Kesi ya Mahalu: Nani kilaza hapa?

Kweli JF kisima cha FIKRA.
Ninaamini michango yenu wanabodi na ninasikitika sana kwa serikali kuamua kuiblow hii kesi kwa kutomuandaa shahidi wake, na Pia ninasikitika zaidi kuwa inawezekana Mwizi (Mahalu) akatoka kifua mbele mahakamani.

Kwa kutoa ushahidi unaoelekea kumruka swahiba wake ni sawa na kujiingiza ktk kitanzi. Hivyo Lumbanga kaumia. Na kesi itakuwa tamu zaidi Hosea akitimuliwa PCCB

Hamkujua kuwa waendesha mashtaka wetu ni vilaza??
 
hivi tanzania mna amnesia, wizara ya mambo ya nje ndiyo ilikuwa na majukumu ya kuomba pesa zile hazina nakuruhusu kununuliwa hilo jengo...hivi nani alikuwa waziri wa mambo ya nje who signed off for that?
 
Ile barua iliyompa Mahalu "power of attorney" ya kununua hiyo nyumba kwa niaba ya serikali ilisainiwa na JK wakati huo akiwa waziri wa mambo ya nje.

Kisheria unapopewa "power of attorney" kufanya transaction kwa niaba ya mwingine, unawajibika binafsi kuyatimiza matakwa ya kisheria ya yule aliyekupa jukumu hilo, ukienda kinyume makosa ni yako na utawajibika nayo.

Hiyo barua ya "power of attorney" ya JK kwenda kwa Mahalu nadhani iliwahi kubandikwa kwenye forum hii (kama sijasahau, ninachokumbuka kwa uhakika ni kwamba nilishawahi kuiona, kwa hiyo kama si hapa basi ni katika hizo sources ambako nina access).

Kwa hiyo kama ni kweli alighushi hiyo mikataba ya kuuziana akawa nayo miwili ya bei mbili tofauti, hilo kwa hakika hakutumwa, "power of attorney" aliyopewa si ya kufanya yaliyo kinyume na sheria. Lakini tunaelewa na tuna uzoefu kuwa sheria na haki ni vitu viwili tofauti, kwa hiyo tunasubiri!
 
Nimekupata Mtanzania,

Unajua tatizo la nchi hii vile vile ni kuwa na very weak prosecutors, wakali wa hii fani hawataki kufanya kazi serikalini na wanaona bora waingie kwenye private practise. Sasa unapokuwa na weak prosecution team kwenye kesi kama hii kushindwa ni lazima.

Mi nawafahamu sana Alex Mgongolwa na Cuthbert Tenga, wako fiti tena kama kesi ndo ina bingo kama hii na burden of proof iko kwa Prosecution. Hii ngoma serikali ishaelekea kushindwa, wameanza na very poor approach kwa kumleta material witness unprepared. Defence team wataivunjilia mbali credibility yake(Lumbanga)na kama unavyoona wameshaanza kumthreat na perjury.

Inaumiza sana roho kwa kesi kama hii, unaona kabisa mtu kakwiba lakini kwa sababu tuna team mbovu ya prosecution ambayo haijafanya reseach ya uhakika na kushindwa kuprepare witness on cross examination. Kulikuwa na ulazima gani wa Lumbanga kuwa first witness?.

Anyway ngoja tuangalie lakini ni mtizamo wangu kuwa kesi hii imeisha.

Mbangaizaji,

Kuna taarifa kwamba hawa prosecutors wameshapewa "hongo"; ni competent lakini kwa sababu ya tamaa ya pesa, wanaamua "kushindwa kesi" .... hapo hakuna kesi; tumeshapigwa bao jingine.
 
Wakuu hebu oneni vituko vya waandishi wa habari tulionao Bongo. Ni tukio moja linaripotiwa hapa, na waandishi wa "The Guardian" na "Nipashe" walikuwepo mahakamani. Wa "Nipashe" anasema Mwanasheria Mkuu wa Italia amekuja Tanzania kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili Prof Mahalu. Wa "Guardian" anasema aliyekuja kutoa ushahidi huo ni padre muitaliano, lakini ndani ya habari wanamtaja kuwa ni wakili pia.

Na wote wawili wanamtaja kwa jina lilelile, maana yake ni mtu huyo mmoja wanayemzungumzia na tukio ni moja. Tofauti hii ni kubwa mno, lazima yupo anayeongopa baina yao, na bila shaka sababu kubwa ni "ukilaza", kwa maneno mengine "lugha haipandi".

