Kikwete aahirisha ziara ya Mbeya

KWANZA NAWAOMBA SAMAHANI SANA KWA KAULI NILIOTOA JANI KWA WANA FORAM.
Nilisoma ile hutuba vibaya na niliilewa viba ila jioni niipitia kwa umakinip; Na nasema: HONGERA SA NA RAISI. HONGERA SANA SPIKA SITA kazi kwenu wabunge mkae muijadili kama ambavo MH:Spika alivosema mtupe majibu;
 
...hii ziara ya mbeya ..inategemea ramli nini..maana kila wakati inaahirishwa bila sababu...mbeya jamani mmemfanya nini huyu mwoga ..... Mbona mikoa mingine ameshatembelea kwa ziara rasmi hadi mara 3.....mbeya kunani..????..au ni nchi nyingine??

Mimi niliweka kaushanga kangu pale Mwanjelwa kuelekea Tukuyu, akikanyaga tu, mambo yangelikuwa mabaya. Inaelekea walinzi wake wakali, wanashutuka kila mara. Inabidi niliondoe la kwangu ili rais aweze kutembelea Mbeya salama.
 
Toka lini ramadhan ikazuia shughuli yeyote? kwanza kuchapa kazi mwezi huu kutatuonyesha ukakamavu wako.Tunalisha nchi nzima halafu tunadharauliwa hivi? Wanajua Mbeya huwa hatuweki kitu rohoni tutamwambia ukweli, kupuuza au kuyafanyia kazi hiyari yenu
 
Swala la yeye kwenda US halikuja leo, mwingine kasema kutakuwa na mitihani ya darasa la saba, siku za mitihani hazikupangwa leo, pia kuhusu mfungo sio jambo geni wala si kwamba hawakujua itakuwa wakati gani. Vinginveyo mseme kwamba wanaoandaa hizo ziara za Kikwete ni wajinga wa kalenda ya nchi hii maana hawajui kutakuwa na nini kesho wala keshokutwa. Kuna jambo hapo, kama sio kugongana vichwa basi huenda ni hofu ya kuzomewa aliyoitaja mwenzetu mwingine hapa, hii nayo ni silaha nzuri. Tunaomba tuitumie tupatapo nafasi, natamani ingekuwa imetumika bungeni akihutubia.

Na mimi nashangaa kwamba Ikulu hakuna kalenda kuonesha mitihani inafanywa lini. Jk ni mwisilamu hajui lini mifungo?? Itakuaje ziara ipangwe bila kufuata kalenda??Hivyo nivisingizio ambavyo havina maana Mkuu wa Mkoa wa Mby aliwekwa pale kumkomoa Mwandosya na hajawahi kufanya kitu cho chote kusaidia mkoa ni malumbano tu na uongo kwa mafisadi. Kwanza alimwambia Jk akiija Mby atazomewa. Aliposikia Rais anakuja hakutaka apangiwe jimboni kwa Mwandosya eti atapata umarufu zaidi!!!.Safari hii katoa visingizio vya kijinga, sijui next time atasemaje!!
 
Mkuu,

Kweli kuna haja ya kutumia lugha kama hiyo dhidi ya rais wa nchi? Pia lazima ujue kwamba statement kama hiyo sio tu kwamba unamtukana JK peke yake lakini unalitukana na kabila lake lote. Iweje makosa ya JK yaingie kwenye kabila zima?

Uhuru bila nidhamu ni fujo.

Samaki moja akioza--------
 
Rais atatembelea Mbeya tarehe 9 mwezi wa kumi( ilikuwa iwe tarehe 23 mwezi wa kumi).Wakati huo, mfungo wa Ramadhan utakuwa umekwisha lakini F. 4 watakuwa kwenye mitihani itakuaje?? Maana mitihani ya darasa la saba ilikuwa sababu Rais kutokwenda ziarani Mbeya!!!
 
Mbeya kuna watu wenye akili timamu huyu msanii anajua na ndiyo maana anaogopa kwenda huko. Kuna Mwandosya, Mwakyembe, Mwakyusa nk.
 
Mbeya kuna watu wenye akili timamu huyu msanii anajua na ndiyo maana anaogopa kwenda huko. Kuna Mwandosya, Mwakyembe, Mwakyusa nk.

Sio Vizuri kumuita Rais wetu (Tanzania) kuwa ni Msanii.
Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ni Rais wa Nchi.
Tafadhali apewe Heshma yake.
Na hao wote uliowataja ni wafuasi wake na wanamuheshimu, na wanajua kuwa ni Rais wao.
 
Heshima zenu wazalendo wenzangu,

Nadhani kwenye forum hapa ndo mahala pekee pananoweza kuonyesha mfano wa ukomavu wa kisiasa. Thus, hata kama humpendi JK, but as The president of our country, ni vema akaheshimiwa. Tuna haki ya kuchallenge yale tunayo yaona kama sababu zinazodumaisha maendeleo, but it should be in a dignified manner. Otherwise kumridicule Rais wa inchi just because humpendi au ni mkwere ni dalili mojawapo ya jazba na immaturity.
 
Rais JK hajatembelea mikoa kama mitano hivi toka aingie madarakani, sasa kwanini kila saa muandame mkoa wa Mbeya tu?

