Kikwete aahirisha ziara ya Mbeya

Ogah,

Zinaweza kuwa ni DATA za kijiweni. Lakini na wewe huoni kama hujaitendea HAKI akili yako kwa kuhitimisha haraka haraka! Au ndio yale aliyoyasema BWM kwamba watanzania tu wavivu wa kufikiri (naongeza kufanya utafiti). Changamoto yangu kwako kabla hujahitimisha HITIMISHO lako fanya utafiti kwanza. Wako wengi tu wanajua hili ninalolisemea............

1. kwamba watanzania tu wavivu wa kufikiri.......kwi kwi kwi.....yaani wewe ukakubali story za vijiweni kuwa pesa zilizopaswa kupanua mwanza airport ndio zilijenga/zilitumika kujenga Uwanja wa Mbeya!!!.......

2.Endelea na utafiti gottee...........

Ushauri........unaweza kucheck na watu wa mamlaka ya viwanja vya ndege ukitaka information sahihi kuhusu viwanja vya serikali
 
Mimi au wewe nani acheki na Mamlaka ya Viwanja vya ndege? Mimi sina mashaka na source wangu, wewe ndio una mashaka hivyo basi nenda huko Viwanja vya Ndege ukacheki na wakikuzungusha Nenda Wizarani na mahala pazuri pa kuanzia unawauliza zile fedha za Ukarabati wa Uwanja wa Mwanza ziliishia wapi?
 
....gottee,

ulikuwa ni ushauri tu...........otherwise....endelea na data zako za vijiweni

NOTE: don't get me wrong........kuna data za vijiweni ambazo ni credible.....lakini si hizo ulizozianzisha
 
Hi Thread ukaimbiwa uitungie kichwa cha habari say kisingekuwepo unaweza kuibuka na paragraph ya maneno Buku!!!!!!!!!!!!!!!!!! Lol
 
Gottee,
Nakuhakikishia kitu kimoja, sina nia ya kuzuia mijadala kuhusu matatizo mkoani Mbeya. Binafsi ni mwumini wa uhuru wa kujadili jambo lolote.

Ninachopinga mimi ni watu kuja na madai makubwa sana ambayo hayana ukweli. Inabidi tuwe responsible kidogo kwasababu haya mambo yote yanaikwamisha Mbeya. Kuna vijana kule kwasababu ya ujinga wao, wanaona kila kitu kilichoandikwa magazetini ni ukweli na wanaanza kuamini.

Hata nikiwa Kyela au Mbeya nawaambia hivyo hivyo kama nilivyoandika hapa, kwamba sio kweli. Ukiwauliza umesikia wapi, wanasema yaliandikwa gazetini.

Prof. Mwandosya na JK walikuwa makundi tofauti na sio marafiki wa karibu kwa miaka mingi, huo ni ukweli lakini je kunachuki kubwa kati yao kwasasa? Siamini hivyo na wala sijaona ushahidi huo.

Kuna watu kwenye kundi la JK wangependa kuendeleza huo mgogoro kama ambavyo wangependa kuendeleza mgogoro wa JK na Salim. What matters here ni msimamo wa JK na profesa mwenyewe. Pia kuna watu wa prof. ambao wangependa kuendeleza mgogoro na JK.

Kuna watu wanafikiri hata kuanguka kwa Lowassa ni njama za prof. eti Dr. Mwakyembe alitumiwa na prof. kumlima JK na kundi lake. Jamani, ina maana wajumbe wale wote wa ile kamati, wataburuzwa na Mwakyembe kwa faida ya prof.?

Kuhusu vijana kumwita Prof. rais wao, kuna tofauti gani na vijana wa CHADEMA kumwita Mbowe rais? Kuna tofauti gani na TLP au NCCR huko nyuma kumwita Mrema rais? Ni kundi dogo la vijana ndio wanaendeleza hayo mambo kwenye vijiwe vyao badala ya kwenda kwenye uzalishaji mali.

Kule Mbeya kuna watu wamefanya ni career kupeleka majungu kwa Mwakipesile au Mwakyembe. Na kukiwa na wanasiasa njiwa, ni rahisi mno kukubaliana na watu kama hao ambao kwa kweli ni waganga njaa.

