Kesi ya Mahalu: Nani kilaza hapa?

Jamani sijasoma magazeti ila taarifa ya mwanzo kabisa ilisema makosa ni wizi na kuhujumu Uchimi . Je kesi ya kuhujumu Uchumi ina dhamana?

Inakuwaje leo Mahalu anapelekwa mahakamani na hapo nyuma PCB walikaririwa wakisema kwamba hakuna ushahidi wa kumweka hatiani ? Kuna kitu gani hapa jamani ?
 
Mahalu charged with corruption
FAUSTINE KAPAMA
Daily News; Tuesday,January 23, 2007

FORMER Tanzania's Ambassador to Italy, Professor Costa Ricky Mahalu, and two officials of the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, yesterday appeared before the Kisutu Resident Magistrate's Court in Dar es Salaam, charged with corruption and theft of over 2bn/-, being property of the government.

Before Senior Resident Magistrate Sivangilwa Mwangesi, Prof. Mahalu, together with the former Embassy's Finance Attache Steward Prosper Migwano and Counsellor Grace Alfred Martin denied the charges.

They were released on bail conditions of securing two reliable sureties each, who could sign a bond of 5m/- each of the same amount.

The accused were ordered to surrender their travelling documents to the court, and were also restrained from leaving the city without court's permission.

The case was adjourned to February 20, for mention, as investigations led by officers of the Prevention of Corruption Bureau (PCB), had not been completed.

Their arraignment attracted wider media coverage as several reporters and photojournalists from different media houses thronged the court premises early yesterday morning.

The accused arrived at the court at around 9.00am in a Prevention of Corruption Bureau (PCB) vehicle, Toyota Land Cruiser with registration number T 385 ALK and attempted to diverge photographers by trying to hide in the vehicle behind the court's building near Juvenile Court premises.

Dressed in a dark blue suit, Prof. Mahalu appeared normal and listened tentatively as PCB prosecutor, Mr Joseph Holle, assisted by Ms Tabu Mzee and Mr Benny Lincoln, was reading the charges.

The prosecution alleged that Professor Mahalu conspired with Migwano and Martin on different dates in Italy, Tanzania and other places in the world to steal the said amount.

Mr Holle charged that on September 23, 2002 at the Tanzanian Embassy in Italy in Rome, the accused being employees of the government, knowingly and with intent to deceive their employer, used payment voucher dated September 23, 2002 that contained false materials.

According to the prosecutor, the accused indicated in the voucher that the purchase price of the Tanzanian Embassy building was 3,098,741/58 Euros, the information they knew to be false and was intended to mislead their employer, which is contrary to the Prevention of Corruption Act.

Mr Holle told the court further that on October 1, 2002 at the Embassy, Prof. Mahalu, Migwano and Martin, who were ambassador, finance attache and counsellor, respectively used sales contract and sales, both dated October 1, 2002, containing similar false information.

On the same day and place, the prosecution claimed, the accused being persons employed by the Tanzanian government stole 2,065, 827/60 Euros, being government property.

The trio was also charged with another offence of occasioning loss of the said amount to the government by their wilful acts and misconduct.

Since Prof. Mahalu was recalled back home from Italy in April last year, his status remained ambiguous, until when he resumed work at the legal department of the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation two weeks ago.

According to the government regulations, when one is accused with criminal charges, he/she is suspended automatically until the final trial of the case. Such a person continues receiving half salary.

PAMOJA NA KUKIMBIA KWENYE GARI BADO ALIPIGWA PICHA
 
Issue ya radar wakifunika wao sisi tuta endelea nayo .Najua kuna picha kibao hapa zinachezwa lakini tusikubali kuyumbishwa kila sisue tukianza lazima ifike mwisho wake .
 
Hay Nduguzanguni,

Niwapatie hongereni watawala kwa kumfikisha huyu ndugu kizimbani,

Mimi napata, tofauti ya mashitaka ya huyu Mr Mahalu otherwise ni lugha kwangu yanichechemea! Is Mahalu charged with CORRUPTION / Rushwa....or He charged with THEFT / Wizi?

Nionavyo huyu ni sawa na Jambazi, Mwizi wa kuaminiwa, Mbadhirifu nk, kwani alichofanya yeye ni kuandaa ripoti ya fedha zinazohitajika ktk ununuzi wa jengo la ubalozi, serikali ikamlipa kama alivyoomba then akanunua kwa bei ya chini kuliko alizorequest. Hapa hatumwiti mlaRushwa kwani hakuhongwa bali ameiba (Labda tusema mtoaji na mpokea rushwa wote wana makosa)! Kama yeye alitoa, hao waliopokea wako wapi?

