KIAMA CUF: Baada ya kugalagazwa Uzini, Temeke yapasuka wanachama zaidi ya 1,400 WAJITOA

wanachama wa ngazi za juu wilaya ya temeke na wanachama zaidi ya 1000 wamerudisha kadi za chama kwa sababu ya kwamba CUF inazingatia maslahi ya zanzibar tu na sio Tanzania nzima. malim Seif anafanya makusudi kumaliza nguvu za Cuf bar. wamesema wanamuunga mkono Hamad Rashid. kadi zimekabidhiwa kwa Shakuwa a.k.a daia daia ambaye amejiunga CUF 23/08/1992. itv
 
Zaidi ya wanachama 1000 wa chama cha wanachi(CUF) wamerudisha kadi zao za uanachama na kujivua uanachama wa chama hicho katika wilaya ya Temeke,Dsm.

Katika madai yao wamedai kuwa chama kimepoteza dira yake kwa kuwa kimekuwa chama cha kifalme kinachoegemea upande mmoja wa Zanzibar na viongozi wake hususani Maalim Seif kuonekana kukidhoofisha chama upande wa bara ili kiwe na nguvu Zanzibar.

Wamesema ni mtu mmoja tu ambaye ni Hamad Rashid aliyeonekana kukitetea chama pande zote za bara na visiwani ila akaonekana hafai.

My take: CUF wasipojinusuru sasa,chama hiki kitakuwa kaburini mwaka 2015.
 
Dalili nzuri kwa CHADEMA kuchukua nchi 2015! Hamad anasubiri nini na chama chake kipya?
CHADEMA geukieni pia mikoa kusini, wilaya za Tandahimba & Newala hakuna siasa ni udini na ubinafsi tu, tunawasubiri mje kuelimisha watu maana ya demokrasia katika siasa ni nini. Kazeni uzi mje mtupe nguvu tuchukue majimbo, CCM & CUF huku ni makapi tu..!
 
nimecheka sana nilipoona itv jamaa wa cuf wakirudisha kadi zao.
Usicheke sana asije akakusikia Marytina and the gang, hao hawakuwa jamaa wa CUF wala CCM! Walikuwa ni mashabiki wa Chadema na naomba usiniulize kadi za CUF walizipata wapi, hiyo ni siri ya Mhe. Hamad Rashidi! Kwanza watu wenyewe hawakai Temeke na labda walisafirishwa kwa fuso kutoka mkoa moja wa kaskazini, kaazi kweli kweli...!
 
Kila siku tunasema hapa na hata majukwaani tunasema, mpinzani wetu kwa sasa ni ccm, hawa wengine si saizi yetu.

Isipokuwa na wao ili waonekane washindani wanalazimisha kushinbdana na chadema. Haya sasa kiko wapi na cuf yenu, mmeambulia aibu tupu.

Mahali ambapo mnaongoza serikali lakini mnapigwa kumbo na chadema, ambayo mmeendesha kampeni kuanzia vibarzani, maskani hadi misikitini kwamba chadema chama cha kikristo lakini bado tu cuf mmekanyagiwa chini!!

Your days are numbered, mtajuta kufunga ndoa na ccm.

Mkuu punguza Valeur! Taingia lini Ritz ni CUF?
 
Naona chadema wanafurahi CUF kudorora as if wao wanapingana na CUF na siyo ccm? connect dots..
 
CUF ilisajiliwa bar chini uongozi wa mzee James Mapalala. Maalim kwa makusudi na kwa kuwatumia usalama wa taifa alihakikisha mapalala anakikimbia chama ili ccm iendelee kuongoza kwa mabavu. Maalim yupo CUF kimwili, ila kiroho hana tofauti na Lyatonga wa Kiraracha. Hao wanachama wamejiunga chama gani? Kwa kuwa ni watoto wa mamdogo lazima watajiunga kwa mwenzao jk.
 
CUF ilisajiliwa bar chini uongozi wa mzee James Mapalala. Maalim kwa makusudi na kwa kuwatumia usalama wa taifa alihakikisha mapalala anakikimbia chama ili ccm iendelee kuongoza kwa mabavu. Maalim yupo CUF kimwili, ila kiroho hana tofauti na Lyatonga wa Kiraracha. Hao wanachama wamejiunga chama gani? Kwa kuwa ni watoto wa mamdogo lazima watajiunga kwa mwenzao jk.
Kwasasa hawana chama....ila dalili zote zinaonyesha wanasubiria chama kipya cha Hamadi Rashidi
 
Huyo hamadi mbona kagoma kutoka CUF
Hicho kipya atakiundaje?
Au anasubiri 2014/15 apate marupurupu ya ubunge ndo abwage manyanga?
 
Unafiki wa cuf ni mbaya sana,
wenzao waliomba kwenda ikulu,
wao wakasema wamefata chai,
nawao wakaomba bila kujua cdm walipeleka tangawizi na sukara,
walipofika wakaparamia chai
sasa yamewafuka tangawizi imezidi kwenye chai na hakuna wakumsaidia mwenzake,
kwa mume kunawaka moto,na kwamke kunateketea,
hapo tunasema ndipo patam
 
Back
Top Bottom