Kijana apiga mbizi kutekeleza agizo la Magufuli!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Ktk hali nisiyo amini, tumepokea taarifa za tukio lenye kufanana na la kigaidi pale feri, na tupofika amini usiamini tumekuta kijana anaekadiriwa kuwa na miaka 26 hivi, akiwa kituo kidogo cha polis kwa kutuhumiwa kuvuka kwa kuogelea,
Imeniwia vigumu sana kuamini, lakini nipo jaribu kumhoji akanimbia kuwa alikosa nauli ya shilingi 200 akaona bora apige mbizi kama agizo la magufuli lilivyo semwa!

Kutokana na taratibu za kiusalama imebidi tumchukue kwenda nae makao makuu kwa mahojiano zaidi!

UPDATES:

Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa kijana alitumwa na wapinga nauli mpya, kijana kabainisha wazi kuwa alipewa elfu hamsini, na watu ambao sasa tunawafatilia ili kujua zaidi kilicho nyuma ya pazia.

Suala hili linaonyesha limeingiliwa na vita ya kisiasa, hasa likilenga kukosoa kauli ya Magufuli!
Katika mahojiano niliyofanya nae kitaalamu zaidi kijana ni mvuvi wa pale feri na tenda hiyo alipewa tangu jana, anazidi kuweka wazi kuwa watu waliompa kazi hiyo walikuwa wawili wakitumia gari plado nyeusi na walivaa mmoja shati jeupe,na mwingine hakumbuki vema!

Kulingana na maelezo yake nimeamua kumtoa mahabusu kwa kutumia oda ya kiwanausalama na sasa nimempa laki moja kwa maelezo kuwa nampongeza kwa ujasiri wa kuvuka bahari, lakini lengo langu anisaidie kujua nani zaidi walimtuma na lengo lao zaidi ya kupinga nauli kingine nini?? Nimemrudisha mpaka feri lakini ktk mazingira ambayo hajui kuwa mimi ni mmoja ya waliyomchukua pale kigambo feri!

Nahisi lipo kubwa zaidi ya nauli, nalo ni vita ya wanasiasa wabunge na waziri magufuli!

Subirini nitawajuza!

Katika kumdhihirishia Magufuli kuwa inawezekana kijana mmoja amepiga mbizi na kuogelea kutoka Mgogoni hadi Kigamboni.

Source: Hahari ITV
 
Kweli serikali legelege hasara yake ndiyo hiyo.
Inanigusa matukio km haya ambayo imekosa mwongozo.
 
Hata sio kichaa, katekeleza agizo la mkuu. na mimi kesho napiga mbizi, maana nataka kwenda kupumzika huko chadibwa
 
Nauli ya 200/- si kigezo cha kupiga mbizi eti kwa kushindwa kulipa. Mbona ubungo Terminal tunalipa 200/- ili uvuke geti kwa miguu yako. Wasafiri na wanawaunga mkono tutafakari zaidi!
 
Mbona huwa wanakatiza bahari? Siyo mara ya kwanza kwa wavuvi kukatiza bahari kutoka magogo to and from kigamboni. Mie sishangai kuogelea, nashangaa kukamatwa kisa umeogelea. Kwani alishindwa kuogelea wakamwokoa?
 
Ktk hali nisiyo amini, tumepokea taarifa za tukio lenye kufanana na la kigaidi pale feri, ... akiwa kituo kidogo cha polis kwa kutuhumiwa kuvuka kwa kuogelea,
Imeniwia vigumu sana kuamini, lakini nipo jaribu kumhoji akanimbia kuwa alikosa nauli ya shilingi 200 akaona bora apige mbizi kama agizo la magufuli lilivyo semwa!

Kutokana na taratibu za kiusalama imebidi tumchukue kwenda nae makao makuu kwa mahojiano zaidi!

Hapo kwa RED, hizo tuhuma zatoka wapi? kwani Pombe hajatoa kibali? Na sidhani kama alikuwa amekunywa pombe! na kijana wa watu ametoa sababu ile ile ambayo kwayo Pombe alitoa Option mbili, aidha waogelee ama wakazunguke kongowe.
Hizo taratibu za kiusalama nyie polisi mngeanza kumhoji kwanza Pombe. Kama angekuwa alikunywa tungesema ulevi, but alikuwa fit tu!
 
Sasa kakamatwa kwa kosa la kuogelea ama kutokuwa na sh 200/- Kwani pale kuna bango la kuzuia watu wasiogelee kuvuka upande wa pili!!!
Kutekeleza agizo la Makufuli nalo ni kosa??? :A S embarassed:
 
YEAH,anaonyesha kuwa kila jambo linawezekana,maana yake hata kama nauri imepanda yeye haoni taabu kupiga mbizi,alikuwa anafikisha ujumbe kwa wahusika
 
Nauli ya 200/- si kigezo cha kupiga mbizi eti kwa kushindwa kulipa. Mbona ubungo Terminal tunalipa 200/- ili uvuke geti kwa miguu yako. Wasafiri na wanawaunga mkono tutafakari zaidi!

Kwani unasindikiza kila siku? Ndo maana hiyo ya kutoa mjoja haiwapi shida lkn pale fery kuna watu wana frequency nyingi za kuvuka ndo maana inawapa tabu.
 
Ktk hali nisiyo amini, tumepokea taarifa za tukio lenye kufanana na la kigaidi pale feri, na tupofika amini usiamini tumekuta kijana anaekadiriwa kuwa na miaka 26 hivi, akiwa kituo kidogo cha polis kwa kutuhumiwa kuvuka kwa kuogelea,
Imeniwia vigumu sana kuamini, lakini nipo jaribu kumhoji akanimbia kuwa alikosa nauli ya shilingi 200 akaona bora apige mbizi kama agizo la magufuli lilivyo semwa!

Kutokana na taratibu za kiusalama imebidi tumchukue kwenda nae makao makuu kwa mahojiano zaidi!

ila wewe bwana mimi huwa nakuamini sana,sasa usiniangushe juu ya hili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom