Kikwete akubali kukutana na CHADEMA

kulingana na taarifa ya ITV JK amekubali kukutana na chadema. atafanya busara akisikia na kuelewa watakayomweleza
mkuu nakuomba ubadilishe heading ya hii thread kwa sababu sioni kama ina manufaa
  1. Raisi kuonana na wananchi wake sio jambo baya tusitumie kusalimu amri inaonekana kama kuna ushindani kati ya raisi na CDM
  2. Tukiendelea kutumia heading ya thread hii inaweza ikawa ikasambaa zaidi na kufanya raisi kushindwa kuyapokea mawazo ya CDM kwa kigezo cha kuona CDM itaonekana kushinda na ccm kushindwa
  3. kwa sababu lengo letu ni kupata katiba itakayotulizisha watanzania kwa njia nzuri na wasii wanachadema wenzangu tuachane na ushabiki wakivyama tuangalie lengo kuu
  4. mtoa mada na mods/invisible jaribuni kuliangalia suala hili
 
Hivi Rais kukubali kukutana ni kuvyata..mm! nafikiri ni muungwana na ana busara

Hivi Rais awaogope chadema kwa lipi hasa?? JK haogopi hoja mkuu??

Kama kukutana na cdm ni uoga I beg to differ siyo kila kitu mnatafuta umaarufu.

Kwa hapa mkuu Topical nakubaliana na wewe, kukubali kukutana nao cdm c jambo baya hata kidogo na wala c 'kuufyata" (neno bovu kabisa) ni busara,kuhusu kuyatekeleza ama kutoyatekeleza ni suala jingine kabisa, let him (mr president) awasikilize.
 
Hapa hakuna anayetafuta sifa. Ni kwamba ana option moja tu. Akubaliane nao. Asipokubaliana tu, tunalianzisha na this time mvua iliyonyesha na kuwasaidia kuharibu movie tuliyoianzisha Arusha haitawasaidia tena. Tutahakikisha tunaikomboa nchi!.

Huwezi kufanya chochote, ni masifa kwenye keyboard period!

Acha wenye busara wakae (wafunge ndoa) wewe utanywea kama maji ..lol
 
As long as wote lengo letu ni ustawi wa Taifa letu twangoja feedback ya kikao chao
 
JK kama amekubali kukutana na kamati ya CDM sisi wazalendo halisi tunampongeza.Lakini atakapo kubali yale masuala yote ya msingi kwa mustakabali wa nchi yetu tu tutampongeza zaidi.
 
Kuwasikiliza atawasikiliza kutekeleza ndo kazi si tuwajua mambo ya mafisadi wanavuta kamba kwao tu
 
Muafaka Toleo La Pili is on the table.

Zitto Sinunuliki Kabwe, Makamu wa nne wa Rais.

John Mnafiki Shibuda, Naibu wa Kwanza wa Waziri Mkuu.

David Migogoro Kafulila, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Lyatonga Mganganjaa Mrema, Waziri wa Nchi, Uratibu na Bunge.
 
mkuu nakuomba ubadilishe heading ya hii thread kwa sababu sioni kama ina manufaa
  1. Raisi kuonana na wananchi wake sio jambo baya tusitumie kusalimu amri inaonekana kama kuna ushindani kati ya raisi na CDM
  2. Tukiendelea kutumia heading ya thread hii inaweza ikawa ikasambaa zaidi na kufanya raisi kushindwa kuyapokea mawazo ya CDM kwa kigezo cha kuona CDM itaonekana kushinda na ccm kushindwa
  3. kwa sababu lengo letu ni kupata katiba itakayotulizisha watanzania kwa njia nzuri na wasii wanachadema wenzangu tuachane na ushabiki wakivyama tuangalie lengo kuu
  4. mtoa mada na mods/invisible jaribuni kuliangalia suala hili

Kwel kaka. Naunga mkono. Ni moja ya wajibu wake. Unadhani yy haupend urais? Hawez kubisha! Kwani nguvu ya uma hata mimi naiogopa aisee!!
 
Arusha kuna nini? sana sana Arusha wanamhitaji JK kuliko JK anavyowahitaji Arusha???

Wewe upo Dodoma. Huijui Arusha! Sio yeye peke yake ambao hatuwahitaji. Chama chake chote hatutaki kukisikia, na yeye anajua hilo. Ndio maana aliingia mitini alipotaliwa kuja kuzindua nchanjo ya watoto! Kama hujui, pole!
 
Naona kasoma nyakati na ishara hasa kwa kuyaona yanayotokea Misri kwa sasa na huku jukwaa la katiba nalo nikijipanga kwa maandamano ya nchi nzima!
 
Ingekuwa ajabu kama angekataa kukutana na kamati hiyo ya chadema kwani mbali ya kuwa nao ni watanzania ambao yeye ndio rais wao chadema pia ndicho chama kikuu cha upinzani. Hivyo sioni ajabu yoyote rais kukutana na chadema.
 
Wewe upo Dodoma. Huijui Arusha! Sio yeye peke yake ambao hatuwahitaji. Chama chake chote hatutaki kukisikia, na yeye anajua hilo. Ndio maana aliingia mitini alipotaliwa kuja kuzindua nchanjo ya watoto! Kama hujui, pole!

JK atakosa nini asipokuja Arusha? bado ni rais na wengi wanamuunga mkono.

Arusha inamhitaji Rais kuliko ambavyo rais anahitaji arusha tumia akili siyo bange lol
 
Hekima ndiyo jawabu la mustakabali wa katiba bora itakayowafaa watz wa leo na vizazi vijavyo.
 
Ngoja tusubiri wakutane na iwe ni dhamira ya kweli tu.ila tukiangalia upande wa pili,Match tayari imeshakubaliwa timu moja list iko hivi1.Proffesor Mwesiga Baregu2.Proffesor Abdala Safari3.Full back ya kushoto Dr W Slaa4.Mh.Said Arfi5.Said Issa Mohamed6.Mh.Tundu Lisu7.Mh.F Mbowekama kuna mtu anafununu upande wa magamba list itakuwaje atuarifu tuanze kupata ulinganifu wa kujenga hoja utakaaje siku hiyo
 
Back
Top Bottom