Kikwete akutana na uongozi wa CHADEMA Ikulu; Dr. Slaa ndani

Jamani sisi wananchi tuwe macho tusije tukahujumiwa tukakosa chama cha upinzani cha kututetea kama walivyokosa wenzetu wa Zanzibar sasahivi wanahaha Seif na Karume walianza hivihivi chinichini.

CHADEMA hawana sera ya muafaka kama cuf
 
Rais wa Tanzania JK, alivyokuwa toto la mjini anawapa kwanza Kahawa na Tende then anawamaliza na Juice za Machenza...Haaa!! Hapo Chadema wanacheka cheka tu..mkutano gani wa usiku imekuwa Party..

sio party raisi wako ndivo alivyo hovyoooo anaitisha kikao usiku.maji ya shingo.
 
Hiki kitendo naweza nikakichukua in a positive way na kumpa Slaa pongezi, but in a negative way..Slaa ameonyesha kuwa weak. Ni mtu asiye na msimamo. Amesusa mwishowe amekubali kiulaini sana. Nilikuwa nategemea kuwe na kitu ambacho ni strong cha kuwakutanisha na iwe sehemu nyingine ambayo si Ikulu. Kitendo cha kujipeleka Ikulu kimeniacha nijiulize maswali mengi!

matokeo yake mtayasikia tu
 
Hii inaonyesha kuwa JK japo na mapungufu mengi aliyonayo bado anania njema na nchi yetu yanayotokea ni nje ya uwezo wake. tuwe makini kumchagua raisi mwenye upeo zaidi ya huu but for this BIG UP JK
 
Naitafuta ile thread yangu ya chadema wakubali yaishe
Ili nii update!.
Usisahau kutafuta na ile thread uliokuwa umekomaa kwamba tuishitaki CCM kwa kuituhumu JF kwamba imesababisha ipate matokeo mabaya, bado tunasubili hiyo mahakama utakayokwenda kufunguwa kesi hiyo. ukiwa muongo make sure usiwe mwepesi wa kusahau.
 
slaa-mbowe-kikwete.jpg


Huu ni ukurasa mpya katika siasa za Tanzania, na ni dalili ya kuanza kukomaa kisiasa Tanzania. Kitu kimoja ninachoweza kubashiri ni Kikwete kuwa karibu na mataifa mbalimbali duniani ikiwepo mataifa makubwa, hayo yamempa changamoto katika mambo ya siasa yaweje ili kujenga hoja za ushindani kwa manufaa ya nchi badala ya uhasama, na papo hapo kutoka kifua mbele vinginevyo dunia isingemweka katika jamvi la wanadiplomasia wa ulimwengu wa leo.

Kikwete kwa vyo vyote alihitaji muda wa kujibu hoja za Chadema si papo kwa papo kama wengi tulivyotarajia siku walipokutana kwa mara ya kwanza Ikulu na Ujumbe wa Chadema. Busara, ushauri mzuri na mapendekezo ya wanadiplomasia wa kimataifa yamefikisha hatua hii ambayo binafsi naanza kufarijika, nikisubiria kwa hamu matunda yake. Hata kama yote hayatakubalika, lakini kuna baadhi ya mapendekezo kuna dalili ya kufanyiwa kazi.

Cha pekee matatizo yetu watanzania yatatuliwe na sisi watanzania wenyewe badala ya kuleta jopo la watu wa kimataifa na hivyo kuonyesha dalili kwamba wenyewe hatuwezi kutatua matatizo yetu wenyewe.