Pelekeni siasa zenu kwingine, Mbeya tumechoka kutuchagulia maadui na marafiki.

Mbona hatusikii mkisema JK anauchukia mkoa wa Morogoro ndio maana hajaenda huko mpaka sasa?
 
Mtanzania
tusaidie mikoa ambayo hajatembelea mimi naanza
1.Rukwa
2.

Kuna gazeti nilisoma mwanzoni mwa mwezi huu na walitaja mikoa mitano ambayo JK hajaitembelea. Nakumbuka ilikuwa Mbeya, Morogoro na mingine mitatu ambayo nimeisahau.

Sasa haya mambo ya kila siku kuongelea Mbeya ni ujinga tu wa kutaka kuwafanya Mbeya waache kuongelea mambo ya maana na kukazania kuongelea migogoro ya siasa ambayo haipo.

Binafsi nimechoshwa na hiyo migogoro, imefika wakati wa kuipiga vita na kuanza kuongelea maendeleo ya mkoa.

Hii migogoro ya kupandikizwa na watu ambao hata hawaujui mkoa wa Mbeya ni ujinga tu. Kwanini msipeleke huo ujinga kwenye mikoa yenu? JK kama angekuwa anawachukia hao maprofesa asingeliwapa nafasi za juu kwenye serikali yake.

Katika watu ambao walipambana na JK kwenye nafasi ya urais ndani ya CCM, ni prof. Mwandosya tu ambaye ni waziri, sasa hiyo chuki mnayovumisha kila siku inatoka wapi?
 
JK ..............na Nchi yetu inaitwa Tanzania...........Urais Kazi sana jamani sio lele mama....
 
Sio Vizuri kumuita Rais wetu (Tanzania) kuwa ni Msanii.
Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ni Rais wa Nchi.
Tafadhali apewe Heshma yake.
Na hao wote uliowataja ni wafuasi wake na wanamuheshimu, na wanajua kuwa ni Rais wao.

Ni vema kuwa wengine bado hawajakata tamaa. Lakini JK akizidi kuipelekesha TZ kama ilivyo sasa, atafanikiwa kutukatisha tamaa wengi wetu, na matokeo yake wengi tutamwita kwa jina lake sahihi kulingana na matendo yake, 'Msanii'. Ni utashi wa binadamu kutomheshimu mtu asiyefanya kazi barabara.
 
Sio Vizuri kumuita Rais wetu (Tanzania) kuwa ni Msanii.
Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ni Rais wa Nchi.
Tafadhali apewe Heshma yake.
Na hao wote uliowataja ni wafuasi wake na wanamuheshimu, na wanajua kuwa ni Rais wao.

Mshaurini basi afanye mambo kama raisi kwakweli ni vigumu kwangu kumuita mheshimiwa hiyo heshima iko wapi kwa jinsi alivyoshughulikia mafisadi au?
 
Lazima kuna kitu uko mbeya si bure!
Ni mara ya 3 sasa,labda anaogopa kuzomewa kama rafiki wa mafisadi.
 
Kuna gazeti nilisoma mwanzoni mwa mwezi huu na walitaja mikoa mitano ambayo JK hajaitembelea. Nakumbuka ilikuwa Mbeya, Morogoro na mingine mitatu ambayo nimeisahau.

Sasa haya mambo ya kila siku kuongelea Mbeya ni ujinga tu wa kutaka kuwafanya Mbeya waache kuongelea mambo ya maana na kukazania kuongelea migogoro ya siasa ambayo haipo.

Binafsi nimechoshwa na hiyo migogoro, imefika wakati wa kuipiga vita na kuanza kuongelea maendeleo ya mkoa.

Hii migogoro ya kupandikizwa na watu ambao hata hawaujui mkoa wa Mbeya ni ujinga tu. Kwanini msipeleke huo ujinga kwenye mikoa yenu? JK kama angekuwa anawachukia hao maprofesa asingeliwapa nafasi za juu kwenye serikali yake.

Katika watu ambao walipambana na JK kwenye nafasi ya urais ndani ya CCM, ni prof. Mwandosya tu ambaye ni waziri, sasa hiyo chuki mnayovumisha kila siku inatoka wapi?

Mwalimu umesema vema,

Kuna watu wanapenda ku trivialize mambo tu, sasa hao wa mikoa mingine mbona hatusikii kulalama? au mnadhani Rais huwa anakata mshiko kwenye ziara? afterall JK mwenyewe kasema hatembei na fuko la pesa so kha!
 
Tumemchoka huyu wakala wa mafisadi... wala asije... abaki hukohuko ukwereni na mambo yake ya kikwerekwere...

Kama mmekosa yakuandika ni afadhari msome tu. Ni jambo la busara kama kungekuwa hata na tone la hoja, this is the lowest of you. Pamoja na kuwa ana mabaya yake lakini hatuna rais mwingine ndio huyohuyo, kwa hiyo anastahili kupewa heshima yake kama Rais, mtanzania, mtu na aliyetoa mchango kwa taifa. Kuna mabaya mengi, ambayo yanaweza kutufanya tumchukie lakini mazuri pia yapo. sio busarakwa mtu mzima kuandika kitu kama hiki.
 
Back
Top Bottom