Elections 2010 Kikwete kufanya mdahalo Ijumaa, aweza kutangaza hali ya hatari Jumapili?

Amruhusu na Rais Mtarajiwa Dr Slaa akashiriki katika mdahalo huo wa October 29 na masaa yaongezwe ili uwe wa masaa matatu na tunamuomba asiingie mitini kumkimbia Rais mtarajiwa. Dr Slaa tafadhali sana omba kushiriki katika mdahalo huo wa October 29.
 
Hakuna ulazima wowote wa Rais Kikwete kufanya "mdahalo hewa" baada ya kura kupigwa na kujijenga kama bado ni Rais wakati wananchi wanasubiri matokeo ya Uchaguzi. Ninawashauri kina kinana kama lengo la "mdahalo hewa" wa Rais Kikwete kuwavutia wapiga kura waufanye wakati wa kampeni yaani (hadi Jumamosi). Watanzania wana haki ya kumsikiliza Kikwete ili awasaidie kufanya uamuzi wa kupiga kura.

Kitendo cha kupanga kufanya "mdahalo hewa" siku ya Jumapili, wakati kura zinasubiliwa na matokeo hayajatoka ni kitendo chenye lengo la kuandaa mazingira ya vitisho na hata kutangaza hali ya hatari hasa kama exit polls zinaonesha CCM kufanya vibaya.

Matokeo yake Rais Kikwete atatumia nguvu ya EPACT ya 1986 ambapo vyombo vyote vya habari vinaweza kupigwa marufuku kutangaza na radio zote kuanza kuimba nyimbo wanazozitaka na hivyo kuchakachua utaratibu wa kutangaza matokeo.

Kwa kufanya mazungumzo hayo usiku wa kuhesabu kura na kabla ya matokeo yote kutoka CCM inawataka wananchi wajikusanye kuandamana au kufanya vurugu ili hatimaye waweze kufungulia virungu dhidi yao.
Tutumie hekima basi tunapopanga baadhi ya mambo. Kwa vile uchaguzi utakuwa umeshapita sidhani kama kuna ulazima wa Kikwete kuzungumza usiku wa kuhesabu kura.

Kama atashinda basi atazungumza na wananchi siku ya kuapishwa. Is that too much to ask?
Kabla sija jiunga rasmi na jf, namaanisha enzi za jambo forum moja ya watu walio ni inspire kujiunga na jf, basi ni mwanakijiji
but now days sikuelewi kabisa,
Kwanza kabisa naomba uombe radhi kwa taarifa yako ya kizushi kuwa JK atafanya mdahalo hewa siku baada ya uchaguzi na atatangaza hali ya hatari.
Mkuu naheshimu sana maandiko yako na uwezo wako wa kujenga hoja lakini katika hili sijui ulikurupuka usingizini na kulibandika pasi na mantiki yoyote?
Kingine chaajabu ni kuwa watau wanarukia tu kureply wanashindwa hata kujiuliza mantiki ya hoja yenyewe iko wapi?
Ni vema ukafanya tathimini kisha uje na hadithi angalau inyofanana na ukweli
 
Jamani nasikia Rais mtarajiwa Dr.Slaa, kesho atafanya mkutano wa kampeni Kawe? Mwenye taarifa sahihi anipatie tafadhali.
 
Oparation nyingi kubwa tunatumia ganzi ya muda mrefu, ila hii ya tarehe 29 hakuna haja ya ganzi, tunapasua jipu la CCM bila ganzi tena halijaiva. Tuna ma Dr. wa ukweli sio feki

Tumuombe Mungu awajaze Watanzania hekima na busara,kumchagua kiongozi wanaompenda,na kila atakayejaribu kuiba kura,natamani azimike ghafla, maana kila chama kinahubiri uwazi na ukweli, je, hawa jamaa wengine akina.....hawatachakachua kura,Upinzani hakikisha wasimamizi wa kura zenu mnawajenga vizuri,kisaikolojia na ikibidi kama binadamu wengine,wape nguvu ya ziada,posho ya uhakika ili hata wakilaghaiwa,wasikubali,haki ya mtu isipotee,maana ikipotea ndo pale nguvu ya umma itaamua cha kufanya,hainiingii hakili,wananchi hawakupendi harafu wewe ung'ang'anie kuwaongoza!Hee mbona wenzetu dunia ya kwanza,ukishindwa unakubali na hakuna aibu!MKUU wa kaya,ikitokea hivo kubali,Dr,ikitokea lakini game likiwa fair kabisa ukubali. MWAKA HUU MSICHAKACHUE KURA,MAANA MWAHUBIRI DEMOCRASIA YENYEWE,LAZIMA MKUBALIANE NA MISINGI YAKE,Vinginevyo Mungu atawalaani mtakaochakachua kura,kama kuna mpango huo
 
Kama watu wangeelewa siasa za nchi zetu za dunia ya tatu ni tofauti na nchi zilizo endelea, basi naamini mageuzi ya kweli yangetoke
Takribani asilimia karibu 90 ya humu JF wanaamini Dr Slaa atashinda uchaguzi na ukuwauliza why? majibu ni CCM mafisadi hawajaleta maendeleo, sabaub hiyo inatosha kabisa kukitoa chama madarakani katika nchi zilizo endelea lakini sio dunia yetu yatatu.
kabla hujadhania chama fulani kitashinda jaribu kufikiria kwanini?
 
