Kikwete amuita Lowassa kwa mazungumzo ya siri!

hivi mi sielewi huyu Lowassa kuwa mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya usalama na mambo ya nje alichagulia au aliteuliwa?? CCM bana sasa leo mnampoka uanachama kwa sababu gani...tatizo ni lichama limejaa usanii...hta mfukuzane vipi jumba linawaangukia hilo
 
hawa watu wanatakiwa huku wanajipanga huku tunaendeleza hoja za msingi ili vikao vyao viishie kujadili hoja zetu,tuache habari za loliondo tukiumwa tutaenda tu! Maana hata magazeti makini yanafata upepo yanasahau hoja
 
ccm ilikuwa ya mwalimu jk, alivyofariki nayomilifaruki muda uleule, wamebaki wachakachuaji tu na huo ndo mwisho wa sura ya ccm ktk ulimwengu wa siasa, it is the same as to say aachwe baraba na Yesu afe. But i belief time will tell.
 
Ccm sasa inataka kumwaga sumu baada ya utoaji wa gamba la juu kutokuleta tija

Wakuu kansa ya CCM (ufisadi) haipo kwenye ngozi (gamba = CC/Secretariat) tu bali hata kwenye damu (Sera/Mfumo)! Kwa hiyo hakuna mabadiliko yoyote tutakayoyapata baada ya hilo gamba kutoka!
 
Nadhani baada ya kuivua gamba la awali,nyoka anaanza kujitengeneze gamba lingine...... unajua nimetafakari kwanini Mungu alimsukuma JK kutumia huu mfano wa nyoka.....

Unajua nyoka kujivua gamba haipunguzi sumu yake,matendo yake nk kwa hiyo sitegemei mabadiliko ya kutisha kutoka matendo ya awali ya CCM...

Nadhani sasa ndio kazi imeanza maana habari nyepesi nyepesi tulizopata, ni kuwa zile kambi za CCM ufisadi na CCM wanafiki aka wapiganaji zilipingana sana...............
 
nchi yetu wenyewe wanagawana kama ice cream za azam,kibaya zaidi tunawaangalia tu,Jwtz,polisi,uwt,umma wooote tupo tu!
Kuna kale kamwimbo...johny johny, yes papaa, eating sugar, no papaa, telling lies? No papaa, open your mouth, hahahaaa!....hii ni nchi ya kina johny, wanakula sugar yetu then wanatudanganya! Mwisho wao upo tu!
 
:yield:

Kikwete: Sasa mkuu, si unajua sie mabesti wa long time toka enzi? sisi hatukujuana barabarani bwana...tehetehee

EL: Ni kweli mheshimiwa, sasa sema fasta umenitia nini maana Regina ananingoja tuna mambo ya kupanga kwa ajili ya 2015

Kikwete: Usiwe na haraka, hii nchi yetu si unajua toka zamani tulikubaliana twende pamoja kisha tuachiane sema tu wanga walitibua...tehetehee

EL: Sawa kabisa, ehee, ulikuwa unasemaje

JK: Sasa hoja yangu ni kuwa jamaa wanalalamika sana wanataka wewe na wengine mtoke ila si unajua tena hawa wengine ni rahisi kuwatosa maana ni wa kuja, sasa wewe inakuwa ngumu hebu tushauriane hapa?...tehetehee

EL: Sasa tushauriane nini tena ndugu yangu,..unahdani mimi ni wa kutoka kwenye chama mimi?

JK: Sasa tunafanyaje maana sauti zai zimezidi...ahaaa, i have an idea, je unajambo la kusema mbele yao ili kuwashawish ikuwa uko "SAFI"?...tehetehee

EL: Kwanza hapo umeongea...unakumbuka jimboni ulikuja ukasema mi msafi, sasa leo ukigeuka ukasema mimi mchafu unadhani watu watakuamini tena? Watakuona msanii zaidi maana juzi ulituombea kura tukashinda sasa leo tukitoka maana yake na ubunge tunapoteza na ile kazi yako yote haina maana na utaonekana msanii zaidi

JK: Sasa vipi? anyway, hawa Wa-tz ni wetu, unaonaje nikumegee kacheo kwenye cabinet langu? au itachafua zaidi...khekekheeee

EL: MMmhhh, ngoja kwanza niongee na Regina na wana-mikakati wangu alafu nitakuambia, ngoja niingie chemba kwanza

JK: Teteheheee...EL bwana, haya ongea nao basi nakusubiri
 
Kama na wao wanaamini ni mafisadi je wataishia wafukuza au wamependekeza wafikishwe kwenye vyombo vya sheria?

Au kama kawaida yao, mwanaccm haguswi na sheria. Kumbukeni baada ya Masauni kukumbwa na kashfa ya kufoji nyaraka za serikali badala ya kupelekwa kwenye mkono wa sheria Mkulu alisema apumzike watampangia kazi nyingine!

Sioni kwanini Mramba na wenzake waende mahakamani na wengine waitwe mafisadi na waishie kutolewa CC na NeC tu?

Je kweli mmevua GAMBA?
 
