Kiini macho cha Kamati ya January Makamba na Dowans

Moelex.. point yangu ni kuwa serikali haina tatizo lolote na kutoa maelezo yoyote ambayo watu wanataka kuyasikia. Historia ni shahidi wa hili. Naweza kutolea mifano ya maelezo ambayo wabunge wamewahi kutaka toka serikalini na wakapewa kwa furaha.
 
Katika kipindi hiki cha siku tano cha kujadili hotuba ya JK, ingelikuwa vyema na hii barua ya Makamba ikaunganishwa. Kwangu mimi ni barua inayoibua maswali mengi kuhusu uwezo na umakini wa serikali iliyoko madarakani,
 
Katika kipindi hiki cha siku tano cha kujadili hotuba ya JK, ingelikuwa vyema na hii barua ya Makamba ikaunganishwa. Kwangu mimi ni barua inayoibua maswali mengi kuhusu uwezo na umakini wa serikali iliyoko madarakani,

...Hata isipojadiliwa bungeni itajadiliwa mtaani. Bunge la kweli lipo mtaani siku hizi.
 
Nakubaliana na wanounga mkono jaribio hili la Mh Makamba Mbunge.

Afcourse kwa makamba atapata majjibu kirahisi kwa sbabau hata yeye barua yake imejiweka kwenye hali ya kupokea majibu mepesi mepesi .
Ukisoma barua unashindwa kuelewa makamba kaandika kama mbunge tu au kaandika kama mbunge mwenye ubia na serikali.

Ukisoma barua utagundua wakati anajaribu kujionyesha yuko serious kukemea matatizo publicity lakini ni kama anajua atakuwa upande huohuo wa serikali siku si nyingi. Mwanakijiji kaseme "anaomba"

unasoma barua unaona mbunge amejaribu kuianisha kwa detail tatizo upande wa kisheria wa Tanesco wich is good Lakini hajafanya hivyo kuanisha weakness na mapungufu kwaserikali

Anyway kama walivyosema wadau mwanzo mzuri kama nia si tu kujenga publicty na kujipandisha chat
 
.......Namalizia kwa kusema; Si sahihi kuamini kwamba wabunge wote wa ccm hawajali maslahi ya nchi.

Uko sahihii kabisa inwezekana asilimia 80 ya wabunge wa CCM wanajali asilimia 90 ya maslaji ya taifa. Lakini ni asilimia chini ya 2% ya wabunge wa CCM wako tayari kupoteza ubnge wao kwa kutetea maslahi ya taifa.

do u think wabunge wangapi wanakerwa na dowans but ni wabunge wangapi wako tayari kuongolea misimamo yao kuhusu dowans public na kukosa public kile wanchozani ni sahihi kama wabunge .

Mfano hapa makamba kafanya kitu kizuri lakini sijui kama alikuwa na guts za kuyasema wazi wazi haya au inawezekana hata aliomba ruhusa ya kuandika barua kama hii. Unaona hata lugha aliyotumia sio ya mbunge wa wananchi kuwasilianana na serikali. bali ni mbunge wa Chama

Anyway Official communication inafanyika in writing tumpongeze kwa hilo hapa inawezekana kawazidi hata wenzake kina Six, Anne kilango and co
 
ki ukweli January makamba hoja yake ni nzuri na ameweka facts na baadhi ya vitu ambavyo labda hata sisi hatukuya jua kama mtambo wa mwanza unaolipwa bila kuzalisha umeme, na jinsi huyo wakili alivyo cheza rough na tanesco, ila mimi na shukuru kwa ujumbe ambao sidhani kama utaleta nafuu kwa wa tanzania, kwa sababu yeye amemwandikia barua waziri naye waziri atajibu kwa utaratibu wake hivyo umma wa wa tanzania unaweza usipate kujua majibu aliyo pewa, mi ninge shuri kama anaonyesha uzalendo kweli, kwanini hii hajapeleka mbugeni kama hoja binafsi, ili ijadiliwe na mbuge kwa kina na mapana! hivyo hii ni changa la macho tu. ila ahsante mhe kwa kutudokezea siri kidogo, usikate tamaa maana na jua ulikuwa ikulu unasiri nyingi tunaomba kuzijua,
 
