Kikwete akutana na uongozi wa CHADEMA Ikulu; Dr. Slaa ndani

Hiki kitendo naweza nikakichukua in a positive way na kumpa Slaa pongezi, but in a negative way..Slaa ameonyesha kuwa weak. Ni mtu asiye na msimamo. Amesusa mwishowe amekubali kiulaini sana. Nilikuwa nategemea kuwe na kitu ambacho ni strong cha kuwakutanisha na iwe sehemu nyingine ambayo si Ikulu. Kitendo cha kujipeleka Ikulu kimeniacha nijiulize maswali mengi!
Maranya, nadhani huko CDM kuna shida kidogo. Kwa nini Slaa hakwenda Ikulu wakati ule? Kwa nini Mbowe alikutana na Rais siku mbili kabla ya viongozi wa CDM kwenda Ikulu mara ya pili muda huu wakiwa na Slaa? Slaa anawaamini wenzake? Je mara ya kwanza Slaa alisusa? Je Mbowe alienda kubembeleza ili Rais akubali kukutana nao Slaa akiwepo? Nina maswali mengi sana kichwani ila majawabu haba! Au Slaa hakukubaliana na yale makubaliano mawili?
 
Kwa kweli nimeipenda hii. Kwa watu wasiofuatilia vizuri watafurahia picha na wataenda kulala vizuri. Vyombo vya habari vilivyotaka picha vitapamba kurasa zao kwa picha hiyo lakini hawatauliza walizungumza bini. Yawezekana ni ultimatum ya aina fulani? Firkiria kwamba wameaua kuweka msimamo wao wazi kwa JK baada ya chai, na kupiga picha na mbwebwe nyingine kuwa "ukiunda tume ya Katiba na ikaanza kazi kabla mabadiliko ya sheria ya mchakato wa katiba hayajafanyika kama tulivyopendekeza basi CDM itajitoa na tutahamasisha wananchi kutoshiriki". Msimamo wa aina hiyo haukuwa na mtu mwingine wa kuuweka wazi mbele ya JK kama Slaa. Think about it.

Binafsi naamini, sasa CDM imejiweka mahali ambapo CCM haikutarajia - imewarushia CCM kamba yenye fundo!
Itategemea na kitakachoongelewa mheshimiwa, wanachotakiwa kufanya CDM ni kuhakikisha kuwa mchakato wa katiba unakuwa ule utakaoleta katiba ya kweli. Kwa jinsi mambo yalivyoenda mpaka sasa, kama itaandikwa katiba mpya ya wananchi na sio ya ccm basi CDM itakuwa ndio chama cha upinzani kilichofanya vizuri kuliko vyote vilivyowahi kutokea. Lakini itakuwa fatal mistake kama CDM watakuwa wameenda kujadili kitu kinaitwa coalition, wakifanya coalition basi watakuwa wameitoa ccm shimoni na kuingia wao wakiungana na CUF.
 
Kwe,li jembe la ukweli Slaa komaa baba sie tupo na wewe hata km kuna njaa....komaa babaaaaaaaaaaaaaaa
 
Hapo zamani Raisi angeweza tu kuitisha kikao cha CCM na kupitisha maamuzi yanayohusu taifa, je ni kitu gani kimetokea hadi Raisi kukaa na Upinzani hata ikibidi usiku? Hii ni dalili ya nini? Kwa nini Raisi hajaunda kamati katika mchakato wa katiba ? Nawapa hongera nyingi wapinzani wa kweli!
 
Haya, hayawi hayawi yamekuwa. Waheshimiwa wamekutana kimasomaso na kusalimiana leo!

xmvkq.jpg
 
Sidhani kama kutakuwa na jipya tena.

Unataka jipya lipi?Jk kumkabidhi Dr u-president. Au?kuna njia nyingi za kuonyesha kuwa umeshindwa siyo kupiga kelele tu bali hata kumkumbatia mpinzani wako kwa muda mrefu. Marefarii makini tunaweza kuelewa situation na kupiga filimbi ya kumaliza mchezo.
 
Invisible, asante kwa taarifa hii.Wanajf wenzangu, ile much anticipated photo ya wakisalimiana, nilioitafuta kwa udi na uvumba, hatimaye nimeiona!. Roho yangu imetulia, tuliyoyasema kule nyuma hatimaye yametimia! Thread ya kutimia iko mbioni kupanda. wale wote mlionitukana sana pale mwanzo nilipoeleza Chadema Yakubali Yaishe!, Yamtambua Rasmi JK!. Mlio hai niombeni msamaha, waliotamgulia nimeshawasamehe!

....Duh! Naona una chuki ya kufa mtu dhidi ya CHADEMA!!! Sijui Viongozi wa juu wa CHADEMA walikukosea nini hadi uwe na chuki kiasi hicho. Wanayofanya Viongozi wa CHADEMA kama chama cha upinzani si kwa ajili ya maslahi yao tu bali ni maslahi ya Watanzania wote na wewe ukiwemo.
 