Vituko vitupu! Oneni hapa chini:

NIPASHE wanasema:

Mwanasheria Mkuu Italia atoa ushahidi.

2008-03-15
Na Hellen Mwango

Mwanasheria Mkuu wa Italia, Marco Papi (59), ambaye amekuja nchini kwa ajili ya kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Ricky Mahalu, ameambia mahakama kuwa alisaini mkataba wa ununuzi wa jengo la ubalozi ulioonyesha kiasi cha Euro 1,032,000 (karibu bilioni sh. 1.8) na si zaidi ya hapo.

Katika kesi hiyo, Profesa Mahalu na wenzake wanadaiwa kuisababishia Tanzania hasara ya Euro 3,078,741.40 (zaidi ya sh. bilioni 3) kwa kile kinachoonekana kama walighushi mkataba huo na kusomeka kiasi kikubwa cha fedha (Euro 1 ni sawa na sh. 1,838).

Mwanasheria Mkuu huyo wa Italia, alidai kuwa alisaini mkataba huo baada ya kuhakikisha kuwa kuna makubaliano yanayoonyesha kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati huo, aliidhinisha Balozi Mahalu amuwakilishe katika kusaini mkataba na ununuzi wa jengo hilo.

Mbali na Profesa Mahalu, mshtakiwa mwingine anayekabiliwa na tuhuma hizo ni aliyekuwa Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin.

Ushahidi huo ulikuwa unasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi, Bw. Sivangilwa Mwangesi, wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Shahidi huyo alikuwa akitoa ushahidi wake kwa lugha ya Kitaliano na kutafsiriwa na Padre Evalist Lefiyo (39), kutoka Parokia ya Boko jijini Dar es Salaam.

Upande wa mashtaka uliongozwa na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Tabu Mzee akisaidiana na wakili wa Serikali Ponzian Lukosi.

Akiongozwa na Mwendesha Mashtaka huyo, shahidi alidai kuwa mwaka 2002, nchini Italia Profesa Mahalu alikwenda ofisini kwake kwa lengo la kusaini mkataba wa ununuzi wa nyumba.

Alidai kuwa mkataba huo ulikuwa unasainiwa kati ya Profesa Mahalu na muuzaji wa nyumba hiyo ambayo ni kampuni ya Cheres ya nchini humo.

Alidai kuwa Profesa Mahalu aliiwakilisha Tanzania baada ya kupewa mamlaka hayo na Waziri aliyekuwa na dhamana hiyo nchini Tanzania, kusaini na kununua jengo hilo.

Ilidaiwa kuwa mkataba huo ulionyesha kuwa jengo hilo limenunuliwa kwa Euro 1,032,000.

Alidai kuwa mbali na mkataba huo, hakuwahi kuidhinisha wala kusaini mkataba mwingine unaoonyesha gharama tofauti na aliouona hapo awali na kuusaini.

Aidha, Mwendesha Mashtaka alipomhoji shahidi na kumuonyesha nakala ya mkataba wa ununuzi wa jengo hilo, ambao aliusaini na kuidhinisha kuwa ni halali, alikiri kuwa nakala halali ya mkataba huo anayo ofisini kwake huko Italia na kwamba ni halali kwa kuwa una mhuri wa ofisini kwake na saini yake.

Hata hivyo, upande wa utetezi uliongozwa na wakili Alex Mgongolwa, akisaidiana na Bw. Mabere Marando ulimhoji shahidi, na hii ni sehemu ya mahojiano yao.

Mgongolwa: Shahidi huo mkataba ulisaini wewe peke yako?

Shahidi: Hapana, baada ya pande zote mbili yaani muuzaji na mnunuaji wanaanza kusaini halafu mimi namalizia.

Mawakili wa utetezi walimuonyesha shahidi huyo hundi inayoonyesha kuwa kampuni iliyouza jengo hilo ilipokea kiwango kikubwa cha pesa kuliko alivyosema na kumtaka aseme kama ni halali ama la.

Yeye alijibu kwamba si mtaalamu wa kutambua kama hundi hiyo ni halali ama la na kuwataka wamuite mtalaamu wa kibenki.

Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, Marten Lumbanga alidai kuwa aliwahi kusikia kwamba kuna mikataba miwili ya ununuzi wa jengo hilo baada ya kuona na kusoma kupitia vyombo vya habari na magazetini.