Nikupe mchapo wangu mmoja wa kweli. Nikiwa likizo Kyela, wakati napita ile barabara ya Kyela, nilimwona diwani mmoja ambaye mimi nilisoma naye msingi, alikuwa pamoja na diwani mwenzake ambaye nilikuwa simfahamu kabla ya hapo. Nikaenda kuwasalimia, tukaanza michapo mbalimbali, baadaye wakaniomba kama kuna mtu namjua Dar awasaidie, wametumwa na wilaya kwenda kutafuta wanunua Kokoa wameuza kiasi gani nje ili wajue kama Halmashauri ya Kyela imelipwa ipasavyo. Mimi nikatafuta contacts zangu na kuwaunganisha na mhusika.

Baada ya siku kama tatu, jamaa yangu mwingine ambaye ni rafiki yake Dr. Mwakyembe akaanza kuniuliza juu ya mimi kuongea na hao madiwani. Akasema kuna wapambe wa Dr wameniona na habari imeenda kwake. Nikacheka tu, hata Dr. naamini aliwadharau tu. Wengine tumekuwa tukiambiwa tunataka kugombea toke 95, 2000, 2005 na sitashangaa tukitajwa 2010. Kumbe hao madiwani wawili ni watu wa mkuu wa mkoa, mimi hata sikujua ingawaje huyu niliyesoma naye niliwahi kusikia alimwunga mkono Mwakipesile mwaka 2005.

Mimi wanaoniuliza nawaambia wazi, siku ikifika nitasema mwenyewe, wala sitasingizia nimefuatwa na wazee au nini. Nikiamua kuingia kwenye siasa kila mtu atajua wala hakuna haja ya kuficha. Kwasasa muhimu ni kwamba tuna viongozi wacha watimize majukumu yao bila bugudha za majungu.

Huko mikoani kuna madudu mengi sana, ndio maana wakati mwingine mimi huwa nachukia juu ya jambo hili. Majungu ya kisiasa na ushirikina yanaua zile wilaya zetu.

Mtanzania,

Najua kuhusu mahusiano ya JK na MJM tangu wakiwa kule Wizara ya Nishati na Madini, JK akiwa Waziri na MJM akiwa Katibu Mkuu. Kuna mambo mengi sana ambayo nimekuwa najiuliza kuhusu Prof. MJM.

Juzi ulisema kwamba baba yake Thomson, Mzee Apson alimsaidia sana JK kuingia pale kwenye Jumba Jeupe. Ninajiuliza ni LINI na KWA NINI Apson aliamua kumtema MJM. Nasema hivyo nikijua Apson ndiye amechangia kwa kiasi kikubwa kumnyanyua MJM hadi kufika pale alipo. Kumbuka MJM sio kada wa CCM na wala hakukulia CCM. Kutoka Chuo Kikuu kwenda serikalini na kuwa Kamishna Wizarani na baadaye kupanda kuwa Katibu Mkuu na baadaye kurudi Chuo Kikuu halafu kugombea Ubunge na kuwa Waziri Mwandamizi. Nimeita Waziri Mwandamizi kwa sababu alianza kuongoza Wizara kubwa tu.

Nakumbuka ule mwaka 2000 pale bungeni Dodoma walipokuwa wakiapishwa Wabunge, habari zilivuma kwamba Mwandosya anaukwaa Uwaziri Mkuu. Ungeona jinsi Wabunge walivyokuwa wanapigana vikumbo kutaka kupiga naye picha! Haya ni huyu MJM tena ndiye aliingia kwenye TATU bora za Wagombea wa CCM. Nani aliyemnyanyua hadi pale? Mimi ninaamini 'mkono' wa Mzee Apson ulikuwepo ila tena najiuliza ni kwa NINI na LINI aliamua kumtosa.

