Kibonde ataka Bia iruhusiwe maofisi ya Serikali

MgungaMiba

JF-Expert Member
Aug 28, 2011
999
815
Kwenye kipindi cha Jahazi jioni hii, mtangazaji Ephraim Kibonde amependekeza Bia (Bariidi!) zipatiwe wafanyakazi maofisini kwa sababu zifuatazo;

1. Wafanyakazi watazidisha biidii ya kwenda kazini.
2. Mazungumzo baina ya wafanyakazi na Mabosi wao yatakuwa ya uwazi zaidi (kwani watu wakishalewa wanaongea kwa uwazi zaidi bila hofu!)
3. Malalamiko ya kuongezwa mishahara hayatakuwepo.
 
Mmmmmmmh....nafikiri sassa tuache kumjadili huyu ****
 
Kibonde yuko sahihi.
Kwanza watumishi wengi wanakunywa bia wakati wa kazi, pili pesa nyingi ya rushwa ndiyo hutumika kunywea bia, tatu kwa matumizi makubwa ya bia tutapata ushuru na kodi kwa serikari.
 
juzi nipo hospital nilienda kwa mishe zangu tu sikuwa mgonjwa walanini,nikamuuliza nesi doctor yuko wapi,kwa kuwa ananielewa akaniambia kuwa kaenda kupata kinywaji kidogo ila kanipa nomber na kusisitiza:(akija mgonjwa tu ni beep) vipi ni mbeep?!(nesi aliuliza)nikamwambia mbepp kweli baada ya nusu saa alikuja nusu mzima nusu pombe nikamzuga gonjwa lisiloeleweka nikasepa(labda ni tamaduni yetu kunywa pombe wakati wa kazi si mbaya wazisambaze maofisini)
 
Kha! KIIBONDEEEE .................. tena? ngoja nikapumzike waungwana kama vip keshoooooooo
 
Ipo siku kibonde akicheka wapuuzi wachache wanaojiita pia great thinkers wataleta hapa jukwaani uzi "leo kibonde kafurai".....kwanini kila akisemacho kibonde mnakifanya wimbo wa taifa....ivi ni kweli hakuna ya maana ya kujadili.au mkimwongelea kibonde kuna posho unarudi nayo home....tubadilike bana!
 
mimi nimjuavyo kibonde ni mtu mwenye utani mwingi,so sitaki kuamini kuwa alikuwaserius ktk hilo ila naamini kunaujumbe alikuwa anaufikisha kwa walengwa hivyo kibonde si mtu wa hovyo kiivyo jipe mda wa kuktafakas4 kauri zake.
 
Tangu majuzi nimeshasema huyu kibonde ni hasara kwa jamii yetu na hasa ukizingatia ni mtumwa wa mafisadi!

Mi nafikiri imefikiwa wakati wa kwenda kumpima akili ya huyu juha!
 
Kwenye kipindi cha Jahazi jioni hii, mtangazaji Ephraim Kibonde amependekeza Bia (Bariidi!) zipatiwe wafanyakazi maofisini kwa sababu zifuatazo;
1. Wafanyakazi watazidisha biidii ya kwenda kazini.
2. Mazungumzo baina ya wafanyakazi na Mabosi wao yatakuwa ya uwazi zaidi (kwani watu wakishalewa wanaongea kwa uwazi zaidi bila hofu!)
3. Malalamiko ya kuongezwa mishahara hayatakuwepo.
hapo red kama yeye anavyozungumzaga maranyingi anatokeaga ulevini
ndo mana mazungumzo yake ni ya kipumbafupumbafu tuuu
 
;
1. Wafanyakazi watazidisha biidii ya kwenda kazini.
2. Mazungumzo baina ya wafanyakazi na Mabosi wao yatakuwa ya uwazi zaidi (kwani watu wakishalewa wanaongea kwa uwazi zaidi bila hofu!)
3. Malalamiko ya kuongezwa mishahara hayatakuwepo.

Nadhani Kibonde anadhani kazi zote ni za kuongea tu; maana katika hizo point tatu zilizotajwa sana sana zinahusu kazi inayohusu kuongea kama yake. Akumbuke kwamba wafanyakazi wakinywa pombe kazini kuna hatari zifuatazo:

1. Hawatakuwa makini na kupitisha mikataba mibovu
2. Watahatarisha maisha yao na wengine pale kazi yao inapohusu kutumia vyombo vya hatari
3. Hawatajadili mambo bali kubishana na hata kuishia kurushiana ngumi
4. Hawatakuwa na staha kwa mmoja na mwenzake ofisini
5. Madereva watasababisha aksidenti zisizo na msingi
6. Waongoza ndege watasababisha ndege hata kugongana
7. Wafanyakazi wengi wa kiume watapatwa na "mifadhaiko" ofisini
8. Madaktari wengi wataishia kupasua watu vichwa badala ya miguu
9. Manesi wengi watapeleka wagonjwa mochari badala ya wodini
10. Askari watawaweka lupango watu wote wanaofika vituo vya polisi, bila kujali wanafika kutoa taarifa za uhalifu au wao ndio wahalifu
11. Wabunge wengi wataishia kuwatwanga mangumi mheshimiwa spika, naibu spika, na wabunge wengi wa sio na hoja za mshiko
 
Back
Top Bottom