Mbona anachomuitia kinajulikana tu! JK na EL hawajawahi kuwa mahasimu. Anaenda kumkumbusha jukumu lake alilonalo coming 2015. Tutake tusitake, Lowassa ndio mrithi wa JK CCM. Issue ya Lowassa kuwa Rais ni nyingine kabisa kwa sababu rais aweza toka chama chochote kile cha siasa hapa Tanzania.
 
lowassa,lowassa! Huyu jamaa atachukua nchi hivi hivi! Hata baba wa taifa atatulilia huko aliko
 
Tihi tihiii, kuna siku mwana ccm mmoja aliniambia kuwa - kwa tabia za watz zilivyo, yaani watu wa kupenda matukia bila kuyatafakari kwa kina, ccm hata ikiweka kichaa kugombea wanaweza kumchagua bila shaka yoyote.

Naelekea kumuelewa huyu mwanaccm alikuwa anamaanisha nini, kwa magamba yanayovuliwa hivi sasa na hali ambayo taifa la tz limefikia na jinsi watu wanavyorudisha imani kwa kasi, kana kwamba kuna muujiza umetendeka wakati ni mvinyo ule ule ndani ya kiriba tofauti.

Kazi kweli kweli
 
Binafsi sishangai sana na chochote atakachofanya JK kwa Lowassa. Ikumbukwe kwamba baada ya lile soo la Richmond ambaalo kwa kiasi kikubwa ndilo lililoleta mgawanyiko mkubwa ndani ya CCM katika moja ya speech zake JK bila kutafuta maneno wala aibu alisema kilichomtokea EL ni ajali ya kisiasa.

Kwa tafsiri isiyohitaji tafakuri yeyote kwa uwazi iliyonayo kauli hiyo, hii ilimaanisha kwamba JK alikuwa anamliwaza na kumuombea radhi kwa watanzania kwamba suala kama lile kisiasa ni la kawaida na kwamba laweza kumtokea mwanasiasa yeyote.

Na alithibitisha hayo alipokwenda kwenye majimbo ya waheshimiwa hawa, wote ni mashahidi kwa yale aliyo yasema kule.

Nitaomba nimalizie kwa swali: Hivi zile kesi za EPA bado zinaendelea?
 
Kama na wao wanaamini ni mafisadi je wataishia wafukuza au wamependekeza wafikishwe kwenye vyombo vya sheria?

Au kama kawaida yao, mwanaccm haguswi na sheria. Kumbukeni baada ya Masauni kukumbwa na kashfa ya kufoji nyaraka za serikali badala ya kupelekwa kwenye mkono wa sheria Mkulu alisema apumzike watampangia kazi nyingine!

Sioni kwanini Mramba na wenzake waende mahakamani na wengine waitwe mafisadi na waishie kutolewa CC na NeC tu?

Je kweli mmevua GAMBA?
Watanzania wenzangu hapa nachanganyikiwa,hawa jamaa wanakiri waziwazi wao ni mafisadi! Tena mbele ya polisi na takukuru wala hawashikiliwi kwa mahojiano zaidi! Wanabadili safu ya mafisadi pengine wenye lugha kama zetu ili tushindwe kuwatofautisha na akina Mnyika,Zitto,Lissu,Mtema,mdee n.k! Mbona hawawataji hao mafisadi wanaochafua chama?(tunawajua ila huyo aliyeanzisha falsafa ya kujivua gamba awataje pia) je wamesafisha mafisadi? Angalizo 1.katiba mpya ni after 2015 2.upinzani kuandamwa na kufaranakishwa haswa hadi wasieleweke tena 3.maisha magumu kuliko ilivyopata kushuhudiwa kwa kipindi kirefu 4.mwanzo wa machafuko makubwa 5.majeshi kuchukua utawala wa nchi kwa muda.haya ni mawazo yangu tu maana mwenye macho......!
 
JK hajamuita EL ila jamaa anajipendekeza anatafuta kupumua, nina data kuwa hajamuita
 
Anaweza kuwa anataka kumtisha -- yeye na RA kwamba wasithubutu kufanya chochote kama malipizo ama sivyo nguvu za dola.....?
burudani zaidi RA kaonekana leo anapanda emirates kwenda dubai yeye na familia yake.
 
Mimi ni miongoni mwa waandishi tulio hapa Dodoma. Nimepata hii taarifa kwa watu waliokuwa karibu na Ikulu sasa hivi usiku huu.

Rais Jakaya Kikwete amemuita swahiba wake wa siku nyingi, Edward Lowassa, Ikulu ya Dodoma kwa mazungumzo ya faragha. Haijulikani watazungumza nini ila ni Kikwete ambaye ame initiate hayo mazungumzo. Inasemekana hata Lowassa amepigwa butwaa na hajui Kikwete amemuitia nini.

JK kufanya mazungumzo ya siri na Lowassa kunakuja baada ya baadhi ya wajumbe wa NEC leo hii kutoa matamshi makali dhidi ya Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge na kutaka vigogo hawa wenye tuhuma lukuki za ufisadi watimuliwe kwenye chama.

Kuna tetesi kuwa JK anataka kufanya Cabinet reshuffle baada ya CCM kujivua gamba. Huenda anataka kumpooza kwa kumrejesha swahiba wake kwenye Baraza la Mawaziri ili ajiandae vyema kumrithi 2015 baada ya kujeruhiwa kwenye NEC ya CCM.

utawala wa maigizo huu.

everthing the guy is doing is proving unpopular.

hata kipimajoto cha ITV kinaonyesha kilichofanywa na kikwete na ccm yake hakiaminiki kwa wananchi kwa 69%
 
Back
Top Bottom