving'ora ni kweli kabisa nilipita maeneo ya makao makuu ya jeshi kwenye mida ya saa kumi na mbili asubuhi nimevisikia mwenyewe kwa masikio yangu ila sikujua hivyo ving'ora vilikuwa na maana gani
 
Kikwete atafnya mdahalo? Katika TV ipi? Imetangazwa lini? Hizi habari zijaona zimetangazwa> Wewe umezipata wapi?
 
Dr. Slaa amemaliza kuhutubia Dar es Salaam. Tulikuwa Kawe tunamsikiliza. Ahadi zake kwa wananchi zinazidi kuongezeka. Sasa ameahidi akichaguliwa,wananchi wataruhusiwa kupika na kunywa pombe ya gongo,pia watasaidiwa kuitengeneza vizuri.
Inaelekea sasa kwamba kama mtu yoyote atamshinda Kikwete,ni huyu Dr. Slaa. Nimemsikiliza jana katika mdahalo wa ITV na leo Kawe,na,ninacho kila ninachohitaji ili kufunya uamuzi wa kumpigia au kutompigia kura Dr, Slaa. Natumani wengine,kama Lipumba na Kikwete watafanya mdahalo kama alivyofanya Dr, Slaa.
Wasipofanya hivyyo,wanaweza kuhesabika kama washindani ambao hawataki kufika kwenye mashindano,kwa hiyo watampa ushindi Dr. Slaa.
Ili mtu achaguliwe kuwa Rais,lazima ajulikane ametoka wapi. Dr. Slaa alikuwa anasema jana kwamba'' kila Mtanzania anafahamu kwamba mimi nilikuwa padre wa Kanisa Katoliki'' Mimi nilikuwa sifahamu kwamba Dr. Slaa alikuwa padre wa Kanisa Katoliki. Kwa hiyo hawa wagombea wafanye mdahalo kama alivyofanya Dr. Slaa,na wasiwalazimishe wananchi kununua mbuzi ndani ya gunia.
Kiongozi lazima ajulikane rafiki zake ni nani,na wanahusiana vipi. Kuhusu Dr, Slaa,tunafahamu kiasi fulani kuhusu rafiki zake,kwa vile tumeelezwa kuhusu Josephine. Lakini kuhusu wagombea wengine wa Urais there is too much opaqueness kuhusu mahusiano yao na rafiki zao. Yaani,bila kuingila mambo ya binafsi ya mtu,ni lazima generally ufahamu anahusiana vipi na swahiba zake.
Dr. Slaa alikuwa anasema kwamba akichaguliwa yeye,angependa Halima Mdee pia achaguliwe,ili aweze kupata wabunge kupitisha sera zake. Hilo ni wazo zuri. Lakini itakuwa ni bora hizi category zote za kura,Urais,Ubunge na Udiwani,zijitegemee,hapo ndipo wapinzani watapata nafasi ya kumuondoa Kikwete. Lakini ikibidi na Mbunge pia itabidi achaguliwe,labda wapiga kura wengine watashindwa.
Huu ni wakati wa kuanza ukurasa mpya. Wachaguliwe wabunge ambao wataiwezesha Tanzania kufungua ukurasa mpya.
Againmwe say,Rais yoyote akichaguliwa,Tanzania haitapata matatizo yoyote. Wanachi wamchague yoyote wanayetaka awe Rais.
 
naamini mdahalo uatafana kama ule wa diamond jubilee wa tarehe 4 mwezi wa tano mbele ya wazee wa mkoa wa Dar es Salaam. Jeikei hana muda wa kuzngumza na vijana wa sikuhizi ni watukutu mno kwahiyo naamini waandaji wamelitazama hilo pia.
 
Hakuna ulazima wowote wa Rais Kikwete kufanya "mdahalo hewa" baada ya kura kupigwa na kujijenga kama bado ni Rais wakati wananchi wanasubiri matokeo ya Uchaguzi. Ninawashauri kina kinana kama lengo la "mdahalo hewa" wa Rais Kikwete kuwavutia wapiga kura waufanye wakati wa kampeni yaani (hadi Jumamosi). Watanzania wana haki ya kumsikiliza Kikwete ili awasaidie kufanya uamuzi wa kupiga kura.