Wanasiasa huwafahamu? Lakini pia kumbuka Slaa ni mkomavu kwenye siasa na anaelewa siasa sivita
 
waooooooooooooo hata siamini mana kama vile hii picha ya kutengeneza? kama syo basi ya zamani.
 
mh yani siasa kweli ni mchezo wa ajabu kweli kweli..! hawa ni watu wawili tofauti wenye fikira tofauti kabisa mmoja ni mkumbatia mafisadi mwingine ni mfichua mafisadi..! ila unaona hata ****** anamuangalia kwa uoga..? anajua kua mambo ni magumu hapo 2015..! kwakweli watanzania tuamke sasa hebu tusiwe na fikira mgando..! CCM ni kama gari lililoshindwa safari.. tukiendelea kukaa humo tutaonekana wajinga hebu tupande kwenye lingine tuone nalo litatuchukua umbali gani kuelekea kwenye tanganyika bora zaidi ya hii iliyo haribiwa
 
Hivi waungwana JK yuko sawa sawa kweli kichwani?tulimuokota wapi huyu mtu!!! daah ama kweli tumepatikana mmmhh!!! 2015 itafika kweli?????????
 
Maranya, nadhani huko CDM kuna shida kidogo. Kwa nini Slaa hakwenda Ikulu wakati ule? Kwa nini Mbowe alikutana na Rais siku mbili kabla ya viongozi wa CDM kwenda Ikulu mara ya pili muda huu wakiwa na Slaa? Slaa anawaamini wenzake? Je mara ya kwanza Slaa alisusa? Je Mbowe alienda kubembeleza ili Rais akubali kukutana nao Slaa akiwepo? Nina maswali mengi sana kichwani ila majawabu haba! Au Slaa hakukubaliana na yale makubaliano mawili?

Chadema ni chama kilicho makini sana na kina watu makini sana ndio maana sasahivi ndio tunarun show za siasa katika nchi hii.

Hayo ya Slaa ninajua ndipo akili yako ilipolala, kwakuwa kila ukiona jina la Slaa limetajwa hukosi kuonyesha wasiwasi lakini ni muhimu utambue kwamba Slaa kwa sasa ni alama muhimu sana katika mustakabali wa siasa ya nchi hii, si umeona watu wanasafiri hadi ifakara, wanapanda juu ya makaburi ili wapate picha yake? Kama una personal issue na Slaa unaweza kumtafuta kwa pm ama kwenye fb na kama unadhani ni vizuri kutushirikisha hapa public unaweza kufanya hivyo kuliko kujificha ficha.

Vyovyote itakavyokuwa na utakavyotafsiri, lakini ukweli unabaki pale pale kwamba kwa sasa hakuna namna raisi atafanya maamuzi ya kisiasa, in particular katiba mpya bila kukubaliana na chadema, wabunge na mawaziri wa ccm wametembea tembea majimboni huko, joto wamelisikilizia.
 
mwisho wa siku sote ni Watanzania, katiba ni yetu sote, kila jambo zuri la kujenga nchi yetu yapaswa lipongezwe, mie ningefurahi sana kama baraza letu la mawaziri nalo lingechanganywa, ingeangaliwa uwezo wa mtu na siyo chama chake natumai tungesonga mbele vizuri tu.
 
Namsubili Pasco wa JF azidi kuumbuka na ripoti zake za Kizandiki eti kwa nini Dr Slaa na JK hawakusalimiana kwenye msiba wa Regia! mijitu mingine hovyo kweli kweli.
Saigon, naomba tuwe wakweli toka ndani ya nafsi zetu, kuuliza sababu za kutosalimiana Ifakara ndio uzandiki?. Baada ya kusalimiana leo mimi ndio nimeumbuka vipi?. Mijitu mingine sio tu ni hovyo kweli kweli, bali ni kweli hovyo hovyo sana!.
 
Maranya, nadhani huko CDM kuna shida kidogo. Kwa nini Slaa hakwenda Ikulu wakati ule? Kwa nini Mbowe alikutana na Rais siku mbili kabla ya viongozi wa CDM kwenda Ikulu mara ya pili muda huu wakiwa na Slaa? Slaa anawaamini wenzake? Je mara ya kwanza Slaa alisusa? Je Mbowe alienda kubembeleza ili Rais akubali kukutana nao Slaa akiwepo? Nina maswali mengi sana kichwani ila majawabu haba! Au Slaa hakukubaliana na yale makubaliano mawili?

Hujaelewa ndugu jk alimwita mh mbowe ili aone uwezekano wa kumshawishi DR akubali ku-reconcile na yeye. Kwa kuwa jk anatambua wazi kuwa DR ni mzizi mgumu.
 
Back
Top Bottom