Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

Haya maandishi ya wanasheria usihangaike kusoma yoooooooote, nimesome vipengele kadhaa na kupata kujua kuwa nini wamelenga... Wanazunguuuuka kufanya reference za kesi za miaka hiyo mfano ukurasa wa 4 mpaka 14 nadhani ni reference za kesi tu, unaachana nazo... Pia kuna errors kadhaa ambazo zinatakiwa kurekebishwa, uzuri ni kuwa Tanzania mtu akiandika 'gay' badala ya 'guy' hata mahakamani wanajifanya wamemwelewa kuwa alitaka kuandika 'guy' kakosea kidogo.

Nasubiri kuona wanasheria wetu wanasemaje kuhusiana na utetezi huu

asante invesible ngoja niicheki upya
 
Kama ni kwel alifanya vitendo hivi inabidi alaniwe ila nina mashaka juu ya mwenendo mzima wa kesi hii katika nyanja zifuatazo wana JF mnisaidie
1.Kwanini iliendeshwa chembani sana
2.Kesi hii imeendeshwa haraka sana tofauti na kesi nyinginezo zinazofanana na hii
3.Kuna friend of mine anilisimulia kuwa(am not sure) mama yake mdogo mwanae alikuwa kaunganishwa kwenye kesi hii ila yy alichomoa sbb ilikuwa ni ya kugushi walitaka kumpa hela nyingi sn akachomoa sbb kaokoka.Anendelea kudai kuwa walioshiri ktk ile kes(watoto walio rawitiwa na wazazi wao) walipewa mihela mingi
4.Kwa mwenendo wa kesi na ushahidi uliotolewa hukum iko sahihi kabisa sbb mahakama zinabase ktk fact na sheria, lakin what is behind the scene?.
5.Iv hakuna ushahidi wa kutungwa na mtu akashinda kesi, iv mahakimu wetu hawawezi kununuliwa,iv mahakim wetu hawareceive order kutoka kwa vigogo&viongozi wakubwa serikalini, ivi ni nani anawateuwa mahakimu&je wanasave interest za nani na kama aliyekuteua akakupa order fulan utapinga kwa hali halisi yetu ya kibongo&ukipinga what next
Naomba nisaidiwe wana JF
 
Niliwahi kusikia kuwa Babu Seya na wanawe wamekosa pa kutokea maana walikuwa wanajirekodi mkanda wa video wakati wanafanya unyama huo, mimi nilikuwa mpenzi wa muziki wao lakini, kama ni wanyama kiasi hicho, let them rot in jail.
 
Ushahidi wote uliopo ni kwamba ni kweli hao Nguza na wanawe walifanya huo ufirauni. Sijui sababu yao ya kufanya hivyo ilikuwa nini. Wanaharakati wa haki za watoto na za binadamu walishiriki pia kwenye hiyo kesi, na kuna mafaili ya kutisha sana. Watoto waliofanyiwa hivyo wapo na walitoa ushahidi, ambao kisheria ili kulinda haki za mtoto aliyelawitiwa na kumkinga dhidi ya unyanyapaa, haipaswi kufanywa hadharani na wala majina yao hayatolewi kwenye vyombo vya habari. Mafaili ya Muhimbili walikopimiwa hao watoto na ripoti za madaktari zipo. Yaani hii ilikuwa soo, hawakuwa na jinsi ya kukwepa.

Na huy si wa kwanza. Miaka ya mwisho ya 1980's alitokea fundi mshona nguo akiitwa Ali Maumba, alikuwa akiwafanyia watoto mchezo huohuo, na alilawiti zaidi ya 100, ila wengine wazazi wao waliwazuia wasijitokeze ili kukwepa aibu kwa familia zao. Ile kesi Maumba alihukumiwa kifungo, lakini alipokata rufaa alishinda kutokana na ushahidi "dhaifu" wa madaktari. Na ile kesi ya Maumba hadi leo inatumika kama reference ya kuwakumbusha madaktari umuhimu wa "ushahidi wa kitaaluma" (expert witness) kuandikwa vizuri. Rafiki zangu wanaharakati wamei-cite mara nyingi sana kwenye papers zao.

Hii ya kina Babu Seya, wanasheria walijaribu sana wakakosa pa kutokea. Na hata wakati wa rufaa, haikuwezekana, akaendelea kubaki hatiani.