ByTheWay, Hapa JK na EL wanacheza mazingaombwe tuu! wameona kuna joto kwa EL kuhusu Ndesamburo( Which is very hot to the Govenrment team), wameona issue ya Rada ni Hot to the Extent...! etc Sasa ili kutusahaulisha wanampeleka Mahalu kizimbani ilhali TWAJUA HAKIKA atashinda kesi, at the time to come watasema hana hatia! Kwani hela aloiba ilimpatia Mkewe ndo kawekeza kwenye Mgodi wa kufulia dhahabu (Mwananchi Gold) Vingunguti akiwa share na BOT

____________________________
"U Can't Change The Nature"
 
SAKATA LA RUSHWA KATIKA KAMATI YA BUNGE

Lowasa huna hatia, mtose Manji, Vinginevyo katiba ibadilishwe Manji apewe nafasi.

KIKATIBA Waziri Mkuu ni mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa serikali na ana nafasi ya kukaimu Urais pindi Rais na Makamu wake wanapokuwa hawapo nchini. Ni kiongozi wa serikali bungeni na mtu muhimu katika shughuli zote za utendaji nchini.

Mbali ya madaraka hayo ya kikatiba, si siri tena kwamba Waziri Mkuu, Edward Lowasa, ni kiongozi mwenye nguvu kubwa na ushawishi ndani ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete, na hata ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa vigezo hivyo, Waziri Mkuu, Lowasa, ni kiongozi ambaye anaweza kutekeleza yale anayoyaamini na yakatimia.

Nguvu zake hazikuanzia ndani ya serikali ya sasa. Alikua na nguvu hata katika serikali zilizopita, ikianzia na serikali ya Awamu ya Pili ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, alipokuwa Waziri wa Ardhi na baadaye katika serikali ya Benjamin Mkapa, akiwa wizara mbalimbali akimalizia na Wizara ya Maji.

Ni mengi mazito aliyoyafanya ikiwa ni pamoja na kutamka wazi kuhusu rushwa inayotolewa na wafanyabiashara wa kiasia inavyoathiri mipango ya serikali katika sekta ya ardhi wakati wa serikali ya Rais Mwinyi lakini alionyesha ushujaa alipofanikisha kuibana Misri kuhusu matumizi ya maji ya Ziwa Victoria.

Huyo ndiye Edo Lowasa, mtu makini na mtu mwenye kuweza kuthubutu na kutimiza dhamira yake, hasa kama anaamini anachokisimamia ni sahihi. Atakitetea na kukifanyia kampeni kwa nguvu zake zote.

Amefanikiwa kujiweka katika chati akiwa nguzo kuu ya kisiasa na kiutendaji ya serikali ya sasa na ilikua vigumu kwa Rais Jakaya Kikwete, kusikiliza maneno ya wanasiasa na watu waliothubutu kutaka Edo asipewe uwaziri mkuu. Wanaomjua wakasema, piga ua, Edo ndiye Waziri Mkuu wa kasi mpya na ndivyo ilivyokua na ndivyo ilivyo.

Sasa kumeanza kujitokeza mambo mengi yanayomhusu. Baadhi ya mambo yamekuwa yakizungumzwa kichinichini na hakuna aliyekuwa na ushahidi wa wazi na hivyo hadi leo yanazungumzwa tu kabla ya kauli ya Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo kupasua jipu katika kamati ya Bunge yenye nguvu ya Haki, Maadili, na Madaraka ya Bunge kwamba Waziri Mkuu alijua kuwa kuna wajumbe waliohongwa.

Ndesamburo hakuanza kwa kuzungumza na waandishi wa habari kama inavyoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari bali alianza kulizungumzia suala hilo ndani ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, ambayo naye ni mjumbe kwa kuwaasa wenzake wasijadili hoja iliyopo ndani ya kikao kabla ya kujisafisha.

Mbunge huyo mwenye umri wa zaidi ya miaka sabini sasa, aliwashauri wenzake kwamba kama kweli hawajahongwa kama anavyojiamini yeye kuwa hajahongwa, wajisafishe kwa kuwaita wahusika yaani Waziri Mkuu Edward Lowasa, ambaye ndiye chanzo cha habari kwamba kuna wabunge waliohongwa na Mfanyabiashara, Yusuf Manji.