Kama ni kweli Jakaya anataka kufanya mdahalo basi utajivunjia heshima kwa kiasi kikubwa sana. Wakati kampeni za uchaguzi zinaanza watu walishaanza kuandaa mdahalo baina yako (JK), Dr Slaa na Lipumba. Bila shaka ulikataa na kusema kwamba huna haja ya kushiriki vitu kama hivyo sababu wewe ni Raisi na unafahamika na wananchi wako vyema. Sasa leo tena inakuwaje unageuka?. Tafadhali kuwa na msimamo unaoeleweka ili kutunza heshima yako. Hii inaonesha wazi kwamba Chadema inakuyumbisha big time. Tulia acha kimpamano ama kiwashawasha.
 
JWTZ, tayari wanafanya maandalizi ya kutangaza hali ya hatari. Na leo asubuhi watakuwa wanajaribu ving'ora vinavyotumika wakati wa kutangaza hali ya hatari. Tangu wakati wa Nyerere haikuwa kutokea kutangazwa hali ya hatari, naona mwaka huu ndo tutaisikia kwa mara ya kwanza.
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewataka wakazi wa Dar es Salaam kutokuwa na hofu yoyote wakati watakaposikia mlio wa ving'ora asubuhi ya leo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ya jeshi hilo, king'ora hicho kitawashwa kwa majaribio, ikiwa ni sehemu ya majaribio ya kawaida kwa utaratibu wa jeshi.

"Tutafanya jaribio la kuwasha king'ora ambacho hutumika wakati wa hali ya hatari ili wananchi waweze kuchukua tahadhari kunapotokea tatizo.

"Zoezi hilo litafanyika Jumapili (leo) Oktoba 24, 2010 saa 12.00 (kumi na mbili alfajiri) katika kambi ya Makao Makuu ya Jeshi iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kutokana na taarifa hiyo, jeshi limesisitiza na kuwataka wananchi kutokuwa na chembe ya hofu.
Source: Habari Leo
 
Kweli disco limeingia maasai tena na silaha kiunoni?tuone kama watu watendelea kucheza huo mziki.......
 
Kama watu wangeelewa siasa za nchi zetu za dunia ya tatu ni tofauti na nchi zilizo endelea, basi naamini mageuzi ya kweli yangetoke
Takribani asilimia karibu 90 ya humu JF wanaamini Dr Slaa atashinda uchaguzi na ukuwauliza why? majibu ni CCM mafisadi hawajaleta maendeleo, sabaub hiyo inatosha kabisa kukitoa chama madarakani katika nchi zilizo endelea lakini sio dunia yetu yatatu.
kabla hujadhania chama fulani kitashinda jaribu kufikiria kwanini?

Acha dharau.Hakuna anayekubeza kwa kuamini tofauti na wengi wetu hapa JF.Hivi hakuna msemo wa kiswahili kuwa mkataa wengi ni mchawi?Kama asilimia 90 ya wana JF wanaamini katika ushindi wa Dkt Slaa,kwanini usikae chini na kujiuliza maswali ya msingi kuhusu hali hiyo?

Eti kabla ya kudhani chama flani kitashinda tujaribu kufikiri kwanini!Mbona wewe hujafanya jitihada ya kufikiri kwanini asilimia 90 ya wana JF wanamsapoti DkT Slaa (according to your own statistics)?

Epuka kutafuta majibu mepesi kwenye maswali magumu
 
Mkuu Mwanakijiji mimi sijaelewa kitu kimoja. Title ya thread ina sema "Kikwete kufanya mdahalo Ijumaa...." Kwenye thread yeneywe una sema kwamba ata fanya mdahalo Jumapili ambayo ita kuwa baada ya kura kupigwa. Sasa kabla hatujaendelea zaidi mkuu naomba ufananue mkuu. Mdahalo huo ana mpango wa kuufanya Ijumaa kama title ya thread inavyo sema? Au ana mpango wa kuufanya Jumapili kama content ya thread inavyo sema? Which is which? Friday or Sunday?
 
Ni threads 2 zimeunganishwa!
 