Hizo habari za kuwasingizia kina nani sijui ni uvumi tu, kungekuwa na ukweli tungeshapata japo chembe ya ushahidi. Hao mnaowataja wakati huo hawakuwa na mamlaka yoyote dhidi ya mahakama, na hata katika kesi hakuna wakili au yeyote aliyeleta ushahidi wa kuwahusisha. Kama ni rushwa, sijui ni rushwa gani watu wangetembeza kila mahali kuanzia kwa watoto wa shule ya msingi, walimu wao, wenyeviti wa serikali za mitaa, askari polisi kwenye posts hadi kwa waendesha mashtaka, wanaharakati wa haki za watoto, mawakili, wafanyakazi wa idara za hospitali (wauguzi, watu wa records, maabara,madaktari, ili ati wote wafoji habari zinazoendana), hakimu mkazi kisutu, majaji wa mahakama kuu, majaji waheshimiwa sana wa mahakama ya rufaa, woote hao utawahonga vipi? Kazi ya ku-organize na ku-stage plot kama hii ni kubwa na haiwezi kuwa siri, lazima ziwepo flaws, hata kama ni fiction unatunga wasomaji wataona tu uongo ulipo!

Kwa hiyo sioni cha kujadili kuhusu Babu Seya na wanawe, alipata haki yake ya fair trial, akawa convicted, na sheria ikachukua mkondo wake. Akatumia pia haki yake ya appeal, nako hatukusikia malalamiko ya unfair trial, akabakia guilty as charged. Basi.

Asante kwa kuiweka vizuri inavyotakiwa, inatia kichefuchefu mtu akianza kuwatetea hawa washenzi wa maadili!
 
Mi nadhani yote yawezekana, hilo la kuingilia nyumba ya kigogo fulani na la imani za kishirikina. Ila ambacho kinanipa taabu akilini mwangu ni kuwa wakati washikaji wanafanya unyama huo mshikaji hakuwa top wa country je aliwezaje kui control mahakama yoote wakati hata sasa mkuu wa nchi sidhani kama anaweza kuipindisha sheria kwa maslahi yake binafsi ila naamini inawezekana kwa maslahi ya uma. Na kuhusu hilo la ushirikina pia lawezekana kwa huku kwetu bongo mbona tumeshudia mauaji ya vikongwe, wenye vipara, na hata maalbino. Ngoja tuache sheria ichukue mkondo wake.
 
Mtu yeyote ambaye anatuhumiwa na ikadhibitishwa amefanya unyama huu sharti ahukumiwe kwa vifungu halali vya sheria ya nchi.Huu ni unyama amabo sidhani kama kuna mtu anaweza akubali mwanawe afanyiwe.Mungu apitishie mbali!

Ila bado maswali ni mengi kuliko majibu kwenye hili.Mzee mzima Nguza inawezekana kweli ashiriki yeye na wanawe?Wanasema "Mtu mzima dawa"!Labda kuwe na mambo ya kishirikina...

Tumeshuhudia mambo ya EPA na kadhalika na watu wamejipatia pesa nyingi tu kwa mgongo wa system zetu mbovu na tamaa ya wachache.Swali linakuja,je inawezekana pia huyo "kigogo" ambaye 'anahisiwa kukomoa' familia ya Nguza akawa na yeye 'alichota'?Kwa sababu katika dunia hii ya sasa sintoshangaa watu wakinunuliwa kwa bei yoyote ile na ushahidi ukapikwa na Jury ikakubaliana.Kuna wataalamu wa haya yote na victims wanakuwa-coached - it is possible.

Ila kama kweli wamefanya hayo,na Mungu awape a fair judgement.Ila kama 'wamechomekewa' then haki itendeke.

Nawasilisha.
 
Shida unajua iko wapi, wanasheria wanacheza na maneno katika kumshawishi jaji kwa kutumia mazingira yanayoleta jaji aamini kosa ama lilitendeka au la. Sasa wenyewe watashindana weeee ili aonekane nani zaidi kati ya mawakili - mshitaki na mtuhumiwa. Usisahau ni jamhuri inamshitaki Seya na wenzake. Sheria ni za serikali, mazingira yakitengenezwa na serikali nani ataizuia? Lakini pia watetezi kama hawakujiandaa milipuko ya mazingira watabanwa tu kwa vipengele ambayo serikali hiyo inavitumia. Baadaye wakijiweka sawa, watuhumiwa watajulikana hawakuwa na makosa, lakini cha moto walichokipata hakitarudi. Pale walipo si wanaisaidia polisi tu upelelezi ukiendelea? Traffic police akitaka kula sahani moja na raia atashinda yeye, hata kama gari imekaguliwa na wataalam waliobobea na TBS ikatia tich, vipengele vitatumiwa ili kukutia hatiani. Pole zake Seya et al., kama wameonewa sababu ya kuwa ugenini, ipo siku ukweli utajajulikana. Kama walifanya kweli na wanataka wasafishwe bado itajulikana tu, kwani walichokifanya hata kwao hakiruhusiwi.

