Kifo cha CCM kimetimia

haitafika mwaka 2015 kabla ya chama hiki kusambaratika kwa baadhi ya wanachama influential kukihama, ntatoa sababu kadhaa..
1. sinema waliyoianzisha ya lwakatare ita 'backfire'
2. mafisadi ndio wenye nguvu ndani ya chama, na hii inawakera sana wale wanaojipambanua kama 'wasafi'
3. vita ya kupewa tiketi na chama ni kali mno, kuna baadhi wameanza kukata tamaa ya kupewa ridhaa ya chama, hivyo watajiengua na kundi kubwa la wanachama
4. kwa sasa chama hakina 'mwenyekiti', kila mtu anafanya atakacho....
 
Dalili zote zinaonesha muda si mrefu chadema itafutika kabisa,tunangoja historia
 
Ukipita mtaani unamkuta bibi kizee anajiita eti yeye mwanaccm, kwenye mikutano kijana anajiita eti yeye mwanaccm, bungeni mbunge wa muhula mmoja badaye kapotea naye eti mwanaccm. Kuwa mwanaccm ni kufaidi kile wanachokula wanaccm pure waliopo lumumba na magogoni. Wanaccm kwa hapa dar wanaishi magogoni, oyesterbay, masaki, mbezi beach na mikocheni, kwa Arusha wapo sana Njiro na mbeya wanapatikana forest, kule Kigoma wapo Mjimwema na Kilimahewa, wanaccm hutembelea Vogue, shangingi mpya, wale wa mikoani ndo hutumia prado. Je we unayejiita mwana ccm unatembelea nin na unaishi wapi? Hebu tazama list hii fupi ya wanaccm halisi.. JK, Kinana, Lowassa, Sumaye, Wassira, Lukuvi, Bilali, Pinda, Makinda, Ndugai, Membe, Sitta, Mwakyembe, Nape, Shigella, Buriani, Marmo, Ridhiwani, Mama Salma, Welema, Mwema, Manumba, Kova, Zoka, na wengne wachache huongezeka hapo. Waliobakia akina Mwigulu na wabunge ni wapga debe au michicha ya kiangaz unapotea muda c mrefu hatutawasikia tena wanatumika kwa manufaa flan then wanadilitiwa.
 
huu ndio mwaka wa wote waliojifanya mabubu kuanza kutangaza nia zao za kuwania uraisi.!
na mara baada tu kutangaza nia (kwa wanachma wa ccm) hizo kashikashi zitakazo tokea, lazima kunakundi kubwa sana la wanachama watakikimbia chama..
R.I.P
 
CDM kaza mwendo mbele kwa mbele. CCM haina kitu imebaki kubwajabwaja na kina nape sijui kinana wote hakuna kitu.
 
huku akitoka povu tarehe 5/2/2011 pale DODOMA kwny maazmisho ya miaka 34 ya ccm(chukua chako mapema) jk aliwaaminisha waliokuwa wanamckiliza kuwa ni wakati kujivua gamba ili kurudisha mvuto wa chama hiki kikongwe kilicho choka. baadae nepi(vuvuzela) alizunguka tz nzima akihubili swala cku 90 zilizo kuwa zinawahusu mapacha watatu(mamvi,vijisent na maji taka). SASA JK NA NEPI WATUELEZE WAMEFIKIA WAPI
 
Chadema Daima na CCM mwisho wao ndio umefika,na alikuwa Gaddafi ambaye aliongoza nchi kwa mda mrefu sana na akatolewa sasa sembuse CCM,wakati wao umefika wa kuachia nchi na tunahitaji mabadiliko...

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Ni nani asiyejua dhahiri kuwa CCM sasa ni mfu?

Uchaguzi wa 2010 ulituthibitishia hilo mapema sana wakati wa kutangaza matokeo ya wagombea Ubunge, Mahali ilipobainika kuwa jimbo fulani CHADEMA ni washindi, mf.Aruma Mjini,Sengerea na kwingineko ambako CHADEMA walijizolea KURA mingi kulikuwa na ukiukwaji na ucheleweshwaji wa kutangaza matokeo kwa makusudi. Kwa namna yoyote ile CCM ilitafuta kupata ahueni kwa kufanya Uchakachuzi,na mahali ambapo NGUVU YA UMMA ili - take place iliwalazimu kukubaliana na hali halisi ilivyo ya kutangaza matokeo hayo kwa shingo upande kuwa CHADEMA ni washindi Jimbo hilo.