Bw. Lumbanga ambaye wakati huo alikuwa Katibu Mkuu kiongozi, alidai pia kwamba baada ya serikali kupanga bajeti ya Shilingi bilioni moja kwa ajili ya ununuzi wa jengo hilo, Profesa Mahalu alimfuata na kumueleza kuwa bei ya hilo jengo imeongezeka zaidi ya kiwango cha awali na hivyo akamtaka ampigie debe kuhakikisha kuwa jengo hilo linapatikana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi April 23, mwaka huu, ambapo shahidi ataendelea kuhojiwa na upande wa utetezi.

SOURCE: Nipashe

=======

GUARDIAN wanasema:

Italian priest testifies against Mahalu
2008-03-15
By Rosemary Mirondo

A legal counsel from Italy, Father Marco Papi, yesterday testified against immediate former Tanzanian ambassador to Italy, Costa Mahalu, in a corruption case he faces alongside former counsellor Grace Alfred Martin.

Papi told the Kisutu Resident Magistrate`s Court in Dar es Salaam that he signed only one contract worth euros 1, 032,913.80 between Prof.

Mahalu and the seller of the building that was acquired by the Tanzanian ambassador in Italy.

Prof Mahalu and Grace Martin are accused of occasioning the government of Tanzania a loss of euros 2, 065, 827.20.

He told the court that because the agreement of sale involved an individual person and a government, they had to seek authority from Tanzania through the Minister for Foreign Affairs and International Cooperation so as to make the contract legally binding.

There was a heated exchange between the prosecution led by an officer from the Prevention and Combating or Corruption Bureau, Tabu Mzee, and State Attorney Ponziano Lukosi and the defence led by counsel Alex Mgongolwa, Mabere Marando and Cuthbert Tenga over the admission of an interpreter.

Tabu: We have one witness from Italy but he can speak neither English nor Kiswahili, so we have brought an interpreter.

Marando: We submit that according to law, an interpreter is for the court and not the prosecution, and anyway, they should tell us how they got him.
Court: Prosecution.

Tabu: The defence alleged that an interpreter is supposed to be brought by the court, but even the witness is for the court and the interpreter is trustworthy because he is a Catholic priest.

Court: So what is your position Marando?
Marando: If the prosecution knew that they were bringing a witness who could not understand either of our official languages, they should have informed the court instead of bringing the interpreter on their own, because the court has to satisfy itself that he is not biased.

Due to that, we pray for two things - a short adjournment of the case so that the court can talk with the interpreter and understand his position here in court or the court can satisfy itself by interrogating him.

This is because the defence wants an interpreter who understands the seriousness of the case and not to interpret what the court wants.

Court: But the prosecution told me that they were bringing an interpreter and I allowed them to do so, but if you have doubts

Marando: I was not aware that you had given the go ahead.
Court: But you also have the privilege to decide.
Marando: Some of us don't trust anyone, even priests (laughter)

Court: Please can we continue? My ruling is: the interpreter was brought by the prosecution after they had consulted me. In this case, I reject the objection raised by the defence.

Court: Prosecution, please bring your interpreter because I have faith in him.

The interpreter is brought forward and says he is a priest of the Roman Catholic Church.

Tabu: Witness, please tell us your name.
Witness: Marco Papi.

Tabu: Witness, can you please tell the court where you are from and your position there?

Witness: From Italy and I am a notary public.
Tabu: What are your duties?

Witness: I go through all the contracts and register them so that they can be legally binding.

Tabu: Do you know the accused in this case?
Witness: I know the former Tanzanian ambassador to Italy, Ricky Mahalu, because he came to my office.

Court: You say that he came to your office to do what?
Witness: To sign a contract.
Tabu: What contract?

Witness: A contract between Cheres Company under Froeella Pagliuca and Mahalu on behalf of the government of Tanzania. It was concluded after I had signed on it.

Tabu: What did the contract contain?
Witness: Property that was being transferred from Cheres to the embassy of Tanzania in Italy.
Court: What property is that?

Witness: According to laws of ownership, it was a house that is now the embassy of Tanzania in Italy.
Tabu: According to that contract, how much was the house sold for?

Witness: As a notary public, I normally don't know the prices. I only know the procedures of obtaining the contract.

Tabu: If you see the contract will you know it?
Witness: The contracts that I go through are many, so it is hard to remember all of them.

Tabu: Is this the contract?

The contract is given to the witness. He goes through it.

Witness: Yes, this is the one, because it bears my signature and my firm`s stamp. I also remember the cost of the house was euros 1, 032,913.80 as indicated in this contract.

