HKigwangalla
JF-Expert Member
- Feb 6, 2008
- 717
- 971
Niliandika status kwenye FB wall yangu, kwenye twitter, wanabidii na mabadiliko forums, na nilikanusha hilo, maana halikuwepo...sijawahi kukamatwa bali ilikuwa kinyume chake na kwamba waliofanya hivyo walikuwa wana-plot kunichafua ili wasababishe nisiteuliwe na Chama kugombea nafasi ya NEC kupitia Nzega (na wamefanikiwa, hongera zao). Namshukuru Mungu ka-bajeti nilikokuwa nikatumie kwa ajili ya kampeni yangu kwenye NEC nimekatumia kwa mambo mengine, na nimewashinda kwenye uenyekiti, uNEC, Uenezi n.k. Kama nilikamatwa waulize hao wenye magazeti kwa nini hawakupiga picha matukio hayo - kwanza la kugawa vitumbua na mbili la kukamatwa na PCCB? waambie waweke hapa kama ni hadithi za ukweli. Mimi niliishaga acha kuyaamini magazeti 100% siku nyingi sana, huwa nawapa 60% tu!mh dr H Kigwangalla, nakupongeza kwa kunitomeza na kujibu baadhi ya hoja hapa jamvini. KEEP IT UP, natamani na vijana wenzio huko katika ccm ( mwigulu nchemba, january, bashe, lusinde 'kibajaji')wataiga huu mfano wako mzuri.
MH, kuna siku ililetwa habari hapa kuwa umekamatwa nzega ukigawa rushwa ya vitumbua na tsh 2000 kwa wajumbe, tulikusubiri sana hapa jf uje uthibitishe au kukanusha KIMYA!
na mpaka leo hatuujui ukweli ni upI mkuu,,
kwa kuwa leo upo hapa naomba ufafanuzi wako