Kitendo cha kupanga kufanya "mdahalo hewa" siku ya Jumapili, wakati kura zinasubiliwa na matokeo hayajatoka ni kitendo chenye lengo la kuandaa mazingira ya vitisho na hata kutangaza hali ya hatari hasa kama exit polls zinaonesha CCM kufanya vibaya.

Matokeo yake Rais Kikwete atatumia nguvu ya EPACT ya 1986 ambapo vyombo vyote vya habari vinaweza kupigwa marufuku kutangaza na radio zote kuanza kuimba nyimbo wanazozitaka na hivyo kuchakachua utaratibu wa kutangaza matokeo.

Kwa kufanya mazungumzo hayo usiku wa kuhesabu kura na kabla ya matokeo yote kutoka CCM inawataka wananchi wajikusanye kuandamana au kufanya vurugu ili hatimaye waweze kufungulia virungu dhidi yao.
Tutumie hekima basi tunapopanga baadhi ya mambo. Kwa vile uchaguzi utakuwa umeshapita sidhani kama kuna ulazima wa Kikwete kuzungumza usiku wa kuhesabu kura.

Kama atashinda basi atazungumza na wananchi siku ya kuapishwa. Is that too much to ask?

Mbona kichwa cha habari kinasema Ijumaa halafu content inaongelea J'pili? Kikatiba hali ya hatari lazima iridhiwe na Bunge ambalo halipo kwa sasa.
 
Mungu ni jibu la yoote, ipo siku yao mmoja baada ya mwingine they will all finish !
 
hakuna umuhimu wa kuongea na sisi baada ya kura kama anaona ni muhimu sana basi siku nyingi Jtatu mpaka Jmos zinatosha sana kwa yeye kutoa masaa mawili ya kusema na wananchi
 
Hata aweke midahalo hewa 100 bado JK ni feki tuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mkuu, Mwanakijiji, Ujumbe huu na maoni haya yaliyosheheni hekima na busara, umewafikia watawala? Fanya lolote lile uwafikie hawa mafisadi!
 
Kama watu wangeelewa siasa za nchi zetu za dunia ya tatu ni tofauti na nchi zilizo endelea, basi naamini mageuzi ya kweli yangetoke
Takribani asilimia karibu 90 ya humu JF wanaamini Dr Slaa atashinda uchaguzi na ukuwauliza why? majibu ni CCM mafisadi hawajaleta maendeleo, sabaub hiyo inatosha kabisa kukitoa chama madarakani katika nchi zilizo endelea lakini sio dunia yetu yatatu.
kabla hujadhania chama fulani kitashinda jaribu kufikiria kwanini?

Nadhani Zambia, Malawi, Kenya, Ghana na hata Zimbabwe wameonesha kuwa walioko madarakani wanaweza kuchokwa na wananchi na kuondolewa kwa kura.

Hawa nao ni ulimwengu wa tatu, na ni Waafrika wenzetu.

Hadanganyiki mtu!
 
Makuwadi wa chadema wanapoandaa mazingira ya vurugu.
Huwezi kupata urais kwa hila za makanisa, NGOs, Media na wanafunzi wa vyuo vikuu. Shame on You!
Endeleeni kutapatapa kwa na kujipa moyo kwa ushindi mtandaoni.
Padri Slaa anaweza kuwa rais wa JF lakini si rais wa nchi.
 
Makuwadi wa chadema wanapoandaa mazingira ya vurugu.
Huwezi kupata urais kwa hila za makanisa, NGOs, Media na wanafunzi wa vyuo vikuu. Shame on You!
Endeleeni kutapatapa kwa na kujipa moyo kwa ushindi mtandaoni.
Padri Slaa anaweza kuwa rais wa JF lakini si rais wa nchi.[/QUOTE]

Mdau naona propaganda za CCM zimekuingia vizuri......
 
Je? waalikwa ni mtu yeyote au Watachakachuliwa ili maswali magumu yasiwepo?
Nadani inaweza kuwa kiini macho, akidhani kila mtu anaamini ahadi zake ambazo zinaudi hata kuzisikiliza?



Nawasilisha
 
tuliokua wilaya ya temeke hapakua na premier league wala nini... kila kitu kilikua itv nadhani wamepata audience ambayo ni record breaker

it was a big score for our next pres. Dr. Anakubalika, and especially how he was responding superbly to each and every question.
 
Back
Top Bottom