Naelewa vizuri uhusiano wa karibu wa MJM na Apson. Ukweli ni kwamba mimi Mzee Apson nilikuwa namuona sana nyumbani kwa Profesa Mathew Luhanga. Hata kama kuna birthday ya mtoto mdogo wa Luhanga lazima yule Mzee aje pale nyumbani kuanzia Mtaa wa Kileleni pale UD na hata alipohamia nyumba namba moja. Najua MJM ndiye alichangia kuwanyanyua Luhanga na kaka yake yule Baruan Luhanga aliyekuwa Tanesco. Hawa jamaa pamoja na kusoma lakini ni 'vyapombe' wa kupindukia. Nani asiyemjua Mathew Luhanga yule 'bonge la mlevi' pale Lufungila na UDASA Club. Aliikuwa hamalizi wiki kabla hajampiga mtu ngumi na ndio alipopewa jina la Tyson. Lakini huyu jamaa alitoka pale UHANDISI akiwa hajaongoza hata kitengo chochote na kunyanyuliwa hadi kuwa CADO (Chief Academic Officer) nafasi ambayo kwa wakati huo ndio alikuwa msaidizi wa VC. Alikaa kwenye nafasi hiyo kwa miezi SABA tu na kupanda kuwa VC na kuvunja rekodi ya kuwa VC aliyekaa kwa muda mrefu kuliko wengine. Nani asiyejua kipindi cha Luhanga ndio UwT walimwagwa kama njugu pale UDSM. Baruan Luhanga ambaye alikuwa Ofisa wa kawaida kule Tanesco Kilombero aliletwa mjini haraka haraka akapanda hadi kuwa MD wa Tanesco. Najua mafaili ya hawa jamaa pale UwT yameandikwa hawajawahi hata kunywa pombe!

Nimewataja hawa jamaa nikiwa najua hawa walipanda ngazi kwa haraka kwa sababu ya Mwandosya kupitia kwa Apson. Kama jamaa hawa walivyopanda vyeo haraka ndivyo Mwandosya naye alivyopanda kwa kuzingatia kwamba hakuwa na mashiko ndani ya CCM! Profesa Luhanga hawezi kuongea sentensi tatu kabla hajamtaja Mwandosya. Kila zuri duniani ni yeye na Mwandosya ndio wamefanya. Wale waliofundishwa naye pale Uhandisi watakubaliana nami. Ni Luhanga huyu huyu alimpa ajira ya kudum MJM pale UD alipotoka Serikalini wakti akijua jamaa alikuwa na ajira ya kudumu pia pale CEST.

Inasemekana Mzee Apson ndiye ambaye alifanya kila njia MJM awe Waziri Mkuu. Inasemekana watu wa kada ya kati pale UwT ambao hawakuwa na mahusiano mazuri na Apson ndio walivujisha jina la Mwandosya pale Bungeni wakijua Ben hakupenda mambo yake yavuje mapema. Zoezi hilo lilifanikiwa kwani taarifa zilitumwa Chamwino kwa BWM kwamba Waziri Mkuu 'keshatangazwa' na Ben kwa hasira aliamua kumrudisha Sumaye kwa kuwa hakuwa na chaguo jingine la haraka. Enewei haya ni ya kijiweni tu.

Usalama wa Taifa pia unahusishwa mwaka 2002 kumdhalilisha JK kwa kumpa nafasi ya 13 katika zile kura ambazo tunaambiwa wao ndio walisimamia zoezi la kuzihesabu.

Mengi yalishasemwa nyuma khs Profesa MJM. Tangu akiwa Wizarani. Unakumbuka kashfa ya TTCL na Wawekezaji na Binti yake Sekela? Unakumbuka kashfa ya CEST. Prof anatuhumiwa kujinyakulia ile NGO ya CEST na kuifanya mali yake wakati ilipaswa kuwa ni taasisi ya utafiti ndani ya UDSM. Unakumbuka Ofisi za CEST za kwanza zilifunguliwa kwenye nyumba yake ambayo ilikuwa haijaisha na kwa kutumia fedha za mradi huo nyumba ilimalizwa na kuwa Ofisi za CEST hadi magazeti yalipoandika ndio wakahamia Mikocheni. Unakumbuka zile Nissan Patrol pacha. Nyeupe na Nyekundu za CEST ambazo MWandosya alikuwa akitumia ile nyekundu na mkewe akitumia ile nyeupe hadi alipoandikwa gazetini ndipo alimpa mwenyekiti mwenza wa CEST profesa Luhanga ile nyeupe! Unakumbuka tuhuma kwamba TIPER ilikuwa ikichangia mamilioni ya fedha kwenye tafiti za CEST kwa kutumia mamlaka yake akiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini?