The hearing, which started on February 27, this year, will continue again on April 13.

SOURCE: Guardian
 
Naona kulikuwepo na Notary Public (Marco Papi) na Mkalimani (Padre Evaristo Lefiyo). Hakuweko Attorney General wa Italy. Si rahisi kumleta Attorney General wa Italy aje kutoa ushahidi hapo Kisutu. Na hausiki kwenye mikataba kama hii. Notary Public ni mtu mwenye mamlaka ya kisheria ya kuwa shahidi wakati wa kutiliana sahihi mikataba. Ni zaidi ya Commissioner of Oaths. Yaani ni kama walivyo akina Lamwai.

Ama kweli waandishi wa Habari wa Tanzania ni vilaza. Nchee Nkapa aliwaambia huo ukweli wakanuna sana! Ukilaza wao unaonekana kwenye magazeti kila siku. Waache kufakamia tu bia, wafanye kazi za kiutu uzima! Wanatuchosha sana.
 
hilo halina mpinzani, waandishi wa habari wa kibongo wengi wanachosha. habari haiandikwi kwa kituo. sijui hata kama yeye mwenyewe anaisoma mara mbili kabla ya kuifikisha kwa editor.
 
...mahallu Na Kimada Wake Grace Wanaelekea Kushinda Hii Kesi..pamoja Na Ufisadi Wao ..serkali Inaelekea Kushindwa Kupeleka Ushahidi Wenye Nguvu....watadai Fidia ..tunaliwa Mara Mbili!!!
 
serikali inashindwa kutoa ushahidi kwa vile pesa hakula peke yake.
wakifikia pa kumuuliza pesa kazipeleka wapi ndo patapozuka balaa.
 
mahalu nifisadi kama lowasa wanataka kuipindisha kesi ili kina lowasa waje kupeta kama mahalu watakavyo mtreat
 
Hii ya Mahalu kushinda ndiyo taswira halisi ya aina ya mawakili wa serikali waliotuwakilisha ktk kesi ya IPTL kule London, Hawakufua dafu mbele ya wazoefu wa mikataba wa kimataifa. Hivyo inaonesha kwa mara nyingine AG hana timu imara ya mawakili and labda serikali imeamua kushindwa kesi kwa kutoa ushahidi hafifu kwa malengo fulani.

Waandishi wengi wa Bongo wanapenda sana bahasha za kaki na dola za fasta...

Kuna mtu anazo data na tarehe ya kesi ya Ditto??
 
Mnatumia vigezo gani kuonyesha Mahalu anashinda hii case?

Nakubaliana kuna mapungufu makubwa upande wa waendesha mashitaka, lakini bado kwenye hii case, naona bado iko katikati.
 
Mnatumia vigezo gani kuonyesha Mahalu anashinda hii case?
Nakubaliana kuna mapungufu makubwa upande wa waendesha mashitaka, lakini bado kwenye hii case, naona bado iko katikati.

.... Vigezo vitumikavyo ni prediction as to sat siku njema huonekana majogoo....
 
Kama DITO alishinda kesi yake na kuwekwa kapuni itakuwa ya Mahalu? Bila kusahau mkong'oto waliopata waandishi wa habari. Labda yeye awe na damu ya kunguni.
 
Kesi ya mahalu si rahisi kama wengi wanavyofikiri hapa.

Kesi hii ndani yake kwa habari za kusadikika toka kwa watu waliokaribu na mahalu na serikalini inahusu mapenzi, siasa na kukosekana kwa mgao ndani ya pesa za kununulia jengo.

Kwa ufupi tu Rostam pia anahusika, balozi aliwahi kupitisha pesa fulani za uchaguzi kupitia embassy Italy, lakini baadaye alikataa kupitisha hela chafu za uchaguzi wa Rais 2005 kwaajili ya Rostam na kundi lake akiwamo Prezidar, kukataa huku kulimjengea chuki na kundi hilo lililoapa kulipa kisasi.

Stori ya pili, balozi alikuwa na mahusiano na Grace wakati Rais pia akiwa waziri alikuwa na mahusiano naye,aidha katika mgao wa pesa hizo inasadikika lumbanga alikosa mgao kwa kuwa walikubaliana kuhusu hizo dili balozi alichofanya alishtuka na kuamua kumlipa huyo mama moja kwa moja kupitia akaunti yake yaani bank to bank transfer ili anayetaka mgao amfuate huyo mama ndio amgawie, kwa hali hii wengi walikosa walichotegemea.

