Washirika wa Japhet Maganga baada ya kula bata Morogoro na Zanzibar sasa ni Mwanza kisha Dubai

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
Kufuatia utafutaji wa uungwaji mkono ndani ya Chama cha Walimu Tanzania, Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Japhet Maganga analaumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha za wanachama wa chama hicho katika juhudi za kuwalaghai viongozi ambo wengi wao ni wajumbe katika vikao vya maamuzi ya chama cha walimu.

Kwa mujibu wa taratibu za Chama cha Walimu vikao hufanyika pale kuna kunapokuwa na hoja muhimu au vikao vya kikanuni katika kuendesha chama, hata hivyo Mwl Maganga ameendesha mkutano Mkoani Morogoro mwezi wa sita na kisha mwezi September mkutano mwingine visiwani Zanzibar ambapo wajumbe kutoka katika mikoa yote hulipwa fedha nyingi zitokanazo na michango ya walimu wanayokatwa.

Aidha, Katibu Mkuu Japhet Maganga ameahidi wajumbe wa mikoa yote (ambao ni wapiga kura) kuwa baada ya sherehe anayotarajia kuifanya Mkoani Mwanza atawapeleka wajumbe hao kufanya mkutano mwingine
Katika Falme za Kiarabu (UAE) mapema mwanzoni mwa mwaka 2024 ikiwa ni muendelezo wa kuwashawishi waendelee kumuunga mkono.

Wanachama wa CWT wanaendelea kutoa hoja na madai mbalimbali kupinga sherehe inayotarajiwa kufanyika Mkoani Mwanza kwa minajili ya kutojali maslahi ya wanachama.
 
Kwani huyu maganga ...si ndio kibali kimezuiliwa ? Akafundishe darada 2 B?
 
Back
Top Bottom