Kwa kweli nimeamini Watanzania hatuko serious na hii barua ya Januari ni kielelezo cha usanii ambao unapelekea Raisi wetu kushangaa kwa nini tu masikini wakati wanaoifilisi nchi ni maswahiba wake. Januari, mtoto wa Katibu Mkuu wa CCM na aliyewahi kuwa msaidizi wa Raisi, leo anakurupuka kama vile alikuwa ndotoni na kuhoji umakini wa serikali huku akimyooshea kidole Waziri Ngeleja ! Anasema,

Tangu mwaka 2006 hadi sasa zimetoka ahadi na matamko sita ya Serikali ya kumaliza tatizo la mgawo wa umeme nchini, lakini hadi sasa bado mgawo unaendelea. "Wewe (Ngeleja) mwenyewe umetoa ahadi kadhaa za kumaliza tatizo hili, lakini ahadi hizo hazikutumia," anamshushua Ngeleja !
Masikini Januari mtoto wa Makamba ambaye kwa muda wote huo amekuwa karibu na Raisi na Mwenyekiti wa chama tawala (ofisini) na pia karibu na Katibu Mkuu wa chama tawala (nyumbani) amesahau hotuba ya bosi wake mwaka 2006 (alishiriki kuiandika ?) Ilisema hivi,
We have been grappling with this problem for quite some time now – but only with ad hoc measures.The recent power problems have afforded us the opportunity to rethink our energy strategy in holistic terms. We have learnt that ad hoc measures are costly in the long run and have their own limits. As we grapple with our energy problem, we are witnessing an upsurge of interest for investments in power generation in Tanzania. We are confident that in two years time, we will be on course to realize reliable power supply in Tanzania.
Huu sasa ni mwaka wa sita tokea tuahidiwe na bosi wake kuwa tatizo la umeme lingekwisha na badala yake wakati tatizo liko pale pale, nchi inazidi kutafunwa mchana na usiku na washikaji wa bosi wake. Januari anataka watwana wanaotupiwa makombo washughulikiwe huku manyang'au wenyewe wakilindwa na Kikwete wakizidi kutumbua wakiwa meza kuu. Januari anendelea,
Mimi naamini kwa dhati kabisa, kama Serikali ikitoa tamko la dhati kabisa bungeni linalobainisha kwa kina na uwazi sababu za ahadi hizi za mara kwa mara basi tutakuwa tumepiga hatua kwenye kuimarisha imani ya wananchi kwa Serikali yao.
Januari, Januari, Januari..je, unaelewa serikali ni nani na nini ? Serikali yenyewe keshatamkia wananchi bila kumung'unya maneno kuwa haiwajibiki na hali hii ya mkanganyiko. Haiwajui wanatudai na kwamba si lazima iwajue wabaya wetu kwani haiwahitaji. Iko tayari kupiga na kuua wananchi wanaoandamana kudai haki lakini kamwe haina nia, sababu wala uwezo wa kuwakamata wanaolihujumu taifa kwani inaogopa nchi kuyumba !
Mzimu wa mikataba ya umeme Tanesco imekuwa ikiitikisa nchi ambayo mwaka 2008, ilisababisha Baraza la Mawaziri la kwanza la Serikali ya awamu ya nne kuvunjwa, baada ya Kamati Teule ya Bunge kubaini mkataba kati ya Kampuni ya Richmond na shirika hilo ulikuwa na walakini.
Ha ha haa ! Baraza la Mawaziri lilivunjwa he he he. Je safari hii kitu gani kitavunjwa kama kuvunjwa kwa baraza hilo hakukusaidia kitu ! Je akina Shimbo na Mwema watatuacha wananchi tulivunjilie mbali serikali nzima kwani tatizo laonekana ni Uongozi wa juu wa nchi ulio na ubia na wabaya wetu ? Januari please come down to earth, yaonekana na wewe umeyakamata ukakuta yamejaa kwenye kiganja ! Acha kutuzuga, ama uko nao ama uko nao, huku kwetu hakukufai. Mwandikie Kikwete hiyo barua !
 
