fundiaminy
JF-Expert Member
- Jun 4, 2009
- 355
- 51
JK na kibaki walipata mualiko kwenda ulaya.walipofika ugenini waliandaliwa karamu ya kukata na shoka.mezani kulikuwa na vijiko vya dhahabu na wote wawili walikuwa na mpango wa kupita na kimoja ila hakuna aliemwambia mwenziwe.wakati wamemaliza kula ikawa tym ya maombi na katika kuomba ilibidi wafunge macho.JK kwa ujanja akajifanya amefunga macho kumbe wapi.ndipo akamuona kibaki akichukua kijiko na kukificha ndani ya koti.baada ya maombi JK aliwaambia wote waliokuwemo kuwa anataka kufanya magic show.akapewa ruhusa.hapo akasema mnaona hiki kijiko.ni takiingiza ndani ya koti langu na kitatokezea kwa koti la kibaki.wenyeji wakasema haiwezekani.hapo JK akachukua kijiko na kukitia ndani ya koti na akaelekea kwa kibaki na kutoa kile alichokificha.watu wote wakampigia makofi na kumpatia dollar mia mia kila mmoja.kijiko akatoka nacho kiulaini.