Ndesamburo aliishauri pia kamati ya imuite Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, ambaye alisema ndiye aliyeambiwa na Waziri Mkuu na hatimaye kumwambia yeye kama mmoja wa wajumbe (Inawezekana Mengi aliwaambia wajumbe zaidi) na kutokana na umri wake akashindwa kuvumilia kuonekana amekula rushwa wakati hajala.

Hoja iliyokuwa ikijadiliwa ni malalamiko yaliyowasilishwa na Mengi na Mbunge wa Mkuranga, Adam Kighoma Malima, kila mmoja akimtuhumu mwenzake. Mengi alimlalamikia Malima kwa kudai kwamba ITV inatumia dakika 1.30 kwa Rais na Waziri Mkuu na dakika kumi kwa mambo yanayomhusu.

Ndesamburo alipata wafuasi ndani ya kamati ambapo baadhi ya wabunge waliapa mbele ya kamati kwamba hawajawaho kuhongwa, lakini baadhi walipuuza na kutaka kuendelea na hoja iliyopo mezani. Baadhi walipinga hadi ripoti na mwisho waliandika ripoti zao.

Hayo ni maelezo ya utangulizi na si hoja. Hoja hapa ni kwamba tunapaswa kuangalia sasa ni hatua gani Waziri Mkuu ataiichukua katika tuhuma nzito zinazohusu rushwa ambayo kwa kumbukumbu za wazi anaipiga vita tokea alipokuwa katika serikali ya Rais Mwinyi akiwatuhumu Watanzania wenye asili ya Kiasia.

Kwa kuwa Lowasa ni mtu makini naamini hawezi kutamka hadharani hasa inapofikia kumtaja mtu jina na zaidi kuhusu jambo linalolihusu Bunge kwani katika utawala bora na unaojali sheria na haki za binadamu, hawezi kumtaja Manji wala wabunge husika hadharani. Bado hana ushahidi wa kisheria hata kama ana uhakika rushwa ilitolewa.

Lakini ni hakika Lowasa ni makini na ana uwezo wa kuagiza vyombo husika kufuatilia ukweli na kupata ushahidi hata wa mazingira kuhusu jinsi rushwa inavyoweza kutumika kupindisha haki kwa maslahi ya mtoaji. Lakini kibaya hapa ni kuhusika kwa taasisi muhimu ya kutunga sheria, Bunge.

Naweza kusema kwamba nawashangaa, wanasiasa wanaomtaka Lowasa ajiuzulu wakati Ndesamburo hakusema kwamba Waziri Mkuu amehusika moja kwa moja na rushwa. Alichosema Ndesamburo ni kwamba Waziri Mkuu alimtahadharishwa Mengi kwamba atashindwa kwa kuwa Manji kahonga wabunge, na hivyo ajitoe.

Waziri Mkuu alionyesha kukerwa na jambo hilo na ndio sababu alimshauri Mengi akiwa rafiki yake wa karibu ajitoe katika kesi hiyo ili asije kudhalilishwa kwa nguvu ya fedha na kwa kuwa kwa wakati huo asingeweza kuingilia uhuru wa Kamati ya Bunge kuzuia wasifanye maamuzi kwa wakati huo. Ulikua ni ushauri wa haraka kumnusuru Mengi.

Naamini kwamba Waziri Mkuu bado anakerwa na rushwa na hahusiki kabisa na rushwa iliyotolewa kwa wabunge ila alifahamu kupitia uwezo wake ambao hauna shaka, lakini sasa nini kinatakiwa kifanyike baada ya suala hili kuanikwa hadharani?

Inawezekana kumekua na makosa kulianika suala hili hadharani kwani kutaharibu baadhi ya ushahidi muhimu ikiwa utahitajika, lakini bado kuna kila sababu kwa Waziri Mkuu kufanya uamuzi wa busara wa kuhakikisha Manji anashughulikiwa kwa kuingiza hasira zake binafsi katika taasisi adhimu ya kutunga sheria kwa kupenyeza rushwa.

Ni busara pekee na ushauri mwema utakaoweza kumsukuma Lowasa kuamua kumtosa Manji ili na kumwacha ashughulikiwe na vyombo husika badala ya kumshauri kukwepa hoja hiyo kisiasa.