Leka
 
Kesi imeahirishwa hadi tarehe 3/dec, hii ni kwa mujibu wa Michuzi blog
http://issamichuzi.blogspot.com/2009/11/rufaa-ya-babu-seya-yaahirishwa-hadi.html#comments

Mtakumbuka ile miaka ya 1994 – 1995 kuhusu habari ya kesi maarufu ya Mmarekana mweusi, mcheza kandanda na msanii O.J Simpson ambaye alikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya mtalaki wake Nicole Brown Simpson na aliyekuwa rafiki ya wanamke huyo (Ronald Goldman).
Kesi ilisikilizwa kwa muda wa miezi nane na ilihusisha mashahidi 150 kwa upande wa mashataka ambao kwa kiasi kikubwa walionekana kuwa makini katika kila walichotakiwa kuieleza Mahakama ili kuusaidia upande wa mashtaka kuthibitisha makosa dhidi ya O.J pasipo kuacha mashaka yoyote.

Katika kesi hii O.J aliajiri wanasheria wazoefu wa kumtetea akiwemo Gerald Uelmen (profesa wa sheria katika chuo cha Santa Clara pamoja na Carl E. Douglas and Johnnie Cochran, (wanasheria walibobea katika taaluma ya sheria za ushahidi wa masuala ya vinasaba (DNA evidence). Na inadaiwa kuwa katika kesi hii, gharama za utetezi wa O.J Simpson zilikuwa kati ya dola za kimarekani milioni 3- 6.

Utetezi wa O.J ulihusisha wanasheria walio na ufahamu kina katika makosa ya jinai na uendeshaji wa mashtaka ambao sio tu waliweza kuendesha kesi mahakamani pia waliweza kufanya upepelezi wa kina katika kila hatua ya kesi kujua undani wa kesi ya mteja wao.

Kesi hii ya O.J Simpson ilitawaliwa na vihoja vingi vya wanahabari na ikiwemo kuitaka Mahakama kuruhusu matumizi ya kamera za video kurekodi mwanendo mzima wa kesi, jambo ambalo lilidaiwa kuhamishisha chuki dhidi ya mthumiwa na wengine kuona inaisukuma Mahakama yenye majaji wazungu kuzinagtia hukumu yao kwa yale ambayo vyombo vya habari ziliripoti na jamiii kuya amini.

Hata hivyo O.J alikuja kuachiwa huru kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani pamoja na mbwembwe zote za upande wa mashtaka.

. Kesi ya Babu Seya

Sijui katika kesi hii ya Babu Seya na wanae tunaweza kujifunza nini kwa mfumo mzima wa usimamizi wa haki nchini kwetu.

Nimesoma hukumu zote mbili za awali (Mahakama ya Hakimu Mkazi) na Mahakama Kuu. Singependa kutoa maoni yangu kwenye hukumu hizo kwa kuwa sasa kesi bado ipo katika ngazi ya mwisho ya rufaa. Lakini sijaweza kufahamu kwa kina katika hiyo rufaa, sababu za rufaa (ground of Appeal) ni zipi! Ambao kisheria ndizo zinazotoa uwezekani wa kujua hatima ya familia ya Babu Seya.

Kwa ujumla, mfumo wetu wa ushughulikiaji haki kuanzia polisi na vyombo vingine vya dola unaoneakana kana kwamba bado hauaminiki mbele ya macho ya jamii. Kuna wengine walitegemea Seya wasitiwe hatiani na wengine wanaona ilifaa asulubiwe!. Haya yote ni mambo ya kisheria, na panapokoskana mfumo mzuri wa kuyashughulikia inakuwa hivi!.

Zipo kesi nyingi ambazo kwa mwonekano wa yale yanayoandikwa au kutangazwa kwenye vyombo vya habari au pengine kusikia kwa mtu zimeonyesha mtazamo ambao labda jamii nayo ni sehemu ya mahakama na hivyo kuwa na uhakika hukumu itakuwaje!.

Kwa mfano, katika kesi ya Kamanda Zombe yale yaliyokuwa yakiripotiwa na vyombo vya Habari au kuelezwa mtaani na “wataalamu wa kupika tetesi”, yalitengeneza mazingira ya Zombe na wenzake kuonekana walitenda kosa na pia asilimia kubwa ya jamii iliamini kuwa kamanda na wenzake wasingeweza kuchomoka!.

