Kikwete anaiogopa CHADEMA?

Kuna wanaJF ambao mawazo yao bado ya mwaka 47, njoo uone huku Nyanda za kusini magharibi uone watu wanavyojiunga na chadema mawazo ya akina Rejeo ni ya wanyama wa mwitu, mtaji wao ulikuwa vijiji, huko wameamka hawawataki, siku ya kiama inakuja siju mtakuwa wakimbizi wapi?
 
Dah thread nyingine bwana, yaani kwa akili zako, Mtukufu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuogopa chama cha vilaza kama Chadema?.
.
"Ama kweli CHADEMA NI SAWA NA NG'OMBE ASIYE NA BEI SOKONI".
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
Mipunga inajiuza tu humu JF!
 
Wako binadamu ambao kwa hula yao hupenda sana kusifiwa, wakikosa Watu wa kuwasifu huamua kujisifu wenyewe ili kumaliza kitu yao ya kutafuta sifa hulks hii ndiyo ulimbukeni. Waswahili wana hadhithi Yao ya sizitaki mbichi hizo. Rais Jakaya Kikwete amemteua James Mbatia kuwa mbunge. Hili ni Jambo la kawaida wala siyo Mara ya kwanza kutokea. Suala hili la kawaida lime za mjadala, nccr-m ambayo siku chache zilizopita walifanya makubaliao na Chadema ambayo yalimwezesha Mbatia kifuta kesi ya kupinga matokeo ya mbunge wa Kawe Halima Mdee na kutangazwa , makubaliano ya ushirikiiano haina ya vyama hivyo. Leo Banda ya Rais kumteua James Mbatia amegeuka kuwa kibaraka wa CCM . Wakati huo huo wanalia kwa nini hakuteuliwa mtu aw Chadema sasa unaweza kujiuliza ikawa mtu akituliwa na Rais atakuwa kibaraka wa CCM , je angeteuliwa aw Chadema angekuwa kibaraka wa CCM? Au kwa vile hakuteuliwa wa Chadema ndiyo mnasema sizitaki mbichi hizo. Hivi Baregu sasa ni kibaraka aw CCM? Achaemeni na m Hoja ambazo haina msingi. Chadema mlishinda viti takriban 23 Kati ya viti 230 vya majimbo, mnajgamba kiasi hicho kwa viti 23 je siku mkifisha 50 itakuwaje. Kwa mwenendo huu wa kujisifu wenyewe uwezo wenu aw kiongozi nchi hautakuwepo. Badala ya kiongozi mtakuwa mna lazimisha Watu wawasifu na wasipowasifu mtakalia kujisifu wenyewe. Pole sana.
 
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimeendelea kuwa tishio kwa ccm baada ya Rais kikwete kuogopa kuteua mbunge kutoka ndani ya chama hicho. Je kwa kuogopa huko ni dalili ya chama hicho kuwatishio kwa ccm?.

Bunge lilopita aliteua Jusa kutoka cuf, na cuf walikuwa chama kikuu cha upinzani.
Najua raisi anaweza kuchagua kutoka chama chochote lakini kushindwa kuteua kutoka cdm nadhani amedhihirisha kuwa cdm ni chama chenye kutishia uwepo wa ccm.
Nawasilisha
Maoni haya ni ya mlala hoi!.

.....inaweza kuwa ni maandalizi ya ccm kutengeneza strong alliance kwenye kambi ya upinzani baada ya 2015 baada ya chadema kushika dola??
 
Kwa mtazamo wangu si vema kwa CHADEMA kukubali kupewa ubunge huu wa kuchaguliwa na Raisi au hata kupewa wadhifa wowote ule (ikiwemo uwaziri) katika serikali hii ya CCM. Siamini katika serikali ya shirikisho na CCM ya sasa. Kwa nini napigana na hili?
1. Kwa sasa CCM na serikali yake wamvunja mifumo yote yenye kuhimiza uwajibikaji; kwa hiyo hata wampate kiongozi mwadilifu kwa kiasi gani ni aidha atachanganyikiwa na kushindwa kufanya kazi au naye atakengeuka na kuwa fisadi tu. Hili ni dhahiri maana hata sasa bado kuna watu waliosmart ndani ya CCM, wenye moyo wa kizalendo na wanaowajibika lakini mara zote wamefungwa mikono, miguu na vinywa waseweze kutenda au kusema lolote. Hawa wamebaki wakiugua tu au kupiga kelele (wanalalamika). Katika kundi hili tunaye Mh. PM Mizengo Pinda, Agrrey Mwanri, watendaji kama Uttoh, nk. Hawa wanaona uharibifu unatendeka katika nchi, wamapewa vyeo fulani lakini wakanyimwa mamlaka ya kiutendaji hasa kuadhibu. Humu wamo maDED wachache na hata wakuu wa taasisi za Serikali. Hana mamlaka maana Bwana mkubwa hayuko upande wao.