Manji amehusishwa na mambo mengi yenye utata na hakuna hata mara moja kiongozi yeyote wa juu wa serikali aliyewahi kutoa tamko ama kuagiza hatua zichukuliwe dhidi ya mfanyabiashara huyo. Ni Lowasa pekee ndiye aliyetoa tamko la kwanza, lakini si hadharani bali pembeni kwa hiyo asonge mbele kuisafisha serikali ya Kikwete.

Ukimya utakaoendelea kuhusiana na mambo aliyoyafanya Manji, utaibua hisia mbaya dhidi ya serikali kuonyesha kwamba Manji yuko juu ya kila kitu na kwamba hakuna yeyote anayeweza kumgusa. Ikiwa Waziri Mkuu atamsema pembeni Manji badala ya kumkamata, ni nani atakayemshughulikia? Manji ana wadhifa gani katika mfumo wa kitawala hata Waziri Mkuu ajitoe kafara kutoanika uozo wake japo kwa kukemea tu?

Kwa uchache tu, Manji ametajwa katika biashara yenye utata mkubwa ya uuzaji majengo kwa NSSF na PSPF kwa kiwango kinachofikia Shilingi bilioni 83; Manji alipanga kuchota NSSF,PSPF na PPF kiasi cha Sh Bilioni 80 ili aanzishe mfuko wa kukopesha wa Sh Bilioni 100 na ni Manji aliyeichanganya CCM na kuchukua kampuni yake ya bahati nasibu (Gaming Management Tanzania Limited);

Kadhalika Manji amehusika katika sakata la sukari na bidhaa nyingine zilizohusisha jeshi; Manji anatajwa tajwa katika matukio mengineyo mengi yenye utata lakini zaidi ni kwamba ni Manji aliyetajwa moja kwa moja kuchezea fedha za mikopo ya Japan (Import Support) na uchunguzi ulifanywa na kukaribia kumshitaki lakini hadi leo hakuna mashitaka yoyote yaliyofunguliwa dhidi yake.

Waziri Mkuu, Edward Lowasa a.k.a Edo, mtose Manji ujisafishe, kwani katika hili la rushwa katika kamati ya Bunge huna hatia, kama kuna linalokusibu subiri na si kukubali kuwa kinga ya mtu ambaye si lolote si chochote katika mfumo wa utawala. Vinginevyo watu watapendekeza katiba ibadilishwe wafanyabiashara kama Manji watajwe katika mfumo wa utawala kwa kuwa wana nguvu isiyoonekana. HAWAGUSIKI (Untouchable).
 
Ndugu yangu Halisi, umekuja na makala nzuri lakini pia imeibua maswali mengi kuliko majibu.

Umemulelezea waziri mkuu kuwa ni mtu makini na mwenye historia ya kupambana na rushwa tangu akiwa katika serikali ya Mwinyi. Kwamba hata kitendo cha kumpigia simu Mengi ilikuwa ni moja ya jitihada zake za kupambana na rushwa. Kajiswali kangu kati hii mada ya Mengi vs Kamati ya Bunge ni haka:

Hivi ni umakini gani kwa waziri mkuu kumpigia simu Mengi kwamba ajitoe katika kesi baada ya kujua kuwa wabunge wamehongwa? Hivi isingekuwa sahihi kwa waziri mkuu kuchukua hatua ya kisheria kwa mhongaji na wahongwaji?

Kama alikuwa hana uthibitisho na hayo madai yake, kwa nini asingechukua hatua ya kuchunguza kwa kutumia vyombo vya dola au kuunda kamati ya uchunguzi? Huyu ni kiongozi makini kweli!!?
 
Mwanasiasa upo sawa,

Halisi, umakini wa Eddo sijauona katika sakata hili, lengo la rushwa ni kupindisha taratibu ili walafi wafanikiwe.Sasa tuseme Mengi angeamua kufuata "ushauri makini" wa eddo na kujitoa, haki ingekuwa imetendeka? Nani angeshinda mengi au mhongaji? Hapa "kiongozi makini" alikuwa anafanikisha lengo la Mengi au mhongaji?

Eddo alichukua hatua zipi kuhakikisha haki inatendeka? Tuache unafiki, ni mara ngapi Eddo Kaingilia bunge kwa mgongo wa uwaziri mkuu na kama mwenyekiti wa wabunge wa CCM? huwatisha wabunge wa CCM wasiongelee baadhi ya mambo katika bunge? Hapa hajaingilia bunge? Kwa nini kwenye sakata hili tu ndio hataki kuingilia kazi ya bunge? Kwanini hajatumia Uenyekiti wake wa wabunge wa CCM kudhibiti wabunge wa CCM kuhongwa?