Wakati mwingine, habari za mahakamani zinaandikwa kwa jinsi ya kumkandamiza mshtakiwa na kujenga hisia kwa jamii ione kweli anaa husika kwenye kosa kwa mfano haya magaeti ya mchana utakuwa kicho cha habari kinasoma “YAANI WE AISHA UMEKOSA NINI MPAKA UIBE SIMU YA MWENZIO….SASA UTAFIA SEGEREA”……Eti ukisoma ukweli wa hiyo habari unaona kumbe Mwandishi anaripoti kesi ya mtuhumiwa ambaye ndo kwanza amesomewa shtaka!

Uwezo wa Kitaaluma wa kushughulikia kesi

Kanuni ya jumla inafundisha kuwa kuwa kwenye taaluma sio kujua kila kitu na ndivyo hivyo hata kwa wapepelezi, waendesha mashtaka, wanasheria, majaji na mahakimu. Wapo wanasheria ambao wamefanikiwa na kupata wateja wengi sio kwa uzoefu wa taaluma zao bali kwa “umaarufu”. Na hii imekuwa chanzo cha watu wengi kupoteza kesi zao kutokana na kumwajiri mwanasheria ambaye pengine hana uzoefu au kutokana na kuwa na kazi nyingi anashindwa kumudu kuendesha kesi zake kwa umakini.

Wapo mahakimu na majaji wengi wamekuwa wakitoa hukumu zao sio kwa kuzingatia weledi bali kwa “uzoefu” na pengine hukumu nyingine zinatolewa na Mahakimu au Majaji sio kwa kutumia busara zao bali kwa kuangalia jamii inasemaje au watu fulani wanasemaje au kwa kuzingatia zaidi utu!

Mazingira nayo ni tatizo kwenye taaluma, (mtakumbuka yule Hakimu wa Mahakam ya Mwanzo aliyewahi kumtia hatiani mbwa kwa kuitwa “Immigration (uhamiaji kwa kikwetu!)” shida haikuwa taaluma bali ni mazingira ambayo alitakiwa kutekeleze taaluma yake (hakuwa hata na nyenzo za rejea).

Hao mapolisi nadhani mnawajua mazingira ya kazi zao.wengi wakitoka chuoni uzoefu ndo huo, akiwa mtaani anafanya "kazi kama tulivyofundishwa polisi koleji".

Kwa upande wa waendesha mashtaka nako balaa tupu!. Kuna niliwahi kusikia ili kuwa mbinde kunadaa mashtaka dhidi ya mtu aliyeingilia mifumo ya kompyuta pasipo halali (computer hacker)
 
BABU SEYA NA MWANAE NI WAHANGA WA MAFANIKIO YAO?
(Rutashubanyuma Nestory – Mpembuzi yakinifu kutoka Arusha.)

