sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Kiingereza cha watanzania wengi kinawasaidia na kinaishia kwenye kuandika status, kuelewa kilichoandikwa kwa kiingereza mfano magazetini na pale kinapotumika kuongea kwa kufatiliza maneno ambayo yameshaandikwa kwa mpangilio kwamfano kutoa hotuba kwa kufatiliza speech iliyochapishwa kwenye karatasi.
Ukija kwenye kiingereza cha kuwasiliana, wengi kusikia maneno na kuyaelewa inakuwa shida, pia kwenye kuongea kwa uhuru mfano kujielezea inakuwa kazi sana tofauti na pale wanaposoma speech, hapa panakuwa na ze ze ze izi izi izi zati.
Nakumbuka hata mwalimu wa kiingereza wa sekondari alikuwa haelewi chochote kwenye nyimbo za marekani zilizojaa matusi, hii ilikuwa mpaka chuoni wengi walikuwa hawaelewi kinachoimbwa zaidi ya ku enjoy biti, flow, kucheza pamoja na kuiga mtindo wa maisha ya wasanii hao wakidhani kwamba kinachoimbwa kina uzito kumbe ni uharo mtupu.
Pia watanzania huwa tunakosea sana tunapoona mtu kasoma speech kwa kiingereza na kumpongeza tukidhani anajua, LA HASHA!! huku ni kupotoshana, wa kupongezwa inabidi awe muandaaji alietumia utashi wake na muda mwingi kupangilia hayo maneno, kuanzia grammer, prepositions, n.k. maana bila hivyo hata huyo ambaye anafatiliza maneno hataweza, tukiachana na kiingereza cha kufatiliza maneno hicho, wengi wakiambiwa waongee kwa uhuru wa kutunga swntensi zake kichwani kama anavyoongea kiswahili, hapo inageuka kuwa aibu.hata mzungu ambae nae kiswahili kinampiga chenga akiandikiwa hotuba anaweza kuonekana anajua kiswahili.
Kwa watu maarufu wanaojua kiingereza kwa hapa Tz naweza kusema ni kina Vanessa mdee, Wema Sepetu, P Funk, n.k. hawa kidogo hata shule na maisba waliyokulia walikuwa exposed na lugha ya kiingereza katika maisba yao.
Pia nawakumbusha kujua kiingereza si9 kipimo cha akili.