Unakumbuka Profesa Mwandosya alivyokiuka taratibu za ajira kwa kumwondoa kazini Kanali Nalingingwa aliyekuwa Mkurugunzi wa Tume ya Mawasiliano kabla haijawa TCRA. Ilibidi Dk Shein aliyekuwa akikaimu Madaraka ya Urais wakati BWM akiwa Uswis kwa matibabu alipoamua kumrudisha Nalingigwa madarakani baada ya kushauriwa na Waziri Mkuu Sumaye.

Unakumbuka Profesa alivyotumia nguvu nyingi kumtetea Profesa Nkhoma bungeni kuhusu ajira yake pale TCRA wakati alikuwa ana ajira nyingine Botswana.

Mimi naamini Profesa wako ana matatizo na nina imani anatumia nguvu zake za Kisiasa alizonazo Mbeya kumvuruga JK. Nawasilisha.
 
Gottee,

Umeandika mengi sana na asante. Hayo ya prof. kuwa waziri mkuu nimeyasikia ingawaje sina uhakika nayo kwahiyo afadhali nisiweke comments zangu.

Ukirudi kwenye ile article ya three Mwa's iliwahi kuletwa hapa. Prof. na watu wake wa karibu walipata mawazo ya ajabu kwamba angeweza kuwa rais. Mimi nilijua haiwezekani, hata kama ni supporter wa prof. Naijua CCM na najua mawazo yao. Prof. hakuwa na nguzo imara ndani ya CCM mpaka kuwa rais. Ilitakiwa awe na mtu kama Nyerere ili kuweza kuchaguliwa na CCM. Hata asingepata urais JK, basi nafasi hiyo ingeenda kwa Salim.

Apson ana uzoefu mkubwa na alijua nani atakuwa rais. Aliamua kwenda na mshindi na kwa kweli hakukosea maana sasa mambo yake yanaenda sawa.

Unaongelea ya prof. mbona unaacha ya Malecela? Hata mzee wetu huyu naye alidhani jamaa yuko kwao, lakini kumbe yeye aliamua kusaidia upande tofauti. Unakumbuka ile picha ya Malecela, Mahita, mkuu wa jeshi na Apson wakati wa harusi yake? Ilikuwa na maana kubwa sana.

Mwulize FMES, kwanini Mkapa akageuka haraka na kumwunga mkono JK? Kama Mkapa na kiburi chake kile aligeuka, Apson naye aliona ukweli kwamba asingeliweza kushindana na ukuta.

Tukiachia mambo mengine yote, Prof. is a very good man. Mimi sijawahi kufaidika kitu chochote na prof. wala yeye hata hanijui. Ukiongelea hayo ya akina Luhanga, nenda hata kwa akina prof. Msola na wengine, utaambiwa hayo hayo.

Katika jamaa zangu wote hao (the three Mwa's) prof. ni binadamu sana na ndio maana naamini ataendelea kuongoza kule Rungwe labda mpaka aamue kuondoka mwenyewe.

Ndio maana nasikitika ninaposoma na kusikia haya wanayomzulia kwani jamaa ni binadamu sana.
 
Ndugu nashukuru kwa ufanunuzi wako ni juu ya watanzania wenyewe watoe maamuzi baada ya kujiridhisha badala ya kufanya maamuzi kwa pupa au kuegemea habari zilizopotoshwa.Nashauri watz waanzishe utamaduni wa kulazimisha viongozi kupitia vyombo huru vya habari kuhojiwa kabla ya kuwachagua kupitia matangazo ya wapambe wao.Uwe ni utamaduni wetu kujenge ngos zisizo na mshikamano wowote na wanasiasa kama ile ya Zimbambwe(Zimbabwe Support Electoral Network) huu ulikuwa muungano wa asasi za kiraia zilizosaidia kuwaelemisha wazimbabwe uzito wa kura zao na matokeo tumeyaona.
 
Gottee,

Umeandika mengi sana na asante. Hayo ya prof. kuwa waziri mkuu nimeyasikia ingawaje sina uhakika nayo kwahiyo afadhali nisiweke comments zangu.

