The Informer
Senior Member
- Jun 14, 2010
- 119
- 29
Mimi ni miongoni mwa waandishi tulio hapa Dodoma. Nimepata hii taarifa kwa watu waliokuwa karibu na Ikulu sasa hivi usiku huu.
Rais Jakaya Kikwete amemuita swahiba wake wa siku nyingi, Edward Lowassa, Ikulu ya Dodoma kwa mazungumzo ya faragha. Haijulikani watazungumza nini ila ni Kikwete ambaye ame initiate hayo mazungumzo. Inasemekana hata Lowassa amepigwa butwaa na hajui Kikwete amemuitia nini.
JK kufanya mazungumzo ya siri na Lowassa kunakuja baada ya baadhi ya wajumbe wa NEC leo hii kutoa matamshi makali dhidi ya Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge na kutaka vigogo hawa wenye tuhuma lukuki za ufisadi watimuliwe kwenye chama.
Kuna tetesi kuwa JK anataka kufanya Cabinet reshuffle baada ya CCM kujivua gamba. Huenda anataka kumpooza kwa kumrejesha swahiba wake kwenye Baraza la Mawaziri ili ajiandae vyema kumrithi 2015 baada ya kujeruhiwa kwenye NEC ya CCM.