Let us take it personal now.
Tuchome mali za Waheshiwa wahusika Magari Nyumba mashamba na biashara zao.
Hiyo isipo fanya kazi tunwabonda kwa staili ya mwizi ushwazi.

We have nothing to lose.
 
Januari kajitahidi katika barua hii kuanika mambo ambayo hata sisi tulikuwa hatuyajui, ila sioni sababu ya kwa nini amuulize Ngeleja leo swala hilo wakati mikataba yote hiyo ilisainiwa wakati yeye (Januari) akiwa ni mshauri mkuu wa rais kiasi kuwa alikuwa na uwezo wa kumshauri rais asiidhinishe miradi hiyo. Kama miradi hiyo ina walakini, mtu pekee wa kumwuliza leo siyo waziri bali ni rais mwenyewe. Mawaziri wengi wamekuta miradi ya aina hiyo ikiwa imeshaidhinishwa
 
Ha ha haa ! Baraza la Mawaziri lilivunjwa he he he. Je safari hii kitu gani kitavunjwa kama kuvunjwa kwa baraza hilo hakukusaidia kitu ! Je akina Shimbo na Mwema watatuacha wananchi tulivunjilie mbali serikali nzima kwani tatizo laonekana ni Uongozi wa juu wa nchi ulio na ubia na wabaya wetu ? Januari please come down to earth, yaonekana na wewe umeyakamata ukakuta yamejaa kwenye kiganja ! Acha kutuzuga, ama uko nao ama uko nao, huku kwetu hakukufai. Mwandikie Kikwete hiyo barua !

Mkuu, kuweka rekodi sahihi Baraza la Mawaziri halikuvunjwa, Rais mwenyewe alisema wiki chache kabla kuwa hakuwa na mpango wa kuvunja baraza la mawaziri. Baraza lilivunjia baada ya Waziri Mkuu kujiuzulu. Baraza linavunjika wenyewe wakati Waziri Mkuu anaondoka madarakani kwa sababu yoyote ile, kufukuzwa, kufa, kujiuzulu au hata kupiga kuwa ya kutokuwa na imani.
 
January atazimwa na "vijisenti" tu hivi karibuni...subirini tu....atanyamazishwa sasa hivi.

Ndio CCM ilivyo.

Kama kweli yeye (January) ni safi...hataiachia hii hoja, na pian ataendelea kutupa

majibu ambayo yeye January (kama alivyoandika awali) wananchi tunastahili kuyajua.
 
Hahahaha again wadanganyika ime kula kwenu, hamna lolote hapo ni mipango imesukwa vizuri kumsafisha January,baada ya kuchafuliwa na kuukosa uwaziri, hakuna kitakajiri ni kupandishana chati tuu hapo, hoja haitajibiwa na january atapandishwa chati si ajabu atapata Uwaziri baara ya kazi nzuri ya kuikemea serikali kama walivyo hawa waasi Mwakyembe na Sitta.
 
Aache upuuzi wake.
Yeye si alikuwa ikulu, inamaana hakuwahi hata kusikia hiyo dili wakati inapita? Kwa nini hakushauri wakati huo? Anaona hali imebadilika sasa hivi ndo anatafuta sapoti ya umma kama walivyofanya uvccm. Wanatakiwa washauri kabla sio kusubiri watu waanzishe ishu ndo wao wadandie.

Jamani! Angeshauri kama nani wkt yeye alikuwa speechwriter? tuwe tunatafakari kabla ya kuhitimisha.
 