Ukirudi kwenye ile article ya three Mwa's iliwahi kuletwa hapa. Prof. na watu wake wa karibu walipata mawazo ya ajabu kwamba angeweza kuwa rais. Mimi nilijua haiwezekani, hata kama ni supporter wa prof. Naijua CCM na najua mawazo yao. Prof. hakuwa na nguzo imara ndani ya CCM mpaka kuwa rais. Ilitakiwa awe na mtu kama Nyerere ili kuweza kuchaguliwa na CCM. Hata asingepata urais JK, basi nafasi hiyo ingeenda kwa Salim.

Apson ana uzoefu mkubwa na alijua nani atakuwa rais. Aliamua kwenda na mshindi na kwa kweli hakukosea maana sasa mambo yake yanaenda sawa.

Unaongelea ya prof. mbona unaacha ya Malecela? Hata mzee wetu huyu naye alidhani jamaa yuko kwao, lakini kumbe yeye aliamua kusaidia upande tofauti. Unakumbuka ile picha ya Malecela, Mahita, mkuu wa jeshi na Apson wakati wa harusi yake? Ilikuwa na maana kubwa sana.

Mwulize FMES, kwanini Mkapa akageuka haraka na kumwunga mkono JK? Kama Mkapa na kiburi chake kile aligeuka, Apson naye aliona ukweli kwamba asingeliweza kushindana na ukuta.

Tukiachia mambo mengine yote, Prof. is a very good man. Mimi sijawahi kufaidika kitu chochote na prof. wala yeye hata hanijui. Ukiongelea hayo ya akina Luhanga, nenda hata kwa akina prof. Msola na wengine, utaambiwa hayo hayo.

Katika jamaa zangu wote hao (the three Mwa's) prof. ni binadamu sana na ndio maana naamini ataendelea kuongoza kule Rungwe labda mpaka aamue kuondoka mwenyewe.

Ndio maana nasikitika ninaposoma na kusikia haya wanayomzulia kwani jamaa ni binadamu sana.

Mtanzania,

Binafsi yangu napenda kusema nimeelimika na michango yako na wengine waliochangia kwenye thread hii. Yapo mengi ambayo mimi na wewe na wengine tunakubaliana nayo na nina imani yapo mengi ambayo mimi na wewe na wengine tukubali kutokukubaliana nayo.

Kwa yote hayo huu ndio mtazamo wangu.

1. Pamoja na yote mchakato wa Maendeleo ya Mbeya unapunguzwa kasi na Wanasiasa. Wanasiasa nao wangekubali kutokukubaliana na wakaamua kukaa meza moja. (Aliyeshindwa na Aliyeshinda) maendeleo yangeharakishwa kidogo.

2. Ningekuwa mimi Rais JK ningefanya jambo la maana kumuhamisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wa sasa John Mwakipesile. Hili lingeondoa ile taswira ya kwamba, JK alifanya vile ili kuwakomoa wapiga kura wa Kyela waliomkataa 'mwanamtandao' huyo katika kura za maoni. Pili hili lingeondoa ile dhana ya kwama Mwakipesile akifanya ziara za kiserikali kule Kyela inaonekana kama anakwenda kufanya Kampeni na pia lingeondoa UWEZEKANO wa Mwakipesile kufanya ziara kiserikali huku 'akijiandaa kurudi' 2010.

3. Profesa Mwandosya kama kweli HAJAVUNJA kambi yake, kama inavyodaiwa na 'wenzake' basi huu ulikuwa wakati mzuri sana wa kuvunja kambi hiyo. Hajachelewa. Madai haya tunaweza kuyapuuza lakini tunaweza tusiyapuuze pia. Mantiki ya kusema hivi ni kujiuliza kwa nini Salim Ahmed Salim Hatajwi kuwa hajavunja Kambi isipokuwa Profesa tu ndio 'anasingiziwa'?. Kumbuka hawa watatu ndio waliingia kwenye TATU bora.