Si ndo hapo! Tunashindwa kumuelewa hapa! Mara ijumaa atangaze hali ya hatari j2! Huo mdahalo wa j2 unatoka wapi?
 
Sasa majaribio ya ving'ora ya nini.?hata mfanyeje mwaka huu hamshindi
 
Kulikuwa na habari mbili ya kwanza ilikuwa inadokeza kuwa mdahalo wa JK ulikuw aufanyike j'pili baada ya uchaguzi na ndio sababu ya mimi kurespond. Baadaye however kuna clarification imefanyika kuwa mdahalo ni Ijumaa. Hata hivyo, kutokana na utete wa homa ya uchaguzi nina wasiwasi kuwa usiku wa kuamkia Jumatatu ya Nov 1 unaweza ukawa ni wivu wa wasiwasi.

Matumaini yangu ni kuwa Ijumaa JK atalituliza taifa kwa kulihakikishia kuwa hatojaribu kutumia kibakiism kubaki madarakani.
 
Shukran kwa clarification! Lets hope he does try kibakism, mugabeism, bushism ndani ya florida, na 'ism' nyingine...maana ITS OVER!

P.S: Shukrani kwa video zako za Mdahalo wa Dr Slaa jana ITV
Ningependa pia kama kwenye ile thread yako nyingine ya wizi wa kura ungejisahihisha kwa kukubali kuwa wizi upo ila wananchi wanatakiwa kuwa makini katika kulinda kura zao. Maana hata Dr Slaa mwenye kakubali kuwa wizi upo na waliufanya Karatu ndani ya ngome yake mwaka 2005 na kudhibitishwa na mahakama mwaka 2006.
 
Kama watu wangeelewa siasa za nchi zetu za dunia ya tatu ni tofauti na nchi zilizo endelea, basi naamini mageuzi ya kweli yangetoke
Takribani asilimia karibu 90 ya humu JF wanaamini Dr Slaa atashinda uchaguzi na ukuwauliza why? majibu ni CCM mafisadi hawajaleta maendeleo, sabaub hiyo inatosha kabisa kukitoa chama madarakani katika nchi zilizo endelea lakini sio dunia yetu yatatu.
kabla hujadhania chama fulani kitashinda jaribu kufikiria kwanini?
Hapo kwenye bold ni assumption yako. Sisi tuna sababu zaidi ya 100 za kutomchagua jamaa yako kikwete. Hiyo ya mafisadi ina upana wake ndani.
Kukumbatia mafisadi ndo maana yake, na tunajua kuwa chama hakiwezi kuwa mafisadi bali wanachama wake wachache kama tunavyoshuhudia leo. Kuna suala la uchumi, umaskini, elimu, fursa, UTAIFA, udini, ukabila na unasaba, visasi, fungate la kuchaguliwa hajalimaliza, kuna mengi ambayo yanamake essay ya kujaza kitabu cha pages 1000.

Tatizo lenu ccm ni kuzoea majibu mepesi kwa maswali magumu. sisi wengi hapa tumeweka hoja za mantiki lakini wewe unajinyakulia vile vyepesi.
Labda utuwekee hapa nani kasema hayo uliyoyasema kuwa ndo sababu pekee? Ujinga GHARAMA SANA, na taifa linagharimika kwa kufanywa WAJINGA

Kwa kweli watamchosha huyu JK, sasa sijui ni saa ngapi atakariri hayo majibu ya mdahalo. Inabidi ambulance iwekwe nje ya TBC sijui ikulu sijui Lumumba kwa sababu anaweza kuishiwa pumzi kutokana na kukariri majibu. Nina hakika tayari sasa hivi anafanya rehearsal ya kujibu hayo maswali aliyotumiwa.
 
Kitendo cha kupanga kufanya "mdahalo hewa" siku ya Jumapili, wakati kura zinasubiliwa na matokeo hayajatoka ni kitendo chenye lengo la kuandaa mazingira ya vitisho na hata kutangaza hali ya hatari hasa kama exit polls zinaonesha CCM kufanya vibaya.
Hivi tunazo taratibu ya kujua exit poll hapa Tanzania?

Nijuavyo JK anaelewa na amekwisha kujulishwa na Idara ya usalama wa Taifa kuwa .."it is all over" na hakuna tiba................labda ndiyo atatumia nafasi hiyo kutuaga...........................lakini ninaafiki pale unaposema atumie busara asubiri kujulishwa kuwa tumemfukuza kazi rasmi halafu atuage na akumbuke kutushukuru kwa imani tuliyompa miaka mitano iliyopita na kuwa kutomchagua ni kwa sababu hana sifa na wala siyo udini hata kidogo....vinginevyo tusingelimchagua 2005 awe na adabu na unyenyekevu...............
 
Back
Top Bottom