Kikwete akubali kukutana na CHADEMA

Hawezi kukaa meza moja na viongozi wa chadema, kazi hiyo atapewa katibu wa ccm akutane nao.
 
Naona kasoma nyakati na ishara hasa kwa kuyaona yanayotokea Misri kwa sasa na huku jukwaa la katiba nalo nikijipanga kwa maandamano ya nchi nzima!

Wala hakuna kitu kama hicho ..ni busara tu rais JK haogopi kuongea na mtanzania yeyote ..ok

Kwasababu hana nia yeyote mbaya kwenye mchakato wenyewe..

Besides..hivi NANI AMEANDIKA BARUA KUOMBA KUONANA???

chadema wameomba kuonana hawajalazimisha kuonana..get your facts right?? lol acha ushabiki
 
Ameonyesha kuwa yeye ni baba mzuri..ngoja awasikilize wanawe na kuwapa ushauri na kuwafunza siasa za TZ!

Bonge la pre-emption. Walitaka kupata cha kuongelea. Hata hivyo kukutana ni kitu kimoja na kuwakubalia hoja zao quite another.
 
Hawezi kukaa meza moja na viongozi wa chadema, kazi hiyo atapewa katibu wa ccm akutane nao.

wanakutana na amri jeshi mkuu upo hapo? wangetaka kukutana naye kama mwenyekiti nadhani taarifa hizi tungezipata kwa nape. usiandike kishabiki.
 
Arusha kuna nini? sana sana Arusha wanamhitaji JK kuliko JK anavyowahitaji Arusha???


Wewe upo Dodoma. Huijui Arusha! Sio yeye peke yake ambao hatuwahitaji. Chama chake chote hatutaki kukisikia, na yeye anajua hilo. Ndio maana aliingia mitini alipotaliwa kuja kuzindua nchanjo ya watoto! Kama hujui, pole!
 
angalia wasii-CUF cdm! Mimi dua yangu ni kuhusu nchi yangu tukufu ya Tanganyika,bunge la tanganyika...kwa ufupi tupewe nafasi ya kujadili aina ya muungano tunaoutaka!
 
kulingana na taarifa ya ITV JK amekubali kukutana na chadema. Je atafanya busara kusikiliza na kuelewa watakayomweleza?

Congrats Mr. President. You have nothing to loose in ensuring that we have a Super Constitution. You have chosen the right track and we are proud of you.
 
Muungwana ni vitendo!kwani alishawahi kataa kukutana nao?kasema hatosaini?kasalimu amri wapi?acha uchochozi na ushabiki usio na hoja
 
Huyo ndio Rais wa wote, wanaomkubali na wasio mkubali, Namna hiyo Kikwete, umewakata Ngebe kama kwenye katiba, walitaka ukatae wapate kufanya maandamano.

Sasa wewe umekubali wao ndio watataka wakupangie muda watafute sababu ukatae. Ngoja tuone.

Sina ushabiki wa kivyama. Rais JK amefanya uamuzi wa busara. Nchi yetu na maisha ya Watanzania ni muhimu kuliko vyama vya siasa, kuliko wabunge, kuliko Rais au mtu mwingine yeyote. Viongozi wa CHADEMA na Rais mjadili kama Watanzania na wala siyo kama WanaCHADEMA na wanaCCM. Ushabiki wa kisiasa unapofusha hekima. Msiende kwa nia ya kushindana bali kwa nia ya kutaka tupate katiba nzuri inayozingatia haki ya watu wetu wote. Sote, nchi hii ni yetu, hakuna aliye na haki zaidi kuliko mwingine. Kwa hili, JK nakupongeza, hekima yako imezidi ya CCM. Watanzania hawatakukumbuka kwa vile ulikuwa Mwenyekiti wa CCM au kwa vile ulikuwa Rais bali watakukumbuka kwa kile ulichowaachia. Mungu awajalie hekima wote mtakaoshiriki kwenye mkutano huo. Mungu ibariki Tanzania, tunataka tuwe na katiba ya mfano, katiba iliyo njema na iliyopatikana kwa amani na mshikamano wetu. Hilo likitokeo, itakuwa ni sifa kwa Taifa letu na sifa kwako binafsi kwa kizazi hiki na vingi vijavyo.
 
kulingana na taarifa ya ITV JK amekubali kukutana na chadema. Je atafanya busara kusikiliza na kuelewa watakayomweleza?

=============
UPDATE
=============



Fungua attachment usome zaidi

Mods, ikiwezekana tunaomba ubadilshe subject ya hii thread, iwe "Kikwete Kukutana na Chandema". Hili ni jambo la kitaifa zaidi ya kishabik.
 
JK atakosa nini asipokuja Arusha? bado ni rais na wengi wanamuunga mkono.