4. Profesa aachane na mawazo ya kugombea Urais kwa sasa kama bado anayo. Hili litamsaidia hata kisaikolojia kuweza kujipanga upya na kufanya mambo mengine ya maana. Ukichukulia kuwa yeye ni Mwanazuoni aliyebobea kwenye NISHATI na MAZINGIRA. (Kumbukumbu zinanionyesha kuwa yeye ni miongoni mwa wanazuoni waliopanda haraka sana pale UDSM kwenye ngazi za kitaaluma nikimaanisha ni miongoni mwa Maprofesa wa mwanzo vijana) Anaweza kutumia nafasi hiyo kuingia kwenye anga za Kimataifa kwenye NISHATI na MAZINGIRA ukichukulia issue kama Global Warming.

5. Jimbo lake la Rungwe ni miongoni mwa majimbo yenye rutuba, uhifadhi mkubwa wa Mazingira. (I wish kungekuwa kwetu), Sasa Profesa angeongeza mkazo wa kuhifadhi na kuboresha mazingira kwa taaluma na umaarufu wake alionao kwa sasa.

6. Rais JK 'afunge safari' haraka kwenda Mbeya. (Taarifa za uhakika nilizonazo, Barabara ya kuingia Uwanja wa Sokoine imepitishwa greda kuandaa ujio wake) Akifika huko popote atakapohutubia ASISITE kuwaomba radhi Wananchi wa Mbeya kwa kuchelewa kwenda kuwatembelea, ambapo sasa anaweza kusema hilo lilizaa maneno mengi ya KIJIWENI kumbe hakuwa na nia mbaya. Yeye nina imani ni Mwuungana. Ada ya Mja Hunena na Muungwana ni Vitendo.

7. Rais JK akiwa Mbeya asisite KUWAKALISHA kitako wanasiasa wenzake. Yeye akiwa ni kinara wa Chama na Nchi pia ni lazima aonyeshe msimamo wake kwamba muda uliobaki kwake ni wa KUJENGA NCHI. BASI. Na si malumbano yasiyo na tija. Sipendi kuyasikia yale maneno, MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA lakini labda ndio wakati huu muafaka wa yeye ku-proove right or wrong, vinginevyo atueleze nani alimtia mdomoni maneno hayo ili 'tufe naye' mtu huyo.
 
Sio Vizuri kumuita Rais wetu (Tanzania) kuwa ni Msanii.
Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ni Rais wa Nchi.
Tafadhali apewe Heshma yake.
Na hao wote uliowataja ni wafuasi wake na wanamuheshimu, na wanajua kuwa ni Rais wao.

Usiwe mpumbavu na mnafiki. Watu kama nyinyi ndiyo mnawapa vichwa wapuuzi watupotezao hapa Tanzania.

Jakaya ni msanii aliyekomaa hilo si la kuficha, anastahili kuitwa hivyo na sababu za kumwita hivyo zipo na ziko hai. Sasa kama una sababu ambazo unaona kwamba Jakaya si msanii ebu niweke hapa. Na kumwita msanii nimemuheshimu sana kwani nikianza kumtaja kwa majina anayostahili bila shaka utarusha ngumi.

Kwa upande wangu sioni tofauti kati ya Jakaya na Jangala ama Jongo.
 
Tofauti zipo tena kubwa sana. Nitataja chache:
1. Jangala anafanya usanii na ndicho mashabiki wake wanachohitaji kutoka kwake, lakini huyu JK usanii anaofanya sio kazi aliyotumwa na wapiga kura wa Tanzania.
2. Jangala malipo anayopata kwa usanii ni halali, analipwa kufanya usanii, na ndicho anachowapa mashabiki. JK tunamlipa kufanya kazi ya urais, lakini yeye anatufanyia kazi ya "usanii"! Ni kama kununua tiketi pale Ubungo ya kwenda Mbeya, wenye basi wanakuahidi watakupeleka Mbeya, lakini unapoingia kwenye basi dereva anafungulia tu muziki, basi limesimama tu kutwa pale Ubungo!
3. Usanii wa Jangala unaburudisha mashabiki, huu "usanii" vwa JK unaburahisha nani?

Na tofauti nyingi nyingine. Nadhani tutafute neno lingine la kutumia hapa, lakini hili la "usanii" ni kama kuwadhalilisha wasanii kina Jangala na wengine.
 