2.Sera za CCM hazitekelezeki na wao (CCM) wanalijua hili; lakini kwa kukosa kwao uzalendo wanashindwa kuchukua sera za vyama vingine na kuzifanyia kazi. Kwa tafsiri yangu kuamua kutumika katika serikali ya CCM ukiamini utachangia kuboresha maisha ya waTz ni kujidanganya tu. Nenda Zanzibar ukajifunze kinachofanyika kwa sasa. Ilani ya CUF ni bora zaidi na sera zao za kiuchumi zinatekelezeka; lakini pamoja na kuwemo katika serikali ya umoja wa kitaifa hakuna hata moja la CUF linalotazamwa.
Kuna haja gani basi ya kutenda kazi na watu wasioamini kile wanachokisema?

Kwa sasa CHADEMA endeleeni kujiimarisha kwa ajili ya 2015; aidha msijerubuniwa kufanya ushirika na CCM; Kabwe LILA NA FILA HAZITANGAMANI!


EJL
 
Acha kufikilia kwa Masaburi wewe, subiri chama chako kitakapokuwa cha upinzani, ndio utoe hoja yako hiii..
 
uchaguz wa meya wa Arusha mjini,wamebembelezwa kama mnahisi taratibu zimekiukwa nendeni mahakamani wamekataa! Lema akageuka Kibwetere kukesha viwanjani na kufunga mpaka Meya aondoke,!!

Songoro ndo maana uko banned na wana jf. point gani sasa hizi. ogopa m4c utake usitake cdm hatutaki kula tuloyatema, ubunge wa mezani na mizani ya kubalansi uwaziri hatuutaki cdm. sisi tunajitosheleza bila mkono wa kusukumiwa. MBATIA KAJIMALIZA MWENYEWE, labda home hapajatulia (tumbo linaunguruma kwa njaa) utafanyaje? Alishafanikiwa kumtoroka farao, lakini katikati ya jangwa ameshikwa na njaa akaona NCHI YA AHADI (KANAANI) NI MBALI, AFANYE LIPI? SOLUTION??? NI KUKUMBUKA MISRI KATIKA MASUFURIA YA NYAMA ZA MCHEMSHO. NJAA BWANA? HUNYIMA UHURU WATU WENGI SANA. SOMA STORI YA WANA ISRAEL, NJIANI WAKASEMA ... UMETULETA HAPA KUFA SISI NA WATOTO WETU? ...BORA TURUDI MISRI KUNA MAMBO FULAAANI YA (MISOSI) PIA STORI NYINGINE SOMA STORI YA ESSAU NA YAKOBO, HAAAA HAPO NDO UTAONA JEURI YA NJAA. ESSAU ALIUZA HADI HAKI YA UZALIWA WAKE WA KWANZA AKAMPA MDOGO WAKE TENA KWA GHARAMA YA KANDE LA DENGU BEST. ACHANA NA NJAA BWANA.
 
James Brown alipata kuimba

I don't want nobody to give me nothing
Open up the door, I'll get it myself
don't give me no animation, give me true communication
don't give me sorrow, give me equal opportunity

Hii ndio CHADEMA bwana, open up the door, we'll get it ourselves
 
Dah thread nyingine bwana, yaani kwa akili zako, Mtukufu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuogopa chama cha vilaza kama Chadema?.
.
"Ama kweli CHADEMA NI SAWA NA NG'OMBE ASIYE NA BEI SOKONI".
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
hakuna cha mtukufu hapa wote wazinguZi tu hasa wa ccm
unawapa utukufu wa nini fikiria kabla ya kubwatuka...
am sory
 
Upinzani sio uadui mkuu wala kupinga kila kitu!

Sasa kuna vyama tanganyika viongozi wake wanadhani kuwa mpinzani maana yake we uwe against na kila linalofanywa

na serikali hilo ndio tatizo la hao CDM, tofauti n vyama vingine ambavyo katika baadhi ya masuala yenye manufaa na

taifa wanakubaliana na serikali au wanatoa maoni yenye kuboresha CDM yenyewe imejengeka katika mfumo wa kupinga

tu.