Dalili njema ambazo Kikwete ameanza kuonyesha zinaweza kumjengea jina zuri katika historia ya uongozi katika nchi hii hata katika kipindi hiki cha mabadiliko makubwa ya uchumi dunianai na mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa ndani ya Jamnhuri yetu
 
Rais wa Tanzania JK, alivyokuwa toto la mjini anawapa kwanza Kahawa na Tende then anawamaliza na Juice za Machenza...Haaa!! Hapo Chadema wanacheka cheka tu..mkutano gani wa usiku imekuwa Party..
Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!
Ahsantee.gif


Hebu utuondolee upuuzi wako hapa......Watu wanajadili mustakabali wa Taifa wewe unaanza kuleta ushabiki wa kijinga!!!!!.....

Ukue bana......Mambo ya kitoto hayafai hapa....

Haya ndiyo Bob Mkandara alikuwa anayazungumzia......Sijui tunaelekea wapi hasa....I wish ningekuwa Moderator....


Hongera kwa Mhe. Mbowe,Dkt. Slaa na viongozi wengine wa CHADEMA kwa uamuzi huu wenye nia njema kabisa kwa mustakabali wa Taifa letu......Hakika huu ni UKOMAVU wa kisiasa...
 
....Inatia matumaini, labda Kikwete amegundua kwamba Katiba itakayopatikana kama itakuwa ni ile ambayo Watanzania tunaitaka atajizolea sifa kemkem si tu toka kwa Watanzania bali jumuiya ya kimataifa na hivyo kuamua kuwashirikisha CHADEMA kwa karibu mno....Labda haya ndio matunda ya mwanzo ya Ambassador Ombeni Sefue.
 
safari na mikutano ya usiku usiku si kitu cha kawaida.... kuna jambo zito na gumu linajadiliwa hapa.
 
Mkuu Pasco,
Kwa kawaida huwa ninaheshimu sana post zako, but for this your argument is too low, It it unfortunate kuwa hata wewe hukuwaelewa CDm tangu mwanzo kuhusu kumtambua rais au la! Najiuliza kama wewe hukuwaelewa vipi kuhusu watanzania wa kawaida?? ambao hawapati bahati ya kusalimiana na Slaa na kuzungumza naye??? Kweli umenihuzunisha sana katika hili.

Invisible, asante kwa taarifa hii.Wanajf wenzangu, ile much anticipated photo ya wakisalimiana, nilioitafuta kwa udi na uvumba, hatimaye nimeiona!. Roho yangu imetulia, tuliyoyasema kule nyuma hatimaye yametimia! Thread ya kutimia iko mbioni kupanda. wale wote mlionitukana sana pale mwanzo nilipoeleza Chadema Yakubali Yaishe!, Yamtambua Rasmi JK!. Mlio hai niombeni msamaha, waliotamgulia nimeshawasamehe!
 
Hiki kitendo naweza nikakichukua in a positive way na kumpa Slaa pongezi, but in a negative way..Slaa ameonyesha kuwa weak. Ni mtu asiye na msimamo. Amesusa mwishowe amekubali kiulaini sana. Nilikuwa nategemea kuwe na kitu ambacho ni strong cha kuwakutanisha na iwe sehemu nyingine ambayo si Ikulu. Kitendo cha kujipeleka Ikulu kimeniacha nijiulize maswali mengi!


Kwa akili yako fupi hujui kwamba hakuna kitu strong na muhimu katika nchi yoyote zaidi ya katiba.

Hayo mengine yote unayoweza kudhani ni strong, hayawezi kuwa hivyo bila katiba na ndio maana unaona mkuu wa kaya amejua kwamba katiba ya nchi si suala la wabunge wa ccm kupitisha muswada tu kwa kuwa wako wengi, bali inahitajika muafaka wa kitaifa na ushirikishwaji wa wadau wote muhimu katiba mpya ipatikane.

Mawaziri na wabunge wake wameshampelekea salamu za moto wanaokutana nao huko wanakoenda kufanya mikutano ya kuhamasisha katiba mpya. imefika sehemu wanaitana ccm wenyewe katika mikutano ya ndani, hawathubutu kuendesha mikutano ya hadhara kwakuwa mambo ni magumu sana.
 
Back
Top Bottom