Asante sana kwa ukweli na kunisahihisha.
 
watu wa mbeya tunakosea kitu kimoja, kama usanii wa kikwete umezidi, na prof ananyanyaswa si mhamie upande wa pili? kwa nini ccm ni mama yenu mshindwe kumwacha?
 
watu wa mbeya tunakosea kitu kimoja, kama usanii wa kikwete umezidi, na prof ananyanyaswa si mhamie upande wa pili? kwa nini ccm ni mama yenu mshindwe kumwacha?

yaani mtu kama mambo hayaendi vizuri solution ni kuhama? lazima watu wabanane humohumo CCM mpaka hawa wezi waliokiingilia chama waondolewe.. hamna kuhama mtu, kuhama ni dalili ya kushindwa.
 
Mheshimiwa JK atakuwa Mbeya kuanzia tarehe 09 Oct. na atakuwa Kyela tarehe 10 labda aahirishe tena.
 
Usiwe mpumbavu na mnafiki. Watu kama nyinyi ndiyo mnawapa vichwa wapuuzi watupotezao hapa Tanzania.

Mie sio Mpumbavu wala mnafiki.
Bado nasisitiza kuwa "Rais wetu SIO msanii".
Lakini maana una uhuru wa kutoa maoni yako we endelea tu kumtukana, siku moja utajua ulilokuwa unalifanya ulikuwa unalifanya ndivyo sivyo.
 
Usiwe mpumbavu na mnafiki. Watu kama nyinyi ndiyo mnawapa vichwa wapuuzi watupotezao hapa Tanzania.

Jakaya ni msanii aliyekomaa hilo si la kuficha, anastahili kuitwa hivyo na sababu za kumwita hivyo zipo na ziko hai. Sasa kama una sababu ambazo unaona kwamba Jakaya si msanii ebu niweke hapa. Na kumwita msanii nimemuheshimu sana kwani nikianza kumtaja kwa majina anayostahili bila shaka utarusha ngumi.

Kwa upande wangu sioni tofauti kati ya Jakaya na Jangala ama Jongo.

Hata utukane "'to the best of your ability'" bado Mh. Jakaya Mrisho Kikwete ni Rais wako na ataendelea kukutawala hadi 2015.

Ushauri wangu kwako ni huu:
(1) Jinyonge au kunywa sumu, yaani jiue ili Mh. JMK asikutawale na uwahi mapema Jehanum ukatawaliwe na Ibilisi pamoja na malaika wake.

(2) Ukane uraia wa Tanzania, ili ukatawaliwe na hao unaowaona kuwa "ndio maraisi" wasio wasanii.

(3) Kama bado utaendelea kuishi, Jitahidi kuandika lugha ya kiungwana kwenye jamvi hili; Kwa mara ya kwanza nimejua kuwa nawe ni "Mtukanaji" kama baba yako "Shetani".

Mwisho:
Ninakusamehe maana wewe ni Mtanzania mwenzangu 'pamoja na kuwa una mapepo.
 
watu wa mbeya tunakosea kitu kimoja, kama usanii wa kikwete umezidi, na prof ananyanyaswa si mhamie upande wa pili? kwa nini ccm ni mama yenu mshindwe kumwacha?

Ingekuwa bora kuhamia upinzani kama akina Augustine Lyatonga na wenzake, mnang'ang'ania nini CCM?.
Hameni tuwaone 'kama hamtachoka na kuchakaa kama Mrema'.

CCM ni Mambo yote ndani ya yote hapa Tanzania.
 
Mheshimiwa JK atakuwa Mbeya kuanzia tarehe 09 Oct. na atakuwa Kyela tarehe 10 labda aahirishe tena.

Katika ziara hiyo ya Rais huko Mbeya, hatokutana na Wafanyakazi wa Kiwira Mine ambao wameandika barua mara kadhaa kuiomba serikali iwalipe malimbikizo ya mishahara yao toka mwaka 2005 walipopunguzwa kazi.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Mkuu wa Mkoa,Rais hatokuwa na muda wa kuonana na wafanyakazi hao,wala kuutembelea mgodi wa Kiwira.Lakini siku ya mwisho ya ziara yake amepangiwa kuonana na Katibu wa Chama cha wachimba migodi (TAMICO) Bw.Michael Cheyo.
 
Back
Top Bottom