Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Kwa hakika, makala iliyohusu EL haikuwa mahsusi katika ukumbi huu, ilipita katika anga zangu nikawa naisukuma kwa wapigania uhuru ambao wameihariri na kuitoa katika gazeti la Mwana Halisi toleo la jana ukurasa wa tano ikiwa na kichwa "Lowasa usinong'one sema hadharani" ikielezea kwamba kama kweli yeye ni msafi ajitokeze kusema, "Manji amewanga wajumbe wa kamati" na ikibidi asaidie kuchukuliwa hatua, ili watu wajue kwamba Manji hana wadhifa juu ya wote na watu wasione kwamba naye alihusika katika huo mgawo.
Cha msingi, mwandishi wa makala ile huenda alikua na lengo la kutaka umma uamini kuwa EL hana rekodi ya rushwa na kwamba tusikumbushie Tume ya Warioba, tusikumbushie kauli za Nyerere na tusikumbukie suala la Richmond, tusichokonoe undani wa kuondoka City Water na mengine mengi.
Kwa hakika EL ana kazi kubwa kuishawishi jamii ya sasa kuwa yeye ni msafi kabla ya safari yake kuelekea anakotaka (IKULU)