Arusha inamhitaji Rais kuliko ambavyo rais anahitaji arusha tumia akili siyo bange lol

jk na sisiem yake tuwapeleke wapi hapa A town? Yani ungekuwa unajua wakazi wa hp walivyochafukwa na mioyo wala usingedhubutu kuongelea mambo ya sisiem hapa.
 
jk na sisiem yake tuwapeleke wapi hapa A town? Yani ungekuwa unajua wakazi wa hp walivyochafukwa na mioyo wala usingedhubutu kuongelea mambo ya sisiem hapa.

Arusha unaongelea wapi? arumeru, monduli, au ngaranaro??

Unajua nyie cdm hapo stendi mnafikri mko wengi sana na hiyo ndio arusha?? big joke
 
.......tusibeze, angekataa tungepiga kelele, sasa kakubali, kaonyesha busara; hapa nimempenda kwa hili; mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! silifurahii sana neno kasalimu amri kama lilivyotumika na baadhi yetu, kwa maoni yangu, halipo ki-hekima, kuna wakati tufikiri kama nchi hii ni yetu sote, naamini JK ameguswa hivyo, BRAVO JK
 
Jk inaonekana kila akilala anaiota chadema maana siku hizi ktk hotuba zake lazma awataje chadema.
Anyway, asije akaleta ulaghai kama walivyowaletea CUF.

Let us think positively. Tuamini kuwa ana nia njema mpaka hapo itakapodhihirika vinginevyo. Tukumbuke kuwa Rais JK amekuwa na mtazamo tofauti na viongozi wenzake ndani ya serikali na CCM kuhusiana na katiba toka mwanzo. Sijawahi kuwa shabiki wa JK, na ninaamini amefanya makosa mengi katika utawala wake LAKINI kwa uamuzi huu nampongeza kwa moyo wangu wa dhati. Tusimchukie JK kwa vile tumeamua kumchukia au kwa kufikiria kuwa hawezi kufanya jambo jema, tumlaumu alipokosea na tumpongeze na kumpa nguvu pale anapofanya vema. Pale anapofanya vema, naomba tumpongeza, la sivyo tutamkatisha tamaa na kuona kuwa hakuna chochote anachoweza kufanya hata kama ni kwa matakwa yetu, tukakikubali.


KWENYE HILI NAMPONGEZA JK. Akifanikiwa kusimamia mchakato wa katiba, ukaenda vizuri, tukapata katiba nzuri, hakika hiyo itatosha kufuta makosa yake yote. Matatizo mengi ambayo nchi hii imepitia chanzo chake ni katiba tuliyo nayo, na hakika tuna bahati kwa kutokupigana kutokana na katiba hii.
 
Kwa mtazamo wa JK matatizo ya nchi hii ni CHADEMA na sio utawala wake wa Kijinga, anaacha kukomaa na matatizo tuliyonayo yy na wenzie kila siku CHADEMA CHADEMA Jamani jamaa anaboa<BR>
 
Kama ningekuwa mshauri wa JK, hana sababu ya kusaini muswada huu mapema kabla ya kukutana na CDM, kisha asubuhi yake unaingia ktk Luninga na kulitangazia Taifa amesitisha kusaini muswada baada ya kugundua makosa machache yafuatayo...Hapo anachukua baadhi ya vipengele lakini muhimu kuurudisha muswada bungeni. Sifa zote zitarudi kwake after all yeye ndiye mwisho wa treni..

CDM lazima wazingatie kwamba he is the President na mwezeshaji wa zoezi hili hivyo ana mamlaka makubwa sana ya kuwezesha ama kutowezesha..na hata wayatakayo wao marekebisho yanaweza fanyika na kurudi tena kwake ambaye ana uamuzi wa mwisho..Na CDM mkilalamika tena hapo watu watajua nyie ndio mnaikwaza Katiba...
 
Huyu Jakaya kukubali ni kazi yake kwani hawezi kusema kuwa anatawala tanzania akakataa kusikiliza watanzania, vingekuwa vichekesho kwani siku moja akihutubia taifa alisema anawashangaa wanaomkataa watake wasitake yeye ndiyo rais wao hivyo warudi kundini. Hiyo kauli angeifutaje?
 
Lazima aufyate mziki wa cdm si ashauona ulivyo.

aliye andika hii thrd jamani...inabid jf muwe waangalifu, eti huyu nae ni great thnker! hivi jk amesalimu amri kwa lipi? wale ni wananchi wake wamemuomba kuonana nae, hili ni ombi lakn kwa kuwa ni rais mwenye busara kw wananchi wake amekubali...ishu ni je, atakubali hayo wanayokwenda kumueleza au ndo umaarufu kama kawaida yao eti tumeonana na rais na kumshka mkono...au wanaenda kuomba umoja wa kitaifa?
 
Back
Top Bottom