Sio tatizo sana. Umeandika kwanza halafu baadae utafikiri ulichokiandikaHakika usemi huu umetimia "mtoto akikunyea mkono hautakiwi kuukata na badala yake unausafisha na maji". Si kitu cha ajabu kuona mtoto wako uliyemzaa anajaribu kujitutumua huku akijua fika kuwa wewe ndiye Baba yake, CHADEMA ni kama mtoto aliyepotoka na Sasa ametambua ya kwamba alifanya makosa na sasa anarudi nyumbani ili kuanza maisha mapya. Kwa maana hii Baba hana sababu ya kukataa kumkaribisha nyumbani kwa kuwa si yule tena aliyepotoka bali ni mtoto mwingine.
Umuhimu wa Baba kukubali kumpokea mtoto wake aliyeshindikana unatokana na mambo mengi, Mtoto huweza kubadilika tabia kutokana na makundi yanayomzunguka na hivyo kujikuta akifanya vitu visivyotarajiwa na hususani kile kipindi cha "Barehe" au anapopevuka na hivyo kuanza kujiona yeye ndiye yeye au inawezekana alikwisha pevuka lakini kwa bahati mbaya mawazo ya maisha yake ni ya utegemezi toka kwa wengine na hivyo siku zote ataendelea kuwa na mawazo tegemezi, hii ni sawa na kusema "TUMEAMBIWA NA MBOWE TOTOKE NJE YA BUNGE " lakini mtoto hapati nafasi ya kujiuliza na hata kama akipata nafasi hana uwezo wa kujua la kutenda au kutafakari kwa kina, Kwa hatua hii mtoto anahitaji maombi pekee toka ndugu zetu wakristu au dua kwa ndugu zetu wa kiislamu.
Nimatumani yangu maombi kwa njia ya sala au dua limeanza kufanya kazi au kipindi cha "Barehe" cha kujifanya mjuaji kimepita na sasa mtoto ametambua makosa aliyoyafanya na sasa anasema "BABA NARUDI NYUMBANI".
HONGERA MWENYEKITI WA CCM TAIFA.