Baba wa Taifa, Mwalimu Nyeyere kwenye moja ya hotuba zake alitukumbusha ya kuwa mfumo wetu wa kutoa haki upo radhi kuwaruhusu wahalifu tisa wapete ili mradi kuhakikisha raia mwadilifu mmoja tu analindwa. Mimi ninaamini kabisa kama waheshimiwa wanahaki wangelipembua ushahidi uliokuwa mikononi mwao bila ya kuangalia hadhi ya watuhumiwa wangeliwafutia mashitaka yote kwa vile ushahidi unapingana vilivyo na ni mdhaifu mno kwa mahakama kutoa maamuzi ya kumfunga mtu kifungo cha maisha. Katika hukumu yenye kurasa 55, Mahakama ya Rufaa ilitegemea sana ushahidi wa kusimuliwa wa watoto wahanga wa kubakwa ambapo mahakama haikutumia uwezo wake iliyopewa na sheria kuupima ushahidi huo ipasavyo. Mahakama ya Rufaa ilikiri ya kuwa ushahidi ulikuwa haukupimwa na hivyo usingeweza kusimama pekee yake na kuwatia watuhumiwa hatiani na hivyo ulihitaji kuungwa mkono na ushahidi mwingine. Ushahidi mwingine ambao Mahakama ya Rufaa iliutumia katika kumtia hatiani Babu Seya na mwanaye ulikuwa una mapungufu mengi na hivyo kuniondolea mashaka kabisa watuhumiwa wote wawili hawakupaswa kutiwa hatiani bali kuachiwa huru. Katika ukurasa wa 46-47 wa uamuzi, Mahakama ya Rufaa ilikuwa na haya ya kusema: “Swali tulilojiuliza kama shahidi Na. 8 aliweza kuwatambua kwa majina mtuhumiwa namba 1 na namba 2 kwa nini alishindwa kuwatambua watuhumiwa wengine? Watuhumiwa namba 3 na namba 4 tunawapa nafuu ya mashaka na hivyo kuwafutia shitaka hili.” Utata ambao Waheshimiwa wanahaki hawakuona ni kuwa washitakiwa namba moja na namba mbili walikuwa ni Babu Seya na mwanaye Papii. Hawa ni watu maarufu kutokana na mchango wao mkubwa kwenye nyanja ya burudani la muziki. Ushahidi wa shahidi namba 8 ulipaswa utupwe kwa kutambua watu maarufu tu na kushindwa kuwatambua watuhumiwa baki. Shahidi namba mbili ilidaiwa alipopimwa alikutwa ameambukizwa kisonono na kulingana na ushahidi wake alidai Babu Seya ndiye aliyembaka. Sasa tatizo hapa ni kuwa kulingana na hati ya mashitaka - haya ni makosa ya kubaka kwa genge ikimaanisha ya kuwa kama kweli Babu Seya ndiye aliyembaka shahidi namba mbili basi ndiye aliyemwambukiza kisonono lakini kizungumkuti kilivurumishwa na mashahidi wengine tisa ambao nao walidai kubakwa na genge lililoongozwa na Babu Seya lakini hakuna hata mmoja wao aliyedai kuambukizwa kisonono! Pia shahidi namba 20 ambaye ni muuguzi alithibitisha ya kuwa shahidi namba mbili hakuwa na kisonono. Vilevile shahidi namba 5 aliyedai kuwemo kwenye kundi la kubakwa ushahidi wake ulibezwa na shahidi namba 20 ambaye alikuwa ni muuguzi kwa kuthibitisha ya kuwa shahidi namba tano alikuwa bado ana bikira yake kinda hivyo asingeliweza kuwa alibakwa. Ushahidi mwingine uliotumika kuwatia hatiani unatokana na ushahidi uliotolewa kuhusiana na magodoro mawili na kitanda ambacho polisi na walalamikaji walivikuta kwenye nyumba ya Babu Seya mtuhumiwa. Ushahidi wa mashahidi ulifanana kwa sababu siyo walitendewa unyama ule ila polisi waliwapa nafasi ya kuivinjari nyumba ya mtuhumiwa Babu Seya. Polisi walipaswa walinganishe ushahidi kabla ya kukagua nyumba ya Babu Seya na ule ushahidi walioukuta baada ya ukaguzi wao ili kujihakikishia walalamikaji kweli wanaijua vizuri undani wa nyumba ya mtuhumiwa. Kwa vile baadhi ya walalamikaji walidai walilazimishwa ngono ya kinywani ni dhahiri waliona maumbile ya uume wa watuhumiwa na hivyo walipaswa waelezee ulivyo. Mfano walipaswa watamke kama watuhumiwa walikatwa jando au hapana na kama wana alama zozote zile sehemu za siri na polisi kuwakagua watuhumiwa ili kuthibitisha ukweli. La mwisho ni utetezi wa Babu Seya kuwa yeye hana nguvu za kiume. Inatosha kusema hapa ya kuwa kisheria Babu Seya alijua makosa yaliyokuwa yanamkabili pale aliposomewa mahakamani kisutu mbele ya hakimu mkazi akiwa rumande mikononi mwa polisi. Alipoomba akapimwe hospitali nguvu za kiume polisi walimkatalia lakini mahakama hawakuiona polisi kitendo ilichokifanya kilikuwa ni cha kupindisha haki kwa kuzuia mahakama kupata ushahidi wote ili kutenda haki. Kwa lugha ya mwingereza wasema: “there was an obstruction of justice and an abuse of public office.” Mazingira haya yote yalikuwa siyo ya kuthibitisha hukumu bali kuwaachilia watuhumiwa wote kwani kuna ushahidi wa kutosha polisi walishindwa kutekeleza majukumu yao na hivyo kushindwa kuthibitisha makosa. Hapa haki ilipindishwa kabisa!!!
 
KESI zenye maslahi yanayowahusu watawala mara nyingi huchinjiwa pale mahakama ya rufaa.
MAHAKAMA kuu ndiyo pekee hutoa haki ambayo huporwa na mahakama ya rufaa.

Kama ushahidi una mashaka, mara nyingi hupelekea uhalali wa kesi kuwa mashakani.
Katika kesi ya babu seya ni kwamba pamoja na ushahidi kuwa na utata, bali pia hata mwenendo wa mahakama dhidi ya kesi ile unatia mashaka matupu lakini mahakama ya juu zaidi imepigilia msumari kukubaliana na makosa haya ya kiufundi ambayo yanatia doa kubwa tasnia ya sheria nchini.

ONLY in Tanzania
 
Back
Top Bottom