Kutapatapa kwingi na kutumia muda mwingi na NGUVU kubwa ili waimalize CHADEMA badala ya CCM kujijenga yenyewe kwa kufanya shughuli za maendeleo hio ni ishara tosha na dalili kubwa kuwa CCM ianajitahidi kuuhadaa UMMA wa Watz kuwa bado iko hai kumbe ni mitambo tu ya kuisaidia kupumua Iko puani mwa CCM LAKINI ukweli CCM ni maiti kwa siku nyingi anayekataa kuingia kwenye jeneza ili iwekwe kaburini ifukiwe na kusahaulika kwenye ulimwengu wa siasa za Nchi hii.

2015 sio mbali anayepanda ngano atavuna ngano na apandaye miiba naye ataambulia miiba,CCM mkazane sana kufanya siasa za kuchafuana ili wananchi wote wajue ninyi ndivyo mlivyo,CHADEMA nao jitahidini sana kuwaonyesha wananchi kuwa ninyi ndiyo wakombozi na waleta mabadiliko ya kweli,mwisho wa yote mwenye kuvuna AIBU na HASARA atafaidi juhudi yake na Wenye kuvuna HESHIMA na FAIDA naye atafaidika na alichokistahili.

ILA NI JAMBO LISILO FICHIKA ENDAPO CCM ITAENDELEA NA SIASA ZA MAJITA TAKA, MAJUNGU NA KUIBAMBIKIZA CHADEMA TUHUMA FEKI UKWELI UKO WAZI CCM INASUBIRIA MAZIKO YAKE RASMI UCHAGUZI UJAO 2015.
 
Najua Kwa kibwagizo hicho ma-CCM mengi yatamwagika kusoma sred hii..

Miaka ya chaguzi Za vyama VINGI Binafsi nilichoka sana kupiga kura nikijua fika CCM watarudi madarakani, sikukipenda Chama hiki tOkea kitambo niseme tu ukweli, Chama kilichojineemesha chenyewe huku wananchi tukitapatapa nani akipende, simaanishi viongozi wewe chokambaya lakini VIONGOZI Wa CCM wengi wana nyodo, uzandiki, kibri, majivuno wainua visigino.

Upepo ukaja ukakua hatimae 2010 CHADEMA ikachipukia kwa kasi, tukalipiga jalamba la nguvu lakini jamaa CCM wakarudi madarakani. Binafsi nikawa nawaza sana uhai wa CHADEMA after 2010, Kwa Sababu changuzi zetu Mara nyingi humalizika sambamba Na kufifia au Kufa Kwa Chama pinzani Kiongozi mf NCCR -1995, CUF-2000 nk.

But From 2010, CHADEMA Ni Kama imetiwa Mafuta mapya, jamaa wana mipango endelevu, mipya everyday, jamaa wanapiga Kazi, jamaa wanawajibika kiasi CCM ikabaki kikopi na kupest CHADEMA strategy. Mara mkutano jangwani-CCM kakopi, M4C Na CCM kakopi M4M, elimu ya uraia all corner CCM ANAKOPI TU HADI KESHO.. Unajua kumkimbiza Mtu usiyejua pumzi yake ni Kazi nzito sana, baada ya kuchoka CCM imejitosa nzimanzima kupambana Na CHADEMA, Kwa kuwatupia gunia la Ugaidi, MATUSI Na kila njia ilimradi CCM wanachojua uhai wao ni kifo cha CHADEMA.

Niseme wazi hapo kwanza Yaani from 2010, nikiona sred au gazeti au Mtu yeyote anaisema vibaya CDM au ukiandika mbaya ilikuwa inaniuma sana, Hata sred inayoisema CHADEMA Vibaya Hata Kuifungua niliogopa, sikupenda Chama kife Kwa chochote, Lakini baada ya kuhudhuria mikutano ya CCM, nikiliangalia Bunge letu, nikiwasikiliza VIONGOZI wakuu Wa CCM hasa NAPE Na Mwigulu nimegundua CCM imeshajichokea sana, nimegundua pia Hata mwananchi wa porini ambaye Zamani alipelekeshwa Na CCM Kama msukule Leo hawezi kukisapoti Chama hiki. Nikagundua CHADEMA Is a God plan.

Labda nitoe RAI Kwa CUF, TLP,UDP Na wengine, chaguzi Za serikali Za mitaa Ndo hizo zimekaribia 2014, Kama hakuna mtandao Wa kitaifa Basi tafuteni maeneo kadha mjiwekezee nguvu kuhakikisha CCM, haipati kiti Hata kimoja kwenye mitaa yote 16,340..Tanzania.

Ni maoni yangu tu ..
 
Back
Top Bottom