Sioni mantiki ya kukimbilia kwenda kwa mangi badala ya PCB, na bado alikuwa na nafasi kumuambia spika kwamba kamati imehongwa inalidhalilisha bunge. Uzalendo wake unahojika hapa, ikiwa alikaa kimya na kuaacha msururu wa vikao kutafuna kodi yetu wakijadili suala la watu waili ihali akijua wamehongwa uamuzi wake unakuwa kuuambia upande mmoja ujitoea? Suala la maadili na haki halikuwa kipaumbele kabisa kwake!! Sijaona umakini kabisa hapa, ameboronga ndio maana yuko kimya, hana hoja, angekuwa ana hoja, viongozi waz Tz ni wapenda sifa angekurupuka kusema.
 
Ongara ume eleweka vyema sana .Nakubaliana nawe . Halisi una harufu ya unafiki rekebisha mzee hapa hapendiw mtu na sisi tuna badilika kutokana na issue .EL ni corrupt na hana upendo na Tanzania ila upendo na watoa rushwa na wala rushwa wenzake .
 
Mi nilichukulia hiyo "makala" ya Halisi (sijui kama iko kwenye gazeti tayari) kuwa inalenga kumsafisha huyo Eddo!
 
Friends.. hii mada ya Mahalu inazua moto sana... legal threats are everywhere.. na hii inaweza kuwa ni sababu ya site hii kufungwa au hii mada kuondolewa mara moja....!! tread careful
 
Mzee Mwanakijiji,

Hiii mada inakuwa ya motto kutokana na walioko nyuma ya huyo mshitakiwa, wanamtandao tunawajua, ukweli ni kwamba huyu mshitakiwa hakula peke yake wako wengi na hapa bongo kuna tetesi kuwa lengo la mashitaka ni kumtafuta kigogo mmoja mstaafu,

ila huyu mshitakiwa ni njia tu ya kumfikia huyo kigogo, kwa hiyo hakuna la ajabu tunajua lakini tutawasema tu waliokula naye kina Lumbanga, let the chips fall where they may!

Wakifunga hiii, itaaanza nyingine waende!
 
Mzee ES, inasikitisha kuwa tumeweza kuzungumza ya Dito, ya Mahita, ya watu mbalimbali lakini kwa kadiri tunavyoenda mbele kuna watu wanadizi kukunwa kusikokunwa! na wanaanza kujichubua!! Wao ndio wataumia!!
 
Mzeee wangu sikiliza, sasa hivi bongo kuna kizaaa zaaa cha radar, ndio chanzo cha motto wote uliopo sasa, maana UK wanalifuatilia kwa makini hilo na inafahamika kuwa kuna wa-UK waliohusika na mlo,

sasa cha ajabu wanachojiuliza wabongo ni iweje wa-UK wakubali kuwa walihusika na mlo, wakati bongo as a government tunakataaa? Na mhindi aliyehusika yupo hapa yaani middleman wa kila deal huyo huyo mtu mmoja tu?

Sasa zinapokuja na presha za hizi forum na baadhi ya magazeti kama ya TD ndio maana wakubwa wanahangaika, kwa hiyo be ready kuona hiii forum ikivamiwa, ila motto wote huku bongo chanzo chake ni radar!
 
Waache kuwaibia maskini ambao hawana lolote na wafanye kazi ambazo wanatakiwa kuzifanya. Once Tony Blair said 'if you want to be out of trouble say the truth all the time, and do what you are supposed to do to serve the people'.
 
Nimesikia kuwa kuna mfanyabishara maarufu nchini naye huenda akapelekwa kizimbani na PCB juma hili au lijalo kwa ufisadi wa mabilioni. Inasemekana ni kijana ana asili ya Kiasia. Naona kumekucha!
 
Balozi Costa Mahalu kortini Dar kwa kuhujumu uchumi, wizi.

Na Nora Damian.

Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, ambaye sasa amerejeshwa nyumbani, jana alipandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, kwa makosa sita ya uhujumu uchumi, wizi na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh2 bilioni.

