Gottee
R I P
- Sep 7, 2008
- 174
- 1
Lazima kuna kitu uko mbeya si bure!
Ni mara ya 3 sasa,labda anaogopa kuzomewa kama rafiki wa mafisadi.
Kwa medani ya Siasa, Mkoa wa Mbeya na hasa Wilaya mbili za Rungwe na Kyela mambo si mazuri sana kwa JK na kundi lake. Kibaya zaidi Wanamtandao kwa njia moja ama nyingine ndio wamekuwa wakichangia hali hii. JK alichopaswa kufanya mara tu baada ya Uchaguzi ni kushirikiana kwa KARIBU na wananchi wa Mbeya na kukubali kuwa kisiasa Mbeya siyo ENEO lake. Kosa kubwa la kwanza la JK alilolifanya mara tu baada ya Uchaguzi ni kumteua Samson Mwakipesile kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Kwenye kura za maoni Mwakipesile alibwagwa mbali na Mbunge wa sasa hivi Dk. Samson Mwakyembe kule Kyela. Kwa wana Mbeya kumuweka Mwakipesile ilionekana kama JK alikuwa hakuridhishwa na namna walivyomkataa na kama alikuwa akiwakomoa.
Mkuu huyo wa Mkoa baada ya kuteuliwa alipaswa kumaliza CHUKI zote za kisiasa na mahasimu wake lakini alichoamua kufanya ni kupandikiza na kuendeleza chuki zisizo na msingi. Nadhani alifanya hivi kwa maelekezo ya wanamtandao ambapo tunaambiwa yeye ni mwanakikundi.
Jambo jingine baya kwa JK na wapambe wake ni namna ambavyo wamekuwa wanajaribu kummaliza Prof Mwandosya kisiasa. Kumbuka namna Thomson Apson Mwang'onda alivyoteuliwa kuwa Mbunge wa nafasi maalum za JK na baadaye kuletwa kugombea ujumbe wa NEC Mkoa wa Mbeya akipambanishwa na Mwandosya. Wapambe wa Thom ni wazi mitaani walikuwa wakiongea kwamba dogo alikuwa na baraka la JK. Sina uhakika na hilo lakini kwa kuwa ilikuwa inatangazwa hadharani ilipaswa JK kwa kutumia wasemaji wake ndani ya CHAMA angelikanusha.
Inasemekana wanamtandao tena walimpandikiza Nawab Mulla ambaye ana nasaba ya karibu na Rostam Aziz kuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mbeya. Hili nalo limeleta kizaazaa kweli ukizingatia historia 'mbaya' ya Nawab katika biashara kwani ni majuzi tu alihusishwa na kukamatwa kwa pembe za ndovu kule Iringa. Nawab pia anahusishwa katika kumsaidia Rostam hadi kufanikiwa kuuziwa yale mashamba ya Mbarali.
Kwa wana Mbeya, Mwandosya ni CHAGUO lao kwa kila hali. Sipendi kusema kwa nini amekuwa KIPENZI chao labda wengine watakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kulisemea.
Likaja hili la Richmond na Dk Mwakyembe. Kwa kila hali wanamtandao wa JK hawakufurahishwa kabisa na Kamati ya Mwakyembe na kimsingi kuna vita baridi inayoendelea dhidi ya Dk Mwakyembe na Wanamtandao. Wananchi wa Mbeya na hasa wapiga kura wake wanafuatilia kwa karibu sana suala hili na hasa kipindi kile alichoanguka na kuugua ghafla bungeni, wengi wanaamini pale kulikuwa na 'mkono wa mtu' kimsingi Dk Mwakyembe amekuwa akipewa ulinzi usio wa kawaida kwa wadhifa wake wa Ubunge na wapiga kura wake.
Kama nilivyosema JK alipaswa kushirikiana na watu wa Mkoa wa Mbeya ikiwemo kufanya ziara za mara kwa mara. Kama anaweza kwenda Mwanza kila mwezi anashindwa nini kwenda Mbeya kila baada ya miezi sita? Yawezekana ziara ya Lowassa iliwashitua sana wanamtandao kwani tunaambiwa hakupokelewa vizuri pamoja na CCM 'kuandaa mapokezi mazito'
BADO NAAMINI JK ANAPASWA KWENDA MBEYA NA LABDA KUUNGAMA HADAHARANI KWAMBA AMEKUWA HAUTENDEI HAKI MKOA HUO VINGINEVYO LABDA KIMAHESABU MKOA HUO SI TISHIO KWA UCHAGUZI WA 2010.