Sasa katika hali hiyo usitegemee atokee mbunge wa kuteuliwa toka kwa hawa watu.
Wala hatutaki wabunge aina hiyo
 
kwenye kampeni zao ubunge nilisikia huyu bwana analipwa hela kila mwezi na chama tawala
 
Upinzani sio uadui mkuu wala kupinga kila kitu!

Sasa kuna vyama tanganyika viongozi wake wanadhani kuwa mpinzani maana yake we uwe against na kila linalofanywa

na serikali hilo ndio tatizo la hao CDM, tofauti n vyama vingine ambavyo katika baadhi ya masuala yenye manufaa na

taifa wanakubaliana na serikali au wanatoa maoni yenye kuboresha CDM yenyewe imejengeka katika mfumo wa kupinga

tu.

Sasa katika hali hiyo usitegemee atokee mbunge wa kuteuliwa toka kwa hawa watu.
We ndo mshauri wa JK nini,naona mtazamo wenu mmoja,na mna ugonjwa wa M4Cphobia
 
Upinzani sio uadui mkuu wala kupinga kila kitu!

Sasa kuna vyama tanganyika viongozi wake wanadhani kuwa mpinzani maana yake we uwe against na kila linalofanywa

na serikali hilo ndio tatizo la hao CDM, tofauti n vyama vingine ambavyo katika baadhi ya masuala yenye manufaa na

taifa wanakubaliana na serikali au wanatoa maoni yenye kuboresha CDM yenyewe imejengeka katika mfumo wa kupinga

tu.

Sasa katika hali hiyo usitegemee atokee mbunge wa kuteuliwa toka kwa hawa watu.

Kwa mtu mwenye independent mind hakuna kitu ndani ya administration ya CCM ambacho hakitakiwi kupingwa, CCM ina mfumo wa hovyo kabisa wa kuongoza, mfumo wa kutegemea wizi, rushwa, ufisadi, kujuana na kulindana.

Ni lipi hapo ambalo hutalipinga if you really are an independent brain
 
Angeiogopa Chadema angeteua watu wa Chadema kwenye ubunge!

Rais wetu ni strategist mzuri anaandaa mazingira mazuri ya demokrasia kwa siku za mbele na offcoz anaweka mazingira mazuri kwa CCM kuendelea kutawala 2015.

Uje uniulize swali baada ya uchaguzi 2015
 
Kwa mtu mwenye independent mind hakuna kitu ndani ya administration ya CCM ambacho hakitakiwi kupingwa, CCM ina mfumo wa hovyo kabisa wa kuongoza, mfumo wa kutegemea wizi, rushwa, ufisadi, kujuana na kulindana.

Ni lipi hapo ambalo hutalipinga if you really are an independent brain

Kwahiyo wewe hujaona hata kimoja ambacho serikali imefanya toka tunapata uhuru?
 
CDM acheni wivu! Rais wetu Jakaya Kikwete anajua sana kubalance mambo sasa mlitaka ateuliwe Slaa ndio mfurahie au mngenuna pia? Mtasubili sana mpaka mtakonda kwa mawazo maana kila siku mtakosa raha kwani CCM na Rais wetu wako makini sana kwa maslahi ya Taifa siyo kwa ajili ya wapiga kelele bila hoja zaidi wakitaka sifa tu.

KIDUMU CHAMA TAWALA CHA CCM!

CCM OYEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!

CCM CCM CCM.
 
Bwana Bangoo. Tanzania ukitaka kupewa cheo inabidi uwe kibaraka, mnafiki na mbabaishaji. Ukiwa mkweli na mchapa kazi huendi popote. Mifano ipo mingi ... angalia kina John Cheyo, Augustine Mrema, na James Mbatia nasikia ameteuliwa kuwa mbunge nk nk nk....

Jibu ni Kweli tena anaogopa sana, lakini zaidi ya yote maji na mafuta hayachangamani, CDM ukweli haki na ustawi wa Umma, CCM wizi, uongo na ustawi wa Mafsadi, sasa utamwambia Dr Slaa akusaidie si atafukuza wezi wote harafu kumbe ndo wenye CCM itakuwaje hapo? acha wakokotane wenye nira moja, CDM itapelekwa bungeni na wananchi, itapelekwa ikulu na UMMA.
 
Back
Top Bottom