Waziri Ngeleja amvutia kasi Makamba Send to a friend Wednesday, 09 February 2011 21:31 0diggsdigg

Ramadhan Semtawa
SIKU moja baada ya kuvuja waraka mzito wa Mbunge wa Bumbuli January Makamba kutaka ufafanuzi wa hali ya umeme, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amesema tayari ameusoma, lakini serikali haijatoa majibu Bungeni na kwamba atamjibu mwenyewe.
Msimamo wa serikali, unazidi kuua mipango mikakati ya kuirejesha bungeni hoja ya Dowans na Richmond kwa mlango wa nyuma, baada ya ofisi ya Bunge kukataa hoja ya Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, kuhusu hali ya umeme na hukumu ya ICC.

Waraka wa Makamba pamoja na mambo mengine, umeibua jambo zito kwa kumwanika mwanasheria mmoja wa Tanesco aliyesimamia kesi ya Dowans, ambaye alishauri mkataba dhidi ya kampuni hiyo, uvunjwe na upande mwingine akiisifia na kuiombea mkopo wa Sh 20 bilioni kutoka Benki ya Stanbic.

Akizungumzia waraka huo, jana kwa njia ya simu kutokea Dodoma Ngeleja alisema hajausoma waraka huo.

"Jana (juzi) sikuwa nimeisoma hiyo, barua, lakini sasa hivi nimeisoma, Ninachoweza kusema ni kwamba tutamjibu yeye mwenyewe," Alisema Ngeleja.

Waraka huo, ulosomeka hivi ‘Yah: Taarifa ya Serikali Bungeni kuhusu Umeme Nchini,' Mbunge Makamba ambaye ni mtoto wa Katibu Mkuu wa CCM, anataja mambo mawili makuu ya msingi, ambayo ni kesi mbili za IPTL zilizopo Hong Kong dhidi ya serikali na mgongano wa mawaziri kuhusu Dowans, ambapo alimtaka waziri afafanulie umma kupitia bunge.

"Kesi hizo ni ICSID No ARB/10/20, dhidi ya Tanesco iliyofunguliwa Oktoba mosi, 2010 na ICSID No ARB/10/12 dhidi ya Jamhuri ya Muungano, iliyofunguliwa Juni 11, 2010, zinaweza kuwa na madhara makubwa kwa umma na zinaweza kuigharimu serikali fedha nyingi kuliko zinazodaiwa katika kesi ya Dowans," alifafanua Makamba.

Lakini, Ngeleja akifafanua zaidi, alisema mbunge huyo ameomba taarifa kwa waziri kwa mujibu wa barua yake, hivyo kitakachofanyika ni kuandaa majibu na kumpatia mwenyewe.

"Tunaandaa majibu na tutampatia mwenyewe, aliomba majibu kwangu nikiwa ni waziri na pia kutoa ushauri, hivyo utaratibu wa kiserikali ni kumjibu yeye mwenyewe na wala si kuzungumza na vyombo vya habari," alisisitiza Ngeleja.

Kwa mujibu wa Waziri Ngeleja, amekuwa akipokea ushauri kutoka kwa wabunge wengine ambao wanataka ufafanuzi wa mambo ambayo, amekuwa akiwajibu katika utaratibu wa mawasiliano.


Ngeleja akizungumzia tuhuma za mwanasheria huyo, aliyecheza karata pande mbili za Tanesco, Ngeleja alisema;"Hilo liko nje ya uwezo wangu. Waulizeni Tanesco waseme wenyewe, kwasababu siwezi kuwasemea. Hilo liko nje ya uwezo wangu," alisema Ngeleja.

Meneja Uhusiano wa Tanesco Badra Masoud alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo, hakuweza kupatikana na simu zake za viganjani hazikuwa hewani.


My Take:

Wanamuachia JM options mbili tu... both not very appealing..
 
Wana JF tuisome barua ya Mh. Januari Makamba kuhusu tatizo la umeme nchini. Naona anataka kufunua uozo katika shirika la umeme na serikali.Samahani kama imeshapita humu jamvini. Naona hii ni dalili ya mwanzo mzuri kwa Kijana Januari pamoja na kwamba sasa hivi amekuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Nishati na Madini.View attachment Barua ya Januari Makamba kwa Ngeleja.pdf
 
Back
Top Bottom