Balozi Mahalu alitiwa mbaroni na maafisa wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (Takuru) pamoja na watu wengine wawili waliokuwa maofisa wa Ubalozi wa Tanzani nchini humo ambao nao wanaohusishwa na tuhuma hizo. Wengine ni Steward Migwano ambaye alikuwa Mtunza Fedha na Grace Martin ambaye alikuwa Afisa Utawala ubalozini hapo.

Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama hiyo ya Kisutu jana asubuhi wakiwa kwenye gari la Takuru aina ya Toyota Landcruiser lenye namba za usajili T385 ALK na kusomewa mashtaka hayo yanayohusiana na upotevu wa Euro 2,065,827.60 wakati wakiwa maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Italia. Euro ni sawa na Sh1,692.74.

Wakiwa bado nje ya majengo ya mahakama hiyo wakisubiri kuingia mahakamani, Profesa Mahalu akiwa amevaa suti nyeusi, alipowaona waandishi wa habari na wapiga picha wa vyombo mbalimbali, alikimbia na kujificha ndani ya gari lililowapeka mahakamani hapo.

Takribani nusu saa baadaye, Balozi Mahalu akiwa na wenzake alioshitakiwa nao, walishuka kwenye gari hilo na kuingia mahakamani huku muda wote kabla ya kuingia katika chumba cha mahakama akionekana akibofya simu yake ya mkononi huku akiwa ameinamisha uso wake chini.

Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Sivangilwa Mwangesi na kusomewa mashitaka sita na waendesha mashitaka.

Katika shitaka la kwanza, Wakili wa serikali, Joseph Haule, alidai kuwa washitakiwa hao kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa katika tarehe tofauti na katika maeneo tofauti huko Italia.

Aliendelea kudai kuwa katika shitaka la pili, watuhumiwa hao walimpotosha mwajiri wao katika hati ya matumizi, kwani Septemba 23, 2002 katika ubalozi wa Italia jijini Roma, washitakiwa wakiwa waajiriwa wa Serikali ya Tanzania, walisaini vocha yenye namba D2/9/23/9/02 ikionyesha kuwa bei ya ununuzi wa jengo la ubalozi ni Euro 3,098,741.58 maelezo ambayo yalikuwa ni ya uongo na yenye nia ya kumdanganya mwajiri wao.

Mwendesha Mashitaka huyo wa serikali aliendelea kudai kuwa shitaka la tatu ni la matumizi ya hati za kupotosha, akidai kuwa Oktoba Mosi, 2002 washitakiwa wakiwa waajiriwa wa serikali kwa pamoja walisaini mkataba wa mauzo ambao ulikuwa na maelezo ya uongo na yenye lengo la kumdanganya mwajiri wao yaliyoonyesha kuwa ununuzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia ni euro 3,098,741.58.

Alieleza kuwa shitaka la nne linahusu matumizi ya hati za kupotosha ambazo washitakiwa walizitumia Oktoba Mosi, 2002, kuonyesha kuwa muuzaji wa jengo la ubalozi mjini Rome alipokea Euro 3,098,741.58, huku wakijua kwamba ni uongo.

Katika shitaka la tano, mwendesha mashitaka mwingine wa serikali, Tabu Mzee, alidai kuwa Oktoba Mosi, 2002 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, washitakiwa hao kwa pamoja waliiba euro 2,065,827.60 ambazo zilikuwa mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika shitaka la sita, Mzee alidai kuwa Oktoba Mosi mwaka 2002, washitakiwa waliisababishia hasara Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya Euro 2,065,827.60.

Washitakiwa wote walikana mashitaka yote na upande wa mashitaka uliiomba mahakama itaje tarehe nyingine ya kuendelea kwa kesi hiyo kwa madai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Wakili anayewatetea washitakiwa hao, Alex Mgongolwa, aliiomba mahakama iwapatie dhamana wateja wake kwa kile alichodai kuwa ni watu ambao kitaaluma hawawezi kuruka masharti ya dhamana.

Katika mazingira ambayo upelelezi wa kesi bado kukamilika, mheshimiwa hakimu tunaomba mahakama yako tukufu iwape dhamana washitakiwa wote watatu, tunaomba masharti nafuu ya dhamana kwa kuwa ni haki yao na hawana kumbukumbu zozote za kuwahi kuruka masharti ya dhamana, alieleza Mgongolwa wakati akiomba dhamana hiyo.

Kwa upande wake, wakili wa serikali, Joseph Haule, aliieleza mahakama kuwa upande wa mashitaka hauna pingamizi la dhamana iwapo tu itazingatia sheria ya uhujumu uchumi.