Hivyo bilioni tatu zote ziliingia kwenye akaunti ya huyo mwenye nyumba, kama Mahalu alipata basi ni kwa huyo mama kutoa hela benki na kumpa mshiko wake akafie mbele. Hapa ndio ugumu unapokuja. Wakati huohuo inasemekana mahalu hana akaunti popote nje ya nchi, akaunti anayotumia siku zote ni ya mke wake hapa na yake binafsi ni ile iliyopo hapa nchini. So which is which yetu masikio ngoja tusubiri.

Ila kweli haowaandishi vilaza, ndio maana beni alikuwa akiwapaka. Aiiiiiiiiiibu
 
Kama ndo ivo,

Basi hatuna viongozi.

Lakini kila walakini unaojitokeza unaleta ushabihiano mzuri kwa kesi hii maana hata ugoigoi wa mashahidi dalili fulani humu.
Hivi huyo shahidi analipiwa kila kitu na serikali au ikoje?
 
Acheni pupa, Subirini Hukumu, yaani mumeanza kuwa majaji!!! na hata mungekuwa majaji hukumu si mpaka siku ya mwisho?
 
Kesi ya mahalu si rahisi kama wengi wanavyofikiri hapa.

Kesi hii ndani yake kwa habari za kusadikika toka kwa watu waliokaribu na mahalu na serikalini inahusu mapenzi, siasa na kukosekana kwa mgao ndani ya pesa za kununulia jengo.

Kwa ufupi tu Rostam pia anahusika, balozi aliwahi kupitisha pesa fulani za uchaguzi kupitia embassy Italy, lakini baadaye alikataa kupitisha hela chafu za uchaguzi wa Rais 2005 kwaajili ya Rostam na kundi lake akiwamo Prezidar, kukataa huku kulimjengea chuki na kundi hilo lililoapa kulipa kisasi.

Stori ya pili, balozi alikuwa na mahusiano na Grace wakati Rais pia akiwa waziri alikuwa na mahusiano naye,aidha katika mgao wa pesa hizo inasadikika lumbanga alikosa mgao kwa kuwa walikubaliana kuhusu hizo dili balozi alichofanya alishtuka na kuamua kumlipa huyo mama moja kwa moja kupitia akaunti yake yaani bank to bank transfer ili anayetaka mgao amfuate huyo mama ndio amgawie, kwa hali hii wengi walikosa walichotegemea.

Hivyo bilioni tatu zote ziliingia kwenye akaunti ya huyo mwenye nyumba, kama Mahalu alipata basi ni kwa huyo mama kutoa hela benki na kumpa mshiko wake akafie mbele. Hapa ndio ugumu unapokuja. Wakati huohuo inasemekana mahalu hana akaunti popote nje ya nchi, akaunti anayotumia siku zote ni ya mke wake hapa na yake binafsi ni ile iliyopo hapa nchini. So which is which yetu masikio ngoja tusubiri.

Ila kweli haowaandishi vilaza, ndio maana beni alikuwa akiwapaka. Aiiiiiiiiiibu

MAHALLU alikula hii pesa na watu wake akamtosa waziri wake [wakati huo]..baadaye grace alikosana na mumewe na wakaachana..mmewe ambaye walikuwa wa ki chill na waziri enzi hizo ..akaamua kutoboa siri ..hasa baada ya hasira ya kuachwa na mkewe ambaye alikuwa akimtuhumu mahallu kumgonga...

Kwa kuwa alikuwa na urafiki na waziri ..mmewe akaamua kumega siri nzima....waziri akaweka moyoni na zamu yake kuingia ilipofika akamua kulipua mara tu baada ya kushika usukani.......hiyo hisia kuwa hata waziri alimzunguka mtoa habari wake na kugonga grace..ni kweli ipo...hasa baada ya kisasi alichoweka....lakini hiyo inabaki hisia tu............pamoja na kuwa kama mnavyomjua waziri ni shap...na enzi zake alikuwa hacheki na nyani dizaini ya grace..anaharibu tu....

"....behind successfully man, theres a womam..and behind corrupt man theres a woman.."
 
Duh JF bwana, sasa kweli tumepanda kichwa, yaaani hata mahakama haijaaamua sisi tumesha iamulia hukumu, duh ukisikia masikio kupita kichwa ndio hii wakuu,

Duh tuiachieni mhakama kwanza iamue wakuu!
 
Back
Top Bottom