JJ Masselo
Member
- Nov 1, 2010
- 40
- 7
Ktk hali nisiyo amini, tumepokea taarifa za tukio lenye kufanana na la kigaidi pale feri, na tupofika amini usiamini tumekuta kijana anaekadiriwa kuwa na miaka 26 hivi, akiwa kituo kidogo cha polis kwa kutuhumiwa kuvuka kwa kuogelea,
Imeniwia vigumu sana kuamini, lakini nipo jaribu kumhoji akanimbia kuwa alikosa nauli ya shilingi 200 akaona bora apige mbizi kama agizo la magufuli lilivyo semwa!
Kutokana na taratibu za kiusalama imebidi tumchukue kwenda nae makao makuu kwa mahojiano zaidi!
Huyu mtu kwa haraka haraka ni kwamba ametaka kutolewa kwenye vyombo vya habari kama JF na kadhalika na kwamba alitaka sisi tujue kwamba anaweza kuogelea lakini si kwamba kukosa sh200 ndo kumemfanya aongelee hadi ng'ambo kama hujui kuogelea kama unabisha kajaribu wewe uliyetoa thret hii kama utaweza, vitu vingine havina umuhimu wowote kuvileta humu watu mnaonekana kama hamna kazi za kufanya.
Hata hivyo siku zote naichukia siasa sana kwa maana kwenye siasa ukichukiwa na wanasiasa wenzio au chama chako kikichukiwa basi hakuna utakalosema wananchi wakaliona la maana, soma kwa makini hapa ili uelewe ninachotaka kusema, Mimi nilimshangaa sana Chapombe John waliposema alimshangaa Mh. Mnyika John, Chapombe alisema alitegemea Mnyika apeleke proposal za jinsi ya kutatua matatizo ya foleni wakat yryr mwenyewe alitakiwa kutoa pendekezo lake la kuongeza nauli kwa Project yake ya Boat kutoka Bagamoyo hadi Dar ambapo kungekua na vitua kadhaa kabla ya kufika Bagamoyo.
Aliteakiwa kuonyesha Presentation yake kwa wananchi na kuchukua maoni yao harafu ndo kupandisha nauli kungefuata sidhani kama wananchi wangempinga, maana mantiki yake inaleta maana sana kuondoa siasa, Kupanda kwa nauli ya kivuko sioni tatizo ila tatizo ni kutangazwa na mwanasiasa ambae chama chake kwa kiasi kikubwa kimepoteza mwelekeo na imani kwa Wananchi wake na hcho ndo chanzo cha marumbano yanayoendelea sasa.
Ngoja nichukulie kwa wanaokaa Ubungo ambako nimeambiwa kuna maendeleo ambayo yamesababishwa na Mh. Mnyika, ukiwa Posta na unataka kurudi Ubungo wewe mwenyewe wala bila tangazo la Chapombe unaenda akiba unapanda gari kwa shs 200 hadi posta na kisha unatoa nauli nyingine ya kwenda ubungo mbona hamlalamiki? Ukiwa Posta na unataka kwenda Gongo la Mboto ni hvyo hvyo, kipi cha ajabu ambacho Chapombe kakifanya? huwezi kupata kingine ila jambo limechukuliwa kisiasa na aliyetangaza chama chake ndo kama hvyo tena,
Ok angalia tena Ubungo terminal, kwa miguu yako mwenyewe unaingia kwa sh200 unapewa ticket na ukipoteza ticket ukiwa bado hujatoka utatozwa sh 200 tena nani alishawahi kulalamika? au watu wa Kigamboni hawatumii Ubungo Terminal kwamba hawajui haya? Yaani Watanzania bana mara nyingi tumekua kigeu geu na hatuna misimamo ya kweli kama mtu anafanya jambo la maendeleo hata kama ni wa chama gani asapotiwe huo ndio Ujamaa,
Mara nyingi nimeona threats ambazo zinatolewa na wadau mbali mbali kama ni za chama tawala zitatolewa lugha ngumu mpaka basi hii ni dalili tosha kwamba chama tawala kimepoteza mwelekeo kaabisa na imani kwa wananchi wake ila ningeona wana JF wamaana sana na watu makini kama wangekua wanachukua muda kuangalia mambo kabla hawajasema chochote na ikumbukwe pia Watanzania sisi ni wavivu saaana wa kujituma na si wabunifu ila ni hodali wa kulaaumu na kutoa visingizio.