Baada ya kusikiliza pande zote, Hakimu Mwangesi, aliahirisha kesi hiyo kwa muda wa dakika kumi ili apate fursa ya kupitia vifungu vya sheria ya masharti ya dhamana katika kosa kama hilo.

Baada ya kupitia vifungu hivyo, majira ya saa 6 mchana, Hakimu alitoa masharti ya dhamana akimtaka kila mshitakiwa ajidhamini kwa maandishi kwa Sh5 milioni pamoja na kuwa na wadhamini wawili watakaosaini Sh5 milioni kila mmoja.

Wadhamini wawili lazima wawe watu ambao wanaaminika na hasa watumishi wa serikali, mnatakiwa kuwasilisha hati zenu za kusafiria na hamruhusiwi kutoka nje ya Dar es Salaam, alisema Hakimu Mwangesi.

Washitakiwa hao walishindwa kutimiza masharti ya dhamana wakati huo na wakili wao akalazimika kuiomba mahakama itoe muda kidogo hadi saa 7:30 mchana ili wakatafute wadhamini.

Mheshimiwa Hakimu washitakiwa leo walienda kazini kama kawaida na walipofika kazini wakakamatwa hivyo suala la kupata wadhamini kwa muda huo likawa gumu, tunaomba muda kidogo hadi saa 7:30 tutafute wadhamini,alisema.

Hakimu alikubali ombi hilo na kuhahirisha kesi hiyo hadi saa 7:30 na washitakiwa hao waliweza kutimiza masharti ya dhamana na kuachiwa huru. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 20 itakapotajwa.

Sakata la Profesa Mahalu limekuwa likigonga vichwa vya habari vya magazeti nchini na katika mkutano wa bajeti bungeni liliibuka, serikali ikitakiwa kutoa msimamo wake.

Katika hotuba yake ya kuchangia kuhusu bajeti ya Wizara ya Sheria na Katiba, msemaji wa kambi hiyo, Fatma Maghimbi, alihoji hatua ya serikali kupeleka suala hilo Takuru badala ya mahakamani.

Tumesoma katika magazeti kwamba kumetokea wizi wa kughushi katika balozi yetu nchini Italia wa fedha za Tanzania Sh2 bilioni, wizi wa kughushi kwa lugha ya kisheria ni forgery (kughushi) na sio corruption (rushwa), alisema
Maghimbi.

Kambi hiyo iliitaka serikali kutoa ufafanuzi wa kwanini tuhuma hizo zisipelekwe mahakamani badala ya Takuru na kama ni kweli limetokea tukio hilo basi ieleze ni nani waliohusika.

Kimya cha muda mrefu cha seriali kilimalizika jana, baada ya suala hilo kufikishwa mahakamani.

Wakati hayo yakitokea, tayari Profesa Mahalu alikuwa amekwisafungua kesi ya madai Mahakama Kuu akidai fidia ys Sh12 bilioni kwa vyombo vya habari zilivyoripoti habari zake, akidai kuwa viliandika habari za uongo dhidi yake.

Profesa Mahalu katika mashtaka yake, alikuwa anadai kuchafuliwa jina lake wakati yeye katika muda wa miaka minne ya utumishi kama balozi aliwahi kutunukiwa tuzo ijulikanayo kama Stella Della Solidarieta Italiana ambayo alitunukiwa na Rais wa Italia Aprili 13 kabla ya kurudi Tanzania.

Katika kesi hiyo anayotetewa na Kampuni ya Uwakili ya Adili, mdai anataka mahakama iamuru waliomuandika wakanushe habari hizo zilizochapishwa kwenye magazeti hayo na kutangazwa kwenye vituo vya televisheni na radio vinavyomilikiwa na mshitakiwa wa kwanza. Anataka pia mahakama izuie walalamikiwa kuchapisha tena habari zozote zenye mwelekeo wa kumchafua na kumkashifu.

Pia mahakama hiyo iwaamuru walalamikiwa kumlipa fidia na riba ya gharama ambazo walalamikiwa wataamuliwa kumlipa pamoja na gharama atakazotumia kuendesha kesi hiyo.

Katika hati yake hiyo, Profesa Mahalu alieleza juu ya mpango wa serikali wa kununua jengo la ubalozi mjini Rome, Italia. Balozi huyo anadai kuwa Juni 2001 alielekezwa na serikali kutafuta jengo mjini humo kwa ajili ya ofisi za ubalozi wa Tanzania. Anadai Julai, 2001 alikamilisha kazi hiyo na kutoa ripoti kwa mwajiri wake.

Alidai kuwa alipata majengo matatu na thamani yake zilikuwa kati ya Dola za Marekani 2.25 milioni na Dola 3 milioni na kuambatanisha barua iliyoandikwa na ofisi yake kwenda Wizara ya Mambo ya Nje kuwajulisha bei za majengo hayo matatu yaliyopendekezwa na balozi kwa serikali ya Tanzania.

Kwa mujibu wa Profesa Mahalu, Julai 2001 mtathmini wa majengo aliyemtaja kwa jina moja la Kimweri kutoka serikali ya Tanzania alienda mjini Rome, Italia kwa ajili ya kutathmini majengo hayo na akapendekeza kununuliwa kwa jengo la Via Cortina D'ampezzo 185 Roma kwa gharama za Dola 3 milioni.

Ripoti ya Kimweri ya Agosti 2001 ilielezea jengo hilo kuwa ni la ghorofa tatu lenye ukubwa wa meta za mraba 1,000 na kiwanja chenye ukubwa wa meta za mraba 2,500. Jengo hilo lilielezwa kuwa liko mahali pazuri kwa vile ghorofa mbili zingefaa kutumika kama ofisi huku ghorofa moja inatumika kama nyumba ya ofisa wa ubalozi.

Profesa Mahalu pia aliambatanisha barua inayoijulisha Wizara ya Mambo ya Nje namna ambavyo mthamini wa serikali alivyopendekeza jengo hilo lishushwe bei kutoka Dola 3.7 milioni hadi hadi kufikia kati ya Dola 2.7 ambazo wakati huo zilikuwa sawa na Sh2.5 bilioni.

Maelezo hayo yanaonyesha kuwa mwaka 2002 Balozi Profesa Mahalu alikuja nchini kufuatilia malipo ya awali ya fedha hizo na wizara ikampatia Sh700 milioni badala ya Sh1 bilioni zilizokuwa zimepitishwa na Bunge kwa ajili ya ubalozi wa Italia.

Julai 03, 2002 Profesa Mahalu aliandika barua nyingine kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje kumweleza majadiliano yake na mmiliki wa jengo lake na ushauri waliopeana ili asiliuze jengo hilo kwa wahitaji wengine. Katika barua hiyo balozi huyo ameeleza sababu ya kufungua akaunti katika benki ya Credito Italiano.

Profesa Mahalu anadai kuwa walilazimika kufungua akaunti hiyo maalum kwa ajili ya kuhifadhi fedha za kununua jengo hilo. Anadai walifungua akaunti namba 725400464 na wakaweka Euro 2 milioni za malipo ya awali ya jengo hilo na malipo mengine ya Euro1.09 milioni ilikuwa ni lazima yaingizwe kwenye akaunti hiyo kabla ya Septemba 2002.

Alidai kutokana na hali hiyo ubalozi ulilazimika kufungua akaunti hiyo na kuweka Sh1.9 bilioni "Maelezo ya akaunti hiyo yatawasilishwa kwako hivi karibuni huku tukisubiri kiasi kingine cha Sh1.2 bilioni," ilisema sehemu ya barua hiyo.

Profesa Mahalu pia aliandika barua Julai 05, 2002 kwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje kumjulisha uamuzi wa ubalozi wa kufungua akaunti hiyo.

Septemba 23, 2002 ubalozi huo uliandika barua kwa meneja wa direzione Territoriale Italia Centrale kumwomba ahamishe Euro 3.08 milioni kutoka kwenye akaunti namba 725-400464 ya ubalozi wa Tanzania. Benki hiyo ilihamisha fedha hizo Oktoba Mosi, 2002.

Katika barua ya Profesa Mahalu ya Oktoba 8, 2002 kwenda kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, inaonyesha kuwa balozi huyo alisaini makubaliano ya kuuziana jengo hilo Oktoba Mosi na jengo hilo likakabidhiwa serikali ya Tanzania.

Katika maelezo ya ziada kwenye malalamiko yake, Profesa Mhalu alidai amewahi kuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu katika Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu. Aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Italia mwaka 2000, Kabla ya hapo aliwahi kuwa ofisa wa ubalozi nchini Ujerumani kuanzia mwaka